Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Jaji Mkuu Kenya apata pigo baada ya uamuzi wake kutangazwa kuwa kinyume cha sheria

Sheria iliyobatilishwa ilikuwa imekataza maoni ya umma juu ya rufaa ya uchaguzi wa urais mara tu itakapowasilishwa katika Mahakama ya Juu Zaidi na wakati bado inasubiri kuamuliwa.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa hii leo. Kwaheri.

  2. Madai ya kujitokeza kwa wapiga kura kwa uchaguzi wa Kenya yanapotosha

      • Author, Peter Mwai
      • Nafasi, BBC Reality Check

    Wafuasi wa mtandaoni wa waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga wamekuwa wakihoji kimakosa matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotangazwa siku ya Jumatatu wakisema kuwa jumla ya kura zilikuwa chini kuliko waliojitokeza kupiga kura.

    William Ruto alitangazwa mshindi, lakini Bw Odinga amepinga matokeo hayo.

    Hoja kuu ya wafuasi wa Odinga ni kwamba mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya uchaguzi, Wafula Chebukati, alikuwa ametangaza waliojitokeza kuwa asilimia 65.4, kulingana na vifaa vya kitambulisho vya kielektroniki vya wapiga kura.

    Kisha wanahesabu kurudi nyuma kwa kutumia jumla ya idadi ya wapiga kura waliojiandikisha, kusema wapiga kura 14.4m lazima wawe wamepiga kura zao Jumanne wiki iliyopita.

    Jumla ya kura halali, kulingana na tangazo la mwisho, ilikuwa 14.2m na unapoongeza kura zilizokataliwa, utapata kura milioni 14.3 zikiwa zimepigwa.

    “Kabla hata hatujaongeza waliopiga kura kwa mikono, kuna kuwa na pungufu ya kura 140,028.

    Je, kura hizi [pamoja] na wapiga kura wa kwenye daftari la sajili ziko wapi?”

    Anauliza mmoja wa wafuasi kwenye Twitter.

    Ni kweli kwamba Bw Chebukati alitaja idadi ya wapiga kura waliojitokeza kuwa 65.4% wakati wa kikao na wanahabari Jumatano wiki jana lakini alijisahihisha punde tu baada ya kusema waliojitokeza kupiga kura ni 64.6%.

    “Kwa kweli takwimu hii itaongezeka mara tu tutakapopata data ya wale waliopiga kura kwa mikono,”alisema.

    Matokeo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii yanaonyesha idadi ya wapiga kura hatimaye ilikuwa 64.8%.

    Soma zaidi:

  3. Ukraine yatangaza uharibifu mkubwa wa kambi ya jeshi la Urusi Nova Kakhovka

    Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine viliharibu msingi wa wanajeshi wa Urusi huko Nova Kakhovka, mkoa wa Kherson, kulingana na huduma ya vyombo vya habari ya Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine na huduma ya mpaka wa serikali.

    Video inayoonyesha athari ya shambulio la kombora imeibuka mtandaoni.

    Upande wa Ukraine unakadiria mauaji ya kati ya 10-15 wa Urusi.

    BBC haiwezi kuthibitisha kwa haraka habari katika hali ya mapigano.

  4. Mambo yanarejea kuwa ya kawaida katika ngome ya Odinga

      • Author, Roncliffe Odit
      • Nafasi, BBC Nairobi

    Mambo yamerejea katika hali ya kawaida huko Migori, magharibi mwa Kenya, eneo ambalo lilikuwa mojawapo ya yaliyokumbwa na maandamano ya ghasia baada ya Mkuu wa Tume ya uchaguzi kutangaza Jumatatu kuwa William Ruto ndiye rais mteule.

    Ni ngome ya mpinzani wake, Raila Odinga, ambaye amekataa matokeo ya uchaguzi wa wiki jana.

    Tulimpata Jeffers Omondi, 24, akijiandaa kuuza kahawa kando ya barabara.

    Alisema anafurahia utulivu uliofuatia vurugu hizo mwanzoni mwa wiki.

    Hata hivyo, aliongeza kwamba anaunga mkono pendekezo la Bw Odinga la kwenda mahakamani, akisema haki lazima itekelezwe.

    Lillian Akinyi, 48, ni mchuuzi wa viatu.

    Alisema biashara ilikuwa nzuri sasa kwa vile maandamano yameisha.

    Lakini tofauti na wafuasi wengi wa Odinga, alihisi pingamizi hizo zinafaa kumalizika.

    “Watoto wetu wanahitaji kurejea shuleni, na tunataka kuendelea na biashara zetu''.Alisema

    Soma zaidi:

  5. Uchaguzi wa Kenya: Ushindi unakuja nyumbani – Karua

    Dakika chache baada ya rais mteule wa Kenya William Ruto kusema kuwa muungano wake utaendelea na kupanga serikali, muungano wa Raila Odinga umeendelea kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais.

    Kwa sasa Bw Odinga anafuatilia chaguo za kisheria na mgombea mwenza wa Bw Odinga, Martha Karua, aliendelea kukataa matokeo ya urais.

    ‘’Katika suala la uchaguzi, ushindi wetu umeahirishwa lakini unakuja nyumbani,’’ aliwaambia waandishi wa habari baada ya muungano wake wa Azimio la Umoja kukutana’’.

    Kinara wa muungano wa Azimio la Umoja Raila odinga amepinga matokeo ya uchaguzi wa Agosti 9, baada ya mpinzani wake mkuu William Ruto kutangazwa mshindi.

    Inakisiwa kuwa huenda Bw Odinga, akawasilisha rufaa ya kupinga matokeo hayo katika Mahakama ya Juu Zaidi yenye jopo la majaji saba.

    Soma zaidi:

  6. Shule kufunguliwa kesho huku zilizoathirika zikifungwa tena wiki ijayo

    Waziri wa elimu George Magoha amesema kuwa wanafunzi wa shule za msingi na upili katika kaunti za Mombasa na Kakamega, watasalia shuleni wakati uchaguzi wa ugavana wa maeneo hayo utakapokuwa unafanyika Jumanne ijayo Agosti, 23.

    Alisema hakuna haja ya kuingilia masomo katika shule hizo kwani uchaguzi hautachukua muda mrefu.

    ‘’Hatutawataka watoto katika shule za bweni kurudi nyumbani katika maeneo ambayo kutakuwa na uchaguzi mpya,’’ alisema.

    ‘’Kwa mfano, ikiwa Watoto tayari wako kwenye shule za bweni, na hizo shule zitatakiwa kutumika kwa siku moja na kitu kama hicho, watoto hao hawatapelekwa nyumbani, wanaweza pengine kuambiwa, kwa siku hii ya leo, mutakuwa michezo na musalie bwenini, ni bora zaidi na rahisi kukabiliana na suala hili kwa njia hiyo.

    Uchaguzi wa maeneo hayo ulisitishwa pamoja na kura za wabunge katika maeneo bunge ya Kacheliba na Pokot Kusini kutokana na mkanganyiko wa kura.

    Shule zitafunguliwa tena hapo kesho baada ya kufungwa kutokana na zoezi la uchaguzi.

    soma zaidi:

  7. Jaji Mkuu Kenya apata pigo baada ya uamuzi wake kutangazwa kuwa kinyume cha sheria

    Jaji Mkuu Martha Koome amepata pigo jana baada ya Mahakama Kuu kutangaza kuwa ni kinyume cha sheria uamuzi wake wa kuwabana mawakili na walalamishi kutoa maoni yao juu ya rufaa za uchaguzi wa urais wakati bado inasikilizwa na Mahakama ya Juu Zaidi.

    Jaji Mugure Thande alipinga (Kanuni za Marekebisho za rufaa ya uchaguzi wa Urais) za Mahakama ya Juu Zaidi za 2022 na kuzitaja kuwa ni kinyume na katiba kwa kutotii matakwa ya ushiriki wa umma.

    Sheria hiyo iliyotangazwa miezi miwili iliyopita ilikuwa imekataza maoni ya umma juu ya rufaa ya uchaguzi wa urais mara tu itakapowasilishwa katika Mahakama ya Juu Zaidi na wakati bado inasubiri kuamuliwa.

    Pia ilipiga marufuku uvumi wa matokeo ya rufaa hiyo.

    CJ Koome, katika kutetea kanuni hiyo, alisema madhumuni ya kanuni hizo ni kulinda uadilifu wa mwenendo wa kesi mahakamani kwa vile kulikuwa na baadhi ya mawakili waliokuwa wakifika mahakamani, kutetea kesi yao na baadaye kupeleka hoja zao kwenye mitandao ya kijamii na kuonesha dharau dhidi ya majaji.

    Alidai kuwa sheria hizo, ambazo zilitangazwa kwenye gazeti la serikali Aprili 12, 2022, zilikusudiwa kuhakikisha hadhi na uhuru wa mahakama unadumishwa na kwamba nia haikuwa kuondoa uhuru wa kujieleza.

    Soma zaidi:

  8. Vita vya Ukraine: Maelfu ya Wayahudi waondoka Urusi baada ya uvamizi wa Ukraine

    Urusi inakabiliwa na wimbi kubwa la Wayahudi wanaondoka nchini humo tangu kuzuka kwa vita kati yake Ukraine kuanza.

    Shirika la Kiyahudi linawasaidia Wayahudi kote duniani kuhamia Israeli.

    Linasema idadi kubwa ya Warusi wenye asili ya Kiyahudi wameondoka nchini humo tangu Machi. Maelfu zaidi wamehamia nchi nyingine.

    Maelfu ya wengine wamehamia nchi zingine.

    Hofu ya mateso ya kihistoria dhidi ya Wayahudi inasadikiwa kuchangia uhamiaji huo wa ghafla na wale ambao bado hawajaondoka wanajitahidi kufanya hivyo.

    Huko Moscow, kumekuwa na jitihada kubwa ya kuendeleza jumuiya ya Wayahudi tangu kuanguka kwa Ukomunisti.

    Miongoni mwa waliokuwa mstari wa mbele ni Pinchas Goldschmidt, rabi mkuu wa jiji hilo tangu 1993.

    "Tulianza tangu mwanzo na masinagogi, shule, shule za chekechea, huduma za kijamii, walimu, marabi na wanajamii," anasema kuhusu uchangamfu ulioanzishwa. Lakini majuma mawili tu ya vita mwaka huu, Rabbi Goldschmidt na familia yake waliondoka Urusi, kwanza hadi Hungaria na kisha Israeli.

    Soma:

  9. Tanzania kutoa huduma ya intaneti mlima Kilimanjaro

    Shirika la simu la Tanzania TTCL limeweka huduma ya intaneti ya kasi kwenye kilele cha Horombo cha Mlima Kilimanjaro kupitia mradi wa taifa wa mkonga wa mawasiliano.

    Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tehama wa Tanzania Bw. Nape Nnauye amesema sasa watalii wanaweza kuwasiliana na sehemu mbalimbali duniani wakiwa kwenye kilele cha mlima huo.

    Mlima huo ni miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa utalii nchini Tanzania.

    Bw Nnauye alisema kuunganishwa kwa huduma hiyo ya intaneti kwenye mlima huo kunatarajiwa kufika hadi katika kilele cha juu cha Uhuru peak, urefu wa mita 5,895 (futi 19,341) kutoka usawa wa bahari ifikapo mwezi Oktoba.

    Wizara imesambaza baadhi ya picha wakati wa uzinduzi wa mradi huo kwenye mlima huo:

    Watalii kwenye mlima walikuwa hawapati huduma ya intaneti na hawakuweza hata kupiga simu kwani huduma hya intaneti iliunganishwa hadi karibu na mahali pa kuanzia karibu 1860m.

    Mlima huu huvutia watalii karibu 50,000 kila mwaka kutoka kote ulimwenguni ambao hujaribu kufikia kilele.

    Utalii ni nguzo muhimu ya uchumi wa Tanzania, unachangia asilimia 18 katika pato la taifa. ilikusanya kiasi cha $1.4bn (£1.1bn) katika mapato ya mwaka jana

  10. Msani nyota wa Rwanda Yvan Buravan afariki dunia

    Msanii wa Rwanda Yvan Buravan amefariki akiwa na umri wa miaka 27, meneja wake aliambia BBC.

    Mwimbaji huyo alikuwa amepatikana na saratani ya kongosho na alikuwa akipatiwa matibabu nchini India.

    Hapo awali alikuwa akitibiwa Rwanda na Kenya kabla ya uhamisho wake kwenda India. Kipaji cha muziki cha Buravan kiligunduliwa akiwa na umri wa miaka 14 alipomaliza wa pili katika shindano la kitaifa la muziki.

    Wimbo wake wa mwaka wa 2016 Malaika ulimpa umaarufu nchini Rwanda. Mwaka wa 2018 alishinda Prix Découvertes - mojawapo ya mashindano makubwa zaidi ya muziki barani Afrika yaliyoandaliwa na RFI na Unesco.

    "Ameenda haraka sana akiacha nyuma mambo mengi ambayo alikuwa bado amalize, lakini anatuacha na sanaa ya ajabu ambayo amefanya. Urithi wake utaendelea," meneja wake Bruce Intore Twagira ameiambia BBC.

    Mashabiki wake nchini Rwanda wamekuwa wakitumia mitandao kijamii kuomboleza kifo chake.

    "Alikuwa mtu wa heshima! Alipata heshima yangu tangu siku ya kwanza tulipokutana!" Nyota wa muziki wa Rwanda Andy Bumuntu alisema.

    Mwanamuziki wa Tanzania AY ametuma rambirambi zake kwenye Twitter:

  11. Viongozi wa SADC kufanya mazungumzo ya ukuaji wa kiuchumi

    Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika Sadc, watakutana leo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa mazungumzo kuhusu ukuaji wa uchumi na utangamano.

    Makumi ya wakuu wa nchi wamewasili katika mji mkuu, Kinshasa, siku ya Jumanne kushiriki kongamano hilo la siku mbili litakaloanza leo Jumatano.

    Viongozi hao watajadili namna ya kukuza uchumi wa viwanda kupitia mageuzi ya kilimo, uendelezaji wa rasilimali za madini na uendelezaji wa minyororo ya thamani katika ngazi ya mkoa.

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia inakusudia kutafuta usaidizi wa jumuiya hiyo kurejesha amani na usalama katika eneo lake.

    Lengo lingine la mkutano huo ni kukabidhiwa kwa uongozi wa kambi hiyo kwa Rais wa Kongo Felix Tshisekedi na mkuu wa sasa wa kambi hiyo,

    Rais wa Malawi Lazarus Chakwera. Ofisi ya Rais wa Congo ilituma picha za baadhi ya viongozi wa Afrika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter:

  12. Bolt Kusitisha huduma ya usafiri kwa wateja binafsi Tanzania

    Kampuni ya usafiri mtandaoni ya Bolt imetangaza kusitisha huduma za usafiri wa magari kwa wateja binafsi kuanzia leo Agosti 17 na kuanisha kuwa huduma hiyo sasa itapatikana kwa wateja wa kampuni na taasisi pekee.

    Hatua hiyo inakuja baada ya mazungumzo na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) kuhusu utaratibu wa utoaji huduma ikiwemo viwango elekezi vya makato na kamisheni kuchukua muda mrefu.

    Kwa upande wa serikali ya Tanzania imetangaza kuwa ukomo wa viwango vya makato ya kamisheni ya nauli za taksi mtandao kwa madereva vitabakia kuwa asilimia 15 kama vilivyopangwa mwezi April mwaka huu.

    Taarifa ya mamlaka ya udhibiti usafiri wa ardhini nchini Tanzania LATRA imesema baadhi ya kampuni za teksi mtandao zilizokuwa zikitoza kamisheni ya asilimia 20 hadi 31 hazikuridhika na kiwango elekezi cha asilimia 15.

    LATRA imethibitisha nia ya kampuni ya Bolt kufunga huduma zake za taksi mtadao nchini humo kuanzia leo Agosti 17.

    Soma:

  13. Matokeo ya uchaguzi Kenya: Sheria ya uchaguzi haikuvunjwa - Mshirika wa Ruto

    Mshirika wa kisiasa wa rais mteule wa Kenya William Ruto amepuuzilia mbali matakwa ya mpinzani wake Raila Odinga kwamba matokeo ya uchaguzi wa urais yafutiliwe mbali na kuwa batili.

    Musalia Mudavadi aliambia BBC kwamba "hakuna tatizo". "Tuna watu wachache ambao daima wako barabarani kupinga matokeo."

    Bw Odinga alidai kuwa mkuu wa tume ya uchaguzi alivunja sheria, kwa kutangaza matokeo Jumatatu jioni bila kuungwa mkono na makamishna wote saba.

    Lakini Bw Mudavadi alisema: "Makamishena hawaamui matokeo, makamishena wanakusanya matokeo... na matokeo yapo hadharani. Hakuna jambo lisilofaa."

    Maelezo zaidi:

  14. Elon Musk atania wazo la kuinunua Manchester United

    Bilionea Elon Musk ametania matarajio ya kuinunua Manchester United.

    Mwanzilishi wa Tesla alitoa maoni hayo katika tweet ya usiku wa manane.

    Musk aliandika: "Ili kuwa wazi, ninaunga mkono nusu ya kushoto ya Chama cha Republican na nusu ya kulia ya Chama cha Kidemokrasia! "Pia, ninainunua Manchester United karibu nawe."

    Ujumbe wake, ambao ulizua gumzo mitandaoni, ulivutia watu wengi kwa kasi na kupokea retweets zaidi ya 36,000 na karibu likes 200,000 ndani ya saa chache.

    Klabu hiyo ya Ligi ya Premia imekuwa ikimilikiwa na familia ya Glazer yenye maskani yake Florida tangu 2005.

    Umiliki wao umekuwa ukishutumiwa mara kwa mara na mashabiki kutokana na deni, mgao na usimamizi mbaya uliofuatia ununuzi wao uliozua utata.

    Glazers pia wamesimamia kushuka kwa kasi kwa maonyesho na matokeo katika miaka ya hivi karibuni.

    Rekodi ya mabingwa hao mara 20 wa Uingereza hawajashinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza tangu msimu wa mwisho wa Sir Alex Ferguson mwaka 2012-13 na hakuna aina ya fedha kwa miaka mitano.

  15. EU yatoa wito wa suluhu ya amani baada ya matokeo ya uchaguzi Kenya

    Muungano wa Ulaya (EU) umewapongeza Wakenya kwa uchaguzi wa amani na kuzitaka pande husika kutatua matatizo yaliyosalia kupitia njia za kisheria.

    Katika taarifa EU ilisema "imezingatia matokeo ya Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC), kumtangaza Bw William Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi na uamuzi wa kukata rufaa wa Bw Raila Odinga".

    “Viongozi wote wa kisiasa na kijamii lazima waepuke vurugu zozote na watoe wito wa utulivu. Ni wakati wa uongozi wa kisiasa na wajibu kutoka kwa wale wote wanaohusishwa na mchakato wa uchaguzi,” Mwakilishi Mkuu wa EU Josep Borrell alisema.

    Bw Borrell pia alimpongeza Rais Mteule Ruto.

    Bw Odinga, mshindi wa pili katika uchaguzi wa urais nchini Kenya, siku ya Jumanne alipina matokeo hayo na kuyataja kuwa "batili na batili" na kurudisha nyuma kidemokrasia.

    Bw Odinga alishindwa kwa kiasi kidogo na Bw Ruto - ambaye alitangazwa mshindi kwa 50.5% ya kura.

  16. Hujambo na karibu.