Ulipizaji kisasi dhidi ya Hamas ndio umeanza, asema Netanyahu wa Israel
Waziri wa ulinzi wa Israel aagiza "kuzingiwra kamili" kwa Ukanda wa Gaza: "Hakuna umeme, hakuna chakula, hakuna mafuta"
Moja kwa moja
Ambia Hirsi and Yusuf Jumah
Wapalestina wafanya mazishi ya waliofariki Gaza
Mazishi pia yanafanyika kote Gaza. Jamaa walikusanyika kuwaaga watu wa familia moja waliofariki katika mashambulizi ya Israel.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Waombolezaji wakibeba mwili wa Mpalestina katika mitaa ya Rafa, kusini mwa Gaza 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Jamaa wakusanyika kwa mazishi ya familia ya Shamalkh 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Wanawake wakiangalia miili iliyofunikwa kwa shuka nyeupe 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Wanawake wenye huzuni wakifarijiana Familia ya Israel yamzika mwanajeshi aliyeuawa katika mashambulizi
Israel inazika wafu wake kufuatia mashambulizi ya Haamas siku ya Jumamosi.
Moja wapo ya mazishi yanaonyeshwa hapa. Wanajeshi wakishusha jeneza la mwanajeshi wa Israel kwenye kibbutz cha Kfar Menahem, kusini mwa Israel.
Yuval Ben Yaakov alifariki wakati wa mapigano na wanamgambo wa Hamas kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza.
Waombolezaji waliohudhuria wanaonekana kufunika nyuso zao kwa huzuni.

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock
Netanyahu: Huu ni mwanzo tu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye amekuwa akizungumza kuhusu jibu la nchi yake kwa mashambulizi mabaya zaidi katika ardhi yake katika miongo kadhaa
Aliwaambia maafisa kutoka kusini mwa Israel, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, kwamba "kile ambacho Hamas itapitia kitakuwa kigumu na cha kutisha".
Netanyahu aliendelea kusema kuwa "huu ni mwanzo tu... sote tuko pamoja nanyi na tutawashinda kwa nguvu, nguvu kubwa sana".
Zaidi ya watu 700 wameuawa nchini Israel tangu Hamas ilipoanzisha uvamizi wake nchini Israel siku ya Jumamosi.
Takriban watu 560 wameuawa huko Gaza baada ya Israel kufanya mashambulizi kujibu mashambulizi ya wanamgambo wa Kipalestina.
Pistorius ana ruhusa ya kuomba msamaha, mahakama yaamuru

Chanzo cha picha, Reuters
Mahakama ya Kikatiba ya Afrika Kusini imeamuru kuwa muuaji aliyepatikana na hatia Oscar Pistorius ametumikia zaidi ya nusu ya kifungo chake kwa mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013, ambayo ina maana kwamba kiufundi anastahili kuachiliwa huru.
Iligundua kuwa mwanariadha huyo wa zamani, anayejulikana pia kama "Blade Runner", alipita alama ya nusu mnamo Machi 21 mwaka huu.
Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka sita mwaka 2016, lakini kifungo hicho kiliongezwa hadi miaka 13 na miezi mitano mwaka 2017.
Kesi ya kuachiliwa huru ilipangwa Machi mwaka jana, lakini ilifeli baada ya idara ya huduma za urekebishaji (DCS) kusema kuwa hakuwa ametumikia nusu ya kifungo chake kama inavyotakiwa kwa msamaha.Siku ya Jumatatu, Mahakama ya Katiba ilibatilisha uamuzi huo.
Mkanganyiko huo unatokana na ukweli kwamba muda wa Pistorius gerezani umevunjwa na rufaa na kwa muda wa kifungo cha nyumbani.
Katika taarifa, DCS ilisema itachunguza uamuzi wa mahakama.
Mahakama ya Kenya yazuia kutumwa kwa maafisa wa polisi nchini Haiti
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Ian Wafula
- Nafasi, Mwandishi wa Masuala ya Usalama BBC News, Nairobi

