Mshauri mkuu wa Benjamin Netanyahu ameiambia BBC Newsnight kwamba Israel
lazima "ijibu kwa nguvu" Hamas.
Akizungumza kutoka Jerusalem, Mark Regev, ambaye pia aliwahi kuwa Balozi wa
Israel nchini Uingereza, alisema nchi hiyo imeshtuka na wanataka ukweli thabiti
zaidi katika eneo hilo.
“Hamas walianzisha vita hivi. Tutaimaliza na tutaimaliza kwa masharti
yetu,” alimwambia Mhariri wa masuala ya Kidiplomasia wa BBC, Mark Urban.
"Ningeuliza watu wengine, raia wa Uingereza, wa nchi nyingine yoyote,
ungefanya nini ikiwa watu wako 1,000 waliuawa kwa siku moja?" alisema.
"Waziri Mkuu amelinganisha hili na mashambulio ya Septemba 11 nchini
Marekani. Lakini ukiangalia ukubwa wa idadi ya Waisraeli na kulinganisha na
Wamarekani ... lilikuwa shambulizi baya zaidi kuliko Septemba 11."
"Ikiwa Israeli haitajibu kwa nguvu, ninahofu kwamba litakuwa funzo katika eneo hili kwamba - unaweza kuipiga Israeli bila kuadhibiwa -
hiyo haikubaliki."
-
Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
-
Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
-
Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
-
Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
-
Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas