Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Hamas wanataka kuiangamiza Israel - Blinken

"Yeyote anayetaka amani na haki lazima alaani utawala wa kigaidi wa Hamas," Blinken alisema.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Kenya kusitisha mkataba na madaktari wa Cuba

    Kenya itasitisha mkataba wa miaka sit ana Cuba ulioruhusu zaidi ya madaktari 100 wa Cuba kufanya kazi katika hospitali za Kenya.

    Waziri wa Afya Susan Nakhumicha amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kukabiliana na changamoto zinazowakabili wahudumu wa afya wa Kenya, ikiwemo ukosefu wa nafasi za ajira.

    "Tumeamua kutofanya upya makubaliano na madaktari wa Cuba. Wataalamu wetu wa afya wamejitolea kwa sababu hiyo, "alisema.

    Mkataba wa 2017 ulianzisha mpango wa kubadilishana ambapo madaktari wa Cuba wangesaidia kujaza pengo katika hospitali za kaunti huku Wakenya wakisafiri hadi Cuba kwa mafunzo maalum ya matibabu.

    Haukupendwa na wataalamu wa matibabu wa Kenya, ambao walilalamika kuwa madaktari wa ndani wana mafunzo yanayohitajika kama vile wenzao wa Cuba walivyofanya.

    Pia kulikuwa na wasiwasi kwamba serikali ya Kenya ilikuwa ikiwalipa wataalamu wa Cuba zaidi ya wenzao wa Kenya - hata kama baadhi ya madaktari waliofunzwa nchini wamesalia bila ajira.

    Madaktari na wahudumu wengine wa afya nchini Kenya mara nyingi wakuwa wakifanya mgomo wakidai nyongeza ya mishahara, mazingira bora ya kazi na madaktari zaidi kuajiriwa.

  2. Mzozo wa Israel na Palestina: Tofauti kati ya chama cha Fatah cha rais wa Palestina na Hamas

    Kama tulivyoripoti hivi punde, waziri wa mambo ya nje wa Marekani anatarajiwa kukutana na Mahmoud Abbas, rais wa Palestina.

    Chama cha Bw Abbas cha Fatah kinatawala Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel, na ni tofauti na wanamgambo wa Kiislamu wa Hamas, ambao wanadhibiti Ukanda wa Gaza.

    Hamas iliiondoa kwa nguvu Fatah katika uongozi wa Ukanda wa Gaza mwaka 2007.

    Hamas ambacho ni chama cha kisiasa cha Kiislamu kilichoanzishwa mwaka 1987, kimetoa wito kwa muda mrefu kuangamizwa kwa Israel.

    Vyama vyote viwili vya kisiasa ni vyombo tofauti, na mazungumzo ya umoja kati ya hizo mbili yamevunjika mara kwa mara.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  3. Mashambulizi ya anga yanalenga mtandao wa njia za Hamas mjini Gaza: Vikosi vya Ulinzi vya Israel

    Jeshi la Israel linasema mashambulio yake ya hivi karibuni ya anga katika ukanda wa Gaza yanalenga kuharibu mtandao wa vichuguu ambao kwa miongo kadhaa umetumika kama kituo cha operesheni cha Hamas.

    "Fikiria ukanda wa Gaza kama safu moja ya raia na safu moja ya Hamas," Jonathan Conricus, msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel alisema katika ujumbe wa video uliotumwa kwenye X (zamani ikiitwaTwitter).

    Njia hizo za chini kwa chini zilizojengwa kwa miaka mingi tangu Hamas kuchukua mamlaka mjini Gaza mwaka 2007, zimetumika kama njia ya Hamas kuhamisha vifaa na pia kupanga na kuanzisha mashambulizi dhidi ya Israel, aliongeza.

    Ukubwa na umuhimu wa njia hizi umefichwa na jamii zenye watu wengi zilizo juu, ambazo nyingi sasa zimekuwa magofu, alisema.

    "Kuna mengi zaidi ya inavyoonekana. Jeshi la anga la Israel limekuwa likishambulia vitongoji vingi vya Gaza. Kipaumbele chetu kwa sasa ni kuwalenga makamanda wanaofanya mashambulizi, na viongozi wakuu wa Hamas katika ngazi zote," alisema.

    "Vyovyote itakavyokuwa, ikiwa ni ya Hamas, tunaigonga."

  4. Habari za hivi punde, Blinken kukutana na rais wa Palestina siku ya Ijumaa: maafisa

    Rais wa Palestina Mahmoud Abbas atakutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken siku ya Ijumaa, kwa mujibu wa Hussein Al-Sheikh, katibu mkuu wa kamati kuu ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina.

    Bw Blinken anatarajiwa kuwasili Israel saa chache zijazo katika juhudi za kuonyesha kuunga mkono nchi hiyo na watu wake baada ya mashambulizi ya Hamas.

    Afisa huyo wa Palestina pia alisema katika chapisho

    kwenye X, zamani ikiitwa Twitter, kwamba Rais Abbas atakutana na Mfalme Abdullah wa Jordan mjini Amman siku ya Alhamisi.

  5. Mzozo wa Israel na Palestina: Roketi, moshi mweusi- Mashambulizi yasiyokoma ya Ashkeloni

      • Author, Lyse Doucet
      • Nafasi, Akiripoti kutoka karibu na Ashkeloni, kusini mwa Israeli

    Katika ukingo wa eneo lililofungwa la kijeshi la Israeli kwenye mpaka wake wa kusini hali ni ya wasiwasi, na tete.

    Leo, katika asubuhi ya tano ya vita, anga ya Gaza, umbali wa maili tatu na nusu, giza na moshi vilitanda kutoka kwenye ukanda huu wa pwani, kutokana na mashambulizi ya mabomu yasiyokoma.

    Unaweza kusikia sauti kubwa ya mizinga ya Israeli na sauti ya ndege zisizo na rubani.

    Kufikia alasiri, Hamas ilikuwa ikirudisha makombora, ikilenga maeneo ikiwa ni pamoja na Ashkelon, mji wa kusini kabisa.

    Roketi zilisambaa katika anga ya Israeli, zikiwa zimeshikiliwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Iron Dome wa Israel.

    Jeshi la Israeli liliwafokea waandishi wa habari waliokusanyika kwenye makutano kwamba ilikuwa hatari sana kwa wao kukaa hapo.

    Kisha amri nyingine ikafuata - chini chini!

    Kila mtu aliambiwa alale chini, ajifiche, huku makombora zaidi ya Hamas yakifyatuliwa angani katika eneo hilo.

    Unaweza kunusa harufu ya moshi kama mashamba yalipochomwa karibu, katikati ya wimbi hili kubwa la mashambulizi

  6. Habari za hivi punde, Idadi ya vifo Gaza yaongezeka hadi 1,200 - wizara ya afya ya Palestina

    Wizara ya afya ya Palestina inasema watu 1,200 wamefariki tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi ya anga katika eneo hilo, kulipiza kisasi shambulio baya lililofanywa na wanamgambo wa Hamas siku ya Jumamosi.

    Idadi ya vifo vya pande zote sasa inafikia karibu watu 2,500.

    Hapo awali, Jeshi la Ulinzi la Israeli lilisema kuwa Waisraeli 1,200 waliuawa na wapiganaji wa Hamas mwishoni mwa juma huku idadi ya vifo ikitarajiwa kuongezeka.

  7. Habari za hivi punde, Takriban watu 51 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Gaza: Wizara ya afya ya Palestina

    Takriban watu 51 wamekufa baada ya msururu wa mashambulizi ya anga ya Israel mjini Gaza katika saa moja iliyopita, wizara ya afya ya Palestina ilisema.

    Wengine 281 pia walijeruhiwa baada ya shambulio hilo kupiga vitongoji vya Sabra, Al Zaytoun, Al Nafaq na Tal Al Hawa.

  8. Kila mwanachama wa Hamas ni mfu, Netanyahu anasema

    Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kila mwanachama wa Hamas ni "maiti" baada ya mkutano wa kwanza wa serikali ya dharura ya nchi yake.

    Akiwa pamoja na Netanyahu, kiongozi wa upinzani Benny Gantz alisema pia kwamba Israeli ipo katika "wakati wa vita".

    Lakini Rais wa Marekani Joe Biden alisema alikuwa amezungumza na Bw Netanyahu na kuweka wazi kwamba Israel lazima "ifanye kazi kwa kuzingatia sheria za vita".

    Idadi ya vifo nchini Israel imefikia 1,200. Zaidi ya watu 1,100 wameuawa kwa mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza.

    Bw Biden alisema anaelewa hasira na kufadhaika kwa watu wa Israel lakini akahimiza Israel kuzingatia kanuni za mikataba ya Geneva.

    Pia aliionya Iran - ambayo imeafiki shambulio la Hamas - "kuwa makini".

    Mapema Jumatano Bw Netanyahu na Bw Gantz walikubaliana kuweka kando uhasama wao mkali wa kisiasa ambao ulikuwa umeongezeka na kusababisha maandamano makubwa.

    Bw Gantz aliwaambia raia wa Israel kwamba serikali mpya iliyoundwa "imeungana" na iko tayari "kufuta kitu hiki kinachoitwa Hamas kutoka kwenye uso wa dunia".

    Pamoja na Bw Netanyahu na Bw Gantz, kiongozi wa chama cha National Unity Party na waziri wa zamani wa ulinzi, baraza jipya la mawaziri la muda pia litajumuisha Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant.

    Kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, Yair Lapid, hajajiunga na muungano huo. Hata hivyo, Bw Netanyahu na Bw Gantz walisema katika taarifa ya pamoja kwamba k atatengewe kiti katika baraza la mawaziri la vita.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  9. Misri iliionya Israel siku chache kabla ya mashambulizi ya Hamas, mwenyekiti wa kamati ya bunge la Marekani asema

    Israel ilionywa na Misri kuhusu uwezekano wa kutokea vurugu siku tatu kabla ya shambulio baya la Hamas kuvuka mpaka, mwenyekiti wa jopo la bunge la Marekani amesema.

    Mkuu wa Kamati ya Masuala ya Kigeni ya Baraza la Wawakilishi Michael McCaul aliwaambia waandishi wa habari kuhusu madai ya onyo hilo.

    Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alizitaja ripoti hizo kuwa za "uongo kabisa".

    Idara za Ujasusi za Israel zinachunguzwa kwa kushindwa kwao kuzuia shambulio baya zaidi la wanamgambo wa Kipalestina katika historia ya miaka 75 ya Israel.

    "Tunajua kwamba Misri imewaonya Waisraeli siku tatu kabla kwamba tukio kama hili linaweza kutokea," Bw McCaul aliwaambia waandishi wa habari kufuatia taarifa ya kijasusi ililiyotolewa faraghani siku ya Jumatano kwa wabunge kuhusu mgogoro wa Mashariki ya Kati, kulingana na shirika la habari la AFP.

    "Sitaki kuingia sana katika uainishaji, lakini onyo lilitolewa," Mbunge huyo wa Republican wa Texas aliongeza. "Nadhani swali lilikuwani kwa kiwango gani."

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  10. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 12.10.2023