Chama tawala cha UDA nchini Kenya chakataa pendekezo la kufuta ukomo wa mihula ya urais

Chanzo cha picha, Muthama/Twitter
Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kimepuuzilia mbali madai kwamba wabunge washirika wa chama hicho wanapanga kufuta ukomo wa mihula miwili ya urais.
Chama hicho cha Rais William Ruto pia kilipuuzilia mbali madai ya Mbunge wa Fafi Salah Yakub kwamba Mswada wa kuongeza muda wa urais ulikuwa ukiandaliwa ikiyataja mawazo yake kuwa finyu, katika Taarifa yake kwa twitter.
Mwenyekiti wa UDA Johnson Muthama alisisitiza kuwa pendekezo hilo haliendani na azma ya chama hicho.
“Kama Mwenyekiti wa Chama Taifa, napenda kutamka wazi kuwa Mhe. Yakub alitoa kauli binafsi ambayo haina uhusiano wowote na UDA. Kama Chama, tunasimamia demokrasia iliyo wazi na tunasalia kuunga mkono ukomo wa mihula miwili ya urais na (hakuna) mijadala inayoendelea ya kuufuta,” Bw Muthama alisema.
Kwa mujibu wa pendekezo la mbunge huyo, baadhi ya wabunge wa UDA walikuwa wakifanyia kazi Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ili kubadilisha ukomo wa mihula miwili na ukomo wa umri wa miaka 75.
Rais Ruto alipochukua wadhifa huo, aliapa kulinda Katiba ya Kenya.
Rais hajazungumzia suala hilo, na wala hajaonyesha nia ya kuhudumu zaidi ya ukomo wa muda wa kikatiba.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe














