Prigozhin alifanya makosa makubwa - Putin
Putin anatoa pongezi kwa mtu huyo ambaye wakati mmoja alijulikana kama "mpishi" wake kutokana na kandarasi nzuri alizokuwa nazo kusambaza chakula kwa Kremlin.
"Nimemjua Prigozhin kwa muda mrefu, tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990," Putin anasema katika hotuba yake kwa njia ya televisheni.
Katika kumbukumbu ya wazi ya uasi wa Wagner mnamo Juni, Putin anaendelea: "Huyu alikuwa mtu mwenye hatima ngumu, na alifanya makosa makubwa maishani, lakini pia alitafuta kupata matokeo muhimu, yeye mwenyewe na wakati nilipomtaka kufanya hivyo, kwa sababu za kawaida, kama vile katika miezi hii ya hivi karibuni."
Hatutasahau jukumu la Wagner nchini Ukraine, rais wa Urusi anaongeza
Aliyeripotiwa kuwa pamoja na Prigozhin kwenye ndege hiyo ni mtu wake wa mkono wa kulia Dmitry Utkin, pamoja na washiriki wengine watano wa Wagner na wafanyakazi watatu.
"Takwimu za awali zinaonesha wafanykazi wa kampuni ya Wagner walikuwa kwenye ndege," Putin anakiri. "Ningependa kutambua kwamba hawa ni watu ambao wametoa mchango mkubwa kwa sababu yetu ya pamoja ya kupigana na utawala wa Nazi mamboleo nchini Ukraine," anaendelea.
"Tunaikumbuka na kuijua, na hatutaisahau." Putin amedai mara kwa mara kuwepo kwa Wanazi mamboleo nchini Ukraine kama uhalali wa uvamizi wake katika nchi jirani, madai ambayo yamekanushwa.
Inafaa pia kuzingatia kuwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensy ni Myahudi.