Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Ukraine na Urusi: Putin asema Urusi inataka ‘kukomboa ardhi yake’ Ukraine

Rais wa Urusi Vladmir Putin amejaribu kuhalalisha uvamizi wa Ukraine kwa kusema kwamba taifa lake sasa linajaribu kukomboa maeneo yakesawa na alivyofanya mtawala wa Urusi Peter the Greatmwanzo wa karne ya 18.

Moja kwa moja

  1. Mauaji ya 'heshima' Iran: Wanawake wauawa na familia zao

    Wanaharakati wa haki za binadamu wameonya kuwa matukio ya udhalilishaji wanawake yameongezeka nchini Iran.

    Mauaji ya "heshima" ni mauaji ya mtu na wanafamilia ambao wanatuhumiwa kuleta aibu kwa familia kupitia tabia zao.

    Suala la mauaji ya heshima lilikuja kwa majadiliano pale msichana mmoja aliyeitwa Mona Haideri alipouawa kikatili mwezi Februari. Baadhi ya maelezo ya kina katika makala hii yaliyotolewa na mwandishi wa BBC Sarah Monetta yanaweza kuonekana kukuaibisha.

    Mona alimuoa binamu yake akiwa na umri wa miaka kumi na miwili.

    Hata hivyo, alikimbilia Uturuki kuepuka unyanyasaji wa kijinsia. Lakini jamaa alimshawishi na kumrejesha nyumbani.

    Aliaminika kuwa na ulinzi. Tayari ana umri wa miaka 17. Mwengine ni Parisa, mwalimu wa shule. Mume wake alimkata kuanzia juu kwenye mkono hadi kwenye kiganja cha mkono.

    Sababu kuu hakuwa amefunika mkono wake. Akamchoma kwa kijiko cha moto kisa hakuamka asubuhi kusali.

    Parisa akalazwa hospitalini baada ya mume wake kumwagia maji ya moto.

    Na hapo ndipo alipogundua kwamba ni mjamzito.

    Akaamua kutafuta eneo salama na kukimbilia Uturuki ambako aliomba hifadhi.

    Lakini bado mume wake alimtumia ujumbe wa kumtishia maisha kwamba atamuua.

    Pamoja na vitisho alivyopokea Parisa, mamlaka ya Uturuki ilifuta hadhi yake ya ukimbizi.

    Yeye na mtoto wake sasa wako hatarini kusafirishwa kwenda Iran.Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa mwaka 2019, inakadiriwa kuwa wanawake 450 huuawa kila mwaka nchini Iran na wanafamilia au waume zao wenyewe kwa jina la mauaji ya heshima.

    Mauaji kama haya hugonga vichwa vya habari pale yanapotokea hadharani, jambo la kikatili zaidi.

    Katika matukio mengi, mauaji kama haya hufanyika bila ya mtu yeyote kuona. Adhabu katika kesi hizi pia ni ndogo.

    Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema idadi ya mauaji yaliyoripotiwa inazidi kuongezeka.

    Mauaji katika familia yamefichwa ndani. Wazazi wa wanawake waliouawa hata hawajafungua kesi dhidi ya muuaji.

  2. Papa Francis aahirisha ziara yake nchini DR Congo na Sudan Kusini

    Papa Francis amelazimika kukatiza ziara yake ijayo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini kwa sababu ya jeraha la goti, Vatican imetangaza.

    Mkuu wa Kanisa Katoliki alipangiwa kusafiri mwezi Julai hadi miji ya Kinshasa na Goma ya Kongo, ikifuatiwa na ziara katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba. Huko Juba alipaswa kuongoza mkesha wa maombi pamoja na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby, na

    Msimamizi wa Mkutano Mkuu wa Kanisa la Presbyterian la Scotland Mchungaji Iain Greenshields. Vatican ilisema ziara hiyo itafanyika katika "tarehe ya baadaye kuamuliwa".

    Uamuzi huo ulikuwa umefanywa "kwa ombi la madaktari [wa Papa], na ili kutohatarisha matokeo ya matibabu ambayo anapitia kwa goti lake". Baraza la Maaskofu Katoliki Sudan na Sudan Kusini bado halijatoa tamko lolote kuhusu kuahirishwa.

