Ukraine yaonya Urusi itazidisha mashambulizi inaposubiri ombi la kujiunga na EU
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonya kuwa Urusi itaimarisha mashambulizi dhidi ya nchi yake katika siku zijazo, wakati Kyiv ikisubiri jibu la ombi la kujiunga na EU.
Moja kwa moja
Baada ya vikwazo vya Magharibi, Urusi sasa ni msambazaji mkubwa wa mafuta wa China
Chanzo cha picha, Getty Images
Urusi imekuwa
msambazaji mkubwa wa mafuta nchini China huku nchi hiyo ikiiuzia Beijing mafuta
ghafi yaliyopunguzwa wakati huu kukiwa na vikwazo kutokana na vita vya Ukraine.
Uagizaji wa
mafuta ya Urusi umepanda kwa asilimia 55% kutoka mwaka mmoja uliopita hadi
kiwango cha rekodi mnamo Mei, na kuiondoa Saudi Arabia kama msambazaji mkubwa wa
China.
China imeongeza
ununuzi wa mafuta ya Urusi licha ya mahitaji yaliyopunguzwa na vizuizi vya
Covid 19 na uchumi unaodorora.
Mnamo Februari,
Uchina na Urusi zilitangaza urafiki wao "usi na kikomo".
Uagizaji huo
nchini China, pamoja na usafirishaji kwa njia ya bahari, jumla ya tani 8.42m
mwezi uliopita, kulingana na takwimu kutoka China.
Hilo liliitoa Saudi Arabia kwenye nafasi ya
kwanza kama msambazaji mkubwa wa mafuta ghafi nchini China - hadi kuwa nafasi
ya pili ikiwa na tani 7.82m.
Nyani amkwapua mtoto kutoka mikononi mwa mama yake nchini Tanzania
Maelezo kuhusu taarifa
Author, Alfred Lasteck
Nafasi, BBC News, Dar es Salaam
Chanzo cha picha, Getty Images
Mtoto
mmoja Magharibi mwa Tanzania, amefariki dunia baada ya kuumia kichwa na shingo
kwenye tukio la kushangaza la kuvamiwa na kundi la nyani wakati alipokuwa
akinyonya nje ya nyumba yao.
Katika
tukio hilo lililotokea juma lililopita (Juni 18), kundi la nyani kutoka
hifadhi ya Gombe inayopakana na Kijiji cha Mwamgongo, wilayani Kigoma
walimvamia, Shayima Said, mama na mkazi wa eneo hilo na kuondoka na mtoto.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama alithibitishia BBC kutokea kwa tukio hilo
mnamo Juni 18 na kueleza kuwa baada ya tukio hilo mwanamke huyo alipiga kelele
kuomba msaada na ndipo majirani zake walipojitokeza kumdhibiti nyani
aliyekuwa amebeba mtoto huyo.
Hata
hivyo alisema kuwa baada ya nyani huyo kuzidiwa, alimtupa mtoto huyo chini
akiwa tayari amejeruhiwa kichwani na shingoni.
"Wananchi
walifanikiwa kulikimbiza kundi hilo la nyani lililomvamia mwanamke huyo wakati
akimnyonyesha wanaye, na kufanikiwa kumpata mtoto akiwa amejeruhiwa
lakini baada ya kufikishwa katika kituo cha afya cha Mwamgongo alifariki
dunia,"amesema Kamanda Manyama.
Kadyrov atangaza kutekwa kwa kijiji cha Toshkovka katika mkoa wa Luhansk
Maelezo ya picha, Taasisi ya utafiti kuhusu vita
Mkuu wa
Chechnya, Ramzan Kadyrov, alitangaza kwamba wanajeshi wa Urusi wamechukua
udhibiti wa kijiji cha Toshkovka katika mkoa wa Luhansk.
Hakuna
uthibitisho huru wa habari hii bado, lakini inajulikana kuwa vita vikali vya eneo
hili vilidumu kwa takriban wiki mbili.
Jana, katika
taarifa ya asubuhi ya mfanyikazi Mkuu wa Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine,
ilisemekana kuwa shambulio la kijeshi la Ukraine katika eneo la Toshkovka, adui
alirudi nyuma na anajipanga tena.
Toshkovka ni
kijiji kidogo katika wilaya ya Popasnyansky ya mkoa wa Luhansk.
Kulingana na
mamlaka ya Ukraine, kwa sababu ya makombora ya mara kwa mara, kijiji kilifutwa
kabisa kutoka kwa uso wa dunia.
Hapo awali,
Taasisi ya Marekani ya Utafiti wa Vita katika uchambuzi wao ilieleza kwa nini
udhibiti wa Toshkovka ni muhimu kimkakati kwa jeshi la Kirusi.
Kulingana na
wataalam wa kijeshi, Urusi inajaribu kuepuka kuvuka hadi Donets Seversky, ambako
tayari amewahi kushindwa na kupata hasara kubwa na itaingia Lisichansk kutoka
kusini.
Kwa hivyo,
wanataka kuingia kwenye mipaka ya kiutawala ya mkoa wa Lugansk.
Maelezo ya picha, Roland, Juliana na Francois Lumumba, watoto wa marehemu Patrice Lumumba wakiwa wamesimama mbele ya jeneza kwenye sherehe iliyofanyika Brussels.
Katika hafla ya heshima katika mji mkuu wa Ubelgiji,
Brussels, mabaki ya pekee ya kiongozi wa uhuru wa Congo Patrice Lumumba
yamerejeshwa kwa familia yake.
Jino lenye taji la dhahabu la kiongozi aliyenyongwa
lilichukuliwa na polisi wa Ubelgiji ambaye alikuwa ameshtakiwa kwa kutupa mwili
wa waziri mkuu wa kwanza wa Congo.
Binti wa Lumumba, Juliana, alitoa hotuba iliyojaa hisia
katika sherehe hiyo:
‘’Baba, ndugu zangu na mimi, pamoja na watoto wetu, na
vitukuu zako, tumejaribu kupitia hotuba hii, kutafuta maneno ya kukuaga miaka
61 baada ya kutoweka kwako, lakini tunapaswa kukiri kwamba hakuna kinachoweza
kueleza kile tunachohisi leo.''
''Tunaweza tu kutamani kwamba popote
ulipo, unaweza kujivunia watoto wako, wajukuu zako na vitukuu zako.''
Baba karibu tena nchini, asante. ‘’Tunatamani tu kwamba
popote ulipo, ujivunie watoto wako, wajukuu zako na vitukuu zako. Baba karibu tena nchini, asante.’’
Ukraine: Wakazi wa Mariupol hawana maji ya kunywa ya kutosha
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mamlaka zinazokalia zinawapa wakazi maji mara moja kwa wiki
Wakazi wa
Mariupol hawana maji ya kunywa ya kutosha - Meya wa jiji la Mariupol, Vadim
Boychenko, alisema kuwa wakaazi wa jiji hilo lililokaliwa na Urusi wako kwenye
hatihati ya kuishi kwa sababu ya ukosefu wa maji ya kunywa.
" Zaidi
ya watu 100,000 ambao bado wamesalia jijini hawana maji safi ya kunywa," meya
wa Halmashauri ya Jiji la Mariupol, alinukuliwa akisema maneno kupitia njia
yake rasmi ya telegram.
Kulingana na
Boichenko, sasa mamlaka zinazokalia zinawapa wakazi maji mara moja kwa wiki, na
wakazi wa jiji husimama kwenye foleni kwa saa 4-8 ili kuyapata.
Kwa
kuongezea, jiji limeachwa bila umeme, gesi na mifumo ya mifereji ya maji, meya
alisisitiza.
Boychenko
anaamini kwamba ni muhimu "kufungua ukanda usioruhusiwa vitakuokoa watu."
Mapema mwezi
wa Juni, katika mahojiano na BBC, Boychenko alisema kwamba ugonjwa wa "kipindupindu,
kuhara damu na magonjwa mengine ya kuambukiza yanazunguka jiji humo, lakini
[mamlaka iliyovamia na kulikalia eneo] inaficha ukweli. Jiji hilo liliwekwa
karantini. Hakuna mtu anayeruhusiwa kutoka au kuingia."
