Mauaji ya 'heshima' Iran: Wanawake wauawa na familia zao

Wanaharakati wa haki za binadamu wameonya kuwa matukio ya udhalilishaji wanawake yameongezeka nchini Iran.
Mauaji ya "heshima" ni mauaji ya mtu na wanafamilia ambao wanatuhumiwa kuleta aibu kwa familia kupitia tabia zao.
Suala la mauaji ya heshima lilikuja kwa majadiliano pale msichana mmoja aliyeitwa Mona Haideri alipouawa kikatili mwezi Februari. Baadhi ya maelezo ya kina katika makala hii yaliyotolewa na mwandishi wa BBC Sarah Monetta yanaweza kuonekana kukuaibisha.
Mona alimuoa binamu yake akiwa na umri wa miaka kumi na miwili.
Hata hivyo, alikimbilia Uturuki kuepuka unyanyasaji wa kijinsia. Lakini jamaa alimshawishi na kumrejesha nyumbani.
Aliaminika kuwa na ulinzi. Tayari ana umri wa miaka 17. Mwengine ni Parisa, mwalimu wa shule. Mume wake alimkata kuanzia juu kwenye mkono hadi kwenye kiganja cha mkono.
Sababu kuu hakuwa amefunika mkono wake. Akamchoma kwa kijiko cha moto kisa hakuamka asubuhi kusali.
Parisa akalazwa hospitalini baada ya mume wake kumwagia maji ya moto.
Na hapo ndipo alipogundua kwamba ni mjamzito.
Akaamua kutafuta eneo salama na kukimbilia Uturuki ambako aliomba hifadhi.
Lakini bado mume wake alimtumia ujumbe wa kumtishia maisha kwamba atamuua.
Pamoja na vitisho alivyopokea Parisa, mamlaka ya Uturuki ilifuta hadhi yake ya ukimbizi.
Yeye na mtoto wake sasa wako hatarini kusafirishwa kwenda Iran.Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa mwaka 2019, inakadiriwa kuwa wanawake 450 huuawa kila mwaka nchini Iran na wanafamilia au waume zao wenyewe kwa jina la mauaji ya heshima.
Mauaji kama haya hugonga vichwa vya habari pale yanapotokea hadharani, jambo la kikatili zaidi.
Katika matukio mengi, mauaji kama haya hufanyika bila ya mtu yeyote kuona. Adhabu katika kesi hizi pia ni ndogo.
Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema idadi ya mauaji yaliyoripotiwa inazidi kuongezeka.
Mauaji katika familia yamefichwa ndani. Wazazi wa wanawake waliouawa hata hawajafungua kesi dhidi ya muuaji.













