Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel yakanusha mapatano ya kusitisha vita kusini mwa Gaza
Israel inaonekana kukanusha ripoti za kusitisha mapigano kusini mwa Gaza, nusu saa baada ya vyanzo vya usalama nchini Misri kuliambia shirika la habari la Reuters kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano yalikuwa yamekubaliwa kuwiana na kufunguliwa tena kwa kivuko cha Rafah.
Taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu inasema: "Kwa sasa hakuna suluhu na misaada ya kibinadamu huko Gaza kwa kuwaruhusu wageni kutoka nje."
Israel yatangaza kuwahamisha jamii karibu na mpaka wa Lebanon
Jeshi la Israel limetangaza mpango wa kuzihamisha jamii za kaskazini mwa Israel karibu na mpaka na Lebanon.
Wakazi wa jamii 28 ambazo ziko ndani ya kilomita 2 (maili 1.24) kutoka mpakani watahamishwa hadi "nyumba za wageni zinazofadhiliwa na serikali", Jeshi la Ulinzi la Israeli lilisema.
Raia mmoja wa Israel aliuawa katika shambulizi la kombora la Hezbollah kwenye kijiji kimoja karibu na mpaka siku ya Jumapili, kulingana na jeshi la Israel.
Israel imefanya mashambulizi ya usiku kucha dhidi ya Lebanon, ikilenga miundombinu ya kijeshi ya kundi la wanamgambo wa Lebanon Hezbollah.Hakuna majeruhi wameripotiwa.
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza
Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina