Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Tanzania yaua ndege wavamizi milioni tano aina ya kwelea

Ndege aina ya Kwelea kwelea mara nyingi huharibu nafaka kama mchele na ngano.

Moja kwa moja

  1. Harusi ya wapenzi wa jinsi moja yazua utata India

    Wakati India ikisubiri uamuzi wa Mahakama ya Juu juu ya kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja, harusi ya hivi majuzi ya wanandoa wa jinsi moja LGBTQ katika jimbo la kaskazini la Punjab imegonga na vichwa vya habari mara kwa mara na kuzua utata.

    Dimple, mwenye umri wa miaka 27 - ambaye anajitambulisha kama mwanaume - na Manisha, anayejitambulisha kama mwanamke 21, walioana katika mji wa Bathinda tarehe 18 Septemba kwa baraka za familia zao - jambo ambalo si la kawaida sana katika nchi ya kihafidhina kama India.

    Lakini jambo lisilo la kawaida zaidi ni kwamba ndoa yao ilifungwa katika gurdwara - hekalu la Sikh - na bibi na bwana harusi wakifanya matambiko yote ya kitamaduni.

    Harusi hiyo imekosolewa na baadhi ya viongozi wa kidini, akiwemo kasisi mkuu wa dini ya Kikalasinga Giani Raghbir Singh ambaye alitangaza kwamba "ndoa za watu wa jinsia moja hazikuwa za asili na ni kinyume na maadili ya Sikh".

    Ndoa ya wanawake wawili mbele ya Guru Granth Sahib - maandiko matakatifu ya Sikh - "ilikuwa ukiukwaji mkubwa wa maadili na kidini", alisema, na kuiagiza kamati ya Bathinda gurdwara kumsimamisha kazi kasisi Hardev Singh, aliyeendesha ndoa hiyo, na watatu wengine kutoka kwa majukumu yao hadi ilani nyingine.

    Hardev Singh tangu wakati huo ameondolewa kwenye nafasi yake. Katika utetezi wake, alisema kuwa hakuweza kufahamu kuwa bibi na bwana harusi wote walikuwa wa kike kwani mmoja wa wanawake hao alikuwa amevaa kilemba.

    Dimple amehoji madai hayo na kusema kuwa walitoa nakala za uthibitisho wa utambulisho wao kwa gurdwara hivyo hakuna sababu ya kuchanganyikiwa.

  2. Meya wa Libya akamatwa kufuatia mafuriko yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu

    Meya wa mji wa Libya wa Derna ulioharibiwa na mafuriko makubwa amekamatwa kuhusiana na maafa hayo, maafisa wanasema.

    Abdulmenam al-Ghaithi alikuwa miongoni mwa maafisa kadhaa walioshtakiwa kuhusiana na maafa yaliyowaua maelfu ya watu mashariki mwa Libya mapema mwezi huu.

    Wiki iliyopita, wakazi wa Derna wenye hasira waliichoma moto nyumba ya meya wakimpinga

    Ofisi ya mwanasheria mkuu, iliyoko katika mji mkuu wa Tripoli, ilisema Jumatatu kwamba maafisa hao "wanawajibika kwa kusimamia vifaa vya mabwawa ya nchi" na kwa hivyo imefungua kesi ya jinai dhidi yao.

    Baadhi ya maafisa hao akiwemo Bw al-Ghaithi tayari wamezuiliwa kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.

    Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, ofisi ya mwanasheria mkuu iliwashutumu maafisa hao kwa makosa mengi, kama vile usimamizi mbaya wa fedha zilizokusudiwa kutunza mabwawa yaliyopasuka na kusababisha mafuriko huko Derna.

    Ofisi yake pia ilisema kuwa maafisa hao wameonyesha kutojali kwa kushindwa kuchukua tahadhari, na kusababisha vifo vinavyotokana na mafuriko na hasara ya kiuchumi kwa Libya.

    Bw al-Ghaithi amezidi kushutumiwa kwa kutumia mamlaka yake vibaya.

    Libya imegawanywa katika tawala mbili pinzani - moja mashariki na moja magharibi. Kwa vile mwanasheria mkuu yuko Tripoli, magharibi, haijabainika ni kwa kiwango gani anaweza kuamuru kukamatwa kwa watu mashariki.

    Siku ya Jumapili, serikali ya mashariki ilisema kwamba idadi ya vifo vilivyothibitishwa kutokana na mafuriko imefikia 3,868.

    Ofisi ya mwanasheria mkuu ilisema kuwa uchunguzi kuhusu maafisa wengine unaendelea na kunaweza kuwa na watu wengine waliokamatwa.

    Soma zaidi:

    • Miili iliyoachwa bila kutambuliwa na mafuriko ya Libya
    • Tazama :Kijiji kizima kilivyosombwa na mafuriko mpaka baharini Libya
  3. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 26.09.2023