Mkuu wa jeshi la Uingereza: 'Lazima tuwe tayari kupigana tena Ulaya'

Mkuu mpya wa Jeshi la Uingereza, Patrick Sanders, amewatangazia wanajeshi kwamba lazima wawe tayari kwa vita vipya barani Ulaya.

Moja kwa moja

  1. Rais Kenyatta aitisha mkutano wa kikanda kujadili usalama DR-Congo

    Rais Kenyatta

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameitisha mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki siku ya Jumatatu kujadili amani na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kulingana na taarifa ya serikali.

    Uhuru ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jumatano alitoa wito wa kupelekwa kwa Kikosi cha Kudumu cha Afrika Mashariki ili kukomesha ghasia katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo.

    DRC hata hivyo inapinga Rwanda kuwa sehemu ya jeshi lililopendekezwa la kikanda na imesitisha uhusiano wa pande mbili na Kigali.

    Nchi hiyo inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao hivi majuzi waliuteka mji wa mpakani Bunagana.

    Rwanda inakanusha madai hayo.

    Rais Felix Tshisekedi katika taarifa yake aliishutumu Rwanda kwa kutaka kuikalia kimabavu nchi yake ili kutumia madini yake na kuitaka Uingereza kuishinikiza Kigali kukomesha uchokozi wake.

    Mvutano kati ya nchi hizo mbili umeongezeka katika wiki za hivi karibuni huku maandamano ya kuipinga Rwanda yakiripotiwa mjini Kinshasa na mashariki mwa Congo.

    Siku mbili zilizopita, mwanajeshi wa Congo aliwafyatulia risasi walinda usalama wa Rwanda katika kituo cha mpakani mjini Bukavu na kuwajeruhi maafisa wawili wa polisi.

    Kenya ndiyo mwenyeji wa mazungumzo ya moja kwa moja ya amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na makundi tofauti vya waasi.

    Mazungumzo hayo bado hayajazaa matokeo yoyote.

  2. Ukraine yapitisha sheria ya kupiga marufuku muziki wa Kirusi katika maeneo ya umma na vyombo vya habari

    Bunge la Ukraine limepiga kura kuidhinisha mswada wa kupiga marufuku muziki wa Kirusi katika maeneo ya umma, vyombo vya habari na pia kuongeza kiwango cha upendeleo wa muziki wa nyumbani kwenye vituo vya redio na vituo vya Televisheni.

    Sheria hii inakataza uigizaji wa umma na utangazaji wa kazi (pamoja na video za muziki) na wasanii ambao walikuwa na au bado wana uraia wa Urusi baada ya 1991.

    Makampuni ya Televisheni na Redio yatakayokiuka kanuni hii yatatakiwa kulipa faini ya 10% ya ada ya leseni.

    Hatua hii haitaathiri kazi ya wasanii ambao walilaani uvamizi wa kijeshi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

    Ili kujumuishwa katika orodha tofauti (na, hasa, kutembelea Ukraine), mswada huo unahitaji wasanii wenye nia au wawakilishi wao kuwasilisha maombi katika fomu iliyowekwa kwa Huduma ya Usalama ya Ukraine (SBU).

    Wasanii hao pia watalazimika kusaini tamko la kulaani uvamizi wa Urusi na kutaka vita hivyo vikomeshwe mara moja.

  3. Uchaguzi wa Kenya 2022: Sakaja apata ishara ya kuwania Ugavana wa Nairobi

    Kamati Maalum ya Tume Huru ya Uchaguzi na Ukaguzi wa Mipaka nchini Kenya IEBC imetupilia mbali malalamishi ya kupinga cheti cha digrii ya Senata wa Nairobi Johnson Sakaja.

    Hatua hiyo sasa inamruhusu Bw. kuendelea mmbele na azma yake ya kuwania ugavana wa Nairobi.

    Kilingana na taarifa za vyombo vya habari vya Kenya Kamati hiyo ilihoji kuwa IEBC haina mitambo ya kuchunguza uhalali wa stakabadhi hizo.

    "Ingawa kuna wasiwasi mkubwa kuhusu uhalali wa hati zake lakini Sakaja hajashtakiwa katika mahakama ya sheria kuhusu madai ya kuhusika katika kosa la kuwa na hati ghushi," ilisema, na kuongeza kuwa madai yaliyotolewa na IEBC dhidi ya Sakaja inaweza kushughulikiwa tu na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Mkuu wa jeshi la Uingereza: "Lazima tuwe tayari kupigana tena Ulaya"

    Majeshi ya Uingereza

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Barua ya Kamanda ilitumwa kwa askari na maafisa wote wa Jeshi la Uingereza, pamoja na watumishi wa umma.

    Mkuu mpya wa Jeshi la Uingereza, Patrick Sanders, amewatangazia wanajeshi wake kwamba lazima wawe tayari kwa vita vipya barani Ulaya.

    BBC imepata risala iliyosambazwa kwa barua kwa jeshi la Uingereza.

    "Sasa ni muhimu kuunda jeshi ambalo linaweza kupigana pamoja na washirika wetu na kuishinda Urusi katika mapigano," Sanders alisema.

    Kulingana na yeye, kazi kubwa sasa ni kuongeza kasi ya kisasa ya vikosi vya jeshi la Uingereza ili kuimarisha NATO na kutoruhusu Urusi kusonga mbele zaidi katika eneo la Ulaya.

    "Sisi ni kizazi kinachopaswa kuandaa jeshi kupigana tena Ulaya," Sanders alisema katika waraka.

    Kulingana na kamanda huyo, yeye ndiye mkuu wa majeshi tangu 1941 kuliongoza jeshi la Uingereza katika vita vya ardhini vilivyohusisha nguvu ya bara huko ulaya.

    Patrick Sanders alichukua wadhifa wa mkuu wa wafanyikazi mnamo Jumatatu, Juni 13.

    "Uvamizi wa Urusi kwa Ukraine unasisitiza dhamira yetu ya msingi - kutetea Uingereza na kuwa tayari kupigana na kushinda vita vya ardhini - na kuimarisha hitaji la kuzuia uchokozi wa Urusi kwa tishio la nguvu zetu."

  5. Mfumo wa ulinzi wa anga waangusha 'kitu' katika eneo la Kyiv

    Mamlaka ya Ukraine inasema kuwa mifumo ya ulinzi wa anga katika eneo la Kyiv ilidungua "chombo cha anga" cha Urusi asubuhi ya leo.

    Milipuko ilisikika katika Wilaya ya Vyshhorod, kaskazini mwa jiji.

    Hawakutoa maelezo juu ya asili ya lengo, ingawa katika wiki za hivi karibuni maeneo ya magharibi na katikati mwa nchi kwa jumla yamekuwa yakilengwa na makombora ya kurushwa kutoka kwa meli.

    Utawala wa Kijeshi wa Mkoa wa Kyiv uliandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba hakuna moshi uliogunduliwa, hakukuwa na moto na hakuna majeruhi walioripotiwa kwa sasa.

  6. "Nyumbani ni salama zaidi": Putin awaomba wafanyabiashara wakubwa wasiondoke Urusi

    Putin

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Urusi Vladimir Putin amewahimiza wafanyabiashara wakubwa kuwekeza katika uchumi wa Urusi ili wasipoteze "mamilioni ya dola" katika nchi za Magharibi.

    Anaamini kuwa wafanyabiashara wanahitaji kuunganisha "mustakabali wao wa baadaye na mustakabali wa watoto wao" na nchi yao. Tayari, wafanyabiashara kadhaa wakubwa waliondoka Urusi, kwa mfano, Oleg Tinkov.

    Wataalam wanaamini kuwa zaidi ya mamilionea elfu 15 wa dola wanaweza kuondoka Urusi ifikapo mwisho wa 2022.

    Akizungumza katika Kongamano la Uchumi la St. Petersburg, Vladimir Putin alitoa wito kwa "wafanyabiashara wakubwa na wasimamizi" kuunganisha "mustakhbali wao na mustakabali wa watoto wao" na nchi yao.

    Alibainisha kuwa biashara ni zaidi ya kupata faida, na kubadilisha maisha na kuchangia maendeleo ya nchi ya asili ni "jambo muhimu sana kwa kujitambua."

    "Matukio ya hivi majuzi yamethibitisha kile nilichosema hapo awali - ni salama zaidi kuwekeza nyumbani. Wale ambao hawakuitikia wito huu wa wazi wamepoteza mamilioni, ikiwa sio mabilioni ya dola katika nchi za Magharibi, alisema Putin.

    Kufikia mapema Aprili, Tume ya Ulaya ilikadiria kuwa kutokana na vikwazo vilivyowekwa baada ya Urusi kuivamia Ukraine, nchi za Umoja wa Ulaya zilizuia mali ya Warusi yenye thamani ya euro bilioni 30, ambapo bilioni 6.7 kati yake ni meli ya kifahari, helikopta, mali isiyohamishika na kazi za sanaa.

  7. Vita vya Ukraine vinaweza kudumu kwa miaka kadhaa, aonya mkuu wa Nato

    Katibu Mkuu wa Nato akizungumza baada ya mkutano na mawaziri wa ulinzi wa muungano wa kijeshi Juni 16.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Katibu Mkuu wa Nato akizungumza baada ya mkutano na mawaziri wa ulinzi wa muungano wa kijeshi Juni 16.

    Nchi za Magharibi lazima zijiandae kuendelea kuunga mkono Ukraine katika vita vitakavyodumu kwa miaka mingi, mkuu wa Nato ameonya.

    Katibu Mkuu Jens Stoltenberg amesema gharama za vita ni kubwa, lakini bei ya kuiruhusu Moscow kufikia malengo yake ya kijeshi ni kubwa zaidi.

    Maoni yake yanakuja wakati Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson pia ameonya juu ya hitaji la kujiandaa kwa mzozo wa muda mrefu.

    Bw Stoltenberg na Bw Johnson walisema kutuma silaha zaidi kutafanya Ukraine kupata ushindi zaidi.

    "Lazima tujiandae kwa hakika kwamba vita hivi vinaweza kuchukua miaka kadhaa. Hatupaswi kukata tamaa katika kuunga mkono Ukraine," mkuu wa Nato alisema katika mahojiano na gazeti la Ujerumani Bild. Hata kama gharama ni kubwa, sio tu kwa msaada wa kijeshi, pia kwa sababu ya kupanda kwa bei ya nishati na chakula."

    Mkuu huyo wa muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi alisema kuwa kuipatia Ukraine silaha za kisasa zaidi kutaongeza nafasi yake ya kuweza kukomboa eneo la mashariki mwa nchi hiyo la Donbas ambalo kwa sasa sehemu kubwa iko chini ya udhibiti wa Urusi.

    Kwa miezi michache iliyopita vikosi vya Urusi na Ukraine vimepigania udhibiti wa eneo la mashariki mwa nchi hiyo - huku Moscow ikipiga hatua polepole katika wiki za hivi karibuni.

    Maelezo zaidi:

  8. 'Majambazi wenye silaha' wanaoshukiwa kuwa waasi waua wawili kusini magharibi mwa Rwanda

    Rwanda

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Polisi nchini Rwanda wanasema “majambazi wenye silaha” wanaoshukiwa kuwa “mabaki” yakundi la waasi National Liberation Front wamewapiga risasi na kuwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine sita siku ya Jumamosi.

    Shambulio hilo lilitokea mwendo was aa nanesaa za Afrika Masharikikatika eneo la Kitabi kwenye barabara ya Nyamagabe – Rusizi ambayo inapitia msitu wa Nyungwe kusini magharibi mwa Rwanda Rwanda.

    Waliojeruhiwa walihamishwa hadi hospitali ya Kigeme na hospitali ya mafunzo ya chuo kikuu huko Butare, kusini mwa nchi.

    Polisi wanasema washambuliaji hao walitokea “upande wa pili wa mpaka.”

    Msitu wa Nyungwe ni mojawapo ya maeneo ya mpakani na Burundi.

    Hapo awali, nchi hizo mbili za Afrika Mashariki zilibadilishana tuhuma za kuwaunga mkono waasi wanaotaka kupindua serikali.

    Kundi la waasi la Rwanda - linalojulikana kwa ufupi wa jina la Kifaransa FLN - bado halijatoa maoni yoyote.

    Kundi hilo lilianza kudai mashambulizi dhidi ya Rwanda - ikiwa ni pamoja na kwenye nyadhifa za jeshi - mwaka 2018 na inasema ina kambi huko Nyungwe, jambo ambalo serikali inakanusha.

    Taarifa ya polisi inasema "iliingilia kati kwa dakika chache katika tukio hilo."

    "Washambuliaji wanafuatiliwa," inaongeza.

    Shambulio hilo linakuja wakati nchi hiyo ikiwa mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola mjini Kigali kuanzia Jumatatu.

    Soma:

  9. Hujambo na karibu