Ukraine 'tayari kwa makabiliano makubwa' dhidi ya Urusi
Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhaylo Podolyak ameambia televisheni ya taifa kwamba "Ukraine iko tayari kwa vita vikubwa" dhidi ya Urusi.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Zaidi ya miili 1,200 yapatikana katika mkoa wa Kyiv
Mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine anasema miili 1,222 imepatikana katika eneo la Kyiv tangu majeshi ya Urusi kuondoka katika eneo hilo.
Iryna Venediktova aliiambia Sky News, mamlaka ya Ukraine inachunguza visa 5,600 vya uhalifu wa kivita unaodaiwa kufanywa na wanajeshi wa Urusi tangu uvamizi huo uanze, na imegundua zaidi ya washukiwa 500 wa uhalifu wa kivita, wakiwemo maafisa wakuu wa kijeshi na serikali nchini Urusi.
"Tunachokiona katika mikoa yote ya Ukraine ni uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, na tunafanya kila kitu kurekebisha hilo," anasema.
Anaongeza kuwa Ukraine ina ushahidi kwamba Urusi ilifanya shambulizi la kombora kwenye kituo cha treni katika mji wa mashariki wa Kramatorsk, ambalo liliua zaidi ya watu 50 waliokuwa wakisubiri treni iwapeleke magharibi, hadi kwa usalama.
Urusi imekanusha kuhusika na shambulizi la Ijumaa na kudai kuwa halikuwa kombora lao. Pia imekanusha kuwalenga raia.
Msafara wa Urusi wanaswa kwenye picha za satellite mashariki mwa Kharkiv

Chanzo cha picha, Maxar Technologies
Kampuni ya picha za satelaiti Maxar Technologies imetoa picha za kile inachosema ni msafara mkubwa wa kijeshi wa Urusi, ulioko mashariki mwa Kharkiv.
Picha hizo, zilizopigwa tarehe 8 Aprili, zinaonyesha mamia ya lori za magari ya kivita yenye mizinga ya kukokotwa, na magari mengine ya kijeshi - yakienda kwa karibi maili nane (12km) na kuelekea kusini kupitia mji wa Velykyi Burluk wa Ukraine.
Katika ujumbe wa Twitter, mchambuzi wa masuala ya kijeshi George Barrow - akiwa na Taasisi ya Utafiti wa Vita (ISW) - alisema kuwa kuna uwezekano msafara huo ulikuwa unaelekea kusini katika mji wa Izyum. BBC haijaweza kuthibitisha dai hili kwa uhuru.
Vikosi vya Urusi viliuteka mji wa Izyum wiki iliyopita na wamekuwa wakiutumia kama uwanja wa kuelekea Sloyansk, mji ambao ni muhimu kwa lengo la Moscow la kuteka eneo lote la mashariki mwa Ukraine.
Vikosi vya Urusi hivi karibuni vimeuteka mji wa kimkakati wa Izyum na kuutumia kama kituo cha kushambulia Sloyansk, kusini mwa nchi hiyo.
ISW inasema ikiwa Ukraine itashikilia Sloyansk, kampeni ya Urusi ya kuteka maeneo ya mashariki ya Donetsk na Luhansk "itafeli".
Unaweza pia kusoma:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- ·SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Ukraine 'tayari kwa makabiliano makubwa' dhidi ya Urusi
Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhaylo Podolyak ameambia televisheni ya taifa kwamba "Ukraine iko tayari kwa vita vikubwa" dhidi ya Urusi.
Anasema Ukraine lazima iipige nyuma vikosi vya Moscow katika eneo la mashariki la Donbas, ambako Moscow inadhibiti maeneo mawili yanayotaka kujitenga, ili kupata mamlaka zaidi ya mazungumzo kabla ya kufanyika kwa mkutano kati ya Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
"Ukraine iko tayari kwa vita vikubwa. Ukraine lazima ishinde, ikiwa ni pamoja na Donbas.
Na mara tu hilo likitokea, Ukraine itakuwa na nafasi yenye nguvu zaidi ya mazungumzo," alisema, kama alivyonukuliwa na shirika la habari la Interfax.
"Baada ya hapo marais watakutana. Inaweza kuchukua wiki mbili, tatu."
Unaweza pia kusoma:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- ·SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Jennifer Lopez na Ben Affleck wachumbiana miaka 18 baada ya kughairi harusi

