Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Ukraine: Lavrov- Rais wa Ukraine na Hitler wote wana damu ya kiyahudi
Waziri wa mambo ya nje wa Israel amekashifu matamshi ya waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov kuwa "hayawezi kusameheka" kwamba kiongozi wa Nazi Adolf Hitler "alikuwa na damu ya Kiyahudi".
Matamshi ya Lavrov yamekuja siku chache baada ya Israel kuadhimisha mauaji ya Nazi
Lavrov alitoa maoni ili kujaribu kukanusha taswira ya Urusi juu ya Ukraine kama "Nazi" licha ya ukweli kwamba rais wa Ukraine ni Myahudi.
Wizara ya mambo ya nje ya Israel ilimwita balozi wa Urusi kwa "ufafanuzi" na kumtaka aombe radhi.
Ujerumani ya Nazi iliwaua Wayahudi milioni sita katika mauaji ya Holocaust katika Vita vya Pili vya Dunia.
Bw Lavrov alisema hayo katika mahojiano katika kipindi cha televisheni cha Italia Zona Blanca siku ya Jumapili, siku chache baada ya Israel kuadhimisha Siku ya Ukumbusho wa Maangamizi ya Wayahudi, mojawapo ya matukio muhimu zaidi katika kalenda ya Israel.
Alipoulizwa jinsi Urusi inaweza kudai kwamba inapigania "kuondoa Unazi" Ukraine wakati Rais Volodymyr Zelensky yeye mwenyewe ni Myahudi, Bw Lavrov alisema: "Basi vipi ikiwa Zelensky ni Myahudi."
"Ukweli haukanushi vipengele vya Nazi nchini Ukraine. Ninaamini kwamba Hitler pia alikuwa na damu ya Kiyahudi," akiongeza kuwa "baadhi ya watu wabaya zaidi wanaopinga Uyahudi ni Wayahudi."
Waziri wa mambo ya nje wa Israel alijibu kwa hasira kauli ya Bw Lavrov, akimshutumu kwa chuki dhidi ya Wayahudi.
Bw Lavrov pia alilaaniwa na mkuu wa kumbukumbu ya mauaji ya Holocaust ya Israeli Dani Dayan.
"Matamshi yake mengi ni ya kipuuzi, ya udanganyifu, hatari na yanastahili kulaaniwa," aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.
"Lavrov anashughulika na kubatilishwa kwa mauaji ya Holocaust: kuwageuza waathiriwa kuwa wahalifu, kwa msingi wa kukuza dai lisilo na msingi kabisa kwamba Hitler alikuwa wa asili ya Kiyahudi."
Kwa miongo kadhaa kumekuwa na madai ambayo hayajathibitishwa kuwa baba yake Hitler ambaye hakutambulika alikuwa Myahudi, yakichochewa na madai ya wakili wa Hitler Hans Frank.
Katika kumbukumbu yake, iliyochapishwa mwaka wa 1953, Frank alisema alikuwa ameagizwa na Hitler kuchunguza uvumi kwamba alikuwa na ukoo wa Kiyahudi.
Frank alisema aligundua ushahidi kwamba babu wa Hitler alikuwa Myahudi kweli - ingawa madai hayo, ambayo yamepata msingi kati ya wananadharia wa njama, yametupiliwa mbali na wanahistoria wakuu.
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine