Rais Xi wa China kukutana na Putin mjini Moscow wiki ijayo

Rais wa China Xi Jinping atasafiri hadi Moscow wiki ijayo kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin, maafisa wanasema.

Moja kwa moja

  1. Rais Samia amkumbuka mtangulizi wake John Pombe Magufuli

    .

    Chanzo cha picha, Ikulu ya Rais Tanzania

    Maelezo ya picha, Rais Samia

    Huku Watanzania wakimuenzi rais wa awamu ya tano marehemu John Pombe Magufuli miaka miwili tangu alipoaga dunia, Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa miongoni mwao.

    Katika chapisho lake la mtandao wa Twitter , rais Samia alimuenzi mtangulizi wake akisema: ‘Leo ni miaka miwili tangu tuondokewe na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.Mwenyezi Mungu aendelee kumpa pumziko jema na aendelee kuwatia nguvu wanafamilia wote. Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kumuenzi kwa kuendeleza mazuri aliyoyaanzisha’.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  2. Upofu na majeraha viliripotiwa baada ya Marekani kutaka kurejeshwa kwa dawa ya macho

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maafisa wa afya wa Marekani wanasema kuwa dawa ya macho kuna uwezekano kuwa imemuua mtu mmoja na kuwajeruhi vibaya wengine kadhaa kutokana na kushindwa kwake kukabili bakteria ambao wanastahili kufa baada ya kutumia dawa hiyo.

    Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) vimegundua wagonjwa 68 katika majimbo 16 walio na aina adimu ya Pseudomonas aeruginosa.

    Aina hiyo ya bakteria haijawahi kupatikana nchini Marekani kabla ya mlipuko huu wa hivi karibuni.

    Mbali na kifo kimoja, wagonjwa wanane wamepoteza uwezo wa kuona, na wanne wametolewa macho kwa upasuaji.

    Wagonjwa wengi waliogunduliwa na maambukizi waliripoti kutumia matone ya dawa hiyo ya macho, kulingana na CDC.

    Chapa kumi tofauti za dawa hiyo zilitambuliwa hapo awali kama zinaweza kuhusishwa na mlipuko huo, CDC ilisema.

    Dawa ya macho ya matone ambayo yanatengenezwa India na kuletwa Marekani chini ya chapa mbili baadaye zilitolewa kwenye rafu za manunuzi mnamo Januari na Februari.

    Mnamo Januari, CDC ilionya watu kuacha kutumia Machozi Bandia ya EzriCare na Machozi Bandia ya Delsam Pharma kwasababu inasemekana pia hilo linachangia katika hali kama hizo.

  3. Rais Xi wa China kukutana na Putin mjini Moscow wiki ijayo

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa China Xi Jinping atasafiri hadi Moscow wiki ijayo kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin, maafisa wanasema.

    Kremlin ilisema watajadili "ushirikiano wa kina na ushirikiano wa kimkakati".

    Ziara hiyo inajiri huku Beijing, mshirika wa Urusi, ikitoa mapendekezo ya kumaliza vita nchini Ukraine, ambapo nchi za Magharibi zilionyesha kutoshabikia mapokezo hayo.

    Nchi za Magharibi zimeionya Beijing dhidi ya kuipatia Moscow silaha.

    Hii itakuwa ziara ya kwanza ya rais Xi nchini Urusi tangu wanajeshi wa Urusi kuivamia Ukraine.

    Anatarajiwa kula chakula cha mchana na Bw Putin siku ya Jumatatu na kufuatiwa na mazungumzo siku ya Jumanne.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje alisema China itashikilia "msimamo wenye lengo na haki" kuhusu vita vya Ukraine na "kuchukua jukumu la kuhakikisha tija kukuza mazungumzo ya amani".

    Ukweli ni kwamba ziara ya kiongozi wa China inaashiria uungaji mkono mkubwa wa Beijing kwa Moscow.

    Hakuna linaloshangaza kuhusu hilo: Putin na Xi wana maoni sawa kuhusu ulimwengu, wote wanakumbatia wazo la ulimwengu wenye nchi zinazoonekana kuwa sawa.

