Ulipizaji kisasi dhidi ya Hamas ndio umeanza, asema Netanyahu wa Israel

Waziri wa ulinzi wa Israel aagiza "kuzingiwra kamili" kwa Ukanda wa Gaza: "Hakuna umeme, hakuna chakula, hakuna mafuta"

Moja kwa moja

Ambia Hirsi and Yusuf Jumah

  1. Mzozo wa Israeli na Hamas: Picha za hivi punde kutoka Gaza na Israel

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Moshi unaongezeka kati ya majengo huko Gaza baada ya makombora ya Israeli
    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wapalestina wakiangalia magari yaliyoteketea baada ya shambulio hilo
    h

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Huko Ashkeloni, kusini mwa Israeli, mwanamume mmoja anatazama nje ya dirisha lake kuona uharibifu kutoka kwa roketi za Gaza
    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mwanajeshi wa Israel ameketi kwenye sanduku la risasi karibu na Ukanda wa Gaza
  2. Tazama video: Raia wa Gaza watoroka mashambulio ya Israel

    Maelezo ya video, Raia wa Gaza watoroka mahambulkio ya Israel

    Picha za video zinaonyesha jengo likishambuliwa na watu wakikimbia kujificha wakati wa shambulio la kombora la Israeli katika kitongoji cha makazi kaskazini magharibi mwa Gaza.

    Mashambulizi ya anga ya Israel yamesababisha vifo vya takriban watu 313 katika Ukanda wa Gaza, na karibu 2,000 kujeruhiwa, maafisa wa Palestina wanasema.

  3. Tazama Video: Wapiganaji wa Hamas waoneshwa kukiteka kifaru cha Israel

    Maelezo ya video, Video ' inaonyesha kifaru cha Israel kilichotekwa na Hamas

    Video imeibuka inayodaiwa kuwaonyesha Wapalestina wakiruka kwenye kifaru cha Israel kilichotekwa na wanamgambo wa Hamas.

    Picha hizo, zilizopatikana na shirika la habari la Reuters, pia zinaonyesha wanamgambo wakiingia Gaza kwa kile kinachosemekana kuwa gari la kijeshi la Israel lililotekwa.

    Msemaji wa jeshi la Israel alikataa kutoa maoni yake kuhusu Waisraeli kukamatwa na Hamas, kulingana na Reuters. BBC haijathibitisha video hiyo.

  4. Mzozo wa Israel na Hamas: Makumi ya raia wa Mauritius walikwama huko Bethlehemu huku kukiwa na vita

    h

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mashirika mengi ya ndege yalisitisha safari za ndege kutokana na mashambulizi ya Hamas nchini Israel

    Makumi ya mahujaji wa Mauritius wamekwama mjini Bethlehem kufuatia mzozo wa unaoendelea kati ya kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas na Israel, wizara ya mambo ya nje ilisema.

    Kikundi kinajumuisha washiriki 36, haswa kutoka parokia ya Kikatoliki ya St-Hélène katika jiji la pili kwa ukubwa la Curepipe.

    Padre Gérard Mongelard, ambaye anaongozana nao, alisema waumini hao wanaendelea vizuri na kwa sasa wanaishi katika hoteli moja mjini Bethlehem.

    Walitakiwa kupanda ndege Jumapili jioni kuelekea Uturuki, ambapo wangerudi nyumbani.

    Hata hivyo, mashirika mengi ya ndege yalisitisha safari za ndege kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya Hamas dhidi ya Israel.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  5. Tazama:Vita vikali vya bunduki kwenye barabara kuu ya Israeli

    Maelezo ya video, Makabiliano makali ya silaha kwenye barabara kuu ya Israeli

    Wenye magari walijificha wakati mapigano ya bunduki yakizuka kwenye barabara kuu ya Route 4, kati ya Ashdodi na mpaka wa Gaza.

    Mapigano kati ya wanajeshi wa Israel na wanamgambo wa Kipalestina yanaendelea katika ardhi ya Israel karibu na Gaza kufuatia shambulio kubwa la Hamas siku ya Jumamosi.

  6. Tazama: kiwango cha uharibifu baada ya mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza

    Maelezo ya video, Picha zaonyesha kiwango cha uharibifu baada ya mashambulizi ya anga ya Israeli katika Gaza

    Picha zinaonyesha matokeo ya mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza, ambapo msikiti uliharibiwa kabisa.

    Israel ilianzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya Hamas baada ya kundi hilo la wanamgambo kuanzisha mfululizo wa mashambulizi siku ya Jumamosi, ikiwa ni ongezeko kubwa zaidi katika eneo hilo katika miongo kadhaa.

    Kwa mujibu wa maafisa wa Palestina, mashambulizi ya anga ya Israel yameua takriban watu 313 katika Ukanda wa Gaza, na karibu 2,000 kujeruhiwa.

    Huko Israel, zaidi ya watu 600 wameuawa, na makumi ya Waisraeli wamechukuliwa mateka.

  7. Jeshi bado linapambana na wanamgambo wa Hamas ndani ya Israel: IDF

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wapalestina wakiwa wamesimama karibu na magofu ya jengo la Benki ya Kitaifa ya Kiislamu

    Vikosi vya Israel bado vinapambana na wapiganaji wa kundi la Hamas katika maeneo saba hadi nane kusini mwa Israel karibu na Ukanda wa Gaza, Jeshi la Ulinzi la Israel limesema katika kikao fupi leo asubuhi.

    Maeneo haya ni pamoja na Be'eri, katika jamii ya wakulima, ambayo yalipenywa na wapiganaji wa Hamas mara moja. Wengi wa wanamgambo hao wameuawa, lakini wengine bado wamejificha katika nyumba za kibbutz, IDF ilisema.

    Jeshi la Israel limeongeza kuwa limeshambulia zaidi ya maeneo 1,000 huko Gaza.

    "Upeo wa operesheni hii ni kitu tofauti kabisa... Inachukua muda zaidi kuliko tulivyotarajia kurudisha mambo katika hali ya ulinzi na usalama," Luteni Kanali Richard Hecht aliambia mkutano na waandishi wa habari.

  8. Habari za hivi punde, Idadi ya watu waliofariki katika tamasha la muziki la Israeli sasa ni 260 - wakala wa uokoaji

    Idadi ya waliofariki katika tamasha la muziki la Supernova imeongezeka hadi 260, vyombo vya habari vya Israel viliripoti, vikinukuu shirika la uokoaji la eneo hilo Zaka.

    Takriban watu 3,000 waliohudhuria tamasha la usiku kucha walilengwa na Hamas kama sehemu ya shambulio kubwa la kushtukiza dhidi ya Israel.

    Tamasha hilo lilifanyika katika jangwa la Negev, karibu na Kibbutz Re'im - sio mbali na Ukanda wa Gaza.

  9. Wengi hawajulikanai walipo baada ya maporomoko ya ardhi kuukumba mji mkuu wa Cameroon

      • Author, Paul Njie
      • Nafasi, BBC News, Yaoundé
    h

    Watu wengi wanahofiwa kupotea katika mji mkuu wa Cameroon Yaoundé, baada ya maporomoko ya ardhi kuharibu nyumba kadhaa katika mtaa unaoitwa Mbankolo.

    Hii ni baada ya mvua kubwa kunyesha katika jiji hilo Jumapili jioni.

    Bado haijulikani ni watu wangapi wamekufa au hawajulikani waliko hadi sasa, lakini msako unaendelea ili kuwaokoa waathiriwa na kupata wengine ambao hawajulikani walipo.

    Mnamo Novemba mwaka jana, maporomoko ya ardhi katika mji mkuu yaliwaua takriban watu 14 waliokuwa wakihudhuria mazishi.

  10. 'Kama sinema ya kutisha' - Washiriki wa tamasha la muziki la Israel walivyokimbia kwa sababu ya risasi

      • Author, Francesca Gillett
      • Nafasi, BBC News
    Maelezo ya video, Washiriki wa tamasha wakikimbia huku milio ya risasi ikisikka Israeli

    Kwa wiki kadhaa, wapenzi wa muziki waliochangamka walikuwa wakitazamia kwa hamu tamasha la Supernova, lililofanyika jangwani kusini mwa Israeli ili sanjari na sherehe ya Kiyahudi ya Sukkot.

    "Wakati umefika ambapo familia nzima inakaribia kukusanyika tena," waandalizi waliandika kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kuanza. "Na ni furaha gani itakuwa!"

    lakini saa chache baadaye, kurasa zao za mitandao ya kijamii sasa zimefurika watu waliokata tamaa wakijaribu kutafuta wapendwa wao, baada ya wanamgambo wa Kipalestina kuvamia tamasha hilo na kufyatua risasi ikiwa ni sehemu ya shambulio la kushtukiza dhidi ya Israel.

    Zaidi ya miili 250 imeripotiwa kupatikana katika eneo la tamasha, kulingana na shirika la uokoaji Zaka.

    Mshiriki mmoja wa sherehe, anayeitwa Ortel, alisema ishara ya kwanza kwamba kuna kitu kibaya ni wakati king'ora kilipolia alfajiri, kuonya kuhusu roketi.

    Walioshuhudia walisema kuwa roketi hizo zilifuatwa haraka na milio ya risasi.

    "Walizima umeme na ghafla wakatoka [wanamgambo] ndani wakiwa na milio ya risasi, wakifyatua risasi kila upande,"aliiambia televisheni ya Israel - Channel 12

    Magaidi 50 walifika wakiwa kwenye magari ya mizigo, wakiwa wamevalia sare za kijeshi," alisema.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  11. Habari za hivi punde, Iran yakanusha kuhusika moja kwa moja na shambulio la Hamas Israel

    Iran "haikuhusika" katika shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa Hamas kusini mwa Israel, ujumbe wake katika Umoja wa Mataifa umesema.

    "Tunasimama kwa nguvu katika kuunga mkono Palestina; hata hivyo, hatuhusiki katika shambulio la Palestina, kwani linatekelezwa na Palestina yenyewe," ilisema katika taarifa ya Jumapili, kulingana na Reuters.

    Hamas hapo awali ilisema kwamba msaada kutoka kwa Iran uliisaidia kutekeleza shambulio la alfajiri mwishoni mwa juma.

    Iran imekuwa ikiunga mkono Hamas kwa miaka mingi na kuwapa wapiganaji wake silaha na mafunzo - na kundi hilo la wanamgambo limesema kuwa msaada uliisaidia kutekeleza mashambulizi yake yaliyoratibiwa.

    Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken aliiambia CNN Jumapili kwamba serikali ya Marekani "bado haijaona ushahidi kwamba Iran ilielekeza au ilikuwa nyuma ya shambulio hili".

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  12. Marekani yasogeza meli za kivita karibu na Israel baada ya shambulio la Hamas

    g

    Chanzo cha picha, PA Media

    Maelezo ya picha, Meli ya kubeba ndege ya USS Gerald R. Ford inaelekea eneo hilo

    Marekani inasema inahamisha shehena ya ndege, meli na jeti hadi mashariki mwa Mediterania na pia itaipa Israel vifaa na risasi zaidi.

    Hii inafuatia shambulio la Hamas kusini mwa Israel, ambalo Rais Biden aliliita "shambulio lisilokuwa na kifani na la kutisha".

    Marekani pia ilikuwa ikifanya kazi ya kuthibitisha ripoti kwamba raia wake walikuwa miongoni mwa waliouawa na kuchukuliwa mateka, Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken amesema.

    Israel inasema zaidi ya watu 700 wameuawa na 100 kutekwa nyara.

    Mjini Gaza, zaidi ya watu 400 wameuawa kufuatia mashambulizi ya anga ya kulipiza kisasi ya Israel, kulingana na maafisa wa Palestina.

    Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alisema meli ya kubeba ndege ya USS Gerald R. Ford, meli ya kubebea makombora na zana za kuharibu makombora vimepelekwa katika eneo hilo. Ndege za kivita za Marekani pia zinapelekwa Gaza.

    Misaada zaidi ya kijeshi kwa Israel itatumwa katika siku zijazo, Ikulu ya White House ilisema.

    Rais wa Iran Ebrahim Raisi ameeleza kuunga mkono shambulio la Hamas akisema Israel inapaswa kuwajibika kwa kuhatarisha eneo hilo.

    Mzozo wa Israeli na Hamas: Mengi zaidi:

    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:
    • Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
  13. Zaidi ya Wapalestina 123,000 wamekimbia makazi yao Gaza - UN

    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Mvulana mdogo anatembea kando ya barabara iliyojaa uchafu huko Gaza

    Zaidi ya Wapalestina 123,000 wameyakimbia makazi yao huko Gaza kuanzia saa tatu usiku kwa saa za eneo (18:00 GMT), huku karibu 74,000 wakitafuta hifadhi mashuleni, Umoja wa mataifa unasema katika taarifa yake Jumapili usiku.

    Israel imejibu mashambulizi ya kushtukiza ya Hamas kwa mfululizo wa mashambulizi ya anga katika eneo la Gaza.

    Ukanda wa Gaza unakaliwa naw atu takriban milioni 2.3 na ni moja ya maeneo yenye msongamano mkubwa zaidi wa watu ulimwenguni.

    Maafisa wa afya wa Palestina wanasema kuwa zaidi ya watu 400 wameuawa, huku zaidi ya 2,000 wakijeruhiwa.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  14. Habari za hivi punde, Ikulu ya White House yathibitisha kuwa raia wa Marekani wameuawa

    Ikulu ya White House inasema Wamarekani "kadhaa" wameuawa nchini Israel, ingawa hakuna idadi maalum iliyotolewa.

    Msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa anasema serikali ya Marekani inafuatilia kwa karibu hali hiyo na inaendelea kuwasiliana na mamlaka za mitaa nchini Israel.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  15. Idadi ya waliouawa kufuatia shambulio la Hamas Israel na Gaza yafikia 1,100

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kombora likilipuka katika Jiji la Gaza Jumapili jioni

    Asante kwa kujiunga na matangazo yetu ya moja kwa moja

    Muda mfupi uliopita, tulipokea uthibitisho kutoka kwa jeshi la Israel kwamba zaidi ya watu 700 huko wameuawa katika mashambulizi baada ya shambulio kubwa lililoratibiwa na wanamgambo wa Hamas lililoanza mapema Jumamosi.

    • Taarifa za hivi punde kutoka kwa upande wa Wapalestina zinasema zaidi ya watu 400 wamekufa baada ya mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyofanywa na Israel huko Gaza. Hapa kuna vichwa vya habari zaidi:
    • ·Waokoaji wanasema wamepata miili zaidi ya 250 kwenye tovuti ya tamasha la muziki la Supernova - ambayo ilikuwa moja ya shabaha za kwanza wakati wa shambulio hilo ambalo halijawahi kushuhudiwa na Hamas.
    • Mama wa Ujerumani anaomba taarifa kuhusu binti yake, akiamini kuwa alitekwa nyara na wanamgambo katika tshambuli hilo.
    • Mataifa mengine kadhaa yanasema raia wao walinaswa na mashambulizi hayo
    • Hospitali za Gaza zimefurika majeruhi baada ya Israel kuanza mashambulizi yake ya kulipiza kisasi

    Mzozo wa Israeli na Hamas: Mengi zaidi:

    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:
    • Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
  16. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara ya leo Jumatatu tarehe 09.10.2023