Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Vita vya Ukraine: Marekani yathibitisha 'mawasiliano' na Urusi

Mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama wa Marekani Jake Sullivan amethibitisha njia za mawasiliano baina ya Washington na Moscow zimeendelea kuwa wazi licha ya vita nchini Ukraine war in Ukraine.

Moja kwa moja

  1. Chama tawala cha UDA nchini Kenya chakataa pendekezo la kufuta ukomo wa mihula ya urais

    Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kimepuuzilia mbali madai kwamba wabunge washirika wa chama hicho wanapanga kufuta ukomo wa mihula miwili ya urais.

    Chama hicho cha Rais William Ruto pia kilipuuzilia mbali madai ya Mbunge wa Fafi Salah Yakub kwamba Mswada wa kuongeza muda wa urais ulikuwa ukiandaliwa ikiyataja mawazo yake kuwa finyu, katika Taarifa yake kwa twitter.

    Mwenyekiti wa UDA Johnson Muthama alisisitiza kuwa pendekezo hilo haliendani na azma ya chama hicho.

    “Kama Mwenyekiti wa Chama Taifa, napenda kutamka wazi kuwa Mhe. Yakub alitoa kauli binafsi ambayo haina uhusiano wowote na UDA. Kama Chama, tunasimamia demokrasia iliyo wazi na tunasalia kuunga mkono ukomo wa mihula miwili ya urais na (hakuna) mijadala inayoendelea ya kuufuta,” Bw Muthama alisema.

    Kwa mujibu wa pendekezo la mbunge huyo, baadhi ya wabunge wa UDA walikuwa wakifanyia kazi Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ili kubadilisha ukomo wa mihula miwili na ukomo wa umri wa miaka 75.

    Rais Ruto alipochukua wadhifa huo, aliapa kulinda Katiba ya Kenya.

    Rais hajazungumzia suala hilo, na wala hajaonyesha nia ya kuhudumu zaidi ya ukomo wa muda wa kikatiba.

  2. Wizara ya Ulinzi inataka kuanzisha mafunzo ya kijeshi katika shule za Kirusi

    Wizara ya Ulinzi ya Urusi iliunga mkono wazo la kiongozi wa Chama cha Just Russia - For the Truth party, Sergei Mironov, kuanzisha mafunzo ya kimsingi ya kijeshi (NVP) katika shule na vyuo vya ufundi, kulingana na jarida la Izvestia.

    Chapisho hilo linamnukuu Naibu Waziri Valery Gerasimov, ambaye anaamini kwamba saa 140 zinapaswa kutengwa kwa mafunzo ya kijeshi na kufundishwa kwa miaka miwili.

    Kulingana na yeye, watu walio na uzoefu wa kivita pekee ndio wanapaswa kuruhusiwa kufundisha NVP.

    Mpango wa Mironov uko tayari kuungwa mkono na vikundi vyote vya wawakilishi wa baraza la Urusi, Izvestia imesema.

  3. Ukraine yapata ushahidi kwamba Iran iliipatia Urusi droni baada ya uvamizi wake Ukraine

    Wawakilishi wa idara ya ujasusi ya kijeshi ya Ukraine wamepata habari ambazo zinaweza kuonyesha kuwa ndege zisizo na rubani za Iran zilikabiliwa Urusi baada ya kuanza kwa uvamizi kamili wa Ukraine mnamo Februari 24.

    "Propeller ya droni ya Mohajer-6 ilitengenezwa tu Februari mwaka huu.. Pia ilichukua muda kuipeleka kwa Shirikisho la Urusi. Zilitolewa mwaka huu," alisema mwakilishi wa shirika la Kurugenzi Kuu ya Ujasusi ya Wizara ya Ulinzi ya Ukraine.

    Mohajer ya Irani imekusanywa kutoka kwa sehemu zinazoundwa kutoka katika nchi tofauti. Vifaa vingi vinatoka Marekani, kuna injini ya Austria na kamera ya Kijapani, na hakuna vifaa vua |urusi vilivyotumika hata kidogo , ulisema ujasusi huo.

    Siku ya Jumamosi, waziri wa mambo ya nje wa Iran alisema nchi hiyo ilisambaza ndege zisizo na rubani kwa Urusi kabla ya uvamizi wa Ukraine kuanza. Kabla ya hapo, Tehran ilikanusha uwasilishaji kama huo kabisa, huku Urusi naypo pia ikikana kupokea silaha hizo baada ya uvamizi

  4. Kwa Picha: Ndege iliyopata ajali Tanzania yatolewa Ziwa Victoria

    Ndege ya shirika la ndege la Precision PW PW 494 iliyopata ajali siku ya jumapili nchini Tanzania imetolewa katika eneo la Ziwa Victoria na kuhifadhiwa katika uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.

    Ajali hiyo ya ndege ilisababisha vifo vya watu 19, huku 26 wakipata majeraha.

    Precision Air ndiyo shirika kubwa la ndege la kibinafsi la Tanzania na kwa sehemu inamilikiwa na Kenya Airways. Ilianzishwa mnamo 1993 na inaendesha safari za ndege za ndani na kikanda.

  5. Vita vya Ukraine: Urusi yayashambulia baadhi ya majimbo ya Ukraine usiku

    Kulingana na mkuu wa ofisi yar ais wa Ukraine Kyrylo Tymoshenko, mashambulio ua makombora 74 yalipiga katika wa saa 24 zilizopita, ambayo 58 miongonimwake yalipiga miundo mbinu ya rai katika makazi 17.

    Usiku uliopta "Gradov na makombora mashambulio mazito "yalirushwa katika jimbo la Dnepropetrovsk, alisema Valentin Reznichenko.

    Ameongeza kuwa katika Nikopol, makombora ya Urusi yalipiga maduka mengi na nyumba za watu binafsi, viwanda viwili, hospitali, shule , magari na bomba la gesi.

    Majimbo ya Zaporozhye na Kherson pia yalishambuliwa,Tymoshenko

    Kulingana na afisa huyo katika ofisi ya rais ya Ukraine "Kombora la mfumo wa ulinzi wa S-300 lilipiga shule. Adui aliangamiza taasisi ya elimu katikaZolotaya Balka."

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  6. Waliomtusi gavana Tiktok wachapwa viboko na kulipa faini ‘ili iwe funzo’

    Hakimu mkazi katika jimbo la Kano nchini Nigeria ameagiza watu wawili waliokuwa wakifanya wakicheza densi ya mzaha uliodaiwa kuwa ''matusi'' kwenye Tiktok kuchapwa viboko 20 , na kulipa faini ya naira 10,000 na kisha kusafisha maeneo yote ya mahakama kwa siku 30 kwa madai ya kumtukana gavana wa jimbo hilo Abdullahi Ganduje.

    Jaji Aminu Gabari aliyeongoza kesi hiyo aliwahukumu Mubarak Muhammad na Nazifi Muhammad, ambao walikamatwa wiki iliyopita kwa kutuma video kwenye Tiktok ambayo inadaiwa kumshutumu Gavana Ganduje kwa ufisadi.

    Katika kesi hiyo wakili wa gavana alisema adhabu hiyo itakuwa funzo kwa wengine.

    Mara baada ya hukumu kutolewa, afisa wa mahakama aliwatandika viboko 20 washukiwa na kuwataka walipe faini ya naira 10,000 kama ilivyoagizwa na mahakama.

  7. Uchaguzi wa nusu muhula Marekani: Mamilioni ya Wamarekani kupiga kura huku congress ikiwa mashakani

    Mamilioni ya Wamarekani watapiga kura katika uchaguzi wa nusu muhula huku mamlaka katika bunge la Congress yakiwa mashakani.

    Vitu vyote vya Bunge lote la wawakilishi la Marekani, takriban theluthi tatu ya seneti na viti vya majimbo muhimu viko tayari kugombewa.

    Rais Joe Biden, kutoka cham cha Democrat, na rais wa zamani Donald Trump, Mrepublican, walitoa hoja zao za mwisho katika mikutano ya mwisho ya kukamilisha kampeni.

    Uwezo wa Bw Biden wa kupitisha sheria utakwisha iwapo Warepublican watachukua udhibiti wa bunge, kama makadirio mengi yanavyoashiria.

    Kwa sasa Wademocrats wanadhibiti White House na - kwa kiwango kidogo sana – mabunge yote ya Congress.

  8. Je Didier Drogba amebadili dini?

    Katika muda wa saa kadhaa, kumekuwa na jumbe nyingi katika mitandao ya kijamii zilizosema kuwa mchezaji maarufu wa zamani kutokaIvory Coast, Didier Drogba, amebadili dini na kuwa Muislamu.

    Taarifa hizi zilisambaa baada ya kiongozi mmoja wa Kiislamu anayefahamika kwa jina Dr. Mohamed Salah anayeishi Marekani kuchapisha picha inayoonyeshaDrogba akisali kama Waislamu.

    Kasisi huyo alisema kwamba Drogba ameslim, na hivyo ndivyo taarifa hiyo ilivyoenea. mtandaoni

    Saa chache baadaye, Bw Drogba alituma ujumbe kwenye mtandao wake rasmi akikanusha madai kwamba alibadilisha dini, na kuongeza kuwa alishangazwa na jinsi taarifa hiyo ilivyosambaa.

    "Nilikuwa ninatoa heshima kwa kaka zangu Waislamu na niliokuwa nimewatembelea. Lilikuwa ni tukio ambapo tulionyesha umoja " alisema Drogba katika ujumbe wake wa Twitter.

    Baadaye Dr. Mohamed Salah alifuta ujumbe wake na kusema kuwa Drogba hajawa Muislamu, lakini alikuwa anamuombea.

  9. Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wajadili hali ya usalama DRC

    Marais wa Burundi, Tanzania, Kenya na Rwanda pamoja na Waziri mkuu wa DRC wamekutana kando na mkutano wa COP 27 Sharm El Sheikh Misri kujadili hali ya usalama mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

    Mazungumzo hayo yaliyoongozwa na Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye yanakuja baada ya mazungumzo yake na mpatanishi katika mchakato wa mazungumzo ya amani ya mashariki mwa Congo, rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, yaliyofanyika mjini Bujumbura wiki iliyopita.

    Haya yanajiri huku hali ya wasi wasi ikiendelea kutokota baina ya DRC na Rwanda huku kila upande ukimshutumu mwenzake kuwaunga mkono wapinzani wake.

    Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo inaishutumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23 walioteka hivi karibuni baadhi ya maeneo ya mashariki mwa Congo, huku Rwanda ikiishutumu DRC kwa kuunga mkono kundi la wapiganaji wa- Kinyarwanda wa FDLR wanaoshutumiwa kufanya mashambulio kwenye maeneo yaliyo karibu na mpaka ndani ya Rwanda. Kila upande unakanusha madai hayo.

    Jumatatu Rwanda iliishutumu DRC kwa kuingiza ndege yake ya kijeshi Rwanda na kulaani kitendo hicho kamacha uchokozi. DRC ilikiri kuingiza ndege hiyo, lakini ikasema kuwa haikuwa na nia mbaya.

    Burundi, Uganda, na Kenya zimeyapeleka majeshi yake mashariki mwa Congo kukabiliana na makundi ambayo yamekuwa yakiyumbisha usalama katika eneo hilo kwa karibu miongo mitatu.

    Unaweza pia kusoma:

    • Tunachokifahamu kuhusu kinachoendelea mashariki mwa DRC
    • Kwa nini jeshi la Kenya linajiunga na mzozo wa DRC
    • Mzozo wa DRC: Je inawezekana kuyamaliza makundi ya wapiganaji Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo?
  10. Hushpuppi: Tapeli maarufu wa Nigeria afungwa miaka 11 Marekani

    Mshawishi maarufu wa Instagram kutoka Nigeria amefungwa kwa zaidi ya miaka 11 nchini Marekani kwa jukumu lake katika harambee ya kimataifa ya utapeli.

    Hushpuppi, ambaye jina lake halisi ni Ramon Abbas, alidhihirisha maisha yake ya kitajiri kwenye ukurasa wake ambao ulikuwa na wafuasi milioni 2.8 hadi ulipolemazwa.

    Jaji wa Los Angeles pia aliamuru alipe dola 1,732,841 ili kuwafidia waathiriwa wawili wa ulaghai.

    Abbas atatumikia kifungo chake cha miezi 135 katika jela ya Marekani.

    Mwaka jana alikiri makosa ya utakatishaji fedha.

    Abbas alikiri kujaribu kuiba zaidi ya dola milioni 1.1 kutoka kwa mtu ambaye alitaka kufadhili shule mpya ya watoto nchini Qatar, nyaraka za mahakama huko California zilisema.