Kenya: Ni lazima kuvaa barakoa katika maeneo ya umma
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Lazima ya kuvaa barakoa katika maeneo ya umma yarejeshwa Kenya
Waziri wa Afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe ametangaza
kurejea kwa uvaaji wa barakoa wa lazima katika maeneo ya usafiri wa umma,
ndege, ofisini katika maduka makubwa na maeneo ya ibada.
Kufuata taarifa zinazotolewa na wizara hiyo mara kwa mara
kufahamisha watu jinsi hali inavyoedelea, waziri alieleza kwamba maambukizi
yamekuwa yakiongezeka katika kipindi cha wiki moja iliyopita.
‘’Ongezeko la taratibu limeshuhudiwa kutoka asilimia 0.6
mwanzoni mwa mwezi mei 2022 hadi wastani wa kila wiki wa asilimia 10.74 katika
wiki iliyoisha ya Juni 19 2022,’’ Waziri kangwe alisema.
Ameongeza kuwa kwa kasi hii ya ongezeko la maambukizi ni
wakati raia wanastahili kuchukua hatua ili kuepuka kilichoshuhudiwa mwaka 2020
na 2021 kupoteza maisha ya watu wengi na mali.
Mikutano ya pamoja ya watu wengi katika sehemu moja ya
ndani, imeruhusiwa mradi washiriki wote wawe wamepata chanjo. Lakini pia
imekuwa lazima kwa wote kuvaa barakoa na pia waonyeshe thibitisho kwamba
wamepata chanjo.
Hali ilikuwa hiyo hiyo kwa maeneo ya kuabudu.
‘’Idadi ya watu katika maeneo ya kuabudu haina kikomo
mradi wote waliokusanyika wamepata chanjo kikamilifu. Pia wote watatakiwa kuvaa
barakoa wakiwa ndani ya maeneo ya kuabudu.’’
Wakati huo huo, Bwana Kagwe aliomba wale ambao bado
hawajapokea chanjo, kuchanjwa kwa haraka sana akisema Wakenya wote wanapaswa
kuchukua tahadhari.
‘’Wale ambao
hawajachanjwa wafanye hivyo mara moja. Waliochanjwa na wanaohitaji nyongeza,
pia wafanye hivyo mara moja,’’ Kagwe alisema.
Kagwe aliongeza kuwa hali ya maambukizi huenda ikawa
mbaya zaidi katika wiki zijazo kutokana na msimu huu ambao ni hali ya hewa ya
baridi.
Waziri Mkuu wa Ethiopia alaani mauaji ya kutisha ya kikabila
Chanzo cha picha, af
Maelezo ya picha, Abiy Ahmed mara nyingi anakosolewa kwa kushindwa kukabiliana na hali mbaya ya ukosefu wa usalama
Abiy Ahmed
mara nyingi anakosolewa kwa kushindwa kukabiliana na hali mbaya ya ukosefu wa
usalama
Waziri Mkuu
wa Ethiopia Abiy Ahmed ametaja mauaji "ya kutisha" ya makabila madogo
madogo katika mashambulizi magharibi mwa nchi hiyo akisema "hayakubaliki" na kwamba
kurejesha amani na usalama ndio kipaumbele cha serikali yake.
Hakuna
takwimu rasmi ya idadi ya waliouawa katika mashambulizi ya Jumamosi lakini
baadhi ya ripoti zinaonyesha inaweza kuwa zaidi ya 100.
Waziri mkuu
mara nyingi anakosolewa kwa kushindwa kukabiliana na hali mbaya ya ukosefu wa
usalama nchini Ethiopia.
Kumekuwa na
ongezeko kubwa la ghasia za kijamii na migogoro ya kikabila ambalo halijawahi
kushuhudiwa tangu aingie madarakani miaka minne iliyopita.
Sasa Bw Abiy
anasema utawala wake "hauna uvumilivu kabisa" kwa mauaji ya raia.
Tukio la
hivi punde zaidi lilikuwa huko Oromia magharibi, eneo kubwa zaidi nchini.
Walioshuhudia
waliambia BBC kuwa watu walizikwa katika makaburi ya halaiki na nyumba
zilichomwa moto wakati wanajeshi wa Oromo Liberation Army (OLA) walipoanzisha
mashambulizi dhidi ya vijiji vinavyokaliwa na watu wa makabila madogo ya
Amhara.
Kundi hilo
linakanusha kutekeleza mashambulizi hayo na badala yake linailaumu serikali.
Mapigano
kati ya serikali na OLA yameripotiwa magharibi mwa Oromia na kusababisha
wasiwasi kwamba raia wanaweza kunaswa katika mapigano hayo.
Urusi inazuia mashambulizi ya Ukraine kwa usafiri wa anga
Chanzo cha picha, AFP
Mkuu wa
Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine alichapisha ripoti ya asubuhi juu ya hali ilivyo
vitani.
Hapa kuna
mambo makuu aliyoangazia:
Katika
ukanda wenye uhasama mashariki na kusini, Warusi wanatumia kikamilifu ndege za
kivita na mizinga katika maeneo mengi - ili kuzuia kusonga mbele kwa askari wa Ukraine.
Mashambulizi
kama hayo yalifanywa na wanajeshi wa Urusi huko Slobozhansky, Kharkov,
Slavyansky, Donetsk, Severodonetsky, Bakhmutsky, Limansky, Avdeevsky,
Kurakhovsky, Novopavlovsky na maeneo ya Zaporozhye, ripoti hiyo inasema.
Katika eneo
la Kharkiv, juhudi kuu za wanajeshi wa Urusi zinalenga kuzuia kusonga mbele kwa
vikosi vya ulinzi kwenye mpaka wa jimbo la Ukraine.
Vikosi vya
Urusi vilifyatua risasi kwa nguvu kutoka maeneo ya makazi ya Kazachya Lopan,
Malye Prohody, Dementievka, Petrovka, Verkhniy Saltov, Rubizhnoye na Kharkov.
Katika eneo
la Donetsk, askari wa Urusi wanaendelea kuzingatia juhudi zao kuu kwenye eneo
la Severodonetsk na Bakhmut, na matumizi makubwa ya anga.
Mapigano
yanaendelea kuchukua eneo la Severodonetsk kuwa chini ya udhibiti.
Katika eneo
la Severodonetsk, askari wa Urusi walifyatua mizinga na makombora katika maeneo
ya makazi ya Lisichansk, Sirotino, Voronovo, Borovskoye, Belaya Gora,
Ustinovka, Mirnaya Dolina, Toshkovka na kuzindua mashambulizi ya anga kutoka
kwa ndege ya Su-25 karibu na Belaya Gora na Mirnaya.
Katika eneo
la Limansky, Avdievsky, Kurakhovsky, Novopavlovsky na Zaporozhye, vikosi vya
Urusi vinajaribu kuzuia kuunganishwa tena kwa wanajeshi wa Ukraine.
Katika eneo
la Liman, wanajeshi wa Urusi walizindua shambulio la anga na ndege mbili za
Su-25 karibu na kijiji cha Prishib na shambulio la kombora karibu na kijiji cha
Mayaki.
Katika eneo
la Yuzhnobuzh, Urusi inaelekeza nguvu zake katika kushikilia maeneo yaliyokaliwa
na kuzuia mashambulizi ya wanajeshi wa Ukraine.
Katika maji ya Bahari Nyeusi na Azov, juhudi kuu
za kikundi cha meli za wanajeshi wa Urusi zinalenga kuzuia shughuli za usafiri
wa raia kaskazini-magharibi mwa Bahari Nyeusi
Jeshi la Ukraine lapoteza udhibiti wa Metolkin karibu na Severodonetsk - Gaidai
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ukraine wapoteza udhibiti wa kijiji cha Metelkino
Mkuu wa
utawala wa kijeshi wa eneo la Lugansk, Sergei Gaidai, alisema kuwa wanajeshi wa
Ukraine wamepoteza udhibiti wa kijiji cha Metelkino karibu na Severodonetsk.
"Mapigano
yanaendelea katika vijiji vingi karibu na Severodonetsk na Lisichansk. Kwa
bahati mbaya, kwa sasa hatudhibiti eneo la Metelkino karibu na kituo cha
kikanda," Gaidai alisema.
Asubuhi ya
Juni 20, Urusi ilizidisha ufyatuaji wa risasi na makombora ya anga, katika eneo
la viwanda la Severodonetsk na nje kidogo ya jiji likateseka zaidi, anaandika
mkuu wa Luhansk OVA Sergei Gaidai.
Urusi
inataka kupata mafanikio na mapigano yanafanyika katika vijiji vingi karibu na
Severodonetsk na Lysychansk.
Anasisitiza
kuwa suluhu iliyopotea sio "kupoteza katika vita".
"Mkoa
wa Luhansk utatetewa hadi mwisho, tutazuia jeshi kwa muda mrefu iwezekanavyo,"
mkuu wa OVA aliandika.
Kulingana na
yeye, "uokoaji wenye utulivu" unaendelea kwenye eneo la Lysychansk.
Gaidai
anadai kwamba Lysychansk inateseka sana kutokana na kushambuliwa kwa makombora,
na kwamba "wasaliti wa ndani" wanachochea.
Kwa picha: Mkutano wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola waanza Kigali Rwanda
Bendera za nchi 54 wanachama wa Jumiya ya Madola (CHOGM) umeanza
mjini Kigali Rwanda. Wakuu wa nchi za CHOGM na wajumbe zaidi ya 5,000 wanakongamana
kushiriki mkutano huu ambao awali
uliahirishwa mara mbili kutokana na janga la Covid-19. Wajumbe wanatarajiwa kujadili ushirikiano
baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya madola katika nyanja mbali mbali, mkiwemo
uchumi na elimu, biashara, utamaduni na mazingira
Serikali ya Rwanda inatazamia kutumia mkutano huu hususan kunadi
utalii wa nchi hiyo huku wafanyabiashara
wa sekta ya hoteli na migahawa wakiytarajiwa kunufaika kutokana na wateja wanaoshiriki
mkutano huu. Hizi ni baadhi ya picha kuhusiana na CHOGM kutoka Kigali:
Chanzo cha picha, CHOGM Rwanda 2022
Maelezo ya picha, Wajumbe wa CHOGM ukiendelea mjini Kigali
Chanzo cha picha, CHOGM Rwanda 2022
Maelezo ya picha, Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa CHOGM mjini Kigali
Chanzo cha picha, Rwanda National Police
Maelezo ya picha, Polisi ya Rwanda ilitoa ramani inayoonyesha barabara za mji wa Kigali zitakazotumiwa Katika CHOGM
Chanzo cha picha, CHOGM RWANDA 2022
Maelezo ya picha, Mikutano ya makundi mbali mbali ya CHOGM ukiwemo mkutano wa vijana imekuwa ikiendelea kabla ya kikao cha wakuu wa nchi. Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa na vijana ni pamoja na ushirikiano baina ya vijana wanachama wa Jumuiya ya Madola katika suala la ubunifu
Maandalizi ya CHOGM Rwanda yamekuwa yakitawala mitandao ya kijamii hususan ni ule wa Twitter ambapo watu mbali mbali wamekuwa wakishirikishana picha za jinsi mji wa Kigali ulivyojiandaa kwa mkutano huu wa kimataifa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Jino la Lumumba lawasilishwa kwa familia yake mjini Brussels
Chanzo cha picha, Jelle Vermeersch
Mamlaka ya Ubelgiji imekabidhi jino la kiongozi wa uhuru wa Congo Patrice Lumumba kwa familia yake katika hafla iliyofanyika Brussels.
Jino hilo nii sehemu pekee ya mabaki ya mwili wake ambayo inadhaniwa kuwa bado ipo baada ya kunyongwa na kisha mwili wake kuyeyushwa kwa tindikali mnamo 1961.
Ubelgiji ilikuwa mamlaka ya zamani ya kikoloni na uchunguzi rasmi ulisema kwamba baadhi ya wanachama wa serikali yake wakati huo "waliwajibika kimaadili kwa hali iliyosababisha kifo".
Polisi wa Ubelgiji Gerard Soete, aliyesimamia kuharibiwa kwa mwili huo, alichukua jino hilo kama "aina ya nyara ya uwindaji", baadaye alisema.
Viongozi wa Afrika Mashariki wawasili Kenya kujadili mzozo wa DR Congo
Viongozi wa mataifa saba yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajiwa kukutana kujadili hali ya usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kulingana na taarifa ya serikali.
