Mama wa
mwanaume mweusi mwenye umri wa miaka 28 ambaye alifariki akiwa katika mahabusu ya
polisi anasema video ya dakika 12 inayoonyesha tukio la mauaji yake inayo "
sumbua na kutia kiwewe" na kisa hicho ni "ukatili".
Polisi saba wa cheo cha sheriff wa Virginia wameshitakiwa kwa mauaji ya daraja cha pili kuhusiana na kifo cha mwanaume huyo anayefahamika kama Irvo Otieno.
Waendesha mashitaka Alhamisi pia
walitangaza mashitaka zaidi ya mauaji ya daraja la pili dhidi ya wafanyakazi watatu
wa hospitali.
Wakili Crump alisema, katika
video Otieno alionekana "akizuiliwa kwa ukatili mkubwa, huku akishindiliwa
chini kwa goti kwenye shingo lake , akiwekewa uzito wa watu saba mwilini mwake,
huku uso wake ukiangalia chini, akiwa amefungwa pingu."
Bw Crump amefananisha kisa cha Bw Otieno na
tukio la George Floyd, Mmarekani mwingine mweusi aliyeuliwa kikatili na polisi.
Bw Otieno alifariki tarehe 6 Machi wakati
alipokuwa akihamishwa kutoka gereza kupelekwa katika kituo cha afya cha watu wenye
matatizo ya akili.
Ripoti ya awali inaonyesha kuwa uchunguzi
wa kimatibabu ulionyesha kuwa alifariki kwa - kukosa hewa, walisema waendeshamashitaka.
Polisi saba wa Kaunti ya Henrico wameshutumiwa
na waendeshamashitaka kwa kumuua Bw Otieno kwa kumkosesha hewa ya kupumua, wakati walipokuwa wakimhamisha.
Waendeshamashitaka wanasema ushahidi zaidi
uliwawezesha pia kuwashitaki wafanyakazi wa hospitali katika Hospitali ya -Central
State Hospital, ambako Bw Otieno alikuwa akihamishiwa.
Video ya tukio ilinaswa na kamera za
usalama, na ilitazamwa Alhamisi na wakili maarufu wa haki za binadamu Ben Crump pamoja na familia ya Bw
Otieno.
Mama yake Otieno, Caroline Ouko, na Bw Crump kwa pamoja
walisema kuwa alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kiakili , na amekuwa akipata
matibabu ya kiakili, lakini hakuweza kuendelea kumeza dawa hizo akiwa gerezani.
Familia ya Otieno ambayo
ilitoka Kenya na kuhamia Marekani alipokuwa na umri wa miaka minne. Bw Otieno alikuwa
na ndoto ya kuwa mwanamuziki na mwanamichezo, walisema, na alikuwa akiandika na
kurekodi muziki wakat iwa muda wake wa ziada