Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanajeshi na raia wa Israeli watekwa nyara katika shambulio la wanamgambo wa Palestina
Wanamgambo wa Kipalestina walishambulia vituo kadhaa vya kijeshi - picha kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wanamgambo ndani ya kambi isiyojulikana, wakichoma moto magari ya Israel 4kikiwemo kifaru cha jeshi aina ya Merkava.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Mashambulio ya Palestina: Mashambulio yasiyo ya kawaida na yasiyotarajiwa
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Jeremy Bowen
- Nafasi, Mhariri wa kimataifa
Kile ambacho kimekuwa kikifanyika asubuhi ya leo hakina mfano katika kipindi cha zaidi ya miaka 15 tangu Hamas ilipochukua udhibiti wa Gaza.
Hatua hiyo inakuja baada ya miezi kadhaa ya ghasia na kuongezeka kwa mvutano kati ya Waisraeli na Wapalestina, ingawa mengi ya hayo yamejikita katika Ukingo wa Magharibi, ambao ni eneo ambalo Israel imelikalia tangu mwaka 1967, linalopakana na Jerusalem na mpaka na Jordan.
Israel imesema imeshambuliwa, kwamba Hamas imetangaza vita dhidi ya Israel, na ingetarajia kwamba mipango ambayo Waisraeli wanaiweka pamoja sasa itasababisha majibu ya nguvu sana - wamesema hilo ndilo litakalotokea.
Nadhani kuna uwezekano mkubwa utakaojumuisha kuwekwa kwa vikosi vya Israeli katika Gaza.
Hali hii itaenda haraka na kuna uwezekano wa kuongezeka kwa mapigano. Swali moja kubwa ni nini kinachotokea sasa - sio tu ndani na karibu na Gaza - lakini kile kinachotokea katika Jerusalem na Ukingo wa Magharibi, ambapo kumekuwa na vurugu za mara kwa mara na kuongezeka kati ya vikundi vya Wapalestina na vikosi vya usalama vya Israeli na walowezi kwa miezi.
Ni dhahiri kwamba hali tete iliyopo tayari katika maeneo hayo itazidi kuwa hata mbaya zaidi kutokana na matukio haya ya sasa.
Kwa hivyo nadhani hivi sasa kwa Waisraeli na Wapalestina, hili ni jambo lisilotarajiwa na lenye kuleta wasiwasi sana na kushuhudia matukio ya leo asubuhi.
Habari za hivi punde, Takriban Waisraeli 22 waliuawa - huduma za dharura
Huduma za dharura za Israel zimesema kuwa takriban Waisraeli 22 wameuawa baada ya shambulizi la kushtukiza ambalo halijawahi kushuhudiwa na Wapalestina.
Wakati huo huo ,Wizara ya afya ya Israel imesema takriban watu 545 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Wapalestina, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Habari za hivi punde, Watu wa Palestina wana haki ya kujitetea - Abbas
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas anasema watu wake wana haki ya kujilinda dhidi ya "ugaidi wa walowezi na wanajeshi" kulingana na shirika la habari la Reuters.
Bw Abbas amezungumzia kuhusu "haja ya kutoa ulinzi kwa watu wetu", akisisitiza haki ya watu wa Palestina ya kujilinda dhidi ya "ugaidi na vikosi vya uvamizi".
Rais huyo alikuwa akiongoza mkutano wa dharura uliofanyika mjini Ramallah na maafisa wakuu wa Mamlaka ya Walestina.
Tuko vitani, asema Waziri Mkuu wa Israel, baada ya shambulio la kushitukiza la Wapalestina
Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amewaambia rais wa nchi hiyo kuwa wako vitani baada ya shambulio la kushitukiza la Wapalestina lililptekelezwa na wanamgambo wa Hamas.
"Raia wa Israeli. Tuko vitani, sio operesheni, sio kuongezeka kwa vita.
