Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Makumi waripotiwa kuuawa katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia huko Gaza

Shirika la habari la Ufaransa AFP limekuwa katika eneo la tukio huko Jabalia baada ya mlipuko katika kambi ya wakimbizi iliyojaa watu.

Moja kwa moja

Yusuf Jumah and Ambia Hirsi

  1. Marekani yakanusha madai ya Putin kwamba nchi za Magharibi zilipanga maandamano dhidi ya Wayahudi katika uwanja wa ndege

    Marekani imepuuzilia mbali madai ya Urusi kuwa "ya kipuuzi" kwamba ghasia dhidi ya Israel katika uwanja wa ndege wa Dagestan siku ya Jumapili ziliandaliwa na Ukraine na nchi za Magharibi.

    Katika mkutano wa televisheni siku ya Jumatatu, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema tukio hilo limekuwa sehemu ya jaribio la kueneza "machafuko" nchini Urusi.

    Mamia ya watu walivamia uwanja wa ndege wa Makhachkala kabla ya kuwasili kwa ndege kutoka mji mkuu wa Israel Tel Aviv.

    Wengi walipeperusha bendera za Palestina na kuimba nyimbo za chuki dhidi ya Wayahudi.

    Dagestan, jamhuri ya eneo la Urusi, ina idadi kubwa ya Waislamu, na tukio hilo linakisiwa kuchochewa na hasira juu ya mzozo wa Gaza.

    Vikosi vya usalama hatimaye vilidhibiti hali hiyo, na zaidi ya watu 60 wamekamatwa, kulingana na mamlaka za eneo hilo.

    "Matukio ya Makhachkala jana usiku yalichochewa kupitia mitandao ya kijamii, haswa kutoka Ukraine, na maajenti wa huduma maalum za Magharibi," Bw Putin aliambia mkutano wa Baraza la Usalama la Urusi.

    "Ni nani anayeandaa machafuko mabaya na ni nani anayefaidika nayo leo, kwa maoni yangu, tayari imekuwa dhahiri.

    Gavana wa Dagestan, Sergei Melikov, pia alisema ghasia hizo zimechochewa "kutoka eneo la Ukraine na wasaliti" kwa kutumia chaneli ya Telegram iitwayo Morning Dagestan.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza

  2. Netanyahu alaani video 'katili' ya Hamas ya mateka wa Israel

    Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelaani kama "propaganda za kikatili" video iliyotolewa na Hamas inayoonyesha mateka wa Israel waliotekwa wakati wa mashambulizi ya Oktoba 7.

    Kanda hiyo, iliyotolewa Jumatatu, inawaonyesha wanawake watatu wa Israel, mmoja wao akimsuta Bw Netanyahu na kutoa wito wa kuachiliwa kwa mateka.

    Hamas iliwakamata mateka wasiopungua 230 katika mashambulizi hayo na Waisraeli wasiopungua 1,400 waliuawa.

    Ni wanne pekee ambao wameachiliwa hadi sasa.

    Israel imeanzisha operesheni kubwa ya kijeshi huko Gaza, ikisema kuwa lengo ni kuangamiza Hamas na utawala wake katika eneo hilo.

    Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas imesema takriban Wapalestina 8,000 wameuawa.

    Video ya mateka hao ilitolewa na mrengo wenye silaha wa Hamas, Brigedi za Izzedine al-Qassam.

    Hatujui chochote kuhusu hali ambayo video hiyo ilirekodiwa.

    Ni mmoja tu wa mateka anayezungumza kwenye kamera katika klipu nzima.

    Hatutachapisha video hiyo .Wafungwa wa kivita na mateka wanalindwa chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu, na BBC haipeperushi nyenzo ambazo zinaweza kuwa zimerekodiwa kwa hali ya kulazimishwa.

    Katika taarifa, Bw Netanyahu alisema: "Hizi ni propaganda za kikatili za kisaikolojia za Hamas-Isis [kinachojulikana kama Dola la Kiislamu].

    "Tunakumbatia familia. Tutafanya kila kitu kuwarudisha nyumbani watu wote waliotekwa nyara na waliopotea."

    Pia aliwataja mateka hao kuwa ni Elena Trupanov, Danielle Aloni na Rimon Kirsht.

    Binti ya Bi Aloni mwenye umri wa miaka mitano, pamoja na dadake na shemeji yake na binti zao mapacha wa miaka mitatu, pia walitekwa nyara tarehe 7 Oktoba.

    Katika kikao na wanahabari siku ya Jumatatu, babake Bi Aloni alisema moyo wake "ulikuwa karibu kukoma kudunda" alipoona picha yake.Alitoa wito kwa Amir wa Qatar, ambaye amehudumu kama mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya mateka, "kufanya kila juhudi kuwarudisha nyumbani".

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza

  3. Ballon d'Or kwa Wanaume: Lionel Messi ashinda tuzo ya nane, akimpiku Erling Haaland na kunyakua taji

    Mshambuliaji wa Argentina na Inter Miami Lionel Messi ameshinda Tuzo ya Ballon d'Or kwa Wanaume kwa mara ya nane.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 alitambuliwa katika sherehe hiyo mjini Paris baada ya kuisaidia nchi yake kushinda Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka jana.

    Kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Uingereza na Real Madrid, Jude Bellingham ameshinda Kombe la Kopa kwa mchezaji bora wa dunia mwenye umri wa chini ya miaka 21.

    Messi alishinda tuzo yake ya Ballon d'Or iliyoongeza rekodi yake mbele ya mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland.

    Fowadi wa Ufaransa Kylian Mbappe - ambaye amekuwa mtu wa pili kufunga hat-trick ya mwisho ya Kombe la Dunia katika kupoteza kwa penalti 4-2 dhidi ya Argentina - alimaliza wa tatu.

    "Ni vizuri kuwa hapa kwa mara nyingine tena kufurahia wakati huu," Messi alisema."Kuweza kushinda Kombe la Dunia na kufikia ndoto yangu."

    Nyota huyo wa zamani wa Barcelona na Paris St-Germain aliongeza: "Sikuweza kufikiria kuwa na kazi ambayo nimekuwa nayo na kila kitu ambacho nimefanikiwa, bahati ambayo nimepata kuwa sehemu ya timu bora zaidi katika historia.

    "Zote [tuzo za Ballon d'Or] ni maalum kwa sababu tofauti."

  4. Netanyahu akataa usitishaji vita, akisema 'huu ni wakati wa vita'

    Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema anataka kuweka wazi msimamo wa Israel juu ya kusitisha mapigano.

    "Kama vile Marekani isingekubali kusitishwa kwa mapigano baada ya kulipuliwa kwa Bandari ya Pearl au baada ya shambulio la kigaidi la 9/11, Israeli haitakubali kusitisha uhasama na Hamas baada ya mashambulizi ya kutisha ya Oktoba 7," amesema

    "Wito wa kusitishwa kwa mapigano ni wito kwa Israeli kujisalimisha kwa Hamas, kujisalimisha kwa ugaidi,"

    “Biblia inasema ‘kuna wakati wa amani, na wakati wa vita’,” ameongeza kusema, “huu ni wakati wa vita”.

    "Vita kwa mustakabali wetu wa pamoja. Leo, tunachora mstari kati ya nguvu za ustaarabu na nguvu za kishenzi."

    Waandamanaji wachuku udhibiti wa ofisi za serikali ya Canada

    Wanaharakati kote Canada wamekalia afisi za wanachama wa ngazi za juu wa serikali huku wakiwataka wabunge watoe wito wa kusitishwa kwa mapigano.

    Miongoni mwa ofisi zilizokaliwa Jumatatu ni zile za Waziri wa Ulinzi Bill Blair na Naibu Waziri Mkuu Chrystia Freeland.

    Maandamano hayo yalifanyika katika ofisi 17 katika miji 12 kote nchini, kulingana na Gazeti la Montreal.

    "Tuko hapa kuitaka serikali ya Kanada itoe wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja na kukomesha vizuizi vilivyodumu kwa takriban miaka 16 katika Ukanda wa Gaza na kukomesha ushirikiano wa Canada na Israel," mmoja wa waandamanaji mjini Toronto aliambia Reuters.

    Waandamanaji huko walishikilia ishara zinazoonyesha Wapalestina ambao wameuawa na mabango ya kutaka kusitishwa kwa mapigano na "Palestina huru".

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza

  5. Hujambo na karibu

    Ni siku ya 25 sasa ya vita vya Israel na Hamas huko Gaza tangu shambulio la kundi hilo Oktoba tarehe saba .

    Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekataa wito wa kusistisha mapigano akisema 'huu ni wakati wa vita'

    Tunachojua kuhusu mapigano hayo ni kwamba Israel imefanya mamia ya mashambulizi ya anga katika siku za hivi karibuni na vifaru vyake vimeonekana ndani ya eneo hilo.

    Wakati huo huo, mamia kwa maelfu ya raia wa Palestina wamelala usiku mwingine wenye wasiwasi huko Gaza, wengi wao wakijificha wanakoweza baada ya kukimbia kutoka sehemu ya kaskazini ya Ukanda huo kujibu maonyo ya Israeli.Karibu kwa habari zetu za moja kwa moja kuhusiana na mzozo huo na mengine kutoka kote ulimwenguni .