Waziri Mkuu wa Uingereza asema mlipuko wa hospitali huenda ulisababishwa na kombora lililorushwa kutoka Gaza

'Serikali ya Uingereza inaamua kwamba mlipuko huo [katika hospitali ya al-Ahli] ulisababishwa na kombora au sehemu ya moja ambayo ilirushwa kutoka Gaza. kuelekea Israeli".

Moja kwa moja

Yusuf Jumah and Ambia Hirsi

  1. Waasi wauteka tena mji wa DR Congo katika mapigano mapya

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Mapigano yamezuka tena mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya vikosi vinavyounga mkono serikali na waasi wa kundi la M23.

    Wakaazi wanasema waasi hao wameuteka mji wa Kitshanga katika jimbo la Kivu Kaskazini tangu Jumamosi.

    Watu kadhaa wamepelekwa hospitalini wakiwa na majeraha ya risasi, kituo cha redio cha eneo hilo kiliripoti.

    "Waasi wako Kitshanga na tunajaribu kutafuta njia ya kuuteka tena mji," chanzo cha usalama kiliambia shirika la habari la AFP.

    Udhibiti wa eneo hilo umebadilika mara kadhaa tangu mwanzo wa mwaka.

    Mapigano yalianza tena wiki tatu zilizopita baada ya makubaliano ya miezi sita. Awali eneo hilo lilikuwa likisimamiwa na kikosi cha kimataifa kilichotolewa na majirani wa Kongo.

  2. Waandamanaji wanaounga mkono Palestina wazuiliwa kwa muda nchini Kenya

    .

    Chanzo cha picha, Kenya for Palestines/X

    Polisi wa Kenya wamewaachilia watu watatu waliokamatwa kwa kushiriki katika mkutano wa kuiunga mkono Palestina katika mji mkuu, Nairobi.

    Watatu hao waliachiliwa Jumapili bila kufunguliwa mashtaka baada ya ukosoaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya Wakenya, wanasiasa na mashirika ya kutetea haki za binadamu.Walisema walikuwa wakifanya "mkutano wa mshikamano".

    Mbunge wa Kenya Yusuf Hassan alishtumu kukamatwa kwa watu hao.

    Mkuu wa Amnesty International nchini Kenya, Irũngũ Houghton, alisema kuwa kuvurugwa kwa mkutano huo ni "kinyume cha sheria" na "kusumbua sana".

    Ilikuwa imeandaliwa na Kamati ya Mshikamano wa Palestina ya Kenya baada ya polisi kusitisha maandamano ya awali ambayo kundi hilo lilikuwa limepanga nje ya ubalozi wa Marekani.

    Rais William Ruto ameeleza kuunga mkono kikamilifu serikali yake kwa Israel katika mzozo unaoendelea.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  3. Habari za hivi punde, Mwanajeshi wa Israel auawa huko Gaza akiwatafuta mateka – IDF

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mwanajeshi wa Israel ameuawa wakati wa uvamizi wa ndani huko Gaza, Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) limesema.

    Wanajeshi wengine watatu wa IDF walijeruhiwa - mmoja kwa wastani na wawili kidogo - katika shambulio hilo, alisema msemaji Daniel Hagari kwenye mtandao wa kijamii.

    Hagari alisema wanajeshi walikuwa wakitafuta Waisraeli waliopotea na kusafisha eneo hilo wakati shambulio lilipotokea.

    "Kombora lilirushwa kwenye kifaru wakati wa uvamizi wa ndani uliofanywa mapema leo katika Ukanda wa Gaza, katika eneo la Kissuf," aliandika.

    Haijulikani ni wapi hasa aliuawa. Eneo la Kissuf liko kwenye mpaka wa Gaza, na gazeti la Times of Israel linasema ilitokea upande wa magharibi wa uzio wa mpaka, ndani ya Gaza.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  4. Katika picha: Majengo ya makazi yameporomoka na kusababisha majeruhi katika mashambulizi ya Israel Gaza

    Israel ilifanya kile wanahabari walichokitaja kuwa mashambulizi makali zaidi ya anga katika Ukanda wa Gaza, ambayo yaliendelea hadi Jumapili usiku.

