Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Nililaani ugaidi wa Hamas waziwazi, asema mkuu wa Umoja wa Mataifa, baada ya kuzozana na Israel

Antonio Guterres anasema matamshi yake "yalipotoshwa" baada ya taarifa ya Jumanne iliyoibua mzozo kati yake na Israel

Moja kwa moja

Yusuf Jumah and Ambia Hirsi

  1. 'Sitaki kumwacha binti yangu aende'

    Binti ya Abdullah Teish aliuawa katika shambulizi la anga la Israel lililopiga nyumba yao huko Khan Younis.

    Alieleza jinsi ambavyo hakutaka kumwachia huku akiwa amembeba mikononi mwake na kumbusu miguu yake.

    "Huyu ni binti yangu, nataka kuwa naye muda mwingi kama nilivyokuwa nae kabla hatujamzika. Walitaka kumfunika uso, lakini nikawaambia hapana, hatufuni nyuso za mashahidi."

    Teish alimpeleka barabarani, akiwa amezungukwa na vifusi vya majengo yaliyobomolewa na mashambulizi ya Israel

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  2. Israel inasema imeshambulia maeneo ya wanajeshi wa Syria

    Mapema siku ya Jumatano asubuhi kwa saa Israeli (IDF), ndege za kivita za Israel zimeshambulia miundombinu ya kijeshi na kupiga kwa makombora makombora mali ya Jeshi la Syria, kwa mujibu wa jeshi la Israel.

    Shambulio hilo limelenga kujibu shambulio dhidi ya Israeli siku ya Jumanne, IDF ilisema.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  3. Israel yafanya shambulizi la ndege zisizo na rubani Jenin huku kukiwa na mapigano kwenye Ukingo wa Magharibi

    Jeshi la Israel (IDF) limefanya shambulio la ndege zisizo na rubani wakati wa mapigano na Wapalestina karibu na mji wa Jenin katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu "muda mfupi uliopita", jeshi la Israel limesema katika mitandao ya kijamii.

    Watu wawili pia wamekamatwa Jenin huku kukiwa na ufyatulianaji wa risasi na "magaidi wenye silaha" kulingana na taarifa ya IDF iliyowekwa mtandaoni.

    Mapigano hayo yalizuka wakati Israel ikifanya doria karibu na kambi ya wakimbizi ya Jenin, Israel inasema, na yalianza baada ya wanamgambo wa Kipalestina kufyatua risasi na kuwarushia mabomu wanajeshi wa Israel.

    Hakuna wanajeshi wa Israel walioripotiwa kujeruhiwa.

    Siku ya Jumapili, Israel ilitekeleza shambulizi la anga dhidi ya msikiti mmoja uliopo Jenin ambao ilisema ulikuwa unatumiwa kama ‘’uwanja wa ugaidi’’

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  4. Je, Biden anaweza kupoteza uungwaji mkono wa Wamarekani Waarabu na Waislamu?

    Basim Elkarra, Mmarekani wa Palestina ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Baraza la Mahusiano ya Kiislamu, anahofia kila ujumbe wa simu anaopokea.

    "Usiku wa jana ulikuwa mbaya zaidi. Nilimpigia simu binamu yangu na mtoto wa dada yake aliuawa – mwanae wa pekee. Tulipoteza wanafamilia wa upande wa mama yangu na baba yangu,” anasema akiwa nyumbani kwake Sacramento, California.

    “Nilipata ujumbe kutoka kwa marafiki hapa California. Watu kadhaa wa familia zao wameuawa.”

    Anasema amesikitishwa sana na msimamo wa Rais Biden kuhusu Israel, akiongeza kuwa anahisi "'hatia kubwa" kwa serikali kutumia dola zake za kodi kulipia silaha zinazotumika Gaza.

    Elkarra alihudumu katika Chama cha Democratykatika jimbo la California kama mwenyekiti wa kamati ya kumaliza ubaguzi kwa miaka 10, lakini anahisi hii ni hatua ya mabadiliko kwake kabla ya uchaguzi wa 2024.

    Anasema hamfahamu kiongozi yeyote wa chama cha Muslim Democratic au kiongozi yeyote wa kiarabu kutoka Marekani ambaye anaunga mkono uungaji mkono wa Biden kwa Israel.

    Viongozi hawa hawataki kumpigia kura Donald Trump, kwa hivyo "wanajaribu kushinikiza mbadala mwingine ndani ya Chama cha democrat kwa sababu Biden hajaonyesha uongozi katika mzozo mkubwa unaoathiri ulimwengu mzima."

    Biden ana hatari ya kupoteza kura ya Waislamu wa Marekani, anasema, isipokuwa akiitisha usitishaji wa mapigano mara moja.

    "Hakuwezi kuwa na Wapalestina wengine waliouawa."

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  5. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 25.10.2023