Hamas yarusha makombora katika mji wa Ashkelon kusini mwa Israel
Wanamgambo hao walianzisha mashambulizi yao ya hivi punde huku idadi ya vifo vya Israel ikifikia 1,000 na mashambulizi yake ya kulipiza kisasi dhidi ya Gaza yakiendelea.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi and Yusuf Jumah
Habari za hivi punde, Mzozo wa Israel na Hamas: Kivuko cha Misri chafungwa, yasema Israel
Jeshi la Israel limebadilisha ushauri wake kwa Wapalestina wanaotaka kuondoka Gaza.
Hapo awali ilisema watu wanapaswa kuondoka kwa kutumia kivuko kimoja kinachodhibitiwa na Misri.
Sasa inasema kwamba kuvuka kumefungwa.
Habari za hivi punde, Miili ya wanamgambo 1,500 wa Hamas yapatikana, IDF yasema
Jeshi la Israel linasema miili 1,500 ya wanamgambo wa Hamas imepatikana nchini Israel na karibu na Ukanda wa Gaza.
Msemaji wa kimataifa wa jeshi la Israel Kanali Richard Hecht aliongeza kuwa uhamishaji wa jumuiya zote za Israel karibu na Ukanda wa Gaza ulikuwa karibu kukamilika.
Raia wa Liberia wanapiga kura kumchagua rais na wabunge
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Liberia ina wapiga kura milioni 2.4 waliojiandikisha
Wagombea 19 wanatumai kuchukua nafasi ya
aliyemaliza muda wake, nyota wa zamani wa soka George Weah, ambaye anawania
muhula wa pili.
Wapinzani wakuu wawili ni makamu wa rais wa zamani
Joseph Boakai na mfanyabiashara Alexander Cummings.
Wote walikuwa katika muungano wa vyama vya upinzani
lakini muungano huo ulivunjika baada ya kutofautiana kuhusu nani anayefaa
kugombea urais.
Licha ya maendeleo kadhaa katika suala la elimu na
usambazaji wa umeme, wakosoaji wanasema kumekuwa na ufisadi mkubwa wakati wa Bw
Weah mamlakani.
Anaahidi kujenga barabara mpya, suala muhimu linalokuja
wakati unaofaa wakati wa uchaguzi katika msimu wa mvua wakati sehemu kubwa ya
barabara za kuelekea mji mkuu Monrovia zikiwa hazipitiki.
Bw,Weah aliingia mamlakani mwaka wa 2017 alipoungwa
mkono na watu wengi baada ya majaribio mawili ya hapo ya awali yakuwania kiti cha urais bila mafanikio.
Unaweza pia kusoma:
George Weah anahitaji muda zaidi licha ya matatizo ya Liberia
Algeria yasitisha upatanishi kuhusu mzozo wa mapinduzi ya Niger
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, jeshi la Niger lilichukua mamlaka kwa mapinduzi mwezi Julai
Algeria imetangaza
kusitisha juhudi zake za kupatanisha mgogoro wa kisiasa nchini Niger kufuatia
mapinduzi ya mwezi Julai.
Wizara yake ya
mambo ya nje ilisema katika taarifa yake Jumatatu kwamba matamko kutoka kwa
mamlaka ya Niger yameibua "maswali halali kuhusu nia yao ya kweli ya
kufuata kukubali kwao upatanishi wa Algeria".
Sasa imesimamisha
mchakato huo ikisubiri kujitolea kutoka kwa junta kuendelea na upatanishi.
Mwezi uliopita,
Niger ilikubali pendekezo la Algeria la kuwa mpatanishi katika mgogoro wake wa
kisiasa unaolenga kuirejesha nchi hiyo katika utawala wa kikatiba.
Mwezi Agosti,
Algeria ilipendekeza kipindi cha mpito cha miezi sita kikiongozwa na mamlaka ya
kiraia.
Lakini mkuu wa
junta, Jenerali Abdourahamane Tchiani, ambaye alichukua mamlaka mwezi Julai,
alitaka kipindi cha mpito cha miaka mitatu.
Algeria pia
ilipinga suluhu la kijeshi kwa mzozo wa Niger kufuatia vitisho vya Ecowas
kuhusu uwezekano wa kuingilia kijeshi kurejesha demokrasia.
Rais wa Nigeria
Bola Tinubu, ambaye pia ni mwenyekiti wa shirikisho hilo la kikanda alikafiki
mchakato wa upatanishi, lakini uamuzi huu wa Algeria utavuruga zaidi juhudi za
kutatua mzozo wa kisiasa nchini Niger.
Tazama: Magari yaliyoharibiwa barabani karibu na eneo la tamasha la Israeli katika video ya kutisha
Maelezo ya video, Magari yaliyoharibiwa yaliwa kwenye mstari kando ya barabara katika video ya kuogofya
Siku ya Jumamosi wanamgambo wa Kipalestina
walivamia tamasha la muziki la Supernova nchini Israel na kufyatua risasi kama
sehemu ya shambulio kubwa la kushtukiza dhidi ya Israel.
Picha za video
zilizorekodiwa kutoka eneo hilo siku iliyofuata zinaonyesha ukubwa wa shambulio
hilo, huku mabaki ya gari yakizunguka barabara, baadhi yakipinduka na mengine kuungua kabisa...Soma zaidi kuhusu shambulio la tamasha la muziki Israel
Habari za hivi punde, Hakuna mpango wa kutuma wanajeshi wa Marekani nchini Israel - White House
Katika dakika chache zilizopita, tumesikia kutoka kwa msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la White House, John Kirby.
Kirby anasema serikali ya Marekani haina nia ya kupeleka wanajeshi Israel, lakini italinda maslahi ya Marekani katika eneo hilo.
Anasema maombi zaidi ya usalama yanatarajiwa kutoka Israel, ambayo Marekani itajaribu kutimiza haraka iwezekanavyo.
Kirby pia anasema "hakuna swali kwamba kuna kiwango fulani cha ushirikiano" na Iran katika kuunga mkono Hamas, Marekani haijaona ushahidi kwamba Iran ilihusika moja kwa moja.
Ripoti katika gazeti la Wall Street Journal inadai kuwa Iran ilishiriki katika kusaidia Hamas kujiandaa kwa shambulio hilo la kushtukiza.
Kuwaokoa mateka ni changamoto - naibu wa zamani wa ujasusi wa Israeli
BBC imezungumza na Doron Kempel, naibu mkuu wa zamani wa Sayeret
Matkal - kitengo cha makomando wasomi wa Israeli.
Bw Kempel, amesema: "Changamoto
ni jinsi ya kujua vya kutosha kuhusu mateka walipo na jinsi ya kuratibu
shambulio hilo ili kwamba wakati mmoja unaweza kuingia popote wanapozuiliwa na
kuokoa wengi wao iwezekanavyo," ameiambia BBC.
Ameongeza kusema kuwa kuwa kinachochanganya hali hiyo ni mateka hawako
ndani ya maeneo ya udhibiti wa Israel.
Rais wa Palestina atarajiwa kuzuru Moscow – ripoti
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais wa Palestina aliyezeeka hapo awali alilaumiwa na vikundi vya Kiyahudi kwa kukana mauaji ya Holocaust.
Shirika la Habari la Reuters linaripoti kuwa juhudi
zinaendelea kwa Rais wa Palestina Mahmoud Abbas kuzuru Moscow, likinukuu chombo
cha habari cha RBC cha Urusi.
Uongozi wa Palestina umegawanyika kati ya Mamlaka ya Palestina ya Bw Abbas
(PA), ambayo inadhibiti sehemu za Ukingo wa Magharibi, na kundi la wanamgambo,
Hamas, ambalo linatawala Gaza.
"Makubaliano yamefikiwa kwamba Bw Abbas atakuja hapa Moscow,"
Abdel Hafiz, mjumbe wa Palestina mjini Moscow anaripotiwa kusema.
"Tunasubiri taarifa rasmi kutoka Kremlin... kuhusu ni lini ziara hiyo
itafanyika," anaongeza.
Unaweza pia kusoma:
Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
Mzozo wa Israel na Hamas: Meli za kivita za Marekani zinaonyesha nguvu
Maelezo kuhusu taarifa
Author, Barbara Plett Usher
Nafasi, Mwandishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, BBC News
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Meli ya kubeba ndege cha USS Gerald R. Ford kinaelekea karibu na eneo Israeli (picha ya faili)
Marekani imeanza kutuma silaha na zana za
kijeshi kwa Israel na inahamisha meli za kivita za jeshi la wanamaji na ndege
za kivita katika eneo hilo ili kuonyesha uungaji mkono.
Meli hizo tayari zilikuwa
katika Bahari ya Mediterania, kwa hiyo hazikuwa na safari ndefu ya Kwenda Israel. Na sio kawaida kwa Amerika kupeleka meli za wanamaji katika eneo hilo
wakati kuna milipuko.
Haijafanya hivyo wakati wa vita vya awali kati ya Hamas na Israel, ambayo
yamekuwa ya kujitegemea. Lakini hii sio kuhusu Hamas. Pentagon
ina wasiwasi kwamba mzozo unaweza kuenea.
Afisa mkuu wa ulinzi alisema meli hizo za kivita na ndege zimekusudiwa
kuonyesha dhamira thabiti kwa ulinzi wa Israel, na kuizuia nchi yoyote au kundi
la wanamgambo kujiunga na vita.
Kauli hiyo inailenga hasa Iran, ambayo inaunga mkono vuguvugu lenye nguvu
la Hizbollah la Lebanon, pamoja na Hamas.
Marekani itakuwa sehemu ya jibu la muda mrefu na lla kuiadhibu la Israel,
ingawa msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa John Kirby alisema hakuna nia ya
kuweka jeshi la Marekani nkatika ardhi ya Israel.
Unaweza pia kusoma:
Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
Hamas yatishia kuwaua mateka iwapo Israel itawashambulia raia
Chanzo cha picha, Getty Images
Msemaji wa wapiganaji wa Hamas amesema wataanza kuwaua mateka
wanaowashikilia katika Ukanda wa Gaza iwapo Israel itaendelea kulipua makazi ya
raia.
Waziri wa mambo ya nje wa Israel amethibitisha zaidi ya watu mia moja
walichukuliwa mateka.
Kundi hilo la wapiganaji wa Kiislamu
ya lilitishia kumuua mateka wa Israel kila mara
Israel inaposhambulia kwa mabomu nyumba ya Wapalestina bila ya onyo, huku
Israel ikiwaita askari wa akiba 300,000 ambao hawakuwahi kushuhudiwa na kuweka
vizuizi katika Ukanda wa Gaza, na kuzusha hofu ilipanga shambulio la ardhini.
Ghasia hizo, ambazo zimegharimu maisha ya zaidi ya watu 1,500, zimesababisha
miito ya kimataifa ya kuiunga mkono Israel baada ya shambulio baya la mwishoni
mwa juma lililofanywa na Hamas, na kuomba kukomeshwa kwa mapigano na ulinzi wa
raia.
Taarifa kadhaa za televisheni za Israel zilisema idadi ya vifo kutokana na
shambulio la Hamas imepanda hadi Waisraeli 900, huku takriban 2,600
wakijeruhiwa, na makumi kadhaa wakichukuliwa mateka.
Miongoni mwa waliouawa Israel ni 260 wengi wao wakiwa vijana waliopigwa
risasi kwenye tamasha la muziki wa jangwani, ambapo baadhi ya mateka walitekwa
nyara.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliapa kulipiza kisasi katika
hotuba yake kali akiwashutumu Hamas kwa kuwanyonga watoto waliokuwa wamefungwa
na ukatili mwingine. "Adui huyu mbaya alitaka
vita na atapata vita," alisema.
Unaweza pia kusoma:
Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara ya leo tarehe 10.10.2023