Chanzo cha picha, Getty Images
Mugizaji na muimbaji Jennifer Lopez ametangaza kuwa atafunga pingu za maisha na Ben Affleck, miaka 18 baada ya wapenzi hao kusitisha harusi yao.
Lopez, 52, alidokeza kuwa amechumbiwa kwa mara ya pili na nyota wa Hollywood Affleck katika ujumbe aliyoweka katika mtandao wake wa OnTheJLo.
Alitania jinsi alivyokuwa na "tangazo kuu" katika chapisho kwa wafuasi wake milioni 202 wa Instagram siku ya Jumamosi.
Lopez hata hivyo alisema wale ambao si "wandani wake wa karibu" watalazimika kujiunga na tovuti yake, ambapo anashirikisha "masuala zaidi ya kibinafsi", ili kujifunza habari zake, aliongeza.
JLO anaonekana akilia kwenye video huku akivutiwa na pete kubwa ya kijani ya uchumba.
Uvumi kwamba wawili hao wamerudiana tena ulizuka baada ya kupigwa picha ya pamoja mwezi Mei mwaka jana.
Lopez alithibitisha rasmi kwamba wamerudiana kupitia chapisho la Instagram akimmbusu mpenzi wake kwenye yacht huko St Tropez,siku yake ya kuzaliwa ya 52.
Soma zaidi:
Man City v Liverpool: Timu mbili bora za EPL kukutana Uwanjani Etihad

Chanzo cha picha, BBC Sport
Manchester City na Liverpool zitakutana kwenye Uwanja wa Etihad Jumapili katika pambano kubwa la Ligi Kuu ya Uingereza ambalo linaweza kusaidia sana kuamua hatima ya ubingwa.
Viongozi wa Pep Guardiola wanaanza na pointi 73 - moja mbele ya Wekundu hao - zikiwa zimesalia mechi saba tu baada ya wikendi hii.
Wakati Liverpool wakiwasili Manchester wakiwa nyuma ya ushindi wa mechi 10 kwenye ligi juu, City - ambao wanaenda kunyakua taji la nne katika misimu mitano - wamepoteza pointi tano katika mechi zao tano zilizopita tangu kushinda 4-0 huko Norwich mnamo. 12 Februari.
Ushindi kwa The Reds utawafanya kumaliza wakiwa juu ya jedwali kwa mara ya kwanza tangu Oktoba 1.
Polisi wanamchunguza Ronaldo baada ya video akivunja simu ya shabiki kuibuka

Chanzo cha picha, PA Media
Polisi nchini Uingereza wanachunguza madai ya shambulio baada ya mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo kuonekana akivunja simu ya shabiki mmoja.
Picha zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na maoni yaliyodai kuwa alivunja simu hiyo alipokuwa akitoka nje ya uwanja baada ya timu yake kupoteza mechi dhidi ya Everton 1-0.
Ronaldo baadaye aliomba msamaha baada ya video inayomuonyesha akivunja simu ya shabiki huyo kuibuka.
Polisi wa Merseyside walisema walikuwa wakichunguza "ripoti za madai ya kushambuliwa" katika bustani ya Goodison Park siku ya Jumamosi.
"Si rahisi kukabiliana na mihemko katika nyakati ngumu kama ile inayotukabili," alisema Ronaldo akiomba radhi.
Matokeo hayo yaliharibu matumaini ya United kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kukutana na timu ya Everton ambayo ilikuwa pointi moja juu ya eneo la kushushwa daraja kabla ya kuanza.
"Hata hivyo, kila mara tunapaswa kuwa na heshima, subira na kuwa mfano mwema kwa vijana wote wanaopenda mchezo huo mzuri," Mreno huyo aliongeza.
"Ningependa kuomba radhi kwa hasira yangu na, ikiwezekana, ningependa kumwalika shabiki huyu kutazama mchezo huko Old Trafford kama ishara ya mchezo wa haki na uanamichezo."
Msemaji alisema wanawasiliana na Manchester United na Everton.
Manchester United walisema wanafahamu "tukio linalodaiwa kutokea baada ya mechi ya Jumamosi Everton na klabu itashirikiana na uchunguzi wowote wa polisi".
Vikwazo kamili vya mafuta vinaweza kukomesha vita - msaidizi wa zamani wa Putin

Chanzo cha picha, ANADOLU / GETTY
Maelezo ya picha, Vita nchini Ukraine vinaweza kukomeshwa ikiwa nchi za magharibi zitaacha kununua mafuta na gesi ya Urusi, asema mshauri mkuu wa zamani wa uchumi wa Rais Putin. "Vikwazo halisi" dhidi ya nishati ya Urusi kutoka kwa nchi za Magharibi vinaweza kusitisha vita nchini Ukraine, mshauri mkuu wa zamani wa Rais Putin wa masuala ya kiuchumi amependekeza.
Dk Andrei Illarionov alisema Urusi "haikuchukulia kwa uzito" vitisho vya nchi zingine kupunguza matumizi yao ya nishati.
Licha ya kujaribu kupunguza utegemezi wake kwa vyanzo vya Urusi, Ulaya inaendelea kununua mafuta na gesi kutoka nchini humo.
Mwaka jana, kupanda kwa bei kulimaanisha mapato ya mafuta na gesi yalichangia 36% ya matumizi ya serikali ya Urusi.
Sehemu kubwa ya mapato hayo yanatokana na Umoja wa Ulaya, ambao huagiza takriban 40% ya gesi yake kutoka nje na 27% ya mafuta yake kutoka Urusi.
Wiki hii, mwanadiplomasia wake mkuu Josep Borrell alisema "bilioni [euro] ndizo tunazomlipa Putin kila siku kwa nishati anayotupatia".
Dk Illarionov alisema ikiwa nchi za Magharibi "zitatekeleza vikwazo kamili vya uuzaji wa mafuta na gesi kutoka Urusi ... sina shaka labda ndani ya mwezi mmoja au miwili, operesheni za kijeshi za Urusi nchini Ukraine, huenda zingesitishwa"
Wakati biashara ya mafuta na gesi imeendelea wakati wa mzozo, vikwazo vilivyoenea vinamaanisha kuwa shughuli nyingi za kiuchumi zimesitishwa, makampuni mengi ya kigeni yamejiondoa na mauzo ya nje yametatizika.
Unaweza pia kusoma:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- ·SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Nato inapanga kuwa na jeshi la kudumu katika mpaka wake - Stoltenberg - Stoltenberg

Chanzo cha picha, Reuters
Katika mahojiano na gazeti la The Sunday Telegraph, Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg anasema muungano huo "uko katikati ya mageuzi ya kimsingi" ambayo yataakisi "matokeo ya muda mrefu" ya vita vya Vladimir Putin nchini Ukraine.
Katika mahojiano hayo, Stoltenberg anasema Nato inapanga kuwepo kwa wanajeshi wa kudumu kwenye mpaka wake katika juhudi za kupambana na uvamizi wa Urusi katika siku zijazo.
Analiambia jarida hilo kwamba lengo lake ni kuhakikisha washirika wengine wa Nato wanatimiza mahitaji ya chini ya muungano ya 2% ya matumizi kama sehemu ya Pato lao la Taifa.
Vita vya Ukraine: Njia tatu vita hivi vinaweza kuongezeka na kuijumuisha Nato

Chanzo cha picha, Getty Images
Mawaziri wa Nato wamekuwa wakikutana mjini Brussels wiki iliopita kujadili ni umbali gani wanapaswa kufikia katika kutoa vifaa vya kijeshi kwa Ukraine.
Changamoto ya Nato katika muda wote wa vita hivi imekuwa jinsi ya kumpa mshirika wake Ukraine msaada wa kijeshi wa kutosha kujilinda bila kujiingiza katika mzozo na kujikuta katika vita na Urusi.
Serikali ya Ukraine imekuwa wazi katika wito wake wa kuomba msaada.
Iwapo itakuwa na nafasi yoyote ya kujikinga na shambulio lijalo la Urusi kwenye eneo la Donbas mashariki mwa nchi, inasema, basi inahitaji haraka ugavi wa mkuki wa Magharibi, NLAW (silaha nyepesi ya kupambana na kifaru cha kizazi kijacho) , Stinger na Starstreak makombora ya kukinga vifaru na ya kutungulia ndege ambayo majeshi yake tayari yamekuwa yakitumia kwa athari hiyo katika vita hivi. Kiasi hicho kinakuja.
Lakini Ukraine inataka zaidi. Inataka vifaru, ndege za kivita, ndege zisizo na rubani na mifumo ya hali ya juu ya ulinzi wa anga ili kukabiliana na ongezeko la Urusi la mashambulio ya angani na makombora ya masafa marefu ambayo yanazidi kuharibu maduka ya kimkakati ya Ukraine ya mafuta na mambo mengine muhimu.
Unaweza pia kusoma:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- ·SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Vita vya Ukraine: Matukio ya hivi punde kwa mukhtasari

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. Ikiwa ndio mwanzo unajiunga nasi, huu hapa ni muhtasari wa kile ambacho kimekuwa kikifanyika.
- Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alifanya ziara ya ghafla katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv. Katika taarifa iliyotolewa baada ya ziara hiyo, alisifu "uongozi thabiti wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na ushujaa na ujasiri wa watu wa Ukraine". Uingereza ilisema itatoa magari 120 ya ziada ya kivita na mifumo mipya ya makombora ya kuzuia meli kwa Ukraine.
- EU imefungua tena ubalozi wake katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, baada ya kuuhamishia Poland kwa muda baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
- Mabadilishano ya wafungwa yalifanyika kati ya Urusi na Ukraine: wanajeshi 12 na raia 14 waliachiliwa.
- Bw Zelensky alisema Ukraine inajiandaa kwa vita muhimu Mashariki mya nchi hiyo.
- Miili ya raia 10 imepatikana chini ya vifusi katika mji wa Borodyanka, karibu na Kyiv siku ya Jumamosi, alisema naibu mkuu wa huduma ya dharura ya Ukraine katika mkoa wa Kyiv, Bogdan Danilyuk.
- Gavana wa Donetsk mashariki mwa Ukraine, Pavlo Kyrylenko, amesema watu watano wameuawa kwa kushambuliwa kwa makombora katika mkoa huo - alisema wanne waliuawa huko Vuhledar na mmoja huko Novomykhailivka.
- Siku ya Jumamosi, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema kwamba kujiondoa kwa Urusi kutoka kaskazini kulifichua makaburi ya halaiki na matumizi ya binadamu kama ngao.
- Klabu kubwa ya kandanda ya Mashariki mwa Ukraine, Shakhtar Donetsk, imefungua ziara yake ya "Soka kwa Amani" kw akucheza mechi ya kirafiki nchini Ugiriki dhidi ya viongozi wa ligi Olympiakos. Ziara hiyo ya hisani inachangisha pesa za kutoa misaada kwa watu walioathiriwa na vita nchini Ukraine.
Uchokozi wa Urusi unalenga Ulaya yote - Zelensky

Chanzo cha picha, EPA
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kwamba uchokozi wa Urusi sio dhidi ya Ukraine pekee bali unalenga Ulaya nzima.
Akizungumza katika hotuba yake usiku wa kuamkia Jumamosi Bw Zelensky alizitaka nchi za Magharibi kuweka vikwazo kamili dhidi ya bidhaa za nishati za Urusi na kuipatia Ukraine silaha za ziada.
Alisema matumizi ya nguvu ya Urusi ni "janga ambalo bila shaka litamkumba kila mtu".
Bw Zelensky alisema Ukraine iko tayari kwa vita vikali, kwani majeshi ya Urusi yalikuwa yakikusanyika mashariki mwa nchi hiyo.
Lakini aliongeza: "Hii itakuwa vita vikali, tunaamini katika mapambano haya na ushindi wetu. Tuko tayari kupigana kwa wakati mmoja na kutafuta njia za kidiplomasia za kukomesha vita hivi."
Mpatanishi wa Ukraine Mykhailo Podolyak alisema Rais Zelensky na Rais wa Urusi Vladimir Putin hawatakutana hadi pale Urusi itakaposhindwa mashariki mwa nchