Mkuu wa jeshi la Sudan azuia akaunti za benki za mpinzani wake wa RSF

Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametoa agizo la kufungia akaunti za benki za kundi la wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) na kampuni zake tanzu.

Moja kwa moja

  1. Sudan mwezi mmoja baadaye, hali bado inatisha

      • Author, Caro Robi
      • Nafasi, BBC Swahili

    Umoja wa Mataifa unasema vita vya Sudan ambavyo vimedumu kwa mwezi sasa vimesababisha takriban watu milioni moja kuyahama makazi yao. Wengi wao wakisalia ndani ya nchi hiyo.

    Licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa kati ya jeshi na kikosi maalum cha wanamgambo cha Rapid Support Forces RSF, pande hizo mbili zimeendelea kupigana hata katika maeneo ya makazi katika mji mkuu Khartoum.

    Mapigano hayo yamesababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu Sudan. Maafisa wa Sudan wamekuwa wakikutana na wajumbe wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kujadili namna ya kuudhibiti mzozo huo na jinsi ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwa waathiriwa wa vita hivyo.

    Mnamo tarehe 15 Aprili 2023,mzozo kati ya Jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na kikosi maalumu cha wanamgambo wa kikosi maalum cha RSF kinachoongozwa na Mohamed Hamdan Daglo ulitibuka kuwa vita,ukianzia katika kitovu cha nchi hiyo,jijini Khartoum.

    Mji huo wa takriban watu milioni tano uligeuka kuwa uwanja wa mapambano,milio ya risasi ikirindima na mabomu yakifyatuliwa kila kona. Hospitali,benki,maduka na maghala ya chakula yaliporwa na kuharibiwa.

    Wafanyakazi wa kutoa misaada walishambuliwa na wengine hata kuuuawa.Nchi za kigeni zilikimbia kuwaondoa raia wao. Mzozo wa Sudan umesababisha vifo vya takriban watu mia saba,maelfu wamejeruhiwa na takriban watu milioni moja kuachwa bila ya makazi ndani ya nchi huku wengine wakikimbilia nchi jirani zikiwemo Sudan Kusini,Ethiopia,Chad na Misri.

    Upatikanaji wa bidhaa za kimsingi ni tabu na bei za vyakula na mafuta zimeongezeka maradufu. Makubaliano ya kusitisha vita hivyo yamefikiwa mara chungu nzima lakini yamekiukwa hata kabla wino ulioandikia makubaliano hayo kukauka na hivyo kudidimiza matumaini ya kupatikana suluhu la mzozo huo hivi karibuni.

    Umoja wa Mataifa,Umoja wa Afrika,Marekani,nchi za kiarabu zikiongozwa na Saudi Arabia zote zimejaribu kuwa mpatanishi katika mzozo huu wa Sudan lakini bado pande zote mbili zikikataa kulegeza kamba.

    Na kwa nchi ambayo tayari ilikuwa katika msukosuko wa kisiasa tangu kupinduliwa madarakani kwa Rais Omar Bashir na jeshi na maeneo kama Darfur yakikumbwa na mzozo wa kibinadamu kwa miongo kadhaa,mashaka ni mengi kuliko matumaini Sudan.

  2. Makanali wawili wa Urusi wauawa katika vita Bakhmut - Urusi

    ,
    Maelezo ya picha, Mwanajeshi akipiga darubini katika mstari wa mbele wa vita Ukraine

    Wakati wa vita karibu na kijiji cha Krasnoe, kamanda wa brigade ya 4 ya gari lenye bunduki , Kanali Vyacheslav Makarov, aliuawa, kulingana na mashirika ya habari ya Urusi, yakitoa taarifa ya Wizara ya Ulinzi.

    Taarifa za Wizara ya Ulinzi ya Urusi mara nyingi huwa na majina ya Soviet kwa maeneo, ambayo baadaye yalibadilishwa na mamlaka ya Ukraine. Bakhmut, kwa mfano, huko Moscow inaitwa Artemovsky.

    "Vyacheslav Makarov, akiwa mstari wa mbele, aliongoza vita binafsi. Mashambulizi mawili ya adui yalikabiliwa .

    Wakati wanejshi wa Urusi wakitafakari shambulio la tatu, kamanda wa kikosi alijeruhiwa vibaya na alikufa wakati akihamishwa kutoka mstari wa mbele," RIA Novosti ilinukuu ujumbe kutoka kwa wizara.

    Kwa kuongezea, kulingana na Wizara ya Ulinzi, Kanali Yevgeny Brovko, naibu kamanda wa jeshi alikufa katika vita hivyo hivyo.

    Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ripoti nyingi za mashambulizi ya kukabiliana na Wanajeshi wa Ukraine katika eneo la Bakhmut.

    Wachambuzi wa Taasisi ya Marekani ya Utafiti wa Vita (ISW) waliandika kuhusu hili katika ripoti yao ya kila siku, na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Anna Malyar alizungumza kuhusu hili Jumamosi.

    Mkuu wa Wagner PMC Yevgeny Prigozhin, ambaye vitengo vyake vinajaribu kuchukua Bakhmut, pia hivi karibuni alisema kuwa vikosi vya Ukraine viliweza kurejesha udhibiti wa sehemu ya eneo kando karibu na mji.

  3. Bei ya Mafuta Kenya yapanda

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Bei ya mafuta yapanda kenya

    Wakenya wataanza kulipa bei ya juu kwa bidhaa tatu za petroli kuanzia Jumatatu, Mei 15, katika ukaguzi wa hivi punde wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA).

    Katika taarifa yake Jumapili, Mkurugenzi Mkuu wa EPRA Daniel Bargoria alisema kuwa ongezeko hilo limechangiwa na wastani wa gharama ya bidhaa za petroli iliyosafishwa kutoka nje ambayo imesababisha gharama ya kutua kwa uagizaji huo kutofautiana kwa bei.

    Gharama ya kutua kwa Super Petrol iliongezeka kwa 8.63% Machi 2023, Dizeli ilipungua kwa 2.51% huku Mafuta ya Taa nayo yakishuka hadi 1.13%.

    Hii itapelekea Super Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa kuongezeka kwa Ksh.3.40 kwa lita, Ksh.6.40 kwa lita na Ksh.15.19 kwa lita mtawalia, ukaguzi ambao utaanza kutumika hadi Juni 14, 2023.

    Marekebisho ya juu ya gharama ya bidhaa zote tatu za mafuta sasa yanatuma gharama ya petroli katika Jiji la Nairobi hadi Ksh.182.70 kwa bei ya Petroli kwa lita, huku Dizeli na Mafuta ya Taa yakipanda hadi Ksh.168.40 na Ksh.161.13 mtawalia.

    Tayari serikali imeondoa ruzuku ya Dizeli na Mafuta ya Taa

    Bargoria aliongeza kuwa bei hizo ni pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani ya 8% (VAT) kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Fedha ya 2018, Sheria ya Kodi (Marekebisho) ya Sheria ya 2020 na viwango vilivyorekebishwa vya Ushuru wa Bidhaa vilivyorekebishwa kwa mfumuko wa bei kulingana na Ilani ya Kisheria nambari 194 ya 2020.

  4. Kamanda wa NATO : Jeshi la Urusi bado liko imara

    .

    Chanzo cha picha, Anadolu

    Vikosi vya kijeshi vya Urusi vimesalia kuwa kikosi kilicho tayari kupambana licha ya hasara kubwa nchini Ukraine, kwa mujibu wa Jenerali Christopher Cavoli, Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Washirika wa NATO barani Ulaya.

    Alisema hayo alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa Lennart Meri, ambao ulifanyika Tallinn Jumamosi na Jumapili.

    Kwa mujibu wa jenerali huyo wa Marekani, wale wanaoamini kwamba Urusi imemaliza nguvu zake katika vita vya Ukraine wamekosea sana.

    "Ni rahisi sana kuamua kwamba wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine wameshindwa kweli, lakini ukweli sio rahisi sana. Ndio, vikosi vya ardhini vina shida kubwa. Walipoteza wanajeshi wengi, silaha nyingi za kijeshi. Lakini kwa upande mwingine, vikosi vya ardhini vya Urusi ni vikubwa kuliko vile vilivyokuwa mwanzoni mwa vita [akimaanisha uvamizi wa Februari 2022].

    Kulingana na jenerali huyo, [NATO] inahitaji kuwa tayari kukabiliana na jeshi la Urusi katika maeneo yote. Aidha, utayari huu, kulingana na yeye, unapaswa kuwa mara kwa mara na kuendelea.

    Christopher Cavoli alibainisha kuwa nchi nyingi za Muungano zinaelewa haja ya kuongeza uwezo wao wa ulinzi katika suala hili.

  5. Matokeo ya hivi punde yanaonesha Erdogan anaongoza, lakini kwa chini ya 50%

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kufikia sasa zaidi ya 95% ya masanduku ya kura yamehesabiwa, kulingana na mashirika yote makuu ya habari.

    Shirika la serikali AA linasema Erdogan ana 49.52% ya kura, Kilicdaroglu anafuatia kwa 44.76%.

    Ankara inatoa nambari sawa: Erdogan ana 49.29% hadi sasa wakati Kilicdaroglu ana 45.01%.

    Kama ambavyo tumekuwa tukiripoti, ikiwa hakunaanayeweza kupata 50%, kutakuwa na duru ya pili ya uchaguzi .

    Bado kuna kura milioni chache kuhesabiwa.

    Tunatarajia kusikia matokeo ya mwisho kutoka kwa Baraza Kuu la Uchaguzi, lakini hatujui ni lini hilo litafanyika.

  6. Vita vya Ukraine: Kyiv haishambulii eneo la Urusi - Zelensky

    g

    Chanzo cha picha, EFE

    Maelezo ya picha, Kansela Chancellor Scholz (kulia ) aliahidi kumsaidia Rais Zelensky (kushoto) na Ukraine "kwa kipindi chote ambacho itakuwa muhimu kufanya hivyo"

    Ukraine haina mipango ya kupiga maeneo ya Urusi, Rais Volodymyr Zelensky amesema nchini Ujerumani, ambako Kyiv imepata msaada mpya wa ulinzi.

    ''Hatushambulii eneo la Urusi,"alisema baada ya mazungumzo mjini na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.

    ''Tunaandaa shambulio la kukabiliana na mashambuliziili kuyarejesha maeneo yaliyonyakuliwa kinyume cha sheria,"Bw Zelensky aliongeza.

    Bw Scholz aliapa kuiunga mkono Ukraine "kwa muda ambao itakuwa muhimu kufanya hivyo",akiahidi kutoa msaada wa thamani ya Euro bilioni 2.7 (£2.4bn) wa silaha.

    Msaada huu unajumuisha vifaru vya Ujerumani vya Leopard na mifumo mingine ya kukabiliana na mashambulio ya anga ili kuilinda Ukraine na makombora ya karibu kila siku ya masafa yanayorushwa na pamoja na yale ya droni.

    Rais Zelensky ameuelezea msaaada mpya uliotelewa awamu hii ni Ujerumani kama ‘’mkubwa zaidi tangu kuanza kwa vita kamili vya uchokozi’’ vya Urusi dhidi yake mwezi Februari, 2022.

    Urusi na Ukraine: Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  7. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 15.05.2023