Makamishna wanne wa tume ya uchaguzi waliojitenga na matokeo
ya uchaguzi yaliyotangazwa hapo jana Jumamatu wamedai kwamba matokeo hayo sio
sahihi kwasababu Jumla ya asilimia iliyotolewa inapita asilimia 100.
Ni madai ambayo yamewekwa mitandaoni na wafuasi wa kiongozi
wa upinzani Raila Amollo Odinga.
Asilimia 100.10% inaweza kuelezewa kupitia hesabu.
Kwasababu ya kukadiria juu au chini wakati unapopiga hesabu za kila asilimia mpaka nafasi mbili za desimali, uwezekano wa kupata chini au zaidi ya 100% hutokea.
Unaweza tu kupata asilimia halisi ya 100% unapofanyia kazi sehemu zote za desimali.
Kulingana na matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa IEBC, mshindi William Ruto alipata 50.49% ya kura, Odinga (48.85%), George Wajackoyah (0.44%) na Mwaure Waihiga (0.23%).Jumla ni 100.01%.
Nambari zote zimekadiriwa hadi nafasi mbili za desimali na 0.01% ya ziada inaonekana kwa sababu nambari ya desimali kabla ya kukadiriwa ilikuwa tano au zaidi.
Makamishna hao hao pia walitoa madai yasiyo ya kweli kuwa 0.01% ya jumla ya kura halali zilizopigwa zingewakilisha kura 142,000 na kusema "italeta mabadiliko makubwa katika matokeo."Hatahivyo, idadi sahihi itakuwa kura 1,420.
Hata hivyo kuna tofauti ya kura 110 kati ya jumla ya kura halali zilizotangazwa na mwenyekiti, 14,213,137, na jumla ya kura zilizopatikana na wagombea wote wanne.
-
Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Raila Odinga apinga matokeo ya uchaguzi
-
Makamishna wa Tume ya Uchaguzi waliojitenga na matokeo wazungumza