    Picha zilizochapishwa na mashirika ya habari zinaonyesha majengo yaliyoporomoka na watu waliojeruhiwa.

    Tahadhari : Baadhi ya wasomaji wanaweza kuona picha hizi ni za kuogofya

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wafanyakazi wa dharura na raia wakichimba vifusi vya jengo katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza
    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mtoto aliyejeruhiwa alisafirishwa katika mji wa Deir al-Balah, katikati ya Ukanda huo, ambao umekuwa ukikabiliwa na mashambulizi ya anga ya Israel kwa muda wa wiki mbili
    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mtu aliyejeruhiwa akiinuliwa kwenye karatasi Deir al-Balah
    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wapalestina wakisafirisha miili ya watu 5 wa familia moja waliouawa katika uvamizi wa Israel, mbele ya chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Al-Aqsa huko Deir al-Balah, katikati mwa Ukanda wa Gaza
    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wafanyakazi wawili wa Hilali Nyekundu wa Palestina wakiwa wamembeba mtoto aliyejeruhiwa
    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wafanyakazi wawili wa Shirika la Msalaba mwekundu wa Palestina wakiwa wamembeba mtoto aliyejeruhiwa katika mji wa Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza
    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Piicha iliyopigwa kutoka mji wa Sderot, kusini mwa Israel, ikionyesha moshi mwingi ukifuka huko

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  5. Mapigano ya Israel na Hamas: Benjamin Netanyahu hataomba msamaha" - Financial Times

    g

    Chanzo cha picha, AFP

    Magazeti ya leo ya Uingereza yaliangazia masuala kadhaa ya kimataifa, na vita vya Gaza kati ya Hamas na Israel viliongoza vichwa vya habari.

    Tunaanza na tahariri ya Financial Times, makala yenye kichwa "Benjamin Netanyahu Hatasema Samahani," iliyoandikwa na John Reid kutoka Jerusalem na Neri Zilber akiwa Tel Aviv.

    Waandishi wa makala hiyo wanasema kuwa jeshi la Israel na viongozi wa usalama walichukua sehemu yao ya lawama, kwani wanamgambo wa Hamas waliua zaidi ya watu 1,400.

    Mkuu wa ujasusi wa jeshi la Israel alisema anabeba "jukumu kamili,"

    Shin Bet alikiri kwamba shirika lake la ujasusi "lilishindwa kuonya juu ya shambulio hilo," na mkuu wa jeshi la Israeli alisema kuwa jeshi "halikufanikiwa chochote katika kuzuia mauaji’’.

    Lakini, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ameepuka kuwajibika, ukiachana na kuomba msamaha.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  6. Vita vya Israeli na Hamas: Wizara ya afya ya Gaza inasema Wapalestina 4,651 wameuawa katika vita

    g

    umla ya watu 4,651 wameuawa huko Gaza tangu mzozo huo ulipozuka tarehe 7 Oktoba, wizara ya afya ya eneo hilo imesema.

    Wizara hiyo ambayo inadhibitiwa na Hamas ilisema katika taarifa yake kwamba waliouawa ni pamoja na watoto 1,873, wanawake 1,101, na wanaume 1,677.

    Imeongeza kuwa, kati ya jumla ya vifo, 839 wameuawa kusini mwa Gaza, ambapo watu wa kaskazini wameambiwa kukimbilia.

    Wizara pia ilisema kuwa watu 14,245 wamejeruhiwa.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  7. Viongozi wa Magharibi waeleza kuunga mkono 'haki ya kujilinda' ya Israel

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Viongozi wa Marekani, Uingereza, Kanada, Ufaransa, Ujerumani na Italia walizungumza Jumapili kuhusu mzozo wa Israel na Gaza na hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.

    Taarifa kutoka Ikulu ya White House ilisema Rais Joe Biden, Waziri Mkuu Rishi Sunak, na viongozi wengine walitumia wito "kusisitiza uungaji mkono wao kwa Israeli na haki yake ya kujilinda dhidi ya ugaidi" lakini wakataka "kuzingatiwa kwa sheria za kimataifa za kibinadamu, ikiwa ni pamoja na ulinzi wa raia".

    "Waliafiki kuachiliwa kwa mateka wawili na wakataka kuachiliwa mara moja kwa mateka wote waliosalia," taarifa hiyo iliongeza.

    "Viongozi hao wameafiki tangazo la misafara ya kwanza ya kibinadamu kuwafikia Wapalestina wanaohitaji msaada mjini Gaza na wamejitolea kuendelea kuratibu na washirika katika eneo hilo ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa salama wa chakula, maji, huduma za matibabu na misaada mingine inayohitajika kukidhi mahitaji ya kibinadamu.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  8. Iran yaionya Israel kusitisha vita Gaza la sivyo eneo hilo 'halitadhibitika’’

    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian ameionya Israel kwamba eneo la Mashariki ya Kati linaweza kudorora ikiwa haitasitisha mashambulizi dhidi ya Gaza.

    Alisema Marekani pia ndiyo "ya kulaumiwa" kwa kutoa msaada wa kijeshi kwa Israel.

    Saa chache baadaye, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwatahadharisha wanajeshi wake kuwa katika vita vya kuokoa maisha yao na kusema vita dhidi ya Hamas ni "fanya au ufe".

    Iran inaunga mkono Hamas, ambayo ilishambulia Israel wiki mbili zilizopita na kuua watu 1,400, na Hezbollah ya Lebanon.

    Zaidi ya Wapalestina 4,600 wameuawa katika muda wa wiki mbili zilizopita huko Gaza, kwa mujibu wa wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas, na Israel ilitangaza siku ya Jumamosi kuwa inazidisha mashambulizi ya anga.

    "Ninaionya Marekani na wakala wake Israel kwamba ikiwa hawatakomesha mara moja uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya halaiki huko Gaza, lolote linawezekana wakati wowote na eneo hilo halitaweza kudhibitika tena," Bw Amir-Abdollahian alisema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran.

    Alisema kuwa matokeo yanaweza kuwa "makali, machungu" na "kuwa na athari kubwa", kikanda na kwa wale wanaotetea vita.

    Waziri huyo wa mambo ya nje aliongeza kuwa uungaji mkono wa kijeshi wa Marekani kwa Israel ni ushahidi kwamba mzozo unaoendelea Gaza ni "vita vya uwakilishi vinavyofanywa na Israel kwa niaba ya Marekani".

    Maafisa wakuu wa Marekani pia wanaonya kwamba mzozo huo unaweza kuenea.

  9. Israel inasema mashambulizi ya Gaza yanaweza kuchukua miezi kadhaa lakini mwisho hakutakuwa na Hamas tena

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant anasema mashambulizi ya jeshi lake Gaza "yanaweza kuchukua mwezi mmoja, miwili au mitatu, lakini mwishoni hakutakuwa na Hamas tena".

    Gallant alikuwa akizungumza baada ya taarifa ya utendaji kazi katika Kituo cha Amri na Udhibiti wa Operesheni za Jeshi la Anga la Israeli.

    "Kwa upande wa vita mwisho wa siku, hakuna kitakachozuia IDF (Vikosi vya Ulinzi vya Israeli)", alisema.

    "Hii inapaswa kuwa operesheni yetu ya mwisho ya ya Gaza, kwa sababu rahisi kwamba baadaye hakutakuwa na Hamas tena."

    Waziri huyo alitoa shukrani zake kwa Jeshi la Anga na kusema hatua inayofuata, ni omashambulizi ya ardhini inayotarajiwa na wengi, "itakuja hivi karibuni".

    Muda gani bado haijulikani. Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wanatarajiwa kufanya ziara nchini Israeli siku zijazo.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  10. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni Jumatatu 23.10.2023