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Polisi wa Kenya wana changamoto za kiusalama nyumbani, anasema Ekuru Aukot, ambaye aliwasilisha ombi la mahakama Mahakama kuu nchini Kenya imezuia mipango ya serikali ya kupeleka maafisa wa polisi nchini Haiti au nchi nyingine yoyote ikisubiri kusikilizwa kwa ombi.
Jaji huyo alitaja masuala yaliyoibuliwa katika maombi hayo kuwa yana umuhimu wa kitaifa na maslahi ya umma.
Mmoja wa walalamishi, aliyekuwa mgombeaji urais, Ekuru Aukot alisema pendekezo hilo ni kinyume cha katiba.
Aukot aliongeza kuwa nchi hiyo haina uwezo wa kuwaacha maafisa 1000 kwa ajili ya kutumwa Haiti kabla ya kushughulikia ukosefu wa usalama nyumbani.
Wiki iliyopita mapigano ya kikabila magharibi mwa Kenya yalisababisha vifo vya watu saba.
Na hivi majuzi eneo la pwani la Lamu limeshuhudia mashambulizi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab lenye uhusiano na Al-Qaeda lenye makao yake nchini Somalia. Eneo hilo sasa liko chini ya amri ya kutotoka nje.
Akizungumza Jumapili, Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala alisisitiza kwamba mpango huo hautahatarisha usalama na usalama wa nchi.
Mahakama itatoa maelekezo zaidi mwishoni mwa Oktoba.
Maelezo zaidi:
Maafisa wa polisi wa Kenya wanaswa wakiwasafirisha raia 13 wa kigeni
Mamlaka nchini Kenya imewakamata maafisa wawili wa polisi waliopatikana wakiwasafirisha watu 13 kutoka Ethiopia kwa kutumia gari la polisi.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, maafisa hao walikuwa wakiwasafirisha Waethiopia wanane, Waeritrea wanne na raia wa Sudan kwa gari la Kitengo cha Polisi wa Mipakani nchini Kenya.
Maafisa hao waliokuwa wamejihami na bunduki zilizotolewa na polisi, walinaswa katika kaunti ya kaskazini-magharibi ya Kenya ya Turkana, ambayo inapakana na Ethiopia.
Mamlaka zinasema kwamba wageni hao pia waliwazuiliwa, huenda wakafikishwa katika mahakama ya Kenya au kurejeshwa katika nchi zao.
Wageni hao walisema walikuwa wakipitia Kenya wakielekea Afrika Kusini.
Vikosi vya Ulinzi vya Israel vyafanya operesheni katika maeneo ya Lebanon

Chanzo cha picha, AFP
Jeshi la Israel linasema kuwa limeshambulia maeneo yaliyolengwa ndani ya Lebanon kwa kutumia helikopta.
Video moja iliyoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii inaonekana kuonyesha kituo cha waangalizi wa Hezbollah kikilipuliwa, lakini BBC haijathibitisha hili.
Hapo awali jeshi la Israel lilisema kuwa limewaua watu wawili waliokuwa na bunduki ambao walivuka kutoka Lebanon na kuingia Israel.
Takriban wanaume sita wanaaminika kuhusika, wawili waliuawa, watatu walijeruhiwa na mmoja alitoroka kuvuka mpaka hadi Lebanon, ingawa kumekuwa hakuna uthibitisho rasmi wa idadi yao.
Kombora pia zilirushwa ndani ya Israeli, ambayo baadaye ilishambulia maeneo ya ambayo yalitumia kurusha makombora hayo Lebanon.
Kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran lilisema halikuhusika katika shambulio la leo - makundi ya wapiganaji wa Palestina pia yameanzisha mashambulizi dhidi ya Israel kutoka eneo la mpakani ambalo limekumbwa hali tete siku za nyuma.
Mzozo wa Israel na Palestina: Mateka watatunzwa, afisa wa Hamas adai

Chanzo cha picha, TWITTER
Mkuu wa uhusiano wa kimataifa wa Hamas Basem Naim amesema kundi hilo "limejitolea na kuwahudumia mateka wetu kwa njia ya kibinadamu na ya heshima".
Akizungumza na kipindi cha The World at One cha BBC Radio 4 hapo awali, alikataa kuthibitisha idadi ya mateka waliochukuliwa au idadi ya raia waliouawa na wanamgambo wa Kipalestina.
Zaidi ya watu 700 wameuawa nchini Israel tangu Jumamosi.
Makumi ya watu pia walitekwa nyara, huku wengi wao waksadikiwa kupelekwa Gaza.
Zaidi ya watu 500 wameuawa huko Gaza tangu Israel ilipoanza kushambulia eneo hilo.
Naim pia alidai kiongozi wa Hamas Mohammad Deif aliwaagiza wanamgambo "kuheshimu wazee, kuheshimu raia, kuheshimu watoto" na "kutomuua mtu yeyote ambaye hahusiki moja kwa moja katika vita".
Lakini wanamgambo walituhumiwa kuua idadi kubwa ya raia wa Israel, ikiwa ni pamoja na mauaji ya karibu watu 300 kwenye tamasha la muziki karibu na mpaka wa Gaza, wengi wao wakiwa vijana.
Maelezo zaidi:
Ya hivi punde katika mzozo wa Israel-Hamas
Iwapo umejiunga nasi basi haya ndio yote ya hivi punde katika mzozo wa Israel na Hamas huko Gaza
Israel inaendelea na mapambano ili kulinda eneo lake
- Zaidi ya siku mbili baada ya shambulio hilo ambalo halijawahi kushuhudiwa, Israel ilisema mpaka wake na Gazabado haujawa salama kabisa
- Lakini ilisema vikosi vyake vilikuwa vinadhibiti kikamilifu jamii zilizoshambuliwa na Hamas, ambao wapiganaji wao waliwapiga risasi raia walipoona.
- Jeshi limekiri baadhi yawanamgambo wa Kipalestina huenda bado wako huru au hata wanaendelea kuingia nchini humo.
Idadi ya vifo kuongezeka kwa pande zote mbili
- Takriban Waisrael 700 na Wapalestina 500 wameuawa hadi sasa katika ghasia hizo
- Raia tisa wa Marekani wamethibitishwa kuuawa nchini Israel, huku zaidi yaraia 10 wa Uingereza wakihofiwa kufariki au kutoweka
- Makumi ya watu wanashikiliwa mateka na Hamas, wengi wao wakiwa Gaza
- Msemaji wa Hamas alisema mateka wanne wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel- hii haiwezi kuthibitishwa.
Kuzingirwa kwa Gaza kumeamrishwa
- Jeshi la Israel lilizidisha mashambulizi ya anga huko Gaza wakati wa chakula cha mchana, baada ya kusema zaidi ya malengo 500 ya Hamas yamepigwa usiku kucha.
- Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant ameamuru kuzuiwa kabisa, ikiwa ni pamoja na kuzuia chakula, maji na umeme kuingia.
- Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya Wagaza 120,000 wamekimbia makazi yao, huku wengi wakitafuta makazi salama shuleni.
Habari za hivi punde, Raia tisa wa Marekani wathibitishwa kufariki nchini Israel huku Uingereza ikisema inahofia raia wake 10 wameaga dunia
Serikali ya Marekani imethibitisha kuwa raia wake tisa wameuawa nchini Israel.
Katika taarifa, Ikulu ya White House ilisema: "Tunatuma rambirambi zetu kwa wahasiriwa na familia za wote walioathiriwa, na tunawatakia majeruhi ahueni ya haraka.
"Tunaendelea kufuatilia hali kwa karibu na kuendelea kuwasiliana na washirika wetu wa Israel, hasa mamlaka za mitaa."
Huku hayo yakijiri taarifa zinazotufikia kutoka kwa chanzo rasmi cha Uingereza ni kwamba "zaidi ya raia 10" wa Uingereza wanahofiwa kufariki au kutoweka nchini Israel kufuatia mashambulizi yaliyoanzishwa na wanamgambo wa Hamas kutoka Gaza.
Tetemeko la ardhi Afghanistan: Zaidi ya 1,000 wamekufa huku wanakijiji wakiwatafuta manusura

Chanzo cha picha, Getty Images
Waokoaji wanawafukua manusura wa tetemeko kubwa la ardhi lililopiga vijiji kadhaa nchini Afghanistan na kuua zaidi ya watu 1,000.
Tetemeko hilo la ukubwa wa 6.3 katika vipimo cha Richter lilitokea Jumamosi asubuhi katika mkoa wa Herat, eneo ambalo ni kame lililo na nyumba za matofali ya udongo.
Wanakijiji bado wanatumia majembe na mikono kutafuta waliopotea - zaidi ya 500, kulingana na UN.
Misaada, iliyocheleweshwa na njia zilizofungwa kutokana na kukatizwa kwa njia za mawasiliano, zilianza kuingia Jumatatu.
Tetemeko hilo lilikumba Zinda Jan, wilaya ya mashambani iliyo umbali wa kilomita 40 kutoka mji wa Herat, ambapo "asilimia 100 ya nyumba zinakadiriwa kuharibiwa kabisa," kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA).
Majaji wa Uingereza waanza kusikiliza kesi ya kuwapeleka wahamiaji Rwanda

Chanzo cha picha, PA Media
Mahakama ya Juu ya Uingereza imeanza kusikiliza kwa siku tatu kesi ya mpango wa serikali wa kuwatuma baadhi ya waomba hifadhi wanaovuka mpaka wa kuingia Uingereza hadi nchini Rwanda.
Kesi hiyo imewasilishwa baada ya Mahakama ya Rufaa kuamua kwa wingi kuwa mpango huo ulikiuka sheria.
Serikali inatarajiwa kusema kuwa sheria ya haki za binadamu iko upande wake, kwa sababu ya uhakikisho uliotolewa na Rwanda kwamba ni nchi salama.
Inapingwa na wahamiaji 10 waliopangwakusafirishwa kupitia mpango huo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi.
Israel kukata usambazaji wa maji hadi Gaza,huku idadi ya waliouawa katika ukingo huo ikipita 500

Chanzo cha picha, Reuters
Huduma za kusambaza maji kutoka Israel hadi Gaza zinakatizwa kulingana na Waziri wa Nishati wa Israel, Israel Katz.
Kambi za wakimbizi zashambuliwa Gaza - wizara ya mambo ya nje ya Palestina
Kambi mbili za wakimbizi zimekumbwa na mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina.
Inasema kambi zote za Al-Shati (pia inajulikana kama kambi ya Pwani) na kambi za Jabalia zilishambuliwa, na kuripotiwa kuwaacha majeruhi na wengine kadhaa kufariki.
Kuna kambi nane za wakimbizi zinazotambulika katika Ukanda wa Gaza wenye wakazi wengi.
Idadi ya waliouawa huko Gaza yapita 500
Wizara ya afya ya Gaza imesema watu 511 wameuawa, na 2,750 wamejeruhiwa, kutokana na mashambulizi ya makombora ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza tangu Jumamosi.
Israel inasema inalenga maeneo ya Hamas huko Gaza kufuatia shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa Jumamosi dhidi ya raia wa Israel na waasi wa Kipalestina walioingia kutoka katika eneo hilo na kufyatua risasi mitaani na katikanyumba za wenyeji
Mateka wanne wauawa katika mashambulizi ya Israel - Hamas
Mashambulio ya anga ya Israel usiku wa kuamkia leo huko Gaza yaliwauwa mateka wanne, na wanamgambo wa Hamas waliokuwa wakiwashikilia, msemaji wa kundi hilo la wanamgambo amesema.
Haijulikani ni watu wangapi hasa wanashikiliwa mateka na Hamas, wakiwa wametekwa nyara nchini Israel, lakini jeshi la Israel asubuhi ya leo lilisema ni "kadhaa".
Vikosi vya usalama vya Uganda vyafunga ofisi ya chama cha Bobi Wine

Chanzo cha picha, Bobi Wine
Maelezo ya picha, Mamia ya wafuasi wa Bobi Wine walikamatwa wiki iliyopita huku polisi wakizuia maandamano ya kumkaribisha nyumbani Maafisa wa polisi na wanajeshi wa Uganda wamefunga ofisi za National Unity Platform (NUP), chama kinachoongozwa na mwanasiasa wa upinzani Bobi Wine.
"Kuna uwepo mkubwa wa maafisa wa usalama katika ofisi zetu huko Kamwokya, na kwa sasa hatuwezi kuzifikia," chama cha NUP kilisema katika chapisho kwenye katika mtandao wa X siku ya Jumatatu.
Bobi Wine pia amesema maafisa hao walivamia makao makuu ya chama na kuwazuia watu kuingia au kutoka nje ya majengo hayo.
Mwanamuziki huyo aliyegeuka kuwa mwanasiasa alisema kwenye mitandao ya kijamii kwamba kizuizi cha maafisa wa usalama kinalenga kusimamisha hafla ya maombi ambayo NUP ilipanga kufanya katika ofisi yake mjini Kampala siku ya Jumatatu.
Maombi hayo yalikusudiwa kwa ajili ya "marafiki waliokufa, waliozuiliwa na kutoweka" wa chama.
Wiki iliyopita, polisi walimpeleka Bobi Wine hadi nyumbani kwake baada ya kurejea Uganda kutoka Afrika Kusini, wakisema kuwa hatua hiyo ilikuwa ni kumzuia kuandaa maandamano.
Pia waliwazuilia makumi ya wafuasi wa Bobi Wine kwa madai kwamba walichochea vurugu na kupanga maandamano haramu.
Bobi Wine amewakosoa maafisa hao wa usalama kwa hatua hiyo, inayoenda sambamba na siku ya uhuru wa Uganda.
“Wanapofanya hivi, watakusanyika bila aibu leo kusherehekea ‘uhuru’ hata wanapokuwa na mwennendo mbaya kuliko wakoloni,” alisema.
Polisi wa Kenya waanza uteuzi wa maafisa wa kupelekwa Haiti
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Ian Wafula
- Nafasi, BBC Africa, Nairobi

Chanzo cha picha, Getty Images
Huduma ya Polisi ya Kenya imeanza uteuzi wa maafisa watakaotumwa Haiti huku wakisubiri idhini ya bunge.
Barua ambayo BBC imeiona kutoka kwa Inspekta Jenerali wa Polisi inaomba kwa dharura orodha ya majina kutoka kwa Kitengo cha maalum cha GSU
Pia inaeleza mahitaji yanayohitajika na maafisa watarajiwa.
Miongoni mwa masharti hayo ni huduma ya chini ya miaka 5, wenye umri kati ya miaka 20-55, ufahamu wa lugha ya Kiingereza, na uwezo wa kushika silaha kwa usalama.
Katiba ya Kenya inaihitaji serikali kupata idhini kutoka kwa bunge kabla ya kupeleka vikosi nje ya nchi .
Hoja bungeni inayojadili misheni ya Haiti haikuweza kuanza wiki iliyopita kutokana na kukosekana kwa idadi ya wabunge kuijadili .
Akizungumza Jumapili, Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa Kithure Kindiki alisema hakutakuwa na njia za mkato au ukiukaji wa katiba katika kuwatuma polisi hao Haiti .
Kenya ilijitolea kuongoza jeshi la polisi la kimataifa katika taifa hilo la Karibea ili kukomesha ghasia za magenge zinazoongezeka. Nchi hiyo iliahidi maafisa wake 1000 kusaidia kurejesha utulivu.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilitoaidhini kwa ujumbe huo kufuatia wito wa msaada kutoka kwa serikali ya Haiti.
Unaweza pia kusoma
Watanzania wawili hawajulikani walipo katika eneo lililokumbwa na mashambulizi Israel
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Alfred Lasteck
- Nafasi, BBC News, Dar es Salaam
Ubalozi wa Tanzania nchini Israel unasema kuwa hauna mawasiliano na raia wawili wa nchi hiyo ambao wanakaa eneo la kusini ambalo limeshuhudia mapambano baina ya wanamgambo wa wa Kipalestina wa Hamas na jeshi la Israeli.
Balozi wa Tanzania nchini Israel, Alex Kallua ameieleza BBC kuwa mpaka leo asubuhi, ubalozi huo umekuwa na mawasiliano na watanzania takribani 350 waliopo nchini humo kasoro wanafunzi hao wawili.
Balozi Kallua amesema, ”Tunaendelea kuwafuatilia watanzania wawili ambao ni wanafunzi waliokuwa wanafanya mafunzo kwa vitendo ‘internship’ kusini mwa nchi hiyo. Tunafanya jitihada za kuwapata kwanza ili kufahamu walipo na hali zao. ”…wanafunzi wengine takribani 260 kati ya watanzania zaidi ya 350 wako salama katika maeneo mbalimbali nchini humo na wamekuwa na mawasiliano na ubalozi,” alisema balozi huyo.
Sambamba, balozi huyo amesema kuwa wanaendelea kufuatilia hali ya usalama nchini humo ili kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa salama.
”Tunafuatilia kwa karibu, na tunaendelea kupata taarifa kutoka Mamlaka za Israel kuhusu hali ilivyo. Tunaendelea kufuatilia na kuwaeleza waliopo hali ilivyo,” alisema balozi huyo.
Miili ya wapiganaji wa Hamas bado imeachwa barabarani

