Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Wanajeshi wa Burkina Faso wajiunga na wenzao Niger kukabili wanamgambo

Majeshi ya Burkina Faso na Niger yameua idadi isiyojulikana ya wanamgambo katika operesheni za pamoja, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Moja kwa moja

  1. Kuogelea baharini na nyoka: Mwanamume mmoja nchini Australia alitozwa faini ya zaidi ya dola 2000.

    Nchini Australia, mwanamume mmoja ametozwa faini baada ya kumchukua nyoka aliyemhifadhi nyumbani kuogelea baharini.

    Igor Fayoza alijulikana sana katika vyombo vya habari vya Australia wakati huo, wakati video zilizochukuliwa akiwa na nyoka wake baharini zilipochapishwa.

    Katika picha hizo, inaonekana bwana Fayoza akiwa amembeba kwenye nyoka , ambaye anaogelea baharini.

    Shirika la sayansi na mazingira la Australia limesema kuwa kumpeleka nyoka huyo baharini kunaweza kuwa tishio kwa watu wengine na pia kuna uwezekano kuwa nyoka huyo akawadhuru watu

    Lakini Higur Feuza, ambaye amempeleka nyoka kwenye maji ya bahari takriban mara kumi, anasema, "Huwa ninampeleka ufukweni, anapenda sana maji. Sikumoja nilienda naye kwenye ubao wa kuogelea ambao ni inafurahisha sana." alitoa."

    Bada ya video za Feijoza kuchapishwa kwenye mtandao, mamlaka ya Wakala wa Ulinzi wa Mazingira wa eneo la Queensland nchini Australia walianza kumchunguza na kumtoza faini ya zaidi ya dola 2,300 kwa hatua hii.

  2. Mwili wa mwanamke uliopatikana mdomoni mwa mamba mwenye urefu wa futi 13 umetambuliwa

    Mamba mwenye urefu wa futi 13 (m 4) ameuawa, polisi wanasema, baada ya kuonekana huko Florida na mabaki ya mwanamke kwenye taya zake.

    Mu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo aliviambia vyombo vya habari kuwa alimuona mamba kwenye mfereji wa Largo akiwa ameshikilia kiwiliwili cha chini mdomoni mwake.

    Ofisi ya Sherifu wa Kaunti ya Pinellas ilisema mnyama huyo aliuawa na kuthibitisha kuwa mabaki ya Sabrina Peckham mwenye umri wa miaka 41 yalipatikana kwenye njia ya maji.

    Uchunguzi utabainisha mazingira yaliyosababisha kifo cha mwanamke huyo.

    Polisi walisema maafisa wao waliitwa sab ana dakika hamisini mchana kwa saa za eneo siku ya Ijumaa baada ya ripoti ya mwili kuonekana kwenye njia ya maji.

    Jamarcus Bullard alisema alikuwa akienda kwenye mahojiano ya kazi alipomwona mamba huyo akiwa na kiwiliwili mdomoni mwake.

    "Niligundua kuwa alikuwa na mwili mdomoni - kama kiwiliwili cha chini - kwa hivyo nilipoona kwamba nilikimbia moja kwa moja hadi kwa idara ya zima moto," aliamwambia mtangazaji wa Fox 13.

  3. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara ikiwa leo ni tarehe 25.09.2023