Rais Putin avunja ukimya kuhusu ajali ya ndege, asema Prigozhin alifanya makosa makubwa

Putin amesema Prigozhin alikuwa mtu mwenye hatima ngumu, na alifanya makosa makubwa maishani, lakini pia alitafuta kupata matokeo muhimu.

Moja kwa moja

  1. Prigozhin alifanya makosa makubwa - Putin

    Prigozhin

    Chanzo cha picha, Reuters

    Putin anatoa pongezi kwa mtu huyo ambaye wakati mmoja alijulikana kama "mpishi" wake kutokana na kandarasi nzuri alizokuwa nazo kusambaza chakula kwa Kremlin.

    "Nimemjua Prigozhin kwa muda mrefu, tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990," Putin anasema katika hotuba yake kwa njia ya televisheni.

    Katika kumbukumbu ya wazi ya uasi wa Wagner mnamo Juni, Putin anaendelea: "Huyu alikuwa mtu mwenye hatima ngumu, na alifanya makosa makubwa maishani, lakini pia alitafuta kupata matokeo muhimu, yeye mwenyewe na wakati nilipomtaka kufanya hivyo, kwa sababu za kawaida, kama vile katika miezi hii ya hivi karibuni."

    Hatutasahau jukumu la Wagner nchini Ukraine, rais wa Urusi anaongeza

    Aliyeripotiwa kuwa pamoja na Prigozhin kwenye ndege hiyo ni mtu wake wa mkono wa kulia Dmitry Utkin, pamoja na washiriki wengine watano wa Wagner na wafanyakazi watatu.

    "Takwimu za awali zinaonesha wafanykazi wa kampuni ya Wagner walikuwa kwenye ndege," Putin anakiri. "Ningependa kutambua kwamba hawa ni watu ambao wametoa mchango mkubwa kwa sababu yetu ya pamoja ya kupigana na utawala wa Nazi mamboleo nchini Ukraine," anaendelea.

    "Tunaikumbuka na kuijua, na hatutaisahau." Putin amedai mara kwa mara kuwepo kwa Wanazi mamboleo nchini Ukraine kama uhalali wa uvamizi wake katika nchi jirani, madai ambayo yamekanushwa.

    Inafaa pia kuzingatia kuwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensy ni Myahudi.

  2. Putin avunja ukimya kuhusu ajali ya ndege

    Putin

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa Urusi Vladimir Putin amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu ajali ya ndege iliyotokea jana.

    Ametuma salamu za rambirambi zake kwa familia za waliopoteza maisha, na anaelezea mwanzilishi wa Wagner Group Yevgeny Prigozhin kama mfanyabiashara mwenye talanta.

    Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni Putin, anasema wachunguzi wataangalia kilichotokea, lakini hilo litachukua muda.

    Anasema aliambiwa kuhusu ajali ya ndege iliyotokea Jumatano asubuhi.

    Prigozhin alikuwa amerejea tu kutoka safari ya Afrika, asema Putin

    Putin pia anasema kwamba "ninavyofahamu", Prigozhin "ni jana tu [Jumatano] alirejea kutoka Afrika.Alikutana na watu fulani rasmi huko".

    Katika siku za hivi karibuni mkuu wa Wagner anaaminika kuwepo Afrika Magharibi, ambako wachambuzi wa nchi za Magharibi wanahofia kuwa kundi hilo lilikuwa likitaka kupanua wigo wake hadi katika nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Niger, ambako mapinduzi yametokea hivi karibuni.

    Wagner ni nguzo muhimu ya sera ya mambo ya nje ya Urusi, huku vikosi vyake vikisaidia kuunga mkono serikali za Syria, Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Libya kwa kubadilishana na haki za uchimbaji madini.

  3. Wagner tishio kubwa katika uongozi wa Putin- Waziri Mkuu wa Poland

    Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kifo cha Prigozhgin, ikiwa kitathibitishwa, inamaanisha Wagner itakuwa tishio kubwa zaidi kwani udhibiti wake unaweza kumwangukia Vladimir Putin, Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki anasema.

    "Kundi la Wagner linakuja chini ya uongozi wa Putin. Hebu kila mtu ajibu swali mwenyewe - je, tishio litakuwa kubwa au ndogo? "Kwangu mimi, hilo ni swali la kejeli," Morawiecki anauambia mkutano wa wanahabari.

    Mnamo Julai, Poland iliimarisha mpaka wake na Belarus kufuatia matarajio ya mamluki kutoka kundi la Wagner kuhamia Belarus.

    Hatua hiyo ilikuwa ni sehemu ya mpango uliofikiwa kumaliza uasi wa kundi hilo mwishoni mwa Juni.

  4. Ukraine haina uhusiano wowote na ajali ya ndege - Zelensky

    Zelensky

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Ukraine haikuhusika katika kifo kilichoripotiwa cha bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin, Rais Volodymyr Zelensky anasema.

    "Hatuhusiki katika hali hii, hiyo ni hakika. Nadhani kila mtu anafahamu ni nani anayehusika," Zelensky aliwaambia waandishi wa habari huko Kyiv.

    Zelensky alifanya mzaha kuhusu wito wa Ukraine kwa mataifa mengine kwa ajili ya ndege zaidi za kupambana na uvamizi wa Urusi.

    "Ukrainia ilipotoa wito kwa nchi za ulimwenguni kuhusu ndege, hatukumaanisha hivi," anasema. "Lakini hii kwa njia fulani hakika itasaidia," anaongeza.

    Alisisitiza juu ya Kyiv kuwa na uhusiano wowote na kifo kilichoripotiwa cha Prigozhin.

  5. Makamanda wawili wa kijihadi wauawa Msumbiji - Jeshi

      • Author, Jose Tembe
      • Nafasi, BBC News, Maputo
    Viongozi wawili waandamizi wa wanajihadi wameuawa katika operesheni ya pamoja na vikosi vya kikanda

    Chanzo cha picha, AFP

    Viongozi wawili waandamizi wa wanajihadi wameuawa katika operesheni ya pamoja na vikosi vya kikanda katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado nchini Msumbiji, jeshi linasema.

    Mmoja wao alikuwa Abu Kital ambaye "alishikilia wadhifa wa naibu kamanda wa operesheni za kundi la Ahlu-Sunnah wal Jama`a (ASWJ)", taarifa ya jeshi ilisema.

    Mwingine alikuwa Ali Mahando, ambaye pia alishika wadhifa wa juu katika kundi hilo.

    Jeshi la Msumbiji na vikosi vya washirika, ikiwa ni pamoja na wanajeshi wa Rwanda na ujumbe wa kijeshi kutoka kambi ya kikanda ya kusini mwa Afrika ya Sadc, wamekuwa wakiendesha operesheni katika jimbo hilo lililoathiriwa na wanajihadi.

    Msumbiji imekuwa ikipambana na waasi wenye uhusiano na kundi la Islamic State tangu Oktoba mwaka 2017.

    Zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kuyahama makazi yao huku wengine zaidi ya 4,000 wakiuawa katika kipindi hicho.

  6. Migogoro na ukame yasababisha Waethiopia milioni nne kukosa makazi - UN

    Mzozo umewalazimu Waethiopia milioni nne kukimbia makazi yao

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji linasema kuwa zaidi ya Waethiopia milioni nne sasa wamekimbia makazi yao ndani ya nchi, hasa kwa sababu ya migogoro au ukame.

    Ripoti ya Kitaifa ya Kuhama Makazi, ambayo inaangazia kipindi cha kati ya Novemba mwaka jana na Juni 2023, inasema theluthi mbili kati yao walilazimishwa kutoka makwao kutokana na migogoro.

    Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2021 ripoti hiyo inajumuisha eneo lililokumbwa na vita la Tigray, ambalo lina wakazi wengi zaidi wa Ethiopia waliong'olewa na vita, zaidi ya watu milioni moja.

    Eneo la Somalia mashariki mwa Ethiopia linashikilia idadi kubwa zaidi ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na ukame. Hapo awali Umoja wa Mataifa ulisema zaidi ya Waethiopia milioni 20 walikuwa wakihitaji msaada wa chakula na $4bn (£3.14bn) zilihitajika kukidhi mahitaji yao.

  7. Putin ahutubia mkutano wa Brics bila kutaja ajali ya ndege inayoripotiwa kumuua Progozhin

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Putin alihutubia mkutano huo kwa njia ya vídeo

    Ikiwa ulikuwa unatafuta maoni ya kwanza kutoka kwa rais wa Urusi kuhusu kifo kilichoripotiwa cha Yevgeny Prigozhin, kwa kweli hakukuwa na chochote katika hotuba yake fupi aliyoitoa kwa njia ya video.

    Putin alizingatia maandishi ya hotuba yake, yaliyojikita zaidi juu ya upanuzi wa kikundi cha Brics "kuhakikisha ushawishi wa Brics ulimwenguni unakua".

    Haishangazi kwamba hakutajwa mshirika wake wa zamani aliyegeuka-muasi. Huenda hili halikuwa jukwaa la maswala ya nyumbani.

    Putin hakuwa katika chumba cha mkutano wa Brics cha Johannesburg. Alisalia Urusi kwa sababu ya hati ya kukamatwa kwa madai ya uhalifu wa kivita nchini Ukraine iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

    Rais Putin alitoa taarifa fupi kupitia video kwenye mkutano huo wa kilele wa Brics

    Alimshukuru Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kwa kuandaa mkutano huo na kwa upanuzi wa kundi hilo zaidi ya mataifa matano ya sasa.

    Hii ni baada ya kundi la Brics kuamua kuzialika nchi sita - Argentina, Misri, Iran, Ethiopia, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu - kuwa wanachama wapya wa umoja huo.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amekuwa akimuwakilisha Putin nchini Afrika Kusini na yuko kwenye mkutano na waandishi wa habari.

    Unaweza pia kusoma:

    • Yevgeny Prigozhin: Tunachojua hadi sasa kuhusu ajali ya ndege
    • Bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin adhaniwa kuwa amefariki baada ya ajali ya ndege ya Urusi
    • Kutoka kuwa mpishi wa Putin hadi mkuu wa jeshi la kibinafsi la Urusi
    • Tazama: Ndege ilivyoanguka huku mkuu wa Wagner akidaiwa kuwa miongoni mwa abiria
  8. Brics yakaribisha nchi sita kujiunga na umoja huo

    Viongozi wa nchi wanachama wa Brics

    Chanzo cha picha, AFP

    Nchi sita, Argentina, Misri, Iran, Ethiopia, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zitakaribishwa kuwa wanachama wapya wa kambi ya Brics.

    Tangazo hilo linatoka kwa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ambaye ni mwenyeji wa mkutano wa kilele wa viongozi wa Brics mjini Johannesburg.

    Nchi hizo zitajiunga ifikapo mwezi Januari mwakani.

    Mjadala wa kupanua Umoja wa Brics unaoundwa na Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, umeongoza ajenda katika mkutano huo wa Johannesburg.

    Kumekuwa na mgawanyiko kuhusu kama upanuzi sasa ndio hatua bora zaidi. Kundi hilo linataka kupata ushawishi zaidi duniani.

    Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akifurahia kuwa nchi yake ni miongoni mwa nchi sita zilizoalikwa kujiunga na Umoja wa Brics kuanzia Januari mwakani.

    Unaweza pia kusoma;

  9. Jinsi wananchi wa Ukraine wanavyopokea habari za kifo cha kudhaniwa cha Prigozhin

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mwandishi wa BBC James Waterhouse aliyeko Kyiv anasema watu nchini Ukraine hawana huruma kidogo na Prigozhin na wanatarajia "mgawanyiko" ndani ya Urusi.

    "Huyu ni kiongozi wa kundi la mamluki ambalo limefanya baadhi ya mashambulio ya ukikatili zaidi nchini Ukraine," anasema.

    "Mpaka mtu yeyote atakaposikia uthibitisho au kuona kumuona Prigozhin mwenyewe akiweka video basi sidhani kama watu wataiamini kikamilifu taarifa - ya kifo chake."

    Wananchi wengi wa Ukraine wamekuwa wakitumai kwamba Vladimir Putin "atapinduliwa" kwa maasi ya Prigozhin, ingawa hayakufanikiwa, yalionekana kama mwanzo wa hayo.

    Maendeleo haya "yanaongeza matumaini yale kwamba serikali ya Putin inaweza kuanguka," Waterhouse anasema.

    Msaidizi wa rais wa Ukraine Mykhaylo Podolyak aliandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba ajali hiyo ya ndege ilikuwa "ishara kutoka kwa Putin kwa wasomi wa Urusi kabla ya uchaguzi wa 2024. 'Jihadharini! Ukosefu wa uaminifu ni sawa na kifo'."

  10. Kwa picha: Mabaki yaliyochunguzwa baada ya ajali ya ndege inayohusishwa na kifo cha Yevgeny Prigozhin

    Tunapata picha mpya kutoka eneo la Tver nchini Urusi, ambako wataalamu wa masuala ya dharura na polisi wanachunguza mabaki ya ndege ya kibinafsi iliyohusishwa na Yevgeny Prigozhin.

    Ikulu ya Kremlin bado haijathibitisha iwapo mkuu wa Wagner alifariki katika ajali ya ndege jana, lakini maafisa wa anga walisema alikuwa mmoja wa abiria sita waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

    g

    Chanzo cha picha, reuters

    f

    Chanzo cha picha, Reuters

    d

    Chanzo cha picha, Reuters

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    f

    Chanzo cha picha, Reuters

    f

    Chanzo cha picha, Reuters

    Unaweza pia kusoma:

    • Yevgeny Prigozhin: Tunachojua hadi sasa kuhusu ajali ya ndege
    • Bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin adhaniwa kuwa amefariki baada ya ajali ya ndege ya Urusi
    • Kutoka kuwa mpishi wa Putin hadi mkuu wa jeshi la kibinafsi la Urusi
    • Tazama: Ndege ilivyoanguka huku mkuu wa Wagner akidaiwa kuwa miongoni mwa abiria
  11. Kimya cha ’ajabu’cha Rais Vladimir Putin kumhusu Prigozhin

    f

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa Urusi Vladimir Putin hadi sasa bado hajazungumza juu ya kifo kilichoripotiwa cha Yevgeny Prigozhin.

    Jana usiku, muda mfupi baada ya habari kuenea kwamba Prigozhin alikuwa kwenye ndege iliyopigwa ya Embraer, Putin alionekana kwenye tukio la kumbukumbu ya vita maarufu vya Vita vya pili vya Dunia katika Mkoa wa Kursk.

    Wakati wa hafla hiyo, alitoa pongezi kwa Warusi waliouawa wakati wa kile kinachoitwa 'operesheni maalum ya kijeshi' nchini Ukraine.

    Haishangazi, kwamba hakuitaja Wagner au Yevgeny Prigozhin.

    Huenda Putin anasubiri hadi taarifa rasmi ya matukio yanayohusu ajali ya ndege ipatikane.

    Bw Putin anajulikana sana kwa mtazamo wake wa "kungoja-na-kuona" baada ya matukio makubwa – ni mara chache hujibu kuhusu tukio mara moja.

  12. Kikundi cha Wagner kitafanya nini bila Prigozhin?

    f

    Chanzo cha picha, CONCORD PRESS SERVICE

    Kuonekana kwa Bosi wa Wagner mara kwa mara na kujitukuza kwenye chaneli ya Telegram ya kikundi hicho, akiwa amevalia kama askari, kulitoa picha kinyume na hali ngumu ya mtandao wa kundi hilo aliouanzisha.

    Kutoka Mali hadi Mashariki ya Kati, mfanyabiashara huyu wa zamani wa hot dog alighushi uhusiano wa kibinafsi na watu ambao waliwezesha kikundi cha Wagner kueneza misimamo yake kwa mafanikio katika angalau nchi saba, hasa katika Afrika Magharibi.

    Pia alifurahia utiifu, uaminifu na labda hata kujitolea, kwa maelfu ya askari wake mamluki.

    Haiba hii ya kibinafsi, tofauti kabisa na tabia ya mara kwa mara ya wakuu wa kijeshwa Urusi, inamaanisha kuwa itakuwa vigumu kwa mtu mwingine kuchukua nafasi yake.

    Unaweza pia kusoma:

    • Yevgeny Prigozhin: Tunachojua hadi sasa kuhusu ajali ya ndege
    • Bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin adhaniwa kuwa amefariki baada ya ajali ya ndege ya Urusi
    • Kutoka kuwa mpishi wa Putin hadi mkuu wa jeshi la kibinafsi la Urusi
    • Tazama: Ndege ilivyoanguka huku mkuu wa Wagner akidaiwa kuwa miongoni mwa abiria
  13. Habari za hivi punde, Miili yote ya abiria wa ndege iliyoanguka imepatikana: mamlaka ya Urusi

    Huduma za dharura za Urusi zimesema kuwa miili ya abiria wote kumi kwenye ndege ya Embraer Legacy sasa imepatikana.

    Kulingana na mamlaka, waliokuwemo ndani ya ndege hiyo ni pamoja na bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin na kamanda wake wa pili Dmitry Utkin - mtu ambaye alipatia kundi hilo la mamluki jina lake.

    Juhudi sasa zinaelekezwa kubaini juu ya kile kilichosababisha ajali hiyo.

    Polisi wameziba eneo karibu na eneo la ajali na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Urusi imeunda tume maalum kuchunguza hilo.

    Warusi wengi hawakushangaa wakati taarifa za kifo cha Prigozhin ziliripotiwa jana.

    Wakati Prigozhin ilipoanzisha uasi ulioshindwa miezi miwili iliyopita, pia alipinga mamlaka ya Vladimir Putin mwenyewe. Na hilo ni jambo ambalo Rais wa Urusi hawezi kulisahau kirahisi.

  14. Kwa picha: Maua na mishumaa katika mji alikozaliwa Prigozhin

    f

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Maua na mishumaa viliwekwa nje kwenye ukumbusho karibu na kituo cha zamani cha Wagner Saint Petersburg, katika jiji anakozaliwa Yevgeny Prigozhin.
    f

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Eneo hili la ukumbusho lilionekana saa chache baada ya ripoti kuibuka kuwa kiongozi wa Wagner alikuwa ndani ya ndege iliyoanguka kaskazini-magharibi mwa Moscow.
    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Umati mdogo ulikusanyika karibu na kituo cha zamani cha Wagner mjini Saint Petersburg
    f

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Baadhi ya watu walionekana kukasirika katika eneo la kumbukumbu

    Unaweza pia kusoma:

    • Yevgeny Prigozhin: Tunachojua hadi sasa kuhusu ajali ya ndege
    • Bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin adhaniwa kuwa amefariki baada ya ajali ya ndege ya Urusi
    • Kutoka kuwa mpishi wa Putin hadi mkuu wa jeshi la kibinafsi la Urusi
    • Tazama: Ndege ilivyoanguka huku mkuu wa Wagner akidaiwa kuwa miongoni mwa abiria
  15. Putin alikuwa wapi wakati wa ajali ya ndege inayodhaniwa kumuua Progozhin?

    R

    Chanzo cha picha, EPA

    Wakati habari zikitokea kuhusu ajali ya ndege ambayo inadhaniwa kumuua kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigozhin, Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwa akizungumza katika hafla huko Kursk kuadhimisha miaka 80 ya ushindi wa vita vya Soviet dhidi ya Ujerumani ya Nazi.

    Vita vya 1943 vinachukuliwa kuwa vita vikubwa zaidi vya vifaru vya kijeshi katika historia.

    Bw Putin hakuitaja ajali ya ndege, lakini alitoa pongezi kwa wanajeshi wa Urusi "wanaopigana kwa ujasiri na uthabiti" nchini Ukraine.

    Mapema siku hiyo, Bw Putin alihudhuria mkutano wa Brics nchini Afrika Kusini ambapo alisema alikuwa amejitolea kumaliza vita vya Ukraine ambapo alizilaumu nchi za Magharibi kwa kuvianzisha.

    G

    Chanzo cha picha, Reuters

    Unaweza pia kusoma:

    • Yevgeny Prigozhin: Tunachojua hadi sasa kuhusu ajali ya ndege
    • Bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin adhaniwa kuwa amefariki baada ya ajali ya ndege ya Urusi
    • Kutoka kuwa mpishi wa Putin hadi mkuu wa jeshi la kibinafsi la Urusi
    • Tazama: Ndege ilivyoanguka huku mkuu wa Wagner akidaiwa kuwa miongoni mwa abiria
  16. Wagner ilimpinga Putin na sasa kiongozi wake anadhaniwa kufariki

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wakati Yevgeny Prigozhin na wanajeshi wake wa Wagner walipoanzisha uasi wao miezi miwili iliyopita, Vladimir Putin aliweka hisia zake wazi zaidi.

    Aliuita uasi huo "usaliti" na "kuuchoma kisu mgongo" wa Urusi. Aliahidi kuwa wahusika wataadhibiwa.

    Uasi huo ulimfanya Rais Putin aonekane dhaifu.

    Ghafla mambo yanaonekana tofauti.

    Miezi miwili kamili baadaye, Prigozhin anadhaniwa kuwa amekufariki baada ya ndege yake ya kibinafsi kuanguka na kulipuka shambani. Kamanda wa Wagner Dmitry Utkin alikuwa kwenye ndege hiyo hiyo.

    Wasomi wa Urusi watatoa machozi kidogo juu ya kuripotiwa kwa kifo cha Prigozhin.

    Hilo ni kwa uongozi wa kijeshi wa Urusi, ambao Prigozhin alikuwa ameulaani hadharani na kwa sauti na kudai ufutwe kazi.

    Unaweza pia kusoma:

    • Yevgeny Prigozhin: Tunachojua hadi sasa kuhusu ajali ya ndege
    • Bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin adhaniwa kuwa amefariki baada ya ajali ya ndege ya Urusi
    • Kutoka kuwa mpishi wa Putin hadi mkuu wa jeshi la kibinafsi la Urusi
    • Tazama: Ndege ilivyoanguka huku mkuu wa Wagner akidaiwa kuwa miongoni mwa abiria
  17. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara ikiwa leo ni tarehe 24.08.2023