Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Ukraine yaonya Urusi itazidisha mashambulizi inaposubiri ombi la kujiunga na EU

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonya kuwa Urusi itaimarisha mashambulizi dhidi ya nchi yake katika siku zijazo, wakati Kyiv ikisubiri jibu la ombi la kujiunga na EU.

Moja kwa moja

  1. Baada ya vikwazo vya Magharibi, Urusi sasa ni msambazaji mkubwa wa mafuta wa China

    Urusi imekuwa msambazaji mkubwa wa mafuta nchini China huku nchi hiyo ikiiuzia Beijing mafuta ghafi yaliyopunguzwa wakati huu kukiwa na vikwazo kutokana na vita vya Ukraine.

    Uagizaji wa mafuta ya Urusi umepanda kwa asilimia 55% kutoka mwaka mmoja uliopita hadi kiwango cha rekodi mnamo Mei, na kuiondoa Saudi Arabia kama msambazaji mkubwa wa China.

    China imeongeza ununuzi wa mafuta ya Urusi licha ya mahitaji yaliyopunguzwa na vizuizi vya Covid 19 na uchumi unaodorora.

    Mnamo Februari, Uchina na Urusi zilitangaza urafiki wao "usi na kikomo".

    Uagizaji huo nchini China, pamoja na usafirishaji kwa njia ya bahari, jumla ya tani 8.42m mwezi uliopita, kulingana na takwimu kutoka China.

    Hilo liliitoa Saudi Arabia kwenye nafasi ya kwanza kama msambazaji mkubwa wa mafuta ghafi nchini China - hadi kuwa nafasi ya pili ikiwa na tani 7.82m.

  2. Nyani amkwapua mtoto kutoka mikononi mwa mama yake nchini Tanzania

      • Author, Alfred Lasteck
      • Nafasi, BBC News, Dar es Salaam

    Mtoto mmoja Magharibi mwa Tanzania, amefariki dunia baada ya kuumia kichwa na shingo kwenye tukio la kushangaza la kuvamiwa na kundi la nyani wakati alipokuwa akinyonya nje ya nyumba yao.

    Katika tukio hilo lililotokea juma lililopita (Juni 18), kundi la nyani kutoka hifadhi ya Gombe inayopakana na Kijiji cha Mwamgongo, wilayani Kigoma walimvamia, Shayima Said, mama na mkazi wa eneo hilo na kuondoka na mtoto.

    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama alithibitishia BBC kutokea kwa tukio hilo mnamo Juni 18 na kueleza kuwa baada ya tukio hilo mwanamke huyo alipiga kelele kuomba msaada na ndipo majirani zake walipojitokeza kumdhibiti nyani aliyekuwa amebeba mtoto huyo.

    Hata hivyo alisema kuwa baada ya nyani huyo kuzidiwa, alimtupa mtoto huyo chini akiwa tayari amejeruhiwa kichwani na shingoni.

    "Wananchi walifanikiwa kulikimbiza kundi hilo la nyani lililomvamia mwanamke huyo wakati akimnyonyesha wanaye, na kufanikiwa kumpata mtoto akiwa amejeruhiwa lakini baada ya kufikishwa katika kituo cha afya cha Mwamgongo alifariki dunia,"amesema Kamanda Manyama.

  3. Kadyrov atangaza kutekwa kwa kijiji cha Toshkovka katika mkoa wa Luhansk

    Mkuu wa Chechnya, Ramzan Kadyrov, alitangaza kwamba wanajeshi wa Urusi wamechukua udhibiti wa kijiji cha Toshkovka katika mkoa wa Luhansk.

    Hakuna uthibitisho huru wa habari hii bado, lakini inajulikana kuwa vita vikali vya eneo hili vilidumu kwa takriban wiki mbili.

    Jana, katika taarifa ya asubuhi ya mfanyikazi Mkuu wa Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine, ilisemekana kuwa shambulio la kijeshi la Ukraine katika eneo la Toshkovka, adui alirudi nyuma na anajipanga tena.

    Toshkovka ni kijiji kidogo katika wilaya ya Popasnyansky ya mkoa wa Luhansk.

    Kulingana na mamlaka ya Ukraine, kwa sababu ya makombora ya mara kwa mara, kijiji kilifutwa kabisa kutoka kwa uso wa dunia.

    Hapo awali, Taasisi ya Marekani ya Utafiti wa Vita katika uchambuzi wao ilieleza kwa nini udhibiti wa Toshkovka ni muhimu kimkakati kwa jeshi la Kirusi.

    Kulingana na wataalam wa kijeshi, Urusi inajaribu kuepuka kuvuka hadi Donets Seversky, ambako tayari amewahi kushindwa na kupata hasara kubwa na itaingia Lisichansk kutoka kusini.

    Kwa hivyo, wanataka kuingia kwenye mipaka ya kiutawala ya mkoa wa Lugansk.

    Soma zaidi:

    • Baba, karibu tena nchini - binti wa Lumumba

      Katika hafla ya heshima katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, mabaki ya pekee ya kiongozi wa uhuru wa Congo Patrice Lumumba yamerejeshwa kwa familia yake.

      Jino lenye taji la dhahabu la kiongozi aliyenyongwa lilichukuliwa na polisi wa Ubelgiji ambaye alikuwa ameshtakiwa kwa kutupa mwili wa waziri mkuu wa kwanza wa Congo.

      Binti wa Lumumba, Juliana, alitoa hotuba iliyojaa hisia katika sherehe hiyo:

      ‘’Baba, ndugu zangu na mimi, pamoja na watoto wetu, na vitukuu zako, tumejaribu kupitia hotuba hii, kutafuta maneno ya kukuaga miaka 61 baada ya kutoweka kwako, lakini tunapaswa kukiri kwamba hakuna kinachoweza kueleza kile tunachohisi leo.''

      ''Tunaweza tu kutamani kwamba popote ulipo, unaweza kujivunia watoto wako, wajukuu zako na vitukuu zako.''

      Baba karibu tena nchini, asante. ‘’Tunatamani tu kwamba popote ulipo, ujivunie watoto wako, wajukuu zako na vitukuu zako. Baba karibu tena nchini, asante.’’

      Soma zaidi:

    • Ukraine: Wakazi wa Mariupol hawana maji ya kunywa ya kutosha

      Wakazi wa Mariupol hawana maji ya kunywa ya kutosha - Meya wa jiji la Mariupol, Vadim Boychenko, alisema kuwa wakaazi wa jiji hilo lililokaliwa na Urusi wako kwenye hatihati ya kuishi kwa sababu ya ukosefu wa maji ya kunywa.

      " Zaidi ya watu 100,000 ambao bado wamesalia jijini hawana maji safi ya kunywa," meya wa Halmashauri ya Jiji la Mariupol, alinukuliwa akisema maneno kupitia njia yake rasmi ya telegram.

      Kulingana na Boichenko, sasa mamlaka zinazokalia zinawapa wakazi maji mara moja kwa wiki, na wakazi wa jiji husimama kwenye foleni kwa saa 4-8 ili kuyapata.

      Kwa kuongezea, jiji limeachwa bila umeme, gesi na mifumo ya mifereji ya maji, meya alisisitiza.

      Boychenko anaamini kwamba ni muhimu "kufungua ukanda usioruhusiwa vitakuokoa watu."

      Mapema mwezi wa Juni, katika mahojiano na BBC, Boychenko alisema kwamba ugonjwa wa "kipindupindu, kuhara damu na magonjwa mengine ya kuambukiza yanazunguka jiji humo, lakini [mamlaka iliyovamia na kulikalia eneo] inaficha ukweli. Jiji hilo liliwekwa karantini. Hakuna mtu anayeruhusiwa kutoka au kuingia."

      Soma zaidi:

    • Kenya: Ni lazima kuvaa barakoa katika maeneo ya umma

      Waziri wa Afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe ametangaza kurejea kwa uvaaji wa barakoa wa lazima katika maeneo ya usafiri wa umma, ndege, ofisini katika maduka makubwa na maeneo ya ibada.

      Kufuata taarifa zinazotolewa na wizara hiyo mara kwa mara kufahamisha watu jinsi hali inavyoedelea, waziri alieleza kwamba maambukizi yamekuwa yakiongezeka katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

      ‘’Ongezeko la taratibu limeshuhudiwa kutoka asilimia 0.6 mwanzoni mwa mwezi mei 2022 hadi wastani wa kila wiki wa asilimia 10.74 katika wiki iliyoisha ya Juni 19 2022,’’ Waziri kangwe alisema.

      Ameongeza kuwa kwa kasi hii ya ongezeko la maambukizi ni wakati raia wanastahili kuchukua hatua ili kuepuka kilichoshuhudiwa mwaka 2020 na 2021 kupoteza maisha ya watu wengi na mali.

      Mikutano ya pamoja ya watu wengi katika sehemu moja ya ndani, imeruhusiwa mradi washiriki wote wawe wamepata chanjo. Lakini pia imekuwa lazima kwa wote kuvaa barakoa na pia waonyeshe thibitisho kwamba wamepata chanjo.

      Hali ilikuwa hiyo hiyo kwa maeneo ya kuabudu.

      ‘’Idadi ya watu katika maeneo ya kuabudu haina kikomo mradi wote waliokusanyika wamepata chanjo kikamilifu. Pia wote watatakiwa kuvaa barakoa wakiwa ndani ya maeneo ya kuabudu.’’

      Wakati huo huo, Bwana Kagwe aliomba wale ambao bado hawajapokea chanjo, kuchanjwa kwa haraka sana akisema Wakenya wote wanapaswa kuchukua tahadhari.

      ‘’Wale ambao hawajachanjwa wafanye hivyo mara moja. Waliochanjwa na wanaohitaji nyongeza, pia wafanye hivyo mara moja,’’ Kagwe alisema.

      Kagwe aliongeza kuwa hali ya maambukizi huenda ikawa mbaya zaidi katika wiki zijazo kutokana na msimu huu ambao ni hali ya hewa ya baridi.

      Soma zaidi:

    • Waziri Mkuu wa Ethiopia alaani mauaji ya kutisha ya kikabila

      Abiy Ahmed mara nyingi anakosolewa kwa kushindwa kukabiliana na hali mbaya ya ukosefu wa usalama

      Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ametaja mauaji "ya kutisha" ya makabila madogo madogo katika mashambulizi magharibi mwa nchi hiyo akisema "hayakubaliki" na kwamba kurejesha amani na usalama ndio kipaumbele cha serikali yake.

      Hakuna takwimu rasmi ya idadi ya waliouawa katika mashambulizi ya Jumamosi lakini baadhi ya ripoti zinaonyesha inaweza kuwa zaidi ya 100.

      Waziri mkuu mara nyingi anakosolewa kwa kushindwa kukabiliana na hali mbaya ya ukosefu wa usalama nchini Ethiopia.

      Kumekuwa na ongezeko kubwa la ghasia za kijamii na migogoro ya kikabila ambalo halijawahi kushuhudiwa tangu aingie madarakani miaka minne iliyopita.

      Sasa Bw Abiy anasema utawala wake "hauna uvumilivu kabisa" kwa mauaji ya raia.

      Tukio la hivi punde zaidi lilikuwa huko Oromia magharibi, eneo kubwa zaidi nchini.

      Walioshuhudia waliambia BBC kuwa watu walizikwa katika makaburi ya halaiki na nyumba zilichomwa moto wakati wanajeshi wa Oromo Liberation Army (OLA) walipoanzisha mashambulizi dhidi ya vijiji vinavyokaliwa na watu wa makabila madogo ya Amhara.

      Kundi hilo linakanusha kutekeleza mashambulizi hayo na badala yake linailaumu serikali.

      Mapigano kati ya serikali na OLA yameripotiwa magharibi mwa Oromia na kusababisha wasiwasi kwamba raia wanaweza kunaswa katika mapigano hayo.

    • Urusi inazuia mashambulizi ya Ukraine kwa usafiri wa anga

      Mkuu wa Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine alichapisha ripoti ya asubuhi juu ya hali ilivyo vitani.

      Hapa kuna mambo makuu aliyoangazia:

      Katika ukanda wenye uhasama mashariki na kusini, Warusi wanatumia kikamilifu ndege za kivita na mizinga katika maeneo mengi - ili kuzuia kusonga mbele kwa askari wa Ukraine.

      Mashambulizi kama hayo yalifanywa na wanajeshi wa Urusi huko Slobozhansky, Kharkov, Slavyansky, Donetsk, Severodonetsky, Bakhmutsky, Limansky, Avdeevsky, Kurakhovsky, Novopavlovsky na maeneo ya Zaporozhye, ripoti hiyo inasema.

      Katika eneo la Kharkiv, juhudi kuu za wanajeshi wa Urusi zinalenga kuzuia kusonga mbele kwa vikosi vya ulinzi kwenye mpaka wa jimbo la Ukraine.

      Vikosi vya Urusi vilifyatua risasi kwa nguvu kutoka maeneo ya makazi ya Kazachya Lopan, Malye Prohody, Dementievka, Petrovka, Verkhniy Saltov, Rubizhnoye na Kharkov.

      Katika eneo la Donetsk, askari wa Urusi wanaendelea kuzingatia juhudi zao kuu kwenye eneo la Severodonetsk na Bakhmut, na matumizi makubwa ya anga.

      Mapigano yanaendelea kuchukua eneo la Severodonetsk kuwa chini ya udhibiti.

      Katika eneo la Severodonetsk, askari wa Urusi walifyatua mizinga na makombora katika maeneo ya makazi ya Lisichansk, Sirotino, Voronovo, Borovskoye, Belaya Gora, Ustinovka, Mirnaya Dolina, Toshkovka na kuzindua mashambulizi ya anga kutoka kwa ndege ya Su-25 karibu na Belaya Gora na Mirnaya.

      Katika eneo la Limansky, Avdievsky, Kurakhovsky, Novopavlovsky na Zaporozhye, vikosi vya Urusi vinajaribu kuzuia kuunganishwa tena kwa wanajeshi wa Ukraine.

      Katika eneo la Liman, wanajeshi wa Urusi walizindua shambulio la anga na ndege mbili za Su-25 karibu na kijiji cha Prishib na shambulio la kombora karibu na kijiji cha Mayaki.

      Katika eneo la Yuzhnobuzh, Urusi inaelekeza nguvu zake katika kushikilia maeneo yaliyokaliwa na kuzuia mashambulizi ya wanajeshi wa Ukraine.

      Katika maji ya Bahari Nyeusi na Azov, juhudi kuu za kikundi cha meli za wanajeshi wa Urusi zinalenga kuzuia shughuli za usafiri wa raia kaskazini-magharibi mwa Bahari Nyeusi

      Soma zaidi:

    • Jeshi la Ukraine lapoteza udhibiti wa Metolkin karibu na Severodonetsk - Gaidai

      Mkuu wa utawala wa kijeshi wa eneo la Lugansk, Sergei Gaidai, alisema kuwa wanajeshi wa Ukraine wamepoteza udhibiti wa kijiji cha Metelkino karibu na Severodonetsk.

      "Mapigano yanaendelea katika vijiji vingi karibu na Severodonetsk na Lisichansk. Kwa bahati mbaya, kwa sasa hatudhibiti eneo la Metelkino karibu na kituo cha kikanda," Gaidai alisema.

      Asubuhi ya Juni 20, Urusi ilizidisha ufyatuaji wa risasi na makombora ya anga, katika eneo la viwanda la Severodonetsk na nje kidogo ya jiji likateseka zaidi, anaandika mkuu wa Luhansk OVA Sergei Gaidai.

      Urusi inataka kupata mafanikio na mapigano yanafanyika katika vijiji vingi karibu na Severodonetsk na Lysychansk.

      Anasisitiza kuwa suluhu iliyopotea sio "kupoteza katika vita".

      "Mkoa wa Luhansk utatetewa hadi mwisho, tutazuia jeshi kwa muda mrefu iwezekanavyo," mkuu wa OVA aliandika.

      Kulingana na yeye, "uokoaji wenye utulivu" unaendelea kwenye eneo la Lysychansk.

      Gaidai anadai kwamba Lysychansk inateseka sana kutokana na kushambuliwa kwa makombora, na kwamba "wasaliti wa ndani" wanachochea.

      Soma zaidi:

    • Kwa picha: Mkutano wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola waanza Kigali Rwanda

      Bendera za nchi 54 wanachama wa Jumiya ya Madola (CHOGM) umeanza mjini Kigali Rwanda. Wakuu wa nchi za CHOGM na wajumbe zaidi ya 5,000 wanakongamana kushiriki mkutano huu ambao awali uliahirishwa mara mbili kutokana na janga la Covid-19. Wajumbe wanatarajiwa kujadili ushirikiano baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya madola katika nyanja mbali mbali, mkiwemo uchumi na elimu, biashara, utamaduni na mazingira

      Serikali ya Rwanda inatazamia kutumia mkutano huu hususan kunadi utalii wa nchi hiyo huku wafanyabiashara wa sekta ya hoteli na migahawa wakiytarajiwa kunufaika kutokana na wateja wanaoshiriki mkutano huu. Hizi ni baadhi ya picha kuhusiana na CHOGM kutoka Kigali:

      Maandalizi ya CHOGM Rwanda yamekuwa yakitawala mitandao ya kijamii hususan ni ule wa Twitter ambapo watu mbali mbali wamekuwa wakishirikishana picha za jinsi mji wa Kigali ulivyojiandaa kwa mkutano huu wa kimataifa.

    • Jino la Lumumba lawasilishwa kwa familia yake mjini Brussels

      Mamlaka ya Ubelgiji imekabidhi jino la kiongozi wa uhuru wa Congo Patrice Lumumba kwa familia yake katika hafla iliyofanyika Brussels.

      Jino hilo nii sehemu pekee ya mabaki ya mwili wake ambayo inadhaniwa kuwa bado ipo baada ya kunyongwa na kisha mwili wake kuyeyushwa kwa tindikali mnamo 1961.

      Ubelgiji ilikuwa mamlaka ya zamani ya kikoloni na uchunguzi rasmi ulisema kwamba baadhi ya wanachama wa serikali yake wakati huo "waliwajibika kimaadili kwa hali iliyosababisha kifo".

      Polisi wa Ubelgiji Gerard Soete, aliyesimamia kuharibiwa kwa mwili huo, alichukua jino hilo kama "aina ya nyara ya uwindaji", baadaye alisema.

      Soma:

    • Viongozi wa Afrika Mashariki wawasili Kenya kujadili mzozo wa DR Congo

      Viongozi wa mataifa saba yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajiwa kukutana kujadili hali ya usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kulingana na taarifa ya serikali.

      Viongozi hao wanakutana kwa mualiko wa mwenyeji wao Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.

      Muda mfupi uliopita Rais wa Uganda Yoweri Museveni amethibitisha kwenye mtandao wake rasmi wa Twitter kwamba amewasili jijini Nairobi kkuhudhuria Kikao cha Tatu cha Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

      Rais Kenyatta alitoa wito wa kupelekwa kwa Kikosi cha Kudumu cha Afrika Mashariki ili kukomesha ghasia katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo.

      DRC hata hivyo inapinga Rwanda kuwa sehemu ya jeshi lililopendekezwa la kikanda na imesitisha uhusiano wa pande mbili na Kigali.

      Nchi hiyo inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao hivi majuzi waliuteka mji wa mpakani Bunagana.

      Rwanda inakanusha madai hayo.

      Rais Felix Tshisekedi katika taarifa yake aliishutumu Rwanda kwa kutaka kuikalia kimabavu nchi yake ili kutumia madini yake na kuitaka Uingereza kuishinikiza Kigali kukomesha uchokozi wake.

      Mvutano kati ya nchi hizo mbili umeongezeka katika wiki za hivi karibuni huku maandamano ya kuipinga Rwanda yakiripotiwa mjini Kinshasa na mashariki mwa Congo.

      Siku mbili zilizopita, mwanajeshi wa Congo aliwafyatulia risasi walinda usalama wa Rwanda katika kituo cha mpakani mjini Bukavu na kuwajeruhi maafisa wawili wa polisi.

      Kenya ndiyo mwenyeji wa mazungumzo ya moja kwa moja ya amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na makundi tofauti vya waasi.

      Mazungumzo hayo bado hayajazaa matokeo yoyote.

    • Watu 20 wauawa katika mashambulio la wanamgambo wa kijihadi Mali

      Karibu watu 20 wameuawa katika shambulio linaotuhumiwa kutekelezwa na wapiganaji wa kijihadi kaskazini mwa Mali, ofisi ya kikanda katika eneo hilo inasema.

      Ghasia za Jumamosi zilitokea karibu na mji wa Gao.

      Afisa huyo aliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba hali ilikuwa tete kwani raia walikuwa wakitoroka wakato wanamgambo hao walipokuwa wakifanya unyama dhidi yao.

      Umoja wa Mataifa unasema hali ya usalama katika maeneo ya Gao na Ménaka imezorota vibaya.

      Mapema Jumapili walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliuawa karibu na mgodi mmoja huko Kidal kaskazini mwa nchi.

    • Uchaguzi wa Ufaransa: Macron apoteza udhibiti wa bunge la Ufaransa

      Chini ya miezi miwili baada ya kuchaguliwa tena kuwa rais, Emmanuel Macron amepoteza udhibiti wa Bunge la Ufaransa kufuatia utendaji mzuri wa muungano wa kushoto na mrengo wa kulia.

      Bw. Macron alikuwa ametoa wito kwa wapiga kura kupiga kura kwa wingi ili wapate uongozi thabiti.

      Lakini muungano wake wa centrist ulipoteza makumi ya viti katika uchaguzi huo ambao umesababisha mgawanyiko mkubwa katika siasa za Ufaransa.

      Waziri mkuu ambaye alikuwa amemteua hivi majuzi, Elisabeth Borne, alisema hali hiyo haikuwa ya kawaida.

      Dhoruba ilipiga Paris aliporejea kwenye makazi yake ya Matignon kutoka kwa mkutano wa muda mrefu katika ikulu ya Élysée kusema kwamba Ufaransa ya kisasa haijawahi kuwa na Bunge kama hili.

      Kiongozi wa mrengo wa kushoto Jean-Luc Mélenchon amekuwa akifurahia mafanikio yake ya kuleta pamoja vyama vikuu kutoka upande wa kushoto na Wakomunisti na Greens katika muungano unaofahamika kama Nupes.

      Aliwaambia wafuasi wake kwamba chama cha urais kimepata pigo kubwa na kwamba uwezo uko mikononi mwao.

      • 'Kitabu cha Hitler na silaha zapatikana' baada ya Macron kuzabwa kofi
      • Je, Ufaransa kuiomba radhi Rwanda?
      • Mke wa rais wa Ufaransa afungua kesi kuhusu madai ya kuzaliwa akiwa mwanamume
    • Philippines: Sara Duterte aapishwa kuwa makamu wa rais

      Binti mkubwa wa Rais wa Ufilipino anayeondoka madarakani Rodrigo Duterte ameapishwa kuwa makamu wa rais wa nchi hiyo.

      Sara Duterte ameapa kuwaunganisha Wafilipino katika hafla ya kuapishwa kwake mjini Davao.

      Ni katika mji huo ambapo Sara mwenye umri wa miaka 44-alichukua usukani kutoka kwa baba yake kama Meya kwa zaidi yamwongo mmoja uliopita -kabla ya kujitosa katika siasa za kitaifa.

      Alikula kiapo kando ya mgombea mwenzake, Ferdinand Marcos Junior, ambaye hivi karibuni atachukua nafasi ya baba yke kama rais.

      "Siku zinazokuja zinatarajiwa kuwa na changamoto ambazo zinatuhitaji kuwa na mshikamano kama taifa," Bi Duterte alisema.

      Muhula wake wa miaka sita madarakani ukiongozwa na Ferdinand Marcos Junior utaanza rasmi Juni 30.

      Kama wangombea katika uchaguzi wa mwezi Mei wawili hao walipata ushindi wa kishindo kwa kubuni muungano thabiti wa kisiasa na kutumia kauli mbiu ya umoja ambao utasaidia baadhi ya washirika wao pia kupata uongozi katika ngazi zingine za serikali.

      Nchini Ufilipino , rais na makamu wake wanachaguliwa kando kando.

      Bw. Duterte ni mtu mwenye utata ambaye aliingia madarakani mwaka 2016 akiahidi kupunguza uhalifu na kukabiliana na janga la dawa za kulevya.

      Lakini wakosoaji wanasema katika kipindi cha miaka mitano madarakani, Bw Duterte alwahimiza polisi kutekeleza maelfu ya mauaji ya kiholela ya washukiwa katika kile alichokiita "vita vyake dhidi ya mihadarati".

      Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imetaka uchunguzi ufanyike rasmi kuhusu maelfu ya mauaji yaliyotokea wakati wa msako huo mkali.

    • Ukraine yaonya Urusi itazidisha mashambulizi inaposubiri ombi la kujiunga na EU

      Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonya Urusi itazidisha mashambulizi dhidi ya nchi yake katika siku zijazo, huku Kyiv ikisubiri jibu kuhusu azma yake ya kujiunga na Muungano wa Ulaya (EU).

      Wanachama wa Muungano huo wanatarajiwa kuamua ikiwa watatoa "hadhi ya mgombea" kwa Kyiv baadaye wiki hii.

      Hatua hiyo itanzisha mchakato wa Ukraine kujiunga na muungano huo, ambao unaweza kuchukua miaka kadhaa kukamilika.

      Lakini Bw Zelensky alionya uamuzi huo unaweza kuifanya Urusi kuongeza mashambulizi yake.

      Akizungumza wakati wa hotuba yake ya usiku kutoka Kyiv, kiongozi huyo wa Ukraine alisema yeye na washauri wake wanatarajia "shughuli kubwa zaidi ya uadui" kutoka Moscow, lakini aliwaambia raia kwamba vikosi vyake "vinajiandaa" na viko tayari kwa mashambulizi yoyote mapya.

      Aliahidi kuendelea mbele kile alichokiita matarajio ya "kihistoria" ya Ukraine kujiunga na EU, ambayo yaliidhinishwa na watendaji wakuu wa umoja huo, Tume ya Ulaya, wiki iliyopita.

      Lakini sasa uamuzi huo uko mikononi mwa Baraza la Ulaya, chombo kilichoundwa na viongozi wa Nchi Wanachama, ambacho kitakutana katika mkutano wa kilele huko Brussels siku ya Alhamisi na Ijumaa.

    • Hujambo na karibu.