Tuliona maiti za wapiganaji wa Hamas zikiwa bado zimetapakaa barabarani- zimeachwa zioze - tofauti na wahanga wao wa Israel ambao wamechukuliwa muda mrefu uliopita kwa ajili ya kutambuliwa na kuzikwa.
Tulitazama jinsi dereva mmoja wa Israel akisimamisha lori lake ili aweze kuokota jiwe la kutupia maiti ya mpiganaji mmoja wa Hamas aliyekufa.Hasira zilizuka pande zote mbili za mpaka.
Wakati wanajeshi wa Israel walio na vifaa vya kutosha na waliopata mafunzo wakijaribu kutokomeza mabaki ya wanamgambo hao waliofanya uvamizi huo, Hamas inaendelea kurusha makombora mengi mpakani - mchana na usiku.
Kinga ya kisasa ya anga ya Israeli - inayoitwa Iron Dome - imekuwa ikifanya kazi kwa muda wa ziada.Haiwezi kuzuia kila roketi iliyorushwa kutoka Gaza.
Operesheni ya kuondoa hatari iliyopo katika maeneo yaliyovamiwa wakati mwingine inaonekana zaidi kama operesheni kamili ya kijeshi - huku ndege za Israel zikiruka angani kila mara na kugonga mamia ya shabaha ndani ya Gaza.
Lakini Israel ni wazi inapanga mengi zaidi.Vifaru, wanajeshi na magari ya kivita yanakusanyika karibu na mpaka wa Gaza.Inaonekana kama maandalizi ya operesheni kubwa ya kijeshi inayoweza kutokea katika Gaza yenyewe.
Ving'ora vya mashambulizi ya anga vinasikika mjini Jerusalem na kote Israel - IDF
Jeshi la Ulinzi la Israel linasema ving'ora vya mashambulizi ya anga sasa vinasikika mjini Jerusalem na kote Israel, huku makombora yakirushwa kutoka Gaza. Takriban milipuko mitatu imesikika huko Jerusalem.
Bado haijabainika iwapo hizi ni roketi zinazotua, au kunaswa na ulinzi wa Israel.
Wakati huo huo msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel Daniel Hagari anasema jeshi limekomboa makazi yote karibu na kizuizi cha Gaza - lakini mapigano yanaendelea kati yao na wapiganaji wa Kipalestina.
Hapo awali, jeshi lilisema mapigano yalikuwa yakifanyika katika maeneo "saba au nane" ndani ya ardhi ya Israel.
Aidha Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant anasema ameamuru "kuzingirwa kabisa" kwa Ukanda wa Gaza: "Hakuna umeme, hakuna chakula, hakuna mafuta."
Israeli kwa sasa inadhibiti anga ya Gaza na ufuo wake, na kuzuia ni nani na bidhaa gani zinazoruhusiwa kuingia na kutoka kupitia vivuko vya mpaka wake.
Vile vile, Misri inadhibiti wanaopita na kutoka katika mpaka wake na Gaza.
Bei ya mafuta yapanda kufuatia mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel

Chanzo cha picha, Getty Images
Bei ya mafuta imepanda kutokana na wasiwasi kwamba hali ya Israeli na Gaza inaweza kuvuruga usambazaji kutoka Mashariki ya Kati.
Brent crude, kiwango cha kimataifa, kilipanda kwa dola 2.50 kwa pipa hadi dola 87.05, wakati bei za Marekani pia zilipanda.
Maeneo ya Israeli na Palestina sio wazalishaji wa mafuta lakini eneo la Mashariki ya Kati linachukua karibu theluthi moja ya usambazaji wa kimataifa.
Shambulio la Hamas dhidi ya Israel lilikuwa ni ongezeko kubwa la uhasama kati ya pande hizo mbili kwa miongo kadhaa.
Mataifa ya Magharibi yalilaani mashambulizi hayo. Msemaji wa Hamas, kundi la wapiganaji wa Palestina, aliambia BBC kwamba kundi hilo linaungwa mkono moja kwa moja na hatua hiyo kutoka Iran - mojawapo ya wazalishaji wakuu wa mafuta duniani.
Iran ilikanusha kuhusika na shambulio hilo katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Jumapili, Reuters iliripoti. Lakini Rais wa Iran Ebrahim Raisi ameeleza kuunga mkono shambulio hilo.
Maelezo zaidi:
- Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
- Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
- Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
- Hamas: Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu

