Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 06.07.2023

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mlinda lango wa Inter Milan raia wa Cameroon Andre Onana, 2
Iliyochapishwa

Manchester United wanatayarisha dau la pauni milioni 39 kwa ajili ya mlinda mlango wa Inter Milan raia wa Cameroon Andre Onana, 27. (Fabrizio Romano)

Chelsea wanatayarisha ofa ya pauni milioni milioni 85 kwa kiungo wa kati wa Brighton wa Ecuador Moises Caicedo, 21. (Diego Arcos, via Football.London)

Harry Kane

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham wamempa mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 29, ofa ambayo itaboresha sana mshahara wake wa sasa wa pauni elfu 200 kwa wiki akiamua kubaki katika klabu hiyo. (Guadian)

Kocha wa Bayern Munich Thomas Tuchel amekutana na Kane nyumbani kwake huku klabu hiyo ya Ujerumani ikijaribu kumsajili mchezaji huyo. (Bild, via Mail)

AC Milan wamewasilisha ofa iliyoboreshwa ya pauni milioni 24 kwa ajili ya winga wa Chelsea na Marekani Christian Pulisic, 24. (Mail).

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal wamefikia mkataba wa £38.5m na Ajax kwa ajili ya beki wa Uholanzi Jurrien Timber, 22. (Standard)

The Gunners watatumia hadi karibu pauni milioni 200 ya bajeti yao ya majira ya joto baada ya kuafikiana na Timber na kiungo wa kati wa West Ham wa Uingereza Declan Rice, 24. (Telegraph)

Ajax defender Jurrien Timber

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mlinziwa Ajax Jurrien Timber.

Newcastle wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Leicester City na Uingereza Harvey Barnes, 25, huku Aston Villa na Tottenham pia zikiwania. (Guadian)

The Blues pia wanavutiwa na kiungo wa kati wa Southampton raia wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19. (Sky Sports).

Mount

Chanzo cha picha, Machester United

Maelezo ya picha, Mount amesaini mkataba wa miaka mitano na Manchester United

Mchezaji mpya wa Manchester United Mason Mount, 24, alikataa ofa ya £200k kwa wiki kutoka kwa Chelsea kujaribu kumbakisha kiungo huyo wa kati wa Uingereza Stamford Bridge mwezi Februari. (Athletic - Usajili unahitajika)

Aston Villa na Everton ni miongoni mwa klabu za Ligi Kuu ya Uingereza zinazomtaka mshambulizi wa Leeds United na Italia Wilfried Gnonto, 19. (Football Insider)

Liverpool bado wanavutiwa na beki wa Uingereza Levi Colwill, 20, ambaye Chelsea bado wanahitaji huduma zake. (Football.London)