Mkuu wa Wagner Prigozhin yuko Urusi, mtawala wa Belarus Lukashenko asema
Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin - ambaye aliongoza uasi wa kutumia silaha kwa muda mfupi nchini Urusi mwezi uliopita - yuko Urusi, kiongozi wa muda mrefu wa Belarus Alexander Lukashenko anasema.
Moja kwa moja
Ghana: Watu wanaopigania haki za LGBT wanaweza kufungwa jela hadi miaka 10

Chanzo cha picha, Getty Images
Bunge nchini Ghana limeunga mkono pendekezo la marekebisho ya mswada dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambao utafanya kuwatambua watu wa jinsia moja kuadhibiwa kwa kifungo cha miaka mitatu jela.
Watu wanaofanya kampeni ya haki za LGBT pia wanaweza kufungwa jela hadi miaka 10.
Marekebisho hayo yaliungwa mkono na kundi la wabunge wa vyama mbalimbali, lakini yatachunguzwa tena kabla ya kuwa sheria.
Mapenzi ya jinsia moja tayari ni haramu nchini Ghana.
Sheria iliyopendekezwa imekabiliwa na lawama ndani na nje ya nchi.
Wakosoaji wanasema inakiuka haki zilizohakikishwa katika katiba ya Ghana.
Wanaounga mkono mswada huo wanasema itasaidia kuhifadhi maadili ya Ghana.
Kesi nyingi pia zimewasilishwa kupinga mswada huo katika mahakama za nchi hiyo.
Soma zaidi:
Cesar Azpilicueta: Nahodha wa Chelsea aondoka baada ya kuichezea miaka 11

Chanzo cha picha, BBC News
Maelezo ya picha, Nahodha wa Chelsea Cezar Azpilicueta Nahodha wa Chelsea Cesar Azpilicueta amemaliza miaka 11 akiwa na klabu hiyo na anatarajiwa kujiunga na Atletico Madrid.
Beki huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 33 alijipatia sifa kila iliohitajika katika uwanja wa Stamford Bridge, ikiwa ni pamoja na mataji mawili ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa.
Azpilicueta alikuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake Chelsea.
"Ni vigumu kueleza jinsi ninavyohisi, ni ajabu," alisema.
Katika video ya mtandao wa kijamii iliyotumwa na klabu hiyo, Azpilicueta aliyekuwa akibubujikwa na machozi aliongeza: "Ninahisi nilitoa kila kitu. Naipenda.
"Nadhani itakuwa wazi sana kuchagua wakati bora zaidi wa maisha yangu, tuliposhinda Ligi ya Mabingwa huko Porto. Lilikuwa kombe langu la kwanza kama nahodha.
"Chelsea ni nyumbani kwangu, itakuwa hivyo kila wakati na natumai ninaweza kurejea katika nafasi tofauti."
Azpilicueta alianza na klabu ya utotoni ya Osasuna na akakaa miaka miwili Marseille kabla ya kukamilisha uhamisho wa £6.5m kwenda Chelsea mnamo Agosti 2012.
Wakenya wakamatwa kwa madai ya kuwavua nguo wafanyakazi wa kike kuangalia ni nani alikuwa kwenye hedhi

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu watatu wanaofanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza chakula nchini Kenya wamekamatwa kufuatia madai ya kuwavua nguo wafanyakazi wa kike kwa nguvu ili kuangalia ni nani alikuwa kwenye hedhi, vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti.
Katika taarifa kwenye tovuti ya Brown's Food Company ilisema "imesikitishwa" na kwamba suala hilo "haliakisi taratibu za kampuni kwa ujumla".
Tukio hilo, ambalo linadaiwa kutokea tarehe 4 Julai, lilisambaa kwa umma baada ya Seneta Gloria Owoba kuitaja kampuni hiyo kwenye ujumbe wa Facebook, kwa kuaibisha wanawake wakati wa hedhi na unyanyasaji wa kijinsia.
Kulingana na ujumbe huo, afisa mkuu wa kampuni ya Brown's anasemekana kupata taulo ya hedhi kwenye pipa lisilo sahihi.
Kisha afisa huyo alishtumiwa kwa kuwaita wafanyakazi wa kike wa idara hiyo na kuwataka kukiri kisa hicho.
Baada ya majaribio ya wanawake kukiri kutofaulu, afisa huyo mkuu anadaiwa kuwataka wanawake hao kuvua nguo ili kuonyesha ni nani alikuwa kwenye hedhi, Seneta Owoba alisema kwenye ujumbe huo.
Kampuni ya Brown's ilisema imemsimamisha kazi mshtakiwa "kusubiri uchunguzi".
Soma zaidi:
Wanne wauawa Lviv wakati shambulizi ya Urusi likipiga jengo la ghorofa Ukraine

Chanzo cha picha, Reuters
Takriban watu wanne, wakiwemo wanawake wawili wenye umri wa miaka 21 na 95, wameuawa baada ya roketi ya Urusi kupiga jengo la ghorofa huko Lviv, magharibi mwa Ukraine.
Watu wengine 34 walijeruhiwa katika shambulio ambalo meya wa Lviv alilitaja kuwa "mojawapo ya mashambulizi makubwa" kwenye miundombinu ya raia wa jiji hilo.
Mkuu wa mkoa wa Lviv Maksym Kozytskyi alisema zaidi ya nyumba 30 zimeharibiwa.
Jeshi la Urusi halijazungumza lolote kuhusu shambulio hilo lililoripotiwa.
Rais Volodymyr Zelensky aliapa kutoa jibu la "dhahiri" kwa shambulio lililotokea usiku ambalo limetekelezwa na "magaidi wa Urusi".
Akiandika kwenye mtandao wa Telegram, Bw Kozytskyi alisema: Msichana mdogo zaidi, ambaye aliuawa kwa roketi katika nyumba yake usiku wa leo huko Lviv, alikuwa na umri wa miaka 21 tu. Urusi inaua vijana wetu. Hatma yetu.
"Mtu mwenye umri mkubwa zaidi kufa alikuwa na umri wa miaka 95. Mwanamke huyo alinusurika Vita vya Pili vya Dunia, lakini kwa bahati mbaya, hakunusurika kutokana na ubaguzi wa rangi."
Bw Kozytskyi alisema huduma za dharura bado zinaendesha shughuli zake kuondoa vifusi na kuwaokoa watu wanaohofiwa kunaswa chini ya vifusi.
"Kuna makazi karibu na jengo ambalo limepigwa na kombora," aliongeza.
"Liko katika hali nzuri na lilikuwa limefunguliwa wakati wa shambulio. Lakini, ni watu watano tu waliokuwa kwenye makao hayo katika jengo lote. Inakatisha tamaa sana."
Pia unaweza kusoma:
Mataifa 12 ya Afrika kupata chanjo mpya ya malaria - WHO

Chanzo cha picha, AFP
Chanjo ya Mosquirix tayari imetumika katika majaribio.
Shirika la Afya Duniani (WHO) na washirika wake wamesema karibu dozi milioni 18 za chanjo ya kwanza ya malaria duniani itawasilishwa kwa mataifa 12 ya Afrika ifikapo 2025.
Miongoni mwao ni Malawi, Ghana na Kenya, ambapo chanjo ya Mosquirix tayari imetumika katika majaribio.
Huku mahitaji yakizidi ugavi, kipaumbele kitaenda kwa nchi zenye uhitaji mkubwa zaidi, na ambapo matokeo ya juu zaidi yatapatikana.
Msumbiji na Sudan zimetengwa kwa sababu ya viwango vyao vya juu vya kuacha chanjo.
WHO inasema chanjo hiyo - iliyotengenezwa na kampuni ya Uingereza ya GSK - inaweza kuokoa maisha ya mtu mmoja kwa kila watoto 200 wanaochanjwa.
Malaria huua takriban watoto nusu milioni wa Kiafrika chini ya miaka mitano kila mwaka.
Soma zaidi:
Afrika na Caribbean zinapaswa kukomesha mchezo wa kulaumiana – Kagame

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Rwanda Paul Kagame amehimiza kuwepo kwa uhusiano wa karibu kati ya nchi za Caribbean na nchi za Afrika katika mkutano wa 45 wa Jumuiya ya Karibea (Caricom) huko Trinidad na Tobago, na kuzitaka kanda zote mbili kuacha kulaumu wengine kwa matatizo yao.
"Hatupaswi kufurahia kuwalaumu wengine kwa matatizo yetu, ikiwa ni pamoja na madhara tunayojiletea wenyewe," Rais Kagame alisema.
"Jambo la kuanzia hapa ni jinsi tunavyotawala nchi zetu binafsi, tukijitahidi kuwa bora tuwezavyo, tukiwa na utamaduni wa uwajibikaji," aliongeza katika taarifa.
"Tunahitaji kuja pamoja katika hali halisi na kuzingatia mipango madhubuti ambayo inashughulikia changamoto ambazo mataifa kama yetu yanakabiliana nayo leo," Bw Kagame alisema.
Alisisitiza kwamba kanda zote mbili zinahitaji kutetea masharti ya kukopa zaidi wakati nchi zinahitaji kuchukua mikopo na ushirikiano mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Pia alizungumza kuhusu fursa kwa mikoa yote miwili kuboresha muunganisho linapokuja suala la "usafiri na mawasiliano".
Pia aliitaja Haiti, ambayo Rwanda imesema hapo awali ilikuwa tayari kuunga mkono katika masuala ya usalama na ulinzi wa amani, kwa mujibu wa Miami Herald.
Rais Kagame alisema nchi yake "haiwezi kunyamaza" na kwamba historia yenye uchungu ya Rwanda inaonyesha kwamba "hakuna kitu kisichoweza kurekebishwa".
Haiti imeingia katika ongezeko la uvunjaji sheria tangu kuuawa kwa Rais Jovenel Moïse mnamo Julai 2021.
Je mtandao wa Threads, unaweza kusababisha matatizo kwa Twitter

Chanzo cha picha, Reuters
Taswira ya Kwanza ya Threads: Meta inaweza kufanya hivi?
Je, huu si kwa namna fulani wizi?
Programu inaonekana karibu sawa na Twitter.
Kikomo cha herufi unazoweza kuandika, kutuma tena na mrejesho. Yote yanafahamika.
Mark Zuckerberg anadai mamilioni ya watu wamejiandikisha katika saa chache za kwanza.
Unapaswa kuwa na shaka kila wakati bosi wa teknolojia anaposema ni watumiaji wangapi wamejisajili kwenye jukwaa la mtandao.
Lakini inahisi kama watu wengi tayari wako kwenye mtandao huo.
Hiyo ni kwa sababu imeunganishwa kwenye Instagram.
Ikiwa tayari uko kwenye Instagram, unapewa chaguo la "kufuata" wafuasi wako wote wa Instagram unapojiandikisha.
Chaguo linakupa orodha ya wafuasi iliyotengenezwa tayari, lakini pia inamaanisha kuwa unaweza kupata wafuasi marafiki wako wa Instagram wanapojisajili.
Hili ni jambo la busara kutoka kwa Bw Zuckerberg, na kwa nini kampuni za kubwa za teknolojia zina faida kubwa ikilinganishwa na ndogo.
Meta haiundi programu kutoka mwanzo.
Inanufaika kutoka kwa wafuasi mabilioni kadhaa pamoja na Instagram ambao wanaifuata.
Majukwaa kama Bluesky na Mastodon hayakuwa na vitu kama hivi ambavyo tayari vilikuwa mkononi mwao.
Walianza na watumiaji sifuri.
Pia unaweza kusoma:
Kylian Mbappe 'anahitaji kusaini mkataba mpya ili kusalia PSG' - rais wa PSG

Chanzo cha picha, Getty Images
Kylian Mbappe lazima asaini mkataba mpya ikiwa anataka kusalia Paris St-Germain, rais wa klabu Nasser Al-Khelaifi anasema.
Al-Khelaifi alikuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kumtambulisha Luis Enrique kama meneja mpya wa PSG baada ya kutimuliwa kwa Christophe Galtier.
Mshambulizi wa Ufaransa Mbappe, 24, ameiambia PSG kwamba hataongeza mkataba wake nao zaidi ya 2024.
"Msimamo wetu uko wazi," alisema Al-Khelaifi.
"Ikiwa Kylian Mbappe anataka kubaki - tunataka abaki - anahitaji kusaini mkataba mpya.
"Hatuwezi kuruhusu mchezaji bora zaidi duniani hivi sasa kuondoka bure. Hilo haliwezekani.
Pia unaweza kusoma:
Mkuu wa Wagner Prigozhin yuko Urusi, mtawala wa Belarus Lukashenko asema

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mkuu wa Wagner Prighozin Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin - ambaye aliongoza uasi wa kutumia silaha kwa muda mfupi nchini Urusi mwezi uliopita - yuko Urusi, kiongozi wa muda mrefu wa Belarus Alexander Lukashenko anasema.
Mahali alipo Prigozhin imekuwa kitendawili tangu alipoonekana kusini mwa Urusi wakati wa maasi.
Chini ya makubaliano ya kumaliza uasi, mashtaka dhidi ya Prigozhin yalifutwa na aliruhusiwa kuhamia Belarusi.
Bw Lukashenko alisaidia maajenti wa mpango huo kukomesha uasi huo.
Zaidi ya wiki moja iliyopita Bw Lukashenko, ambaye ametawala Belarus tangu 1994 na anafikiriwa kuwa aliiba uchaguzi wa 2020 ili kuendelea kuongoza , alisema Prigozhin alikuwa amewasili Belarus.
Lakini siku ya Alhamisi Bw Lukashenko aliwaambia waandishi wa habari: "Kuhusu Prigozhin, yuko St Petersburg. Hayuko katika eneo la Belarus."
BBC ilifuatilia ndege ya kibinafsi ya Prigozhin iliyokuwa ikiruka hadi Belarus mwishoni mwa Juni, na kurejea Urusi jioni hiyo hiyo.
Tangu wakati huo imefanya safari kadhaa za ndege kati ya St Petersburg na Moscow - ingawa haijulikani wazi ikiwa Prigozhin amekuwa kwenye ndege. BBC pia haiwezi kuthibitisha madai ya Bw Lukashenko kuhusu eneo aliko kiongozi huyo wa Wagner.
Siku ya Alhamisi Bw Lukashenko aliongeza kuwa "nijuavyo" wapiganaji wengine wa Wagner bado walikuwa kwenye ngome zao - ambazo zinaweza kujumuisha mashariki mwa Ukraine au kituo cha mafunzo katika mkoa wa Krasnodar nchini Urusi.
Kiongozi wa Belarus amesema pendekezo la Wagner kuwaweka wapiganaji wake huko Belarusi – ni suala ambalo limezitia wasiwasi nchi jirani za Nato
Bw Lukashenko alisema haoni kuwa ni hatari kwa Belarus na haamini kwamba wapiganaji wa Wagner wangeweza kuchukua silaha dhidi ya nchi yake.
"Sina wasiwasi kabisa na baadhi ya wapiganaji hapa, kama wanahitaji kuhamasishwa, tutafanya hivyo kwa haraka. Tutaona ujuzi wote walioupata kwenye mstari wa mbele na tutautumia kwa mafunzo yetu. ," alisema.
Kundi la Wagner ni jeshi la kibinafsi la mamluki ambalo limekuwa likipigana pamoja na jeshi la kawaida la Urusi nchini Ukraine.
Maasi ya Prigozhin yalishuhudia mamluki wa Wagner wakivuka mpaka na kuingia Urusi kutoka kambi za mashambani nchini Ukraine na kuingia katika mji wa kusini wa Rostov-on-Don, wakichukua amri ya baadhi ya vituo vya usalama.
Wapiganaji wa Wagner kisha walisafiri kuelekea Moscow, na kusababisha Kremlin kuanzisha ulinzi mkali katika mikoa mingi, ikiwa ni pamoja na mji mkuu.
Vladimir Putin alishutumu kundi hilo kwa uhaini, lakini chini ya mpango huo uliokomesha maasi hayo, Prigozhin aliahidiwa usalama na kesi ya jinai ya Urusi dhidi ya Wagner ikatupiliwa mbali.
Wapiganaji wake waliambiwa wanaweza kusaini kandarasi za kawaida za jeshi, kwenda nyumbani au kuelekea Belarus.
Roketi ya Ariane-5 ya Ulaya yakamilisha uzinduzi wa mwisho

Maelezo ya picha, Roketi ya mwisho ya Ariane-5 barani Ulaya ililipuka Gari hilo, ambalo limesaidia bara la Afrika kufikia angani kwa takriban miongo mitatu, lilimaliza kazi yake kwa kuchukua satelaiti mbili za mawasiliano ya simu.
Inakubaliwa kwa ujumla kuwa kizindua kilichofanikiwa sana, baada ya kupata hitilafu mbili tu za moja kwa moja katika matembezi 117.
Lakini kustaafu kwa Ariane-5 kunaiacha Ulaya katika wakati mgumu, na hakuna mbadala aliye tayari kuchukua nafasi hiyo.
Roketi ya kizazi kijacho, Ariane-6, bado inapitia awamu ya ukuzaji na majaribio na inaweza isifanye kwanza hadi mwaka ujao.
Ulaya haiwezi tena kutumia roketi za Soyuz za Urusi, na gari lake dogo, Vega-C, limewekwa benchi kufuatia hitilafu ya ndani ya ndege Desemba mwaka jana.
Satelaiti za Ulaya zimelazimika kutumia huduma za Marekani badala yake.
Polisi wamekamata bangi yenye thamani ya £130m katika msako nchini Uingereza

Chanzo cha picha, PA Media
Maelezo ya picha, Takriban mimea 182,422 ilikamatwa, yenye thamani ya wastani wa £115m-£130m. Polisi wamekamata mimea ya bangi yenye thamani ya hadi £130m na kuwakamata karibu watu 1,000 katika msako mkubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Uingereza dhidi ya uhalifu wa kupangwa.
Zaidi ya mimea 180,000 iligunduliwa katika uvamizi uliofanyika kote Uingereza na Wales mnamo Juni.
Maafisa pia walikamata bunduki 20, pesa taslimu £636,000 na kilo 20 za kokeini, zenye thamani ya mtaani ya £1m.
Operesheni hiyo imeelezewa kuwa "muhimu zaidi" ya aina yake kuwahi kutekelezwa na vyombo vya sheria vya Uingereza.
Operesheni Mille iliyalenga magenge ya uhalifu uliopangwa (OCGs) ambao pia wanahusika wako katika makosa mengine kama vile utakatishaji fedha, ulanguzi wa dawa za kulevya wa Daraja A na vurugu.
Bangi ni dawa ya Daraja B, si ya Hatari A kama heroini au kokeini, lakini kilimo kikubwa cha bangi kinaonekana kama chanzo kikuu cha mapato haramu kwa magenge ya wahalifu.

Maelezo ya picha, Polisi wa Dorset walihusika katika kutekeleza uvamizi kama sehemu ya Operesheni Mille Lengo la operesheni hiyo ya mwezi mzima lilikuwa kuvuruga OCG kwa kuchukua chanzo kikuu cha mapato yao, kuwakamata waliohusika na kukusanya taarifa za kijasusi kuhusu jinsi mitandao hiyo inavyofanya kazi.
Takriban maafisa 11,000 kutoka vikosi vyote 43 vya polisi nchini Uingereza na Wales, pamoja na Shirika la Kitaifa la Uhalifu na Utekelezaji wa Uhamiaji, waliratibu zaidi ya vibali 1,000 mwezi Juni.
Kati ya waliokamatwa, zaidi ya watu 450 wamefunguliwa mashitaka.
Coco Lee: Nyota wa Disney na mwimbaji wa pop afariki akiwa na umri wa miaka 48

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwimbaji Coco Lee, ambaye alifurahia umaarufu wa pop huko Asia katika miaka ya 1990 na 2000, amefariki akiwa na umri wa miaka 48.
Akiwa mzaliwa wa Hong Kong, Lee alihamia Marekani akiwa mtoto na akatoa albamu katika lugha za Mandarin na Kiingereza.
Pia alikuwa mhusika mkuu katika toleo la lugha ya Mandarin katika filamu maarufu ya Disney ya Mulan, na akaimba wimbo kwa sauti ya Crouching Tiger, Hidden Dragon katika Tuzo za Oscar za 2001.
Dada zake walisema alikuwa katika hali ya kukosa fahamu tangu alipofanya jaribio la kujitoa uhai mwishoni mwa juma.
Lee alikuwa akiugua mfadhaiko kwa miaka michache, dada wakubwa Carol na Nancy waliandika kwenye taarifa iiyotumwa kwenye Facebook.
Alijaribu kujiua akiwa nyumbani Jumapili na akapelekwa hospitalini, ambapo alifariki Jumatano, waliandika.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Aliigiza kwenye tuzo za Oscar za 2001 huko Hollywood Lee aliingia katika kitengo cha pop ya lugha ya Mandarin maarufu kama Mandopop mnamo 1994 na kutoa albamu mbili katika lugha ya Mandarin. Katika mwaka uliofuata, alitoa albamu ya lugha ya Kiingereza na albamu ya tatu ya Mandarin.
"Siyo tu kwamba alituletea furaha na nyimbo na dansi zake katika kipindi cha miaka 29, pia alifanya kazi kwa bidii kuwafungulia waimbaji wa Kichina katika anga ya kimataifa ya muziki na amekuwa akifanya kila awezalo kuwaangazia Wachina," dada zake Lee waliandika.
Burundi na DRC, miongoni mwa nchi 12 za Afrika zilizopewa chanjo ya malaria
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Dorcas Wangira
- Nafasi, Mwandishi wa BBC wa masuala ya Afya, Afrika

Chanzo cha picha, WHO
Dozi milioni 18 za chanjo ya kwanza ya malaria, inayojulikana kama RTS,S, imesambazwa kwa nchi 12 za Afrika - ikiwa ni pamoja na Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - katika miaka miwili ijayo.
Takriban nchi 28 za Kiafrika zimesema zinataka chanjo hiyo ya malaria, lakini ni 14 pekee ndizo zimeliandikia shirika la kimataifa la kusambaza chanjo hiyo-Gavi, kuiomba.
Ghana, Malawi na Kenya zitakuwa za kwanza kupokea dozi hizi katika muda wa miezi mitatu ya mwisho ya mwaka huu.
Takriban kila dakika barani Afrika, mtoto wa chini ya umri wa miaka 5 hufa kutokana na malaria.
Wale wanaohitaji dozi milioni 18 za kwanza za chanjo ya RTS,S wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupokea chanjo hiyo.
Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), Gavi na washirika wengine, walisema katika kutoa chanjo hiyo kwa kuzingatia nchi maskini zaidi, kunaweza kuleta mabadiliko makubwa na kwa wastani.
Nchi za Malawi, Ghana na Kenya, ambazo tayari zilikuwa zimetoa chanjo hiyo katika awamu ya majaribio kwa angalau watoto milioni 1.7, zilipokea dozi milioni 6.9 za chanjo hiyo.
Kwa mara ya kwanza, nchi nane – Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Benin, Uganda, Burkina Faso, Cameroon, Liberia na Sierra Leone – zitaanza kutoa chanjo ya malaria katika programu zao zilizopo.
Niger pia ni sehemu ya nchi zitakazopewa chanjo itakayotolewa.
Lakini Msumbiji na Sudan hazitapokea dozi zozote za chanjo hiyo, kutokana na kiwango kikubwa katika nchi hizo cha wale wanaokataa kutumia chanjo hiyo.
RTS,S ni chanjo ya kwanza kuidhinishwa kutumika dhidi ya malaria kwa watoto katika maeneo yenye maambukizi ya wastani hadi juu.
Threads: Watu milioni 10 wajiunga na Meta, hasimu wa Twitter ,asema Zuckerberg

Watumiaji milioni kumi walijiandikisha kwa programu mpya ya Meta iliyozinduliwa ya Threads katika kipindi cha saa saba tangu kuzinduliwa mkuu wa kampuni hiyo Mark Zuckerberg anasema.
Zuckerberg aliweka programu kama mpinzani "rafiki" kwa Twitter, ambayo ilinunuliwa na Elon Musk mnamo Oktoba.
Wataalamu wanasema Threads inaweza kuvutia watumiaji wa Twitter kutofurahishwa na mabadiliko ya hivi majuzi katika jukwaa hilo.
Threads - ambayo haijazinduliwa katika Umoja wa Ulaya kwa sasa - inaruhusu watumiaji kuchapisha hadi herufi 500, na ina vipengele vingi sawa na Twitter.
Katika taarifa yake, Bw Zuckerberg alisema kuwa kuweka jukwaa "rafiki... hatimaye kutakuwa ufunguo wa mafanikio yake".
Lakini mkuu wa Twitter Elon Musk alijibu: "Inapendeza sana kushambuliwa na watu wasiowajua kwenye Twitter, kuliko kujiingiza katika furaha ya uongo ya kujificha-uchungu ya Instagram."
Alipoulizwa kwenye Threads ikiwa programu hiyo itakuwa "kubwa kuliko Twitter", Bw Zuckerberg alisema: "Itachukua muda, lakini nadhani kunapaswa kuwa na programu ya mazungumzo ya umma iliyo na watu bilioni 1 na zaidi.
"Twitter imepata fursa ya kufanya hivi lakini haijahimili. Tunatumai tutaweza."
Washindani wamekosoa kiasi cha data ambacho programu inaweza kutumia.
Hii inaweza kujumuisha data za afya, fedha na kuvinjari zinazounganishwa na utambulisho wa watumiaji, kulingana na Apple App Store.
Threads sasa inapatikana katika zaidi ya nchi 100 , ikiwemo Uingereza, lakini bado haiko katika Umoja wa Ulaya kwa sababu ya masuala ya udhibiti wa mitandao ya kijamii.
Programu hiyo iliidhinisha usajili wa watu milioni mbili katika saa zake mbili za kwanza, Bw Zuckerberg amesema.
'Toleo la awali'
Meta, ambayo inamiliki Facebook na Instagram, iliita programu hiyo mpya "toleo la awali", ikiwa na vipengele vya ziada vilivyopangwa ukiwemo uwezo wa kuingiliana na watu kwenye programu nyingine za mitandao ya kijamii kama Mastodon.
"Maono yetu na Threads ni kuchukua kile ambacho Instagram hufanya vyema na kupanua maandishi," kampuni hiyo ilisema kabla ya kuzinduliwa.
Habari za hivi punde, Vita vya Ukraine: Watu wanne wauawa katika shambulio la roketi la Urusi dhidi ya Lviv, meya asema
Roketi ya Urusi imepiga jengo la ghorofa katika mji wa Lviv, magharibi mwa Ukraine, na kuua takriban watu watatu, meya wa eneo hilo amesema.
Andriy Sadovyi alisema watu wengine wanane walijeruhiwa, akiwemo mmoja vibaya. Kuna hofu kwamba huenda watu wengi zaidi wamenaswa chini ya vifusi.
Mkuu wa mkoa Maksym Kozytskyi alisema "kituo muhimu cha miundombinu" kilipigwa katika jiji hilo. Hakutoa maelezo.
Bw Sadovyi alichapisha video inayoonyesha madirisha yaliyovunjika ya jengo lililogongwa, ambalo lilionekana kuwa na orofa nne. Magari yaliyoharibiwa na vifusi vya majengo pia yalionekana kwenye picha.
"Nyumba nyingi zimeharibiwa -zaidi ya 50," meya alisema katika ujumbe mfupi wa video.
Bw Sadovyi alisema watu wawili walikuwa wametolewa kwenye vifusi muda mfupi uliopita - lakini vikundi vya uokoaji vinaendelea na msako wao.
Mengi zaidi zaidi kuhusu vita vya Ukraine:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Afrika Kusini: Watu 17 washukiwa kufariki kutokana na gesi inayoshukiwa kuvuja

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Kuna hofu kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi Uvujaji wa hewa ya gesi ya nitrate oxide nchini Afrika Kusini unashukiwa kusababisha vifo vya watu 17, maafisa wa eneo hilo wanasema.
Wengine kumi na watano wanapata matibabu hospitalini huku watatu kati yao wakiwa mahututi. Maafisa wanasema tukio hilo linahusiana na shughuli haramu katikamigodi ya dhahabu
Waathiriwa - ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto - walikufa baada ya kuvuta gesi kwenye makazi yasiyo rasmi katika eneo la Boksburg, mashariki mwa Johannesburg.
Uvujaji huo uliotokea Jumatano umehusishwa na uchimbaji haramu wa dhahabu katika eneo hilo.
Gesi ya nitrate oksidi mara nyingi hutumiwa na wachimbaji haramu wa dhahabu - wanaojulikana nchini kama zama zamas - kuchimba dhahabu kutoka kwenye udongo ulioibwa kutoka katika mashimo ya migodi yaliyotelekezwa.
Moja ya mitungi ya gesi ilipatikana ikivuja katika mji wa Angelo wenye wakazi wengi wa Boksburg.
Waathiriwa walipatikana ndani ya eneo la mita 100 (futi 328) kutoka eneo la tukio.
Hakuna mtu aliyeweza kupelekwa hospitalini, maafisa wa huduma ya dharura wameambia BBC.
Lakini wanahofia miili zaidi inaweza kupatikana huku timu za uokoaji zikiendelea na kazi yao.
Mkasa huu unakuja miezi sita tu baada ya lori la gesi kulipuka katika mkesha wa Krismasi na kusababisha vifo vya watu 41 katika mji huo huo.
Soma zaidi:
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo ikiwa ni tarehe 06.07.2023