"Leo asubuhi Hamas ilitekeleza shambulio la kushtukiza la mauaji dhidi ya taifa la Israel na raia wake. Tumekuwa nalo tangu mapema asubuhi.
“Niliwaita wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, kwanza niliwaagiza kusafisha makazi ya magaidi waliojipenyeza – operesheni hii inafanyika saa hizi.
"Wakati huo huo, niliamuru vita vya kulipiza kisasi kwa nguvu na kwa kiwango ambacho adui hakuwahi kujua.
"Adui atalipa gharama ambayo hajawahi kujua. Wakati huo huo, natoa wito kwa raia wote wa Israeli kutii maagizo ya jeshi na mengine watakayopewa na mamlaka.
"Tuko kwenye vita na tutashinda.'
Tazama: Roketi zilizorushwa kutoka Gaza zikiruka angani kuelekea Israel
Makumi ya wanamgambo wa kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Hamas wanaonekana kuingia kusini mwa Israel kwa shambulio la kushtukiza na kwa sasa wako huru.
Jeshi la Israel linasema kuwa linalenga shabaha katika Ukanda wa Gaza huku kukiwa na "tathmini ya hali".
Hapo awali, roketi nyingi zilirushwa kuelekea Israel, zikifyatua ving'ora vya mashambulizi ya anga nchini kote.
Picha za video zinaonyesha makombora yakiruka angani huko Gaza, na matokeo ya mashambulizi huko Ashkeloni, Israel.
Mtu mmoja ameuawa na kumekuwa na ripoti za milipuko karibu na Tel Aviv na maeneo yanayozunguka Gaza.
Video za kutisha zinaonekana kuonyesha ufyatuaji risasi mitaani kusini mwa Israel
Video za kutisha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonekana kuwaonyesha wanamgambo wa Kipalestina wakiwafyatulia risasi wapita njia katika mitaa ya kusini mwa Israel.
Kuna ripoti za nyumba kuchukuliwa na watu wenye silaha mjini Sderot kutoka kundi la Kiislamu la Hamas, ambalo linatawala Gaza.
Jeshi la Israel lilikuwa limewaambia wakaazi wa eneo hilo kusalia majumbani mwao kufuatia ripoti za kujipenyeza kwa wapiganaji wa Hamas.
Mashambulio makali ya roketi na makombora ya masafa marefu - kilianza baada ya alfajiri mwishoni mwa likizo ya Sukkot na shambulio hili limekuwa la ghafla kwa walinzi wa Israeli. Moto mkubwa unawaka katika maeneo ya kusini mwa Israel ambako roketi zimepiga.
Kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Hamas alitangaza kuanza kwa operesheni hiyo katika matangazo kwenye vyombo vya habari vya Hamas, akitoa wito kwa Wapalestina kila mahali kupigana.
Jeshi la Israel limesema litawatetea raia wa Israel na kwamba Hamas italipa gharama kubwa kwa vitendo vyake.
Israel yatangaza utayari wa vita baada ya mashambulizi kutoka Gaza
Makumi ya watu wenye silaha kutoka kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas wamejipenyeza kusini mwa Israel kutoka Ukanda wa Gaza katika shambulio la kushtukiza.
Video zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zilionekana kuwaonyesha wanamgambo wa Kipalestina wakiwafyatulia risasi wapita njia katika mitaa ya mji wa Sderot nchini Israel.
Shambulio la roketi kali ya Wapalestina kutoka Gaza pia ilimuua mwanamke mmoja wa Israel.
Waziri wa ulinzi wa Israel alisema Hamas "ilifanya makosa makubwa na kuanzisha vita" dhidi ya nchi yake.
"Wanajeshi [wa Israeli] wanapambana na adui katika kila eneo," Yoav Gallant aliongeza. "Taifa la Israel litashinda vita hivi".
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limesema limehamia kwenye kituo cha vita na kwamba makumi ya ndege za kivita zilikuwa zikifanya mashambulizi ya anga kwenye maeneo ya Hamas huko Gaza.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo tarehe 07.10.2023