    Tapeli huyo alimhadaa mwathiriwa wake kutoa fedha kwa ajili ya shule "kwa kutekeleza majukumu ya maafisa wa benki na kuunda tovuti ya uwongo", kulingana na taarifa kutoka kwa aliyekuwa Kaimu Mwanasheria wa Marekani Tracy Wilkinson kwenye tovuti ya idara ya sheria ya Marekani.

    Washukiwa wengine pia walidaiwa kuhusika, idara ya sheria ya Marekani ilisema, huku Abbas akichukua jukumu muhimu.

    Abbas pia alikiri "mipango mingine mingi ya mtandao na barua pepe ya maelewano ya barua pepe ambayo kwa jumla ilisababisha hasara ya zaidi ya dola milioni 24", idara ya sheria ya Marekani ilisema.

    "Ramon Abbas... aliwalenga wahasiriwa wa Marekani na kimataifa, na kuwa mmoja wa wabadhirifu wa fedha zaidi duniani," Don Alway, mkurugenzi msaidizi anayesimamia Ofisi ya FBI ya Los Angeles, katika hati ya mahakama siku ya Jumatatu.

  11. Vita vya Ukraine vimesababisha vifo vya raia wapatao elfu 7

    Rais waliojeruhiwa katika vita vya Ukraine kuanzia mwanzo wa uvamizi kamili wa Urusi tarehe24 Februari hadi Novemba 6 ilifikia hadi watu 16,462, wakiwemo 6,490 waliokufa, Tume ya masuala ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema.

    "Vingi kati ya visa vya vifo vya raia au majeruhi vilivyoripotiwa vilisababishwa na matumizi ya silaha za vilipuzi ambazo zilisababisha athari katika eneo kubwa, vikiwemo vile vilivyofyatuliwa kutoka kwenye silaha nzito, pamoja na roketi na mashambulio ya anga ,"ilisema taarifa ya tume hiyo.

    Kulingana na Umoja wa Mtaifa UN, miongoni mwa vifo hivyo - 2533 walikuwa ni wanaume,1731 wanawake, 201 wavulana na 168 wasichana(jinsia za watoto 34 na watu wazima 1828 bado hazijajulikana).Miongoni mwa majeruhi 9,972 walikuwa ni wavulana 295 na wasichana 208, pamoja na watoto 242 ambao jinsia yao haijafahamika.

    Raia wengi zaidi – 3298, waliuawamwezi Machi.

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  12. Vita vya Ukraine: Marekani yathibitisha 'mawasiliano' na Urusi

    Mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama wa Marekani Jake Sullivan amethibitisha njia za mawasiliano baina ya Washington na Moscow zimeendelea kuwa wazi licha ya vita nchini Ukraine war in Ukraine.

    Akizungumza mjini New York, Bw Sullivan alisema kuwa ni " katika maslahi" ya Marekani kuendeleza mawasiliano na Kremlin.

    Lakini alisisitiza kuwa maafisa walikuwa "macho- wazi kuhusu ni nani wanaye shughulika naye".

    haya yanajiri huku Ikulu ya Marekani -White House ikikataa kukanusha ripoti kwamba Bw Sullivan amekuwa akiongoza mazungumzo na Urusi ya kuzuia matumizi ya nyuklia nchini Ukraine.

    Taarifa za jarida laWall Street zilisema kwamba Bw Sullivan ameongoza mazungumzo na mwenzake wa Urusi, katibu wa baraza la usalamaNikolai Patrushev,na afisa wa ngazi ya juu wa Kremlin wa masuala ya sera ya kigeni Yuri Ushakov, kwa miezi kadhaa iliyopita.

    Maafisa wa ngazi ya juu waliliambia jarida hilo kwamba wanaume hao walijadili njia za kulinda hatari ya kuongezeka haraka kwa uwezekano wa matumizi ya nyuklia katika vitavya Ukraine, lakini hawakuwa na mazungumzo kuhusu njia za kumaliza mzozo.

    Mwezi uliopita, Bw Sullivan alisema kwamba matumizi yoyote ya silaha za nyuklia yatakuwa na "athari za janga kwa Urusi".

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  13. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara leo tarehe 8.11.2022