    Nchi za DR Congo na Sudan Kusini zina idadi kubwa ya Wakatoliki wa Kirumi. Papa huyo mwenye umri wa miaka 85 amefanya ziara kadhaa barani Afrika tangu kuwa papa mwaka 2013.

  3. Urusi yatetea hukumu za kifo kwa Waingereza waliokamatwa

    Waziri wa mambo ya nje wa Urusi amedai kuwa watu watatu waliohukumiwa kifo - Waingereza wawili na mmoja wa Morocco - walifanya uhalifu katika eneo la kile kinachojulikana kama Jamhuri ya Watu wa Donetsk (DPR).

    Sergei Lavrov alisema kesi hizo zilifanyika kwa "msingi wa sheria ya Jamhuri ya Watu wa Donetsk, kwa sababu uhalifu unaohusika ulifanyika katika eneo la DPR".

    DPR, ambapo vikosi vya wanaotaka kujitenga vilianza kampeni ya kijeshi ya kujitenga na Ukraine mwaka 2014 kwa msaada wa Moscow, inatambulika kimataifa kama sehemu ya Ukraine.

    "Kila kitu kingine tayari ni suala la uvumi, na nisingeingilia kazi ya mfumo wa mahakama na utekelezaji wa sheria wa Jamhuri ya Watu wa Donetsk," Lavrov alinukuliwa akisema na shirika la habari la serikali la RIA Novosti.

  4. Urusi inapungukiwa na makombora ya hali ya juu - Ukraine

    Urusi inaishiwa na makombora ya uhakika na itaweza kuendeleza vita kwa kasi yake ya sasa baada ya mwaka mmoja tu, Ukurugenzi wa ulinzi ya Ukraine imedai.

    Kurugenzi kuu ya kijasusi ya Wizara ya Ulinzi ya Ukraine ilisema Urusi ilikuwa ikifanya mashambulizi machache sana ya makombora na ilikuwa ikitumia makombora ya Kh-22, ambayo ilisema ni "makombora ya zamani ya Soviet yaliyotengenezwa miaka ya 1970".

    "Hii inaonyesha kwamba Urusi inaishiwa na makombora ya hali ya juu," alisema Vadym Skibitskyy kutoka kurugenzi katika chapisho la Facebook.

    Kurugenzi hiyo imesema rasilimali za kiuchumi za Urusi zitaiwezesha kuendeleza vita kwa kasi yake ya sasa kwa mwaka mmoja.

    "Uongozi wa Kremlin unaweza kujaribu kusimamisha vita kwa muda ili kuzishawishi nchini za Magharibi kufuata vikwazo, na kisha kuendeleza uchokozi," kurugenzi iliongeza.

    "Lengo lao ni Ukraine yote na sio Ukraine pekee."

  5. Habari za hivi punde, Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Tanzania aachiwa huru

    Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai na wenzake sita wameachiliwa huru .

    Mahakama ya Arusha ikitoa uamuzi huo imesema kwamba ushahidi uliotolewa dhidi ya Mkuu huyo lengai Ole sabaya na wenzake sita ulikuwa na utata.

    Hakimu Mkazi wa Arusha amesema kwamba ushahidi huo umeshindwa kuthibitisha mashtaka yaliokuwa yanawakabili ili kuwapata na hatia.

    Mbali na Sabaya sita hao ni pamoja na Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya..

    Kulingana na gazeti la mwananchi , hata hivyo Sabaya, Nyegu, Aweyo na Msuya wataendelea kubaki mahabusu katika gereza la Karanga kwa kuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.

    Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Juni 10 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.

    Hii ni kesi ya pili Sabaya kushinda ambapo Mei 6, 2022 na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, walishinda rufaa iliyokuwa ikisikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, waliyokata kupinga hukumu ya miaka 30 iliyokuwa imetolewa.

  6. Moscow inataka kuharibu utaifa wetu - Ukraine

    Moscow inataka "kuharibu kabisa serikali ya Ukraine", msemaji wa wizara ya ulinzi ya Kyiv anasema.

    "Lengo la kimkakati la Urusi ni uharibifu kamili wa Ukraine ... Hawatatuacha tuishi kwa amani," Oleksandr Motuzyanyk aliiambia TV ya kitaifa.

    "Shirikisho la Urusi linataka kuharibu kabisa serikali ya Ukraine na kuweka serikali ambayo inaweza kuidhibiti ."

    Moscow inasema inatekeleza "operesheni maalum ya kijeshi" na haina mpango wa kuikalia Ukraine.

    Urusi inatafuta maeneo dhaifu katika ulinzi wa Ukraine karibu na Mto Siversky Donets mashariki mwa Ukraine, aliongeza.

    Ikiwa Urusi itaiteka miji ya Severodonetsk na Lysychansk kwenye Donets za Siverskyi, itashikilia Luhansk yote, mojawapo ya majimbo mawili katika eneo la Donbas ambayo Moscow inadai kwa niaba ya wanaotaka kujitenga.

  7. Habari za hivi punde, Putin asema Urusi inataka ‘kukomboa eneo lake’ Ukraine

    Rais wa Urusi Vladmir Putin amejaribu kuhalalisha uvamizi wa Ukraine kwa kusema kwamba taifa lake sasa linajaribu kukomboa maeneo yakesawa na alivyofanya mtawala wa Urusi Peter the Greatmwanzo wa karne ya 18.

    Peter the Great alipigana vita vya kaskazini vya miaka 21 , na itaonekana kama alipigana na Uswidi na kuchukua kitu kutoka kwake . Lakini hakuteka eneo lolote , alikuwa akikomboa eneo la Urusi, Putin aliambia mkutanao wa wafanyabiashara wadogomjini Moscow siku ya Alhamisikatika matamshi yaliopeperushwa moja kwa moja katika chombo cha habari cha Rossiya 24 Rolling.

    Akisema kwamba alikuwa akizungumzia kuhusu eneo ambalo mji wa St Petersburg ulianzishwa , Putin aliongezea kwamba hakuna taifa hata moja ambalo sio la Ulaya lililotambua eneo hilo kuwa la Urusi.

    ‘Kila mtu alilitambua eneo hilo kuwa Sweden na raia wa Slav waliishi hapo tangu zamani pamoja wakiwa na Finno -Ugric .Eneo hilo lilikuwa chini ya udhibiti wa taifa la Urusi’, alisema Putin.

    ‘Kwa vyovyote vile ni wakati wetu kukomboa na kujiimarisha’’

  8. Tanzania: Maandalizi ya kuwahamisha 'kwa hiari' Wamasai wa Ngorongoro yakamilika

      • Author, Aboubakar Famau
      • Nafasi, BBC News, Dodoma

    Serikali ya Tanzania imesema wakati wowote kuanzia sasa familia 100 za jamii ya kimasai zitawasili katika kijiji cha Msomera kilichopo Handeni Mkoani Tanga ikiwa ni sehemu ya kuwahimisha kutoka yaliyokuwa makazi yao yaliyopo katika Hifadhi ya Ngorongoro.

    Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Pindi Chana alipotembelea kijiji hicho kwa lengo la kufanya tathmini ya maandalizi ya kuwapokea wageni hao.

    “Tumekuja kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa makazi, na huduma za kijamii kwa wananchi watakaohamia hapa. Nimeridhika sehemu kubwa ya miundombinu imekamilika, muda wowote kuanzia sasa wanangorongoro waliojiandikisha kwa hiari watahamia hapa kuendelea na maisha ili kupisha shughuli za Uhifadhi ndani ya eneo,” amesema Waziri Chana.

    Pia ameendelea kusema kuwa, pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa nyumba 103 na huduma zingine za kijamii,

    Serikali inajipanga kuanza awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba za makazi 400 kwa ajili ya kuwezesha wananchi wanaoendelea kujiandikisha kuhamia Msomera.

    Nae Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ingawa amekiri kuwepo kwa baadhi ya changamoto ikiwemo kasi ndogo katika uboreshwaji wa baadhi ya miundombinu kama vile umeme, mawasiliano pamoja na barabara, lakini amesema yote yanafanyiwa kazi.

