Habari za hivi punde, Israel inataka watu milioni 1.1 kaskazini mwa Gaza kuondoka katika saa 24 zijazo - UN
Jeshi la Israel limeuambia Umoja wa Mataifa kwamba kila mtu anayeishi kaskazini mwa Wadi Gaza anapaswa kuhamia kusini mwa Gaza katika muda wa saa 24 zijazo, anasema msemaji wa Umoja wa Mataifa.
Umoja wa Mataifa unasema kiasi hiki kinafikia takriban watu milioni 1.1 - karibu nusu ya wakazi wa Ukanda wote wa Gaza.Eneo lililoathiriwa ni pamoja na Mji wa Gaza wenye wakazi wengi.
Tahadhari hiyo ilitolewa kabla tu ya usiku wa manane, saa za Gaza na Jerusalemu (23:00 GMT).
"Umoja wa Mataifa unaona kuwa haiwezekani kwa harakati kama hiyo kufanyika bila matokeo mabaya ya kibinadamu," Umoja wa Mataifa ulisema katika taarifa yake.
Israel imekuwa ikijiandaa kwa mashambulizi ya ardhini, kukusanya wanajeshi, mizinga mikubwa na vifaru kwenye mpaka wa Gaza.
Imekuwa ikiafanya mashambulizi ya anga mjini Gaza tangu Jumamosi baada ya wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel kwa kushtukiza.
Unaweza pia kusoma:
- Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
- Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
- Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
- Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas

