Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Raia wakimbilia kusini mwa Gaza baada ya onyo la Israel

Mamia ya familia zinasafiri kwenye barabara kuu kutoka kaskazini kuelekea kusini mwa Gaza baada ya Israel kuwataka raia kuondoka kwa usalama wao.

Moja kwa moja

  1. Habari za hivi punde, Israel inataka watu milioni 1.1 kaskazini mwa Gaza kuondoka katika saa 24 zijazo - UN

    Jeshi la Israel limeuambia Umoja wa Mataifa kwamba kila mtu anayeishi kaskazini mwa Wadi Gaza anapaswa kuhamia kusini mwa Gaza katika muda wa saa 24 zijazo, anasema msemaji wa Umoja wa Mataifa.

    Umoja wa Mataifa unasema kiasi hiki kinafikia takriban watu milioni 1.1 - karibu nusu ya wakazi wa Ukanda wote wa Gaza.Eneo lililoathiriwa ni pamoja na Mji wa Gaza wenye wakazi wengi.

    Tahadhari hiyo ilitolewa kabla tu ya usiku wa manane, saa za Gaza na Jerusalemu (23:00 GMT).

    "Umoja wa Mataifa unaona kuwa haiwezekani kwa harakati kama hiyo kufanyika bila matokeo mabaya ya kibinadamu," Umoja wa Mataifa ulisema katika taarifa yake.

    Israel imekuwa ikijiandaa kwa mashambulizi ya ardhini, kukusanya wanajeshi, mizinga mikubwa na vifaru kwenye mpaka wa Gaza.

    Imekuwa ikiafanya mashambulizi ya anga mjini Gaza tangu Jumamosi baada ya wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel kwa kushtukiza.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  2. Mzozo wa Israel na Palestina: Mabomu 6,000 yaangushwa Gaza

    Israel inasema kuwa imedondosha mabomu 6,000, yenye uzito wa tani 4,000, katika maeneo ya Hamas huko Gaza katika kipindi cha siku sita.

    Jeshi la anga la Israel limesema mashambulizi ya anga yameshambulia zaidi ya maeneo 3,600.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  3. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 13.10.2023