Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mamia ya wagonjwa wamekwama katika hospitali za Gaza-UN

Alisema watu wengi wa kaskazini - sio wagonjwa pekee - pia "hawawezi kusonga kwa sababu hawana usafiri, hawana njia".

Moja kwa moja

Yusuf Jumah and Ambia Hirsi

Karibu

Ni siku ya 24 ya vita vya Israel na Hamas huko Gaza tangu shambulio la kundi hilo Oktoba tarehe saba .

Huko Gaza kumekuwa na sauti ya mara kwa mara ya mlipuko, sauti ya ndege za mashambulizi na sauti ya ndege zisizo na rubani kwenye video inayoonyesha Jiji la Gaza kwa mbali, kwa kiasi kikubwa na kufunikwa na giza.

Mamia kwa maelfu ya raia wa Palestina wamestahimili usiku mwingine wenye wasiwasi katika Ukanda wa Gaza, ngome ya kundi la Hamas ambayo Israel imeahidi kuliangamiza tangu shambulio lake baya la tarehe 7 Oktoba.

Hospitali ya Al-Quds katika Mji wa Gaza, imekuwa ikiangaziwa baada ya madaktari wa Kipalestina kuripoti kwamba waliambiwa na Waisraeli kuhama - ombi ambalo wanasema haliwezekani kwa wagonjwa walio ndani.Mashambulizi ya anga yaliripotiwa karibu na hospitali hiyo siku ya Jumapili.

Rais wa Marekani Joe Biden amemwambia Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwamba mtiririko wa misaada katika Gaza unahitaji kuongezwa kwa kiasi kikubwa.Siku hiyo hiyo, mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu alionya kwamba kuzuia usambazaji wa misaada kwa Gaza kunaweza kuwa uhalifu wa kivita.

Endelea kuwa nasi kwa matangazo ya moja kwa moja kuhusu kinachoendelea huko gaza na matukio mengine kote duniani.Mimi ni Yusuf Jumah.