    Mwaka jana watu hao wawili walitangaza ushirikiano wao hauna kikomo. Hiyo si kweli kabisa.

    Mwaka jana watu hao wawili walitangaza ushirikiano wao hauna kikomo.

    Hiyo si kweli kabisa.

    Hadi kufikia sasa, China haijaipatia Urusi misaada hatari ili kuisaidia kushinda vita vya Ukraine, ingawa Marekani inadai kuwa China inafikiria kufanya hivyo.

    Pia unaweza kusoma:

  4. Uranium ya Libya: Mapipa yaliyokosekana yapatikana - vikosi vya mashariki

    .

    Chanzo cha picha, LNA

    Vikosi vya kijeshi mashariki mwa Libya vinasema kuwa wamepata takriban tani mbili na nusu za madini ya urani yaani uranium ambayo yaliripotiwa kutoweka na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki.

    Mapipa kumi yenye madini hayo yalipatikana karibu na mpaka na Chad, alisema mkuu wa kitengo cha vyombo vya habari vya vikosi hivyo.

    IAEA ilisema "inafanya kazi kikamilifu ili kuthibitisha" ripoti za vyombo vya habari.

    Shirika hilo lilipiga yamgambo baada ya ziara ya wakaguzi wake mapema wiki hii kwenye tovuti ambayo haijatajwa

    Eneo hilo halikuwa katika eneo linalodhibitiwa na serikali.

    Uranium ni kipengele kinachotokea kawaida ambacho kinaweza kuwa na matumizi yanayohusiana na nyuklia mara tu kitakaposafishwa, au kurutubishwa.

    Uranium ambayo ilitoweka haiwezi kufanywa kuwa silaha ya nyuklia katika hali yake ya sasa, lakini inaweza kutumika kama malighafi ya mpango wa silaha za nyuklia, wataalam waliiambia BBC.

    Mnamo Desemba 2003, chini ya mtawala wa wakati huo wa kijeshi Kanali Muammar Gaddafi, Libya iliachana hadharani na silaha za nyuklia, kibayolojia na kemikali.

  5. Patrick Vieira: Crystal Palace yamfuta kazi meneja baada ya kushindwa mechi 12

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Nahodha wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira alichukua nafasi ya Roy Hodgson huko Crystal Palace mnamo Julai 2021.

    Crystal Palace imemfuta kazi meneja Patrick Vieira baada ya kucheza mechi 12 na kutoka bila kushinda yoyote.

    Palace hawajashinda mechi yoyote mwaka wa 2023 na walichapwa 1-0 na Brighton kwenye Ligi ya Premia Jumatano, kikiwa ni kipigo chao cha tatu mfululizo.

    Wako nafasi ya 12 kwenye jedwali lakini wako pointi tatu pekee juu ya Bournemouth walio katika nafasi ya 18, ambao wana mchezo unaowasubiri.

    "Ni kwa masikitiko makubwa kwamba uamuzi huu mgumu umefanywa," mwenyekiti Steve Parish alisema.

    "Hatimaye, matokeo ya miezi ya hivi karibuni yametuweka katika hali mbaya ya ligi na tuliona mabadiliko ni muhimu ili kutupa nafasi nzuri zaidi ya kubaki na hadhi ya Ligi Kuu.

    "Mfaransa Vieira, 46, aliteuliwa kabla ya kuanza kwa msimu wa 2021-22 na kuiongoza Eagles kumaliza katika nafasi ya 12, na kujipatia sifa kwa mtindo wa kushambulia.

    Hata hivyo, msimu huu wamefunga mabao 21 pekee katika mechi 27 - ni Wolves, Everton na Southampton walio mkiani mwa jedwali.

    Kabla ya kushindwa na Brighton, Palace walikuwa wamecheza mechi tatu mfululizo bila shuti lililolenga lango.

    Hakuna timu ya Premier League iliyoshinda pointi chache zaidi mwaka wa 2023 kuliko Palace.

    Wanachama watatu wa makocha wa Vieira - Osian Roberts, Kristian Wilson na Said Aigoun - pia wameiacha klabu hiyo na mchakato wa kumteua meneja mpya unaendelea.

    Alama tano pekee zinatenganisha vilabu tisa vilivyo chini ya Premier League kuelekea miezi ya mwisho ya msimu.

    Palace itasafiri kwa viongozi Arsenal, klabu ya zamani ya Vieira, Jumapili (14:00 GMT).

    Mechi zao 10 za mwisho msimu huu zitawakutanisha na wapinzani wao wote wanane walioshuka daraja.

    pia unaweza kusoma:

  6. Kwa picha : Shughuli ya mazishi ya mchezaji soka Christian Atsu yaanza Accra Ghana

    H
    Maelezo ya picha, Jeneza la Mchezaji soka wa Ghana Christian Atsu, likiwasili kwa ajili ya shughuli ya mazishi mjini Accra Ghana

    Mchezaji soka wa Ghana Christian Atsu, ambaye alifariki baada ya tetemeko la ardhi kuikumba Uturuki anazikwa leo Ijumaa katika nchi yake ya asili Ghana.

    Atsu alipatikana akiwa amefariki baada ya tetemeko la ardhi kuangusha nyumba ya gorofa ambamo alikuwa anaishikusini mwa Uturuki . Alikuwa akiichezea klabu ya soka ya Hatayspor.

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Atsu alifariki katika tetemeko la adrhi lililoikumba Uturuki

    Shuguli ya mazishi yake ambayo yamesaidiwa na taifa la Ghana inafanyika katika mji mkuu Accra.

    Maelfu ya waombolezaji wamefika katika eneo la mazishi kutoa heshima zao za mwisho kwa Christian Atsu, katika mazishi yanayofanyika kwa utamaduni wa Ghana.

    Hizi ni baadhi ya picha za mazishi ya Christian Atsu, zilizochukuliwa na mwandishi wa BBC wa Ghana Thomas Naadi:

    B
    g

    Unaweza pia kusoma:

    • Christian Atsu wa Ghana alikuwa na 'moyo wa kipekee'
    • Christian Atsu anaamini Ghana watashinda kombe la AFCON
  7. Burna Boy kutumbuiza katika fainali za UEFA

    Msanii wa Nigeria na mshindi wa Tuzo za Grammy Burna Boy atatumbuiza katika sherehe za uzinduzi wa fainali za kuwania Kombe la Ligi ya championi ya UEFA mjini Istanbul, Turkey.

    Nyota huyo wa Nigeria ataleta nguvu na ladha ya muziki wa Solo wenye mapigo ya afrobeat kabla ya kuanza kuanza kwa mechi za fainali ya UEFA , imesema taarifa

    "Dunia haiko tayari kwa kile tulichoiandalia," Burna Boy alinukuliwa akisema, kabla ya onyesho lake katika Uwanja wa Atatürk Olympic.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  8. Mahujaji wa Uganda watahadharishwa dhidi ya kunywa ’maji matakatifu’

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Waumini wanaochukua maji wanadai kuwa yana nguvu za uponyaji wa kiroho

    Mahujaji wa Kikatoliki wanaotembelea eneo la mashahidi wa Uganda la Namugongo wametahadharishwa dhidi ya kunywa maji katika kile kinachoitwakisima kitakatifu .

    Maafisa wa kanisa hilo wanasema maji hayo yanaweza kutumiwa kwa malengo mengine ya kiroho kama vile kufanya ishara ya msalaba , lakini hayafai kunywa.

    Katibu mkuu wa Baraza kuu la mkutano wa maaskofuwa Uganda, John kauta, Alhamisi alisema kuwa ingawa waumini waliochukua maji wanadai kutibiwa kiroho, wataalamu wa afya wamewashauri viongozi wa kanisa kwamba maji hayo sio masafi na sio salama..

    “Maji katika Namugongo yamechujwa, lakini bado sio salama kwa kunywa. Hii ni kwasababu pia yanapita kutoka katika maeneo mengi. Watu wanaweza kuyachukua na kuyagusa wanapofanya ishara ya msalaba, lakini sio kuyanywa,” Bw Kauta aliuambia mtandao wa gazeti llinalodhibitiwa na serikali la New Vision.

    Bw Kauta alisema kwamba siku zijazo kanisa litaweka mabomba mengi katika kisima hicho kwa ajili ya kuwasaidia watu kuyafikia kwa urahisi zaidi kutokana na kwamba idadi ya wanaoyataka ni wengi.

    f

    Chanzo cha picha, UGANDA MARTYRS CATHOLIC SHRINE/FACEBOOK

    Maelezo ya picha, Maelfu kwa maelfu ya watu hufika Namugongo kila mwaka kutoka maeneo mbali mbali duniani kuhudhuria sherehe za Siku ya Mashahidi wa Uganda mwezi Juni

    Mahujani wameanza kuwasili katika eneo la makaburi ya mashahidi wa Namugongo kwa ajili ya sherehe za Siku ya Mashahidi inayoadhimishwa mwezi Juni.

    Tukio hilo la kila mwaka linahusu mashahidi 22 wa kikatoliki na 23 wa kianglikani waliuawa kwa ajili ya Imani yao kutokana na amri yaKabaka Mwanga wa Buganda baina yam waka 1885 na 1887.

  9. Marekani: Video ya kifo cha mwanaume mwenye asili ya Kenya inaonyesha polisi wakimfanyia ukatili – familia

    k

    Chanzo cha picha, BEN CRUMP LAW

    Maelezo ya picha, Familia ya ya Irvo Otieno (kulia) ilisema alikuwa na matatizo ya kiakilialipofariki katika mahabusu

    Mama wa mwanaume mweusi mwenye umri wa miaka 28 ambaye alifariki akiwa katika mahabusu ya polisi anasema video ya dakika 12 inayoonyesha tukio la mauaji yake inayo " sumbua na kutia kiwewe" na kisa hicho ni "ukatili".

    Polisi saba wa cheo cha sheriff wa Virginia wameshitakiwa kwa mauaji ya daraja cha pili kuhusiana na kifo cha mwanaume huyo anayefahamika kama Irvo Otieno.

    Waendesha mashitaka Alhamisi pia walitangaza mashitaka zaidi ya mauaji ya daraja la pili dhidi ya wafanyakazi watatu wa hospitali.

    Wakili Crump alisema, katika video Otieno alionekana "akizuiliwa kwa ukatili mkubwa, huku akishindiliwa chini kwa goti kwenye shingo lake , akiwekewa uzito wa watu saba mwilini mwake, huku uso wake ukiangalia chini, akiwa amefungwa pingu."

    Bw Crump amefananisha kisa cha Bw Otieno na tukio la George Floyd, Mmarekani mwingine mweusi aliyeuliwa kikatili na polisi.

    Bw Otieno alifariki tarehe 6 Machi wakati alipokuwa akihamishwa kutoka gereza kupelekwa katika kituo cha afya cha watu wenye matatizo ya akili.

    Ripoti ya awali inaonyesha kuwa uchunguzi wa kimatibabu ulionyesha kuwa alifariki kwa - kukosa hewa, walisema waendeshamashitaka.

    Polisi saba wa Kaunti ya Henrico wameshutumiwa na waendeshamashitaka kwa kumuua Bw Otieno kwa kumkosesha hewa ya kupumua, wakati walipokuwa wakimhamisha.

    Waendeshamashitaka wanasema ushahidi zaidi uliwawezesha pia kuwashitaki wafanyakazi wa hospitali katika Hospitali ya -Central State Hospital, ambako Bw Otieno alikuwa akihamishiwa.

    Video ya tukio ilinaswa na kamera za usalama, na ilitazamwa Alhamisi na wakili maarufu wa haki za binadamu Ben Crump pamoja na familia ya Bw Otieno.

    Mama yake Otieno, Caroline Ouko, na Bw Crump kwa pamoja walisema kuwa alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kiakili , na amekuwa akipata matibabu ya kiakili, lakini hakuweza kuendelea kumeza dawa hizo akiwa gerezani.

    Familia ya Otieno ambayo ilitoka Kenya na kuhamia Marekani alipokuwa na umri wa miaka minne. Bw Otieno alikuwa na ndoto ya kuwa mwanamuziki na mwanamichezo, walisema, na alikuwa akiandika na kurekodi muziki wakat iwa muda wake wa ziada

  10. Uteuzi wa Manaibu Waziri wazua mjadala Kenya

      • Author, Caro Robi
      • Nafasi, BBC Swahili
    William Ruto

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Rais wa Kenya William Ruto

    Rais wa Kenya William Ruto mnamo Alhamisi 16.03.2023 amewateua Mawaziri Wasaidizi (CAS) 50 ambao wamepewa kusimamia wizara 22.

    Kwenye orodha hiyo iliyotangazwa kupitia taarifa ya Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, idadi kubwa ya wateuzi hao ni wanasiasa wa Muungano wa Chama tawala Kenya Kwanza walioshindwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

    Miongoni mwao ni aliyekuwa Gavana wa Kaunti ya Nairobi Evans Kidero, Seneta mteule wa zamani Millicent Omanga, aliyekuwa mbunge wa Starehe Margaret Wanjiru na mbunge wa zamani wa Rarieda Mhandisi Nicholas Gumbo miongoni mwa wengine.

    Uteuzi huo wa mawaziri wasaidizi 50 wa wizara 22 walioidhinshwa na Tume ya Utumishi wa Umma,umepokelewa kwa hisia mseto na Wakenya.

    Wengi katika mitandao ya kijamii wamehoji utashi wa Rais Ruto wa kutimiza ahadi yake wakati wa kampeini mwaka jana ambapo aliahidi kuwa serikali yake itajumuisha kwa kiasi kikubwa wananchi wa tabaka la chini aliowaita 'Mama Mboga na Boda Boda'.

    Serikali inakosolewa pia kwa kufeli kupunguza mzigo wa kuajiri maafisa wengi serikalini wanaolipwa fedha nyingi za walipa ushuru,wakati ambapo uchumi wa Kenya unasuasua na Wakenya wengi wakilalamikia ugumu wa maisha.

    Aidha darubini inamulikwa kwa kutowapa fursa zaidi vijana katika serikali na teuzi kutokuwa na sura ya kitaifa. Baadhi ya wizara zimetengewa zaidi ya mawaziri wasaidizi wawili katika uteuzi huo wa Alhamisi.

    Katika serikali iliyopita ya Rais Uhuru Kenyatta, ambayo Rais wa sasa William Ruto aliikosoa vikali kwa teuzi nyingi alizozitaja mzigo kwa 'Mahustler',kulikuwa na mawaziri 23, hivyo basi uteuzi huu wa sasa ni karibu mara mbili ya ilivyokuwa awali.

    Katika ukurasa wake wa Twitter,Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ametetea uteuzi huo akisema wizara zina masuala mengi ambayo yanahitaji kushughulikiwa na wanaleta nguvu mpya kupiga jeki utendakazi na uwezo wa serikali.

    Walioteuliwa kuchukua wadhifa huo wa mawaziri wasaidizi ambao haujaanishwa katika Katiba ya Kenya, watapigwa msasa na bunge kabla ya kuanza rasmi kutekeleza majukumu yao.

  11. Mtaalamu wa afya ya akili:Felician Kabuga hataki kesi yake iendelee kwasababu anaumwa

    g

    Chanzo cha picha, SCREENGRAB IRMCT LIVE EVENT

    Maelezo ya picha, Profesa Henry Kennedy makiwa katika Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC, Alhamisi, akitoa ushahidi kuhusu afya ya akili ya Bw Kabuga

    Mmoja wa wataalam wa afya ya akili waliotoa ripoti kuhusu afya ya mtuhumiwa maarufu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994,Felician Kabuga, amesema kuwa afya yake haimruhusu "kuhusdhuria kesi dhidi yake mahakamani" – akihojiwa na waendesha mashitaka na mawakili wake.

    Kabuga, ambaye alifuatilia kesi yake katika gereza la Mahakama kwa njia ya video, hakupewa muda wa kuzungumzia kuhusu maelezo yaliyotolewa na mtaalamu wa afya ya akili kumuhusu.

    SCREENGRAB IRMCT LIVE EVENT

    Chanzo cha picha, SCREENGRAB IRMCT LIVE EVENT

    Maelezo ya picha, Félicien Kabuga ambaye anashitakiwa kwa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya 1994, akifuatilia kesi yake akiwa gerezani

    Kesi ya Bw Kabuga ambaye anashutumiwa kama mmoja wa wahusika wakuu waliodhamini mauaji ya kimbari ya Rwanda, imekuwa ikiendelea katika mahakama ya kimataifa ya jinai ICC, mjini The Heague Uholanzi.

    Katika kikao cha mahakama Alhamisi wiki hii, jopo la waendesha mashitaka lilifuatilia kesi hiyo kwa njia ya mtandao kutoka Arusha -Tanzania, huku mawakili wa Bw Kabuga wakiwa The Heague -Uholanzi.

    Awali Bw Kabuga alikana mashitaka yote kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda anayoshitakiwa.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mauaji ya Rwanda: Jinsi Felicien Kabuga alivyojificha kwa miaka 26
    • Félicien Kabuga: Mshukiwa mkuu wa mauaji ya kimbari Rwanda akamatwa
    • Félicien Kabuga: 'Huo wote ni uongo, sikumuua Mtutsi yeyote'
  12. Kamanda wa Ukraine 'aliyetoa siri' kwa waandishi wa habari ashushwa cheo

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kamanda wa kikosi cha jeshi la Ukraine Anatoly al maarufu "Kupol", ambaye aliliambia gazeti la Marekani la Washington Post kuhusu kushindwa vibaya kwa vikosi vya Ukraine, alishushwa cheo, limeripoti gazeti la Ukraine "Ukrainian Pravda" likimnukuu afisa wa vikosi vya uvamizi wa anga nchini humo.

    Taarifa ya mwanajeshi huyo ilichapishwa baada ya kufanya mazungumzo na kundi la waandishi wa habari wa Marekani ambao walichapisha taarifa hiyo tarehe 13 Machi, kuhusiana na hali katika eneo la Bakhmut kufuatia mashambulizi ya Warusi.

    Alidai kuwa kushindwa kwa jeshi la Ukraine katika mapigano ya Bakhmutkulipelekea kupungua pakubwa kwa idadi ya wanajeshi wa Ukraine, jambo ambalo awali liliangaliwa kama faida ya Ukraine ikilinganishwa na Urusi. Matokeo yake , baadhi ya maafisa walianza kuhoji utayari wa Ukraine wa kukabiliana na vita siku zijazo.

    Miongoni mwa mambo mengine , kamanda hiyo wa Ukraine alisema kuwa takriban wanajeshi 100 kati ya 500 katika kikosi chake waliuawa na wengine 400 wakajeruhiwa katika mashambulio ya Bakhmut.

    Mwakilishi rasmi wa kikosi cha anga cha Ukraine, Valentin Shevchenko, katika mahojiano na gazeti la Ukraine -Ukrayinska Pravda, alisema taarifa zilizotolewa na mwanajeshi huyo zilizidi makadirio na sio za kuaminika na akasema kwamba maafisa wanachunguza zaidi kuhusu taarifa alizozitoa.

  13. Vita vya Ukraine:Poland kutuma ndege nne za kivita Ukraine 'katika siku zijazo'

    h

    Chanzo cha picha, EPA

    Poland itatuma ndege nne za maoigano za aina ya Mig jetza enzi ya Usovieti nchini Ukraine – na kuwanchi ya kwanza ya Nato kutuma ndege zaketangu Urusi uanze uvamizi wa Urusi nchini Ukraine .

    Rais wa Poland Andrzej Duda alisema kwamba ndege hizo zitapelekwa katika siku zijazo, na nyingine zitapelekwa baadaye.

    Ingawa msada huo unapokelewa vyema kwa maana kwamba utaboresha utendaji wa kikosi cha ulinzi wa anga cha Ukraine, jeti hizi za ziada hazitarajii kuleta mabadiliko yoyote katika vita.

    Naibu spika wa bunge la Ukraine Olena Kondratyuk amesema kuwa anatumaini nchi zaidi zitafuata mfano wa Poland.

    Nchi nyingine za Nato zinaangalia uwezekano wa kutuma ndege za enzi ya Usovieti, ambazo ndizo marubani wa Ukraine wamefunzwa kuzitumia .

    Awali Ukraine iliyaomba mataifa ya Magharibi kuipatia ndege za kisasa za aina ya jeti kama vile F-16.

    Uingereza inawapatia mafunzo marubani wa Ukraine kuhusu uendeshwaji wa ndege zenye viwango vya NATO.Lakini kwasabababu ya mafunzo ya kipindi kirefu, imeonya kuwa kupeleka jeti za Magharibi nchini Ukraine utakuwa ni mpango wa baadaye.

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
  14. Afya: Idadi ya wanaume wanaofunga uzazi kuongeza – madaktari

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Idadi ya wanawaume wanaotumia njia ya kufunga uzazi ya kudumu (vasectomy) inatarajiwa kuongezeka zaidi, kuliko inavyoripotiwa kwa sasa, wanasema madaktari wa Uingereza waliofanya utafiti kuhusu suala hilo.Madaktari hao wanasema baada ya kufanyiwa upasuaji wa kufunga uzazi, wanaume wanaweza kuhisi maumivu kidogo , lakini wanasema ni nadra kwa wanaume waliofunga uzazi kwa njia hiyo kupata madhara makubwa ya kiafya.

    m

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Upasuaji wa kufunga uzazi kwa njia ya vasectomy, huchukua dakika 15 pekee

    Kundi la madaktari hao lilitoa matokeo ya utafiti wake katika kongamano la matibabu lililomalizika Alhamisi Milan nchini Italia, baada yakuwafanyia utafiti wanaume 94,000 ambao walifungwa uzazi kwa njia ya vasectomy.

    Upasuaji wa kufunga uzazi kwa njia ya vasectomy, ambapo mwanaume hudungwa sindano ya ganzi, huchukua dakika 15 pekee.

    Kwa ujumla takwimu zinaonyesha kuwa wanaume wengi bado hawajitolei kufanyiwa upasuaji wa vasektomi kama njia ya kufanya uzazi wa mpango, zaidi kutokana na imani zinazozingira njia hii.

    Ufungaji wa kizazi kwa wanaume ni nini?

    • Njia ya kufunga uzazi kwa wanaume ni njia ya uzazi wa mpango ambayo hufanywa kwa njia ya upasuaji kukata au kufunga mirija inayosafirisha mbegu za uzazi za mwanaume, ili kuzuia mwanamke asipate mimba.
    • Upasuaji mara nyingi hufanywa kwa muda wa dakika takriban 15, mgonjwa huwa macho lakini huwa hapati maumivu yeyote.
    • Njia hii inafanya kazi ya kuzuia mimba kwa silimia 95.
    • Njia ya kufunga uzazi kwa wanaume haiathiri nguvu za kiume au uwezo katika tendo au kulifurahia tendo.Mwanaume ataweza hayo yote,isipokuwa hataweza kumpa mwanamke ujauzito.
    • Njia hii haizuii mwanaume dhidi ya maradhi ya zinaa, kama mipira ya kiume ambayo inaelezwa kuwa njia ya kuaminika kwa asilimia 98 ikiwa itatumika vyema.

    Unaweza pia kusoma:

    • ''Mwanamume afunguka kuhusu hatua yake ya kufunga njia ya uzazi''
    • Wanaume wengi Kenya wanakubali kufunga mirija ya mbegu za uzazi-Vasektom
  15. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Ijumaa tarehe 17.03.2023