    Ingawa hatua ya kuwahamisha wananchi wa jamii ya Kimasai kutoka Ngorongoro imekuwa ikikosolewa na baadhi ya wanaharati, serikali imekuwa ikisisitiza kwamba wananchi hao wanaondoka kwa hiari ili kupisha shughuli za uhifadhi kufanyika katika eneo hilo ambalo liko katika orodha ya urithi wa dunia.

    Maelezo zaidi:

  9. Britney Spears anafunga ndoa na mchumba wake Sam Asghari

    Britney Spears amefunga ndoa na mchumba wake Sam Asghari, miezi saba baada ya kupata uhuru kutoka kwa mkataba wa usimamizi wa babake ambao alisema ulikuwa umemzuia kuolewa.

    Wanandoa hao walifunga pingu za maisha katika sherehe ya faragha huko Los Angeles siku ya Alhamisi.

    Mwaka jana, mwigizaji huyo wa muziki wa pop, 40, aliiambia mahakama kwamba ulezi wa kisheria wa miaka 13 ulimaanisha kuwa "hakuweza kuolewa na kupata mtoto".

    Mkataba huo ulivunjwa kisheria mwezi Novemba mwaka jana na baadaye akapata ujauzito, lakini mwezi Mei akatangaza kuwa mimba hiyo iliharibika.

    Muda mfupi kabla ya harusi, mume wa zamani wa nyota huyo alizuiliwa nje ya nyumba yake baada ya kujaribu kuvuruga hafla hiyo.

    Jason Alexander, ambaye alikuwa mume wa Spears kwa muda wa chini ya saa 55 mwaka 2004, alifanikiwa kuingia katika eneo hilo kwa muda mfupi, baaada ya kufanikiwa kumpita mlinzi na watu wengine.

    Bw Alexander alikamatwa na polisi wa Kaunti ya Ventura kwa kibali kutoka kaunti tofauti kwa kosa ambalo halijafichuliwa, lakini maafisa walilazimika kuamua ikiwa mashtaka ya uvunjaji sheria yatashinikizwa.

  10. Kenya yaiweka tozo jipya kwa mayai ya kuku kutoka Uganda

    Wafanyabiashara wanaouza kuku na mayai wanatozwa shilingi 70 za Kenya sawa na shilini 2500, kupata idhini ya kuingiza mayai yao nchini Kenya, jambo linalokwenda kinyume na makubaliano ya awal, limeripoti gazeti la Daily Monitor nchini Uganda.

    Wafanyabiashara wengi pamoja na vyama vya wafanyabiashara wameliambia gazeti hilo kuwa tozo hilo ni miongoni mwa masharti ambayo yamewekwa dhidi ya mayai kutoka Uganda.

    Hii inkuja miezi sita baada ya Kenya kuondoa marufuku iliyokuwa imeiweka dhidi ya kuku na bidhaa za kuku kutoka Uganda kwa ajili ili kuwalinda wakulima wake na athari za Covid-19.

    Taarifa ya pamoja iliyotolewa mwezi Januari na Waziri wa kilimo wa Kenya Peter Munya, Waziri wa biashara Betty Maina, na Waziri wa kilimo wa Uganda Frank Tumwebaze ilionyesha kuwa Kenya itaruhusu mauzo ya mayai, kuku na vifaranga, baada ya kuzuiwa kuingia nchini Kenya tangu Februari 2021.

  11. Ukraine inapoteza wanajeshi 200 kwa siku - msaidizi wa Zelensky

    Msaidizi mkuu wa rais wa Ukraine ameambia BBC kuwa kati ya wanajeshi 100 hadi 200 wa Ukraine wanauawa itani kila siku.

    Mykhaylo Podolyak alisema Ukraine inahitaji mamia ya mifumo ya silaha za Magharibi ili kusawazisha uwanja na Urusi katika eneo la mashariki la Donbas.

    Pia alisema Kyiv haiko tayari kuanza tena mazungumzo ya amani na Moscow. Wanajeshi wa Ukraine wanakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara huku majeshi ya Urusi yakijaribu kuchukua udhibiti wa Donbas nzima.

    "Vikosi vya Urusi vimetumia kila aina ya silaha nzito dhidi yetu ikiwa ni pamoja na mifumo mingi ya kurusha roketi na anga," Bw Podolyak alisema.

    Alirudia ombi la Ukraine la kutaka silaha zaidi kutoka kwa nchi za Magharibi, akisema kwamba "ukosefu kamili wa usawa" kati ya majeshi ya Urusi na Ukraine ndio sababu ya kiwango kikubwa cha vifo vya wanajeshi wa nchi hiyo.

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  12. Kusikizwa kwa ghasia Capitol: Trump ashutumiwa kwa 'jaribio la mapinduzi'

    Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alianzisha ghasia za mwaka jana katika makao makuu ya bunge la nchi hiyo katika "jaribio la mapinduzi", uchunguzi wa bunge wabaini.

    Liz Cheney, makamu mwenyekiti wa kamati ya chama cha Republican, alisema Bw Trump "aliwasha moto wa shambulio hili".

    Bennie Thompson, wa chama cha Democratic, alisema ghasia hizo zilihatarisha demokrasia ya Marekani.

    Wafuasi wa Trump walivamia Congress mnamo 6 Januari 2021 wakati wabunge walikuwa kwenye kikao cha tkudhibitisha ushindi wa Joe Biden.

    Baada ya uchunguzi wa takriban mwaka mzima, kamati teule ya Baraza la Wawakilishi la Marekani inayoongozwa na chama cha Democratic ilifunguliwa Alhamisi jioni kwa kuonyesha sehemu za mahojiano iliyofanya na wanachama wa karibu wa Bw Trump.

    Kanda za video zilitumiwa ili kutoa ushahidi na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani Bill Barr akisema madai ya rais huyo wa zamani kwamba uchaguzi ulichkachuliwa hayana msingi.

    “Hatuwezi kuishi katika ulimwengu ambao utawala ulioko madarakani unabaki madarakani kwa kuzingatia mtazamo wake, usioungwa mkono na ushahidi maalum kwamba kulikuwa na udanganyifu katika uchaguzi huo,” alisema mwanasheria mkuu huyo wa zamani.

    Kesi hiyo pia ilikuwa na ushahidi uliorekodiwa na Ivanka Trump, bintiye rais wa zamani, akisema "alikubali" hatua ya Bw Barr kupinga nadharia iliyokuwa ikitumiwa na babake.

  13. Putin: Nchi za Magharibi haziwezi kususia nishati ya Urusi kwa miaka kadhaa

    Rais wa Urusi Vladimir Putin anasema nchi za Magharibi hazitaweza kususia mafuta na gesi ya Urusi kwa miaka kadhaa.

    Aliongeza kuwa hakuna mtu anayejua nini kinaweza kutokea wakati huo, kwa hivyo kampuni za Urusi hazitakuwa "zikitengeneza visima vyao vya mafuta".

    Haya yanajiri wakati afisa wa Marekani amekiri kwamba faida ya nishati ya Urusi inaweza kuwa juu sasa kuliko ilivyokuwa kabla ya vita.

    Muungano wa Ulaya( EU) kwa sasa unaagiza karibu asilimia 40 ya gesi yake kutoka Urusi.

    Muungano huo umeahidi kupunguza utegemezi wake kwa mafuta ya Urusi kwa asilimia 90 ifikapo mwisho wa 2022, lakini hadi sasa haujatoa ahadi yoyote juu ya gesi.

    Marekani imeweka vikwazo dhidi ya bidhaa zote za nishati za Urusi. Vikwazo hivyo vimewekwa kwa lengo la kuadhibu Moscow kwa kuivamia Ukraine.

    Lakini kupanda kwa bei ya mafuta na gesi duniani kunamaanisha kwamba faida ya Urusi inaweza kuongezeka katika miezi ya hivi karibuni, licha ya kupunguzwa kwa usambazaji wa jumla.

    "Kiasi cha mafuta kinapungua katika soko la dunia, bei inapanda," Rais Putin aliambia kundi la wajasiriamali vijana.

    Soma:

  14. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja leo Ijumaa 10.06.2022.