Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Nililaani ugaidi wa Hamas waziwazi, asema mkuu wa Umoja wa Mataifa, baada ya kuzozana na Israel

Antonio Guterres anasema matamshi yake "yalipotoshwa" baada ya taarifa ya Jumanne iliyoibua mzozo kati yake na Israel

Moja kwa moja

Yusuf Jumah and Ambia Hirsi

  1. Kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Hadi kesho kwaheri.

  2. Je, Hamas wanahifadhi mafuta huko Gaza?

      • Author, Adam Durbin
      • Nafasi, Ripota wa moja kwa moja

    Mashirika mengi ya misaada yanasema kitu kimoja - kwamba Gaza inahitaji sana mafuta, huku hospitali zikiwa tayari zimefungwa.

    Israel hairuhusu mafuta kuingia na imeishutumu Hamas kwa kuhifadhi mamia ya maelfu ya lita za mafuta katika hifadhi.

    Jana, jeshi la Israel lilichapisha picha ya angani ya matangi 12 karibu na mpaka wa Gaza na Misri, ambayo ilisema inatumika kuhifadhi mafuta.

    Dk Frank Ledwidge, mchambuzi wa kijeshi na afisa wa zamani wa ujasusi wa Uingereza, ananiambia haoni sababu ya kijeshi kuhifadhi mafuta hapo na "angependa kuona ushahidi zaidi" wa mizinga hiyo inayotumika kabla ya kufikia hitimisho.

    Kuna uwezekano mkubwa wa mafuta kuhifadhiwa chini ya ardhi katika mtandao wa vichuguu wa Hamas, ambao wataalam wanaamini kuwa hadi urefu wa kilomita 500 (maili 310), mtaalamu wa Chuo Kikuu cha Portsmouth anasema.

    Hamas isingetumia akiba ya mafuta kama dizeli au petroli kupaka makombora wanayorusha Israel, kwani silaha hizo zinahitaji mafuta maalum, Dk Ledwidge anaongeza.

    Mfanyakazi mwenzake na mtaalamu wa ghasia za kisiasa nchini Israel, Dk Veronika Poniscjakova, ananiambia "haitakuwa mara ya kwanza" Hamas kuiba mafuta, misaada ya kibinadamu au vifaa vingine kwa matumizi yake.

    Juu ya nini hifadhi zinazodaiwa zinaweza kutumika, anaelezea hakuna anayejua kwa uhakika - lakini anasema pengine ni pamoja na kuweka taa katika mtandao wao wa chini ya ardhi, kuhakikisha magari yao yanakimbia na kusukuma maji kutoka kwenye vichuguu ili kuzuia mafuriko.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  3. Ndege ya Uingereza iliyobeba misaada kwa Wagaza yawasili Misri

    Misaada ya Uingereza kwa watu wa Gaza imetua Misri, waziri wa mambo ya nje James Cleverly ameandika kwenye mtandao wa X, iliyokuwa Twitter.

    "Misaada ya kibinadamu lazima iendelee kuwafikia wale wanaohitaji zaidi," alisema, pamoja na picha ya ndege ikiwasili.

    Waziri Mkuu Rishi Sunak hapo awali alitangaza kwamba ndege ya RAF ilikuwa ikisafiri kuelekea Misri ikiwa na tani 21 za vifaa vya kibinadamu - kama sehemu ya kifurushi cha msaada cha Uingereza cha £30m kwa Gaza.

    Nchi nyingi zimepeleka misaada Gaza.

  4. Ninalaani mashambulizi ya kutisha ya Hamas - Guterres

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasisitiza kuwa analaani "vitendo vya kutisha vilivyofanywa na Hamas Oktoba 7 nchini Israel".

    Guterres anadokeza kuwa jana alisema "hakuna kitu kinachoweza kuhalalisha mauaji ya kimakusudi, kuwajeruhi na kutekwa nyara kwa raia - au kurusha roketi dhidi ya makazi ya raia".

    Anaendelea kusema: “Kwa hakika niliangazia malalamiko ya watu wa Palestina.

    "Kwa kufanya hivyo, nilisema kwa uwazi, na ninanukuu: 'Lakini malalamiko ya watu wa Palestina hayawezi kuhalalisha mashambulizi ya kutisha ya Hamas'

    Hatimaye, Guterres anasema anaamini ni muhimu kuweka mambo sawa.

    "Hasa kwa heshima ya waathiriwa na familia zao," anasema kabla ya kumalizia hotuba yake fupi.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  5. Israel yasema maafisa wa UN hawatapata visa huku mzozo unavyoongezeka

    Sasa tunaelekeza macho yetu kwa mzozo uliozuka jana usiku, baada ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kusema mashambulizi ya Hamas tarehe 7 Oktoba - ambapo zaidi ya 1,400 waliuawa nchini Israel - hayakufanyika "katika ombwe".

    Matamshi hayo yaliibua hisa kali kutoka kwa waziri wa mambo ya nje wa Israel, ambaye alisema "hakuna sababu ya kushabikia mauaji hayo".

    Sasa Israel inasema haitatoa visa kwa maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa.

    "Tunahitaji kuushtua Umoja wa Mataifa," Balozi wa Israel kwenye Umoja wa Mataifa Gilad Erdan aliviambia vyombo vya habari vya Israel.

    Alisema kiongozi wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu Martin Griffiths alitaka kuja Israel - na amekataliwa.

    "Mimi, kwa uratibu na Wizara ya Mambo ya Nje, niliwajulisha juu ya kukataa," alisema Erdan.

    "Hataweza kuja hapa katika kanda. Mashirika yao yanahitaji kuleta watu wapya mara kwa mara, kwa hakika katika wakati kama huu. Watakataliwa."

  6. Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas: Zaidi ya 700 wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita huko Gaza

    Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza inasema jumla ya vifo kutokana na mashambulizi ya Israel sasa imefikia zaidi ya watu 6,500 tangu tarehe 7 Oktoba, wakiwemo watoto 2,704.

    Katika saa 24 zilizopita, Wapalestina 756 wakiwemo watoto 344 waliuawa katika mashambulizi ya Israel, wizara hiyo inaongeza.

    Imesema eneo la kusini mwa Gaza lilikumbwa na mashambulio ya hivi punde zaidi.

    Israel yasema maafisa wa Umoja wa Mataifa hawatapata visa huku mzozo ukiongezeka

    Zaidi sasa kuhusu mzozo uliozuka jana usiku, baada ya mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kusema mashambulizi ya Hamas tarehe 7 Oktoba - ambapo zaidi ya 1,400 waliuawa nchini Israel - hayakutokea "katika ombwe".

    Maoni hayo yaliibua maoni ya hasira kutoka kwa waziri wa mambo ya nje wa Israel, ambaye alisema "hakuwezi kuwa na sababu ya mauaji hayo".

    Sasa Israel inasema itakataa kuwapa viza maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa.

    "Tunahitaji kuushtua Umoja wa Mataifa," Balozi wa Israel kwenye Umoja wa Mataifa Gilad Erdan aliviambia vyombo vya habari vya Israel.

    Alisema kiongozi wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu Martin Griffiths alitaka kuja Israel - na amekataliwa.

    "Mimi, kwa uratibu na Wizara ya Mambo ya Nje, niliwajulisha juu ya kukataa huko," alisema Erdan.

    "Hataweza kuja hapa katika kanda. Mashirika yao yanahitaji kuleta watu wapya mara kwa mara, kwa hakika katika wakati kama huu. Watakataliwa."

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  7. Katika picha: Siku ya 18 ya vita vya Israel-Gaza

    Ni siku ya 18 ya vita vya Israel na Hamas huko Gaza -Hizi hapa ni baadhi ya picha za hivi punde kutoka kwa mzozo huo.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  8. Kiongozi wa Uturuki aita Hamas 'kundi la ukombozi'

    Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Hamas ni kundi la ukombozi linaloendesha vita kulinda ardhi yake.

    Hamas - au katika hali nyingine tawi lake la kijeshi - limetajwa kuwa kundi la kigaidi na Israel, Marekani, EU na Uingereza, pamoja na mataifa mengine yenye nguvu.

    Zaidi ya watu 1,400 waliuawa katika mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba.

    Katika hotuba yake katika bunge la Uturuki, Erdogan alisema alikuwa akighairi mipango ya awali ya kuzuru Israel.

    Alisema amewahi kumsalimia kwa mkono Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, lakini ametumia vibaya nia njema ya Uturuki.

    Viongozi hao wawili walikutana mwezi uliopita katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa mjini New York - katika kile kilichoonekana wakati huo kama ishara nyingine muhimu ya kuboreka kwa uhusiano kati ya nchi zao.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  9. Mwanajeshi wa Kenya auawa katika shambulio la waasi DR Congo

      • Author, Wycliffe Muia
      • Nafasi, BBC News Nairobi

    Mwanajeshi wa Kenya aliye katika kikosi cha jeshi la Afrika Mashariki mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameuawa kufuatia shambulio la kuvizia na waasi.

    Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Patrick Muyaya aliiambia BBC kwamba mwanajeshi huyo alifariki siku ya Jumanne wakati wa mapigano kati ya wanajeshi wa eneo hilo na waasi wa M23 katika eneo la Kibumba.

    Ni kifo cha kwanza kuripotiwa miongoni mwa wanajeshi wa Kenya tangu wajiunge na kikosi hicho mwaka jana.

    Taarifa kutoka kwa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ililaani mauaji hayo, na kuwalaumu M23.

    Ilisema waasi hao walifyatua kombora katika ngome za Jeshi la Kikanda la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF).

    Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilisema shambulio hilo lililenga "kuzua mtafaruku" kati yake na EACRF.

    Waasi wa M23 hawajatoa tamko lolote kuhusiana na shutuma hizo.

    Mapigano yameanza tena hivi majuzi kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali wanaojulikana kwa jina la Wazalendo katika maeneo ya jimbo la Kivu Kaskazini.

    Kikosi cha kikanda kimekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka DR Congo kwa kushindwa kukomesha ghasia.

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema haitaidhinisha upya mamlaka ya EACRF, ambayo itakamilika mwezi Desemba.

    Kenya imechangia zaidi ya wanajeshi 1,000 katika ujumbe huo ambao pia unajumuisha wanajeshi kutoka Uganda, Sudan Kusini na Burundi.

  10. Hospitali za Gaza zasitisha baadhi ya huduma huku UN ikionya kwamba mafuta yataisha leo usiku

      • Author, Rushdi Abualouf
      • Nafasi, Reporting from Khan Younis, Gaza

    Hospitali ya Nasser huko Khan Younis ndio kituo kikuu cha matibabu kwa Wagaza kusini.

    Hospitali hiyo inasema shughuli za kuokoa maisha zitasitishwa hivi karibuni huku wakihangaika kutafuta mafuta.Damu na vifaa vya kuokoa maisha pia vinaisha.

    Tuko ukingoni mwa hali ya janga.

    Watu hawateswi tu na vifo na mashambulizi ya anga.Umoja wa Mataifa unasema takriban watu milioni moja wamekimbia makazi yao - karibu nusu ya idadi ya watu.

    Hapa, watu wanalala uani nje ya hospitali na mitaani.

    Nilitembelea shule moja ya Umoja wa Mataifa ambako watu kutoka kaskazini mwa Gaza wanajihifadhi.Wanapewa lita moja ya maji safi kwa siku na chakula kidogo sana - na kuna ufikiaji mdogo sana wa bafuni.

    Shule hiyo ilikuwa na wanafunzi 500, sasa inaishi watu 5,000.Nafasi na vifaa havitoshi kuwahudumia watu hawa.

    Niliona nyumba ya vyumba viwili jana ambapo watu 120 walikuwa wamejihifadhi.Mtu anayeishi huko aliniambia hakuna oksijeni ya kupumua.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  11. Je, Israel inasitasita kuivamia Gaza?

      • Author, Jeremy Bowen
      • Nafasi, Mhariri wa masuala ya Kimataifa

    Ni wazi kabisa kuna kusitasita - kwanza kabisa kwa sababu ya onyo ambayo Marekani imetoa kuhusu ugumu wa kazi iliyopo mbele ya kuingia Gaza.

    Mfano wa mapiganao makali sana ya mijini ambayo wamekuwa wakiashiria ni operesheni ya kutokomeza ISIS kutoka mji wa Mosul wa Iraq mnamo 2017.

    Nilikuwa pale nikaona kikosi kikubwa cha makomando wa Iraq, wengi wao wakiwa wamefunzwa vyema sana na Wamarekani, wakisaidiwa na jeshi la anga la Marekani, RAF na wengine, wakiwemo vikosi maalum vya magharibi.Operesheni yao ilibidi ifanye kazi nyumba hadi nyumba.

    Ilichukua miezi - na maelfu ya raia waliuawa wakati wa juhudi hizo.

    Hiyo siyo sababu pekee ya kusitasita - uwepo wa mateka huko Gaza ni suala la kweli kwa Israeli sasa.Katika kuwaachilia baadhi ya mateka, Hamas wanacheza michezo ya kisaikolojia yenye ujanja sana kwa sababu wanamaanisha kunaweza kuwa na njia ya kuwatoa baadhi ya watu hawa wakiwa hai .