Viongozi hao wanakutana kwa mualiko wa mwenyeji wao Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Muda mfupi uliopita Rais wa Uganda Yoweri Museveni amethibitisha kwenye mtandao wake rasmi wa Twitter kwamba amewasili jijini Nairobi kkuhudhuria Kikao cha Tatu cha Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Rais Kenyatta alitoa wito wa kupelekwa kwa Kikosi cha Kudumu cha Afrika Mashariki ili kukomesha ghasia katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo.
DRC hata hivyo inapinga Rwanda kuwa sehemu ya jeshi lililopendekezwa la kikanda na imesitisha uhusiano wa pande mbili na Kigali.
Nchi hiyo inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao hivi majuzi waliuteka mji wa mpakani Bunagana.
Rwanda inakanusha madai hayo.
Rais Felix Tshisekedi katika taarifa yake aliishutumu Rwanda kwa kutaka kuikalia kimabavu nchi yake ili kutumia madini yake na kuitaka Uingereza kuishinikiza Kigali kukomesha uchokozi wake.
Mvutano kati ya nchi hizo mbili umeongezeka katika wiki za hivi karibuni huku maandamano ya kuipinga Rwanda yakiripotiwa mjini Kinshasa na mashariki mwa Congo.
Siku mbili zilizopita, mwanajeshi wa Congo aliwafyatulia risasi walinda usalama wa Rwanda katika kituo cha mpakani mjini Bukavu na kuwajeruhi maafisa wawili wa polisi.
Kenya ndiyo mwenyeji wa mazungumzo ya moja kwa moja ya amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na makundi tofauti vya waasi.
Watu 20 wauawa katika mashambulio la wanamgambo wa kijihadi Mali
Chanzo cha picha, Getty Images
Karibu watu 20 wameuawa katika shambulio linaotuhumiwa kutekelezwa na wapiganaji wa kijihadi kaskazini mwa Mali, ofisi ya kikanda katika eneo hilo inasema.
Ghasia za Jumamosi zilitokea karibu na mji wa Gao.
Afisa huyo aliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba hali ilikuwa tete kwani raia walikuwa wakitoroka wakato wanamgambo hao walipokuwa wakifanya unyama dhidi yao.
Umoja wa Mataifa unasema hali ya usalama katika maeneo ya Gao na Ménaka imezorota vibaya.
Mapema Jumapili walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliuawa karibu na mgodi mmoja huko Kidal kaskazini mwa nchi.
Uchaguzi wa Ufaransa: Macron apoteza udhibiti wa bunge la Ufaransa
Chanzo cha picha, Reuters
Chini ya miezi miwili baada ya kuchaguliwa tena kuwa rais, Emmanuel Macron amepoteza udhibiti wa Bunge la Ufaransa kufuatia utendaji mzuri wa muungano wa kushoto na mrengo wa kulia.
Bw. Macron alikuwa ametoa wito kwa wapiga kura kupiga kura kwa wingi ili wapate uongozi thabiti.
Lakini muungano wake wa centrist ulipoteza makumi ya viti katika uchaguzi huo ambao umesababisha mgawanyiko mkubwa katika siasa za Ufaransa.
Waziri mkuu ambaye alikuwa amemteua hivi majuzi, Elisabeth Borne, alisema hali hiyo haikuwa ya kawaida.
Dhoruba ilipiga Paris aliporejea kwenye makazi yake ya Matignon kutoka kwa mkutano wa muda mrefu katika ikulu ya Élysée kusema kwamba Ufaransa ya kisasa haijawahi kuwa na Bunge kama hili.
Kiongozi wa mrengo wa kushoto Jean-Luc Mélenchon amekuwa akifurahia mafanikio yake ya kuleta pamoja vyama vikuu kutoka upande wa kushoto na Wakomunisti na Greens katika muungano unaofahamika kama Nupes.
Aliwaambia wafuasi wake kwamba chama cha urais kimepata pigo kubwa na kwamba uwezo uko mikononi mwao.
'Kitabu cha Hitler na silaha zapatikana' baada ya Macron kuzabwa kofi
Je, Ufaransa kuiomba radhi Rwanda?
Mke wa rais wa Ufaransa afungua kesi kuhusu madai ya kuzaliwa akiwa mwanamume
Philippines: Sara Duterte aapishwa kuwa makamu wa rais
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Sara Duterte alikula kiapo akiwa amesimama kando ya wazazi wake, akiwemo babake Rais Rodrigo Duterte
Binti
mkubwa wa Rais wa Ufilipino anayeondoka madarakani Rodrigo Duterte ameapishwa kuwa
makamu wa rais wa nchi hiyo.
Sara Duterte ameapa kuwaunganisha
Wafilipino katika hafla ya kuapishwa kwake mjini Davao.
Ni katika mji huo ambapo Sara
mwenye umri wa miaka 44-alichukua usukani kutoka kwa baba yake kama Meya kwa zaidi
yamwongo mmoja uliopita -kabla ya
kujitosa katika siasa za kitaifa.
Alikula kiapo kando ya
mgombea mwenzake, Ferdinand Marcos Junior, ambaye hivi karibuni atachukua
nafasi ya baba yke kama rais.
"Siku zinazokuja
zinatarajiwa kuwa na changamoto ambazo zinatuhitaji kuwa na mshikamano kama
taifa," Bi Duterte alisema.
Muhula wake wa miaka sita
madarakani ukiongozwa na Ferdinand Marcos Junior utaanza rasmi Juni 30.
Kama wangombea katika
uchaguzi wa mwezi Mei wawili hao walipata ushindi wa kishindo kwa kubuni muungano
thabiti wa kisiasa na kutumia kauli mbiu ya umoja ambao utasaidia baadhi ya
washirika wao pia kupata uongozi katika ngazi zingine za serikali.
Nchini
Ufilipino , rais na makamu wake wanachaguliwa kando kando.
Bw.
Duterte ni mtu mwenye utata ambaye aliingia madarakani mwaka 2016 akiahidi
kupunguza uhalifu na kukabiliana na janga la dawa za kulevya.
Lakini wakosoaji wanasema katika kipindi cha miaka mitano madarakani, Bw Duterte alwahimiza polisi kutekeleza maelfu ya mauaji ya kiholela ya washukiwa katika kile alichokiita "vita vyake dhidi ya mihadarati".
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imetaka uchunguzi ufanyike rasmi kuhusu maelfu ya mauaji yaliyotokea wakati wa msako huo mkali.
Ukraine yaonya Urusi itazidisha mashambulizi inaposubiri ombi la kujiunga na EU
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais Zelensky alitia saini ombi la kuwa mwanachama wa Muungano wa Ulaya siku chache tu baada ya Urusi kuanzisha uvamizi dhidi ya Ukraine.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonya Urusi
itazidisha mashambulizi dhidi ya nchi yake katika siku zijazo, huku Kyiv
ikisubiri jibu kuhusu azma yake ya kujiunga na Muungano wa Ulaya (EU).
Wanachama wa Muungano huo wanatarajiwa kuamua ikiwa watatoa "hadhi ya mgombea" kwa Kyiv baadaye wiki hii.
Hatua hiyo itanzisha mchakato wa Ukraine kujiunga na muungano huo, ambao unaweza kuchukua miaka kadhaa kukamilika.
Lakini Bw Zelensky alionya uamuzi huo unaweza kuifanya Urusi kuongeza mashambulizi yake.
Akizungumza wakati wa hotuba yake ya usiku kutoka
Kyiv, kiongozi huyo wa Ukraine alisema yeye na washauri wake wanatarajia
"shughuli kubwa zaidi ya uadui" kutoka Moscow, lakini aliwaambia raia
kwamba vikosi vyake "vinajiandaa" na viko tayari kwa mashambulizi yoyote
mapya.
Aliahidi kuendelea mbele kile alichokiita matarajio
ya "kihistoria" ya Ukraine kujiunga na EU, ambayo yaliidhinishwa na
watendaji wakuu wa umoja huo, Tume ya Ulaya, wiki iliyopita.
Lakini sasa uamuzi huo uko mikononi mwa Baraza la
Ulaya, chombo kilichoundwa na viongozi wa Nchi Wanachama, ambacho kitakutana
katika mkutano wa kilele huko Brussels siku ya Alhamisi na Ijumaa.