    Kwa mfano, gazeti moja maarufu la Israel la Haaretz - pamoja na kwamba huwa linaikosoa serikali ya Israel - lilisema jana katika tahariri yake kuu kwamba kusiwe na hatua za kijeshi wakati kuna mateka huko Gaza.

    Lakini nilizungumza na waziri mkuu wa zamani na mkuu wa zamani wa jeshi la Israeli, Ehud Barak.Alisema tazama, uchaguo gumu linaweza kufanywa - hatuwezi kuwaacha Hamas kukosa adhabu kwa kufanya hili.Kimsingi alikuwa akisema Waisraeli wanaweza kusonga mbele na hatua ya kijeshi.

    Waziri mkuu wa sasa wa Israel Bejnamin Netanyahu - licha ya mazungumzo yake magumu - anajulikana kwa kusitasita, juu ya aina hizi za maamuzi magumu.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  12. Daktari wa Nigeria Olufemi Olaleye ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa ubakaji huko Lagos

    Mahakama nchini Nigeria imemhukumu mkurugenzi wa matibabu kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mpwa wa mke wake.

    Dkt Olufemi Olaleye alimdhulumu msichana huyo kingono kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi mkewe alipojua na kuwaarifu polisi, mwendesha mashtaka alisema.

    Daktari huyo alikana mashtaka wakati wa kesi hiyo.

    Lakini hakimu katika mahakama ya Lagos alisema alipata ushahidi dhidi ya daktari kuwa na hatia na akakataa ombi lake la kuhurumiwa.

    Olaleye alifikishwa mahakamani Novemba mwaka jana akikabiliwa na mashtaka mawili ya ubakaji kati ya Desemba 2019 na Julai 2022, msichana huyo alipoenda kuishi na familia yao.

    Wakati wa kesi hiyo, mke wa daktari huyo, Aderemi Olaleye, alisema aligundua unyanyasaji huo baada ya msichana huyo kumwambia shangazi yake na dereva wa familia hiyo.Msichana huyo, ambaye sasa ana umri wa miaka 18, alisema daktari huyo amekuwa akilala naye na alitishia kumuua iwapo atamwambia mtu yeyote, mke wa daktari huyo alisema.

    Pia alishtakiwa kwa kumlazimisha kutazama ponografia.

    Mashahidi sita - msichana, mke wa mshtakiwa, daktari, mtaalamu wa malezi ya watoto na maafisa wawili wa polisi waliohusika katika uchunguzi - walitoa ushahidi katika kesi hiyo.

    Daktari huyo pia alitoa ushahidi katika utetezi wake pamoja na daktari wake wa uchunguzi ambaye alikosea ushahidi wa matibabu uliotolewa na upande wa mashtaka.

    Lakini wakati akitoa hukumu siku ya Jumanne, Hakimu Rahman Oshodi alisema ushahidi uliowasilishwa mbele ya mahakama "unamhusisha sana" mshtakiwa.

    Jaji Oshodi alielezea mkurugenzi wa matibabu wa Optimal Cancer Care Foundation kama mkosaji "hatari" ambaye hakuonyesha dalili yoyote ya kujuta.

    Kulingana na hakimu, maungamo ya awali ya Olaleye kwa polisi yalithibitisha kwamba alitenda makosa hayo.

    Hakimu alikataa hoja za jopo la wanasheria wa daktari huyo kuwa msichana huyo alifunzwa na mke wa mshtakiwa kusema uwongo dhidi yake ikiwa ni mpango wa kuchukua mali yake.

    "Kwa hivyo, nampata mshtakiwa na hatia kama alivyoshtakiwa," hakimu aliamua.

    “Shitaka hili lina adhabu ya lazima ya kifungo cha maisha jela,” alisema.

    Katika ombi lake la kuhurumiwa, wakili wa daktari huyo, Adebisi Oridate, aliomba serikali kutambua huduma za Olaleye kama daktari wa saratani na kwamba alikuwa mkosaji wa mara ya kwanza.

    Lakini hakimu alitupilia mbali ombi hilo na kusema kwamba Olaleye lazima azuiliwe katika gereza hilo kwa muda mrefu kama dhibitisho kwamba mfumo wa haki wa Nigeria ulipuuza unyanyasaji wa kingono.

    Pia aliamuru jina la daktari kuongezwa kwenye sajili ya wahalifu wa ngono ya Jimbo la Lagos.

    Haijabainika iwapo daktari atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

  13. Kinyang'anyiro cha urais nchini Liberia chaingia duru ya pili

    Duru ya pili ya uchaguzi itafanyika mwezi ujao nchini Liberia kufuatia kumalizika kwa awamu ya kwanza ya uchaguzi ambapo Rais George Weah na mpinzani wake mkuu Joseph Boakai wote hawakupata wingi wa kura kuweza kushinda uchaguzi huo.

    Bw Weah alipata 43.83% ya kura huku Bw Boakai, aliyekuwa makamu wa rais akipata 43.44%.

    Uchaguzi wa Oktoba 10 ulikuwa wa mchuano mkali zaidi wa urais nchini Liberia tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kumalizika takriban miongo miwili iliyopita.

    Duru ya pili ilitabiriwa, lakini Bw Boakai, 78, amefanya vyema kuliko ilivyotarajiwa kwa kukaribia hesabu ya Bw Weah.

    Ilibidi duru ya pili ya uchaguzi kufanyika kwani hakuna mgombeaji aliyepata zaidi ya 50% ya kura katika duru ya kwanza. Duru ya pili ya uchaguzi itafanyika tarehe 14 Novemba, mkuu wa tume ya uchaguzi Davidetta Browne alisema baada ya kutangaza matokeo ya mwisho.

    Bw Boakai alimfuata Bw Weah katika duru ya kwanza ya upigaji kura katika uchaguzi wa 2017, na akapoteza ushindi katika kura ya mchujo kwa kura nyingi.

    Unaweza pia kusoma:

    • George Weah anahitaji muda zaidi licha ya matatizo ya Liberia
  14. Katika picha: Baada ya mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza

    Picha hizi zimewasili hivi punde, zikionyesha uharibifu katika Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, baada ya usiku mwingine wa mashambulizi ya anga ya Israel.

    Israel inasema mashambulizi yake yalilenga miundo mbinu ya Hamas, ikijumuisha vichuguu na maeneo ya silaha.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  15. Habari za hivi punde, Serikali inayoongozwa na Hamas imesema watu 80 waliuawa Gaza usiku kucha

    Serikali inayoongozwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza inasema takriban watu 80 waliuawa na mashambulio ya Israel la usiku kucha.

    Taarifa kutoka ofisi ya vyombo vya habari vya serikali ilisema "zaidi ya watu 80" wameuawa na "mamia kujeruhiwa" baada ya uvamizi wa Israel, kulingana na shirika la habari la AFP.

    Israel imekuwa ikiwalenga Hamas huko Gaza tangu watu wenye silaha walipoanzisha mashambulizi yao dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba, na kuua zaidi ya watu 1,400.

    Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas inasema zaidi ya watu 5,800 wameuawa huko Gaza tangu wakati huo.

  16. Habari za hivi punde, Syria inasema wanajeshi wanane wameuawa katika mashambulizi ya Israel

    Wanajeshi wanane wa Syria wameuawa na saba kujeruhiwa na mashambulizi ya Israel kwenye maeneo ya kijeshi katika mkoa wa kusini wa Daraa, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

    Shirika la habari la Syria SANA linasema shambulio hilo lilitokea mwendo wa saa saba na dakika 40 saa za huko siku ya Jumatano.

    Jeshi la Israel limethibitisha kuwa lilishambulia maeneo ya Syria - likisema ndege zake za kivita zilifanya shambulio kwenye miundombinu ya kijeshi na virusha kombora baada ya kurushwa kwa roketi nchini humo kutoka Syria.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  17. Kwanini Benki kubwa zinawekeza katika bidhaa zinazohusiana na kakakuona na chui

    Mashirika makubwa ya benki duniani yanawekeza katika makampuni ambayo yanazalisha dawa za jadi za Kichina zenye viungo vya chui na pangolin, ripoti imebaini.

    Aina zote mbili za spishi hawa zimewekwa katika orodha ya spishi zilizomo katika hatari ya kutoweka

    Mamlaka ya uchunguzi wa mazingira (EIA) ilibaini kuwa benki 62 na taasisi za fedha ambazo zinawekeza kwenye vikundi vitatu vya dawa vinavyotengeneza bidhaa tisa ambazo wamesema zina viungo vya chui au kakakuona.

    BBC imewasiliana na kampuni zinazohusika ili kutoa maoni.

    Kampuni hizo ni pamoja na makampuni makubwa ya huduma za kifedha za Uingereza kama vile HSBC, Prudential, na Legal & General, pamoja na makampuni ya uwekezaji ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Goldman Sachs, UBS, Deutsche Bank na BlackRock.

    Chui na kakakuona wanaweza kuwa hatarini katika siku zijazo.

    Wanyama hao pia wameorodheshwa kwenye mkataba wa CITES (Mkataba wa Biashara ya Kimataifa ya Wanyama na Mimea Walio Hatarini Kutoweka) ambao unakataza biashara ya kimataifa zinazohusiana na wanyama hao, kwa nia ya kuhakikisha uhai wao katika pori hautishiwi.

    Kampuni tatu za dawa, zilizoangaziwa katika ripoti ya EIA ni kikundi cha Tong Ren Tang, kikundi cha Dawa cha Tianjin na Kikundi cha Dawa cha Jilin Aodong.

    Sio kampuni zote zilizoorodheshwa katika ripoti ya EIA huwekeza katika kampuni zote tatu, lakini zote zinawekeza katika angalau moja.

    Katika dawa za jadi za Kichina (TCM) mfupa wa chui hutumiwa kama mbadala wa mfupa wa simbamarara. Mfupa wa simbamarara unaaminika kuimarisha mifupa na mishipa ya binadamu, na kuzuia maumivu.

    Magamba ya Pangolin yanasemekanakusaidia mzunguko wa damu, kunyonyesha na kusaidia kupunguza maumivu ya mishipa. Madai haya hayaungwi mkono na ukweli wa kisayansi.

  18. Canada, Marekani zakataa wito wa kusitishwa kwa mapigano

    Awali Malkia wa Jordan Rania ambaye alihoji ni kwanini jumuiya ya kimataifa haitoi wito wa kusitishwa kwa mapigano baina ya Israel na Hamas.

    Hii inakuja wakati nchi kama Marekani, Australia na Canada ambazo zimetoa wito wa "kusitishwa kwa misaada ya kibinadamu", zimeacha kutetea hadharani kusitishwa kwa mapigano.

    "Sitarajii kwamba shirika la kigaidi lingeheshimu sheria za kimataifa au wito wowote wa kusitisha mapigano," Waziri wa Ulinzi wa Canada Bill Blair aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumanne.

    "Kusema ukweli kabisa, Hamas inapaswa kuondolewa kama tishio, sio tu kwa Israeli, bali kwa ulimwengu."

    Mapema maafisa wakuu wa Ikulu ya Marekani na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pia walisema sasa si wakati muafaka wa kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Hamas.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  19. Tazama Video: Ajali moja ya barabarani Marekani yahusisha magari 158

    Watu 25 walijeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Interstate 55 katika Parokia ya St John the Baptist, walisema polisi, ambao walionya kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

    Ukungu mzito na moshi kutoka kwa moto ilichanganyika na kupunguza mwonekano wa magari yanayosafiri siku ya Jumatatu.

    Tazama video hii kutoka eneo la tukio, ikionyesha msururu wa magari 158 yaliyohusika katika ajali hiyo.

  20. Israel inataka Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ajiuzulu

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Israel ameiambia BBC News kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres lazima ajiuzulu kwa matamshi "ya kuudhi" aliyotoa katika hotuba mapema Jumanne.

    Katika hotuba yake akidai ukiukwaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu, Gutteres alisema: "Ni muhimu pia kutambua mashambulizi ya Hamas hayakutokea bila sababu. Watu wa Palestina wamekuwa wakikaliwa kwa mabavu si chini ya miaka 56."

    "Lakini malalamiko ya watu wa Palestina hayawezi kuhalalisha mashambulizi ya kutisha ya Hamas. Na mashambulizi hayo ya kutisha hayawezi kuhalalisha adhabu ya pamoja ya watu wa Palestina,” alisema.

    Akizungumza na kipindi cha BBC Radio 4 - The World Tonight, msemaji wa Israel Lior Haiat alisema hotuba ya mkuu wa Umoja wa Mataifa ilikuwa na "dakika moja tu ya maneno matupu kuhusu ukatili wa magaidi wa Hamas" na "kuhalalisha ugaidi".

    "Badala ya kusimama na waathiriwa, analaumu waathiriwa kwa ukatili ambao hatujaona tangu yafanyike mauaji ya Holocaust," aliendelea.

    "Badala ya kuunga mkono na ujumbe unaosema 'Never again' anawaambia magaidi 'Unaruhusiwa kufanya hivyo, tunakubali ugaidi wako wa kikatili kwa sababu Israel ndio wa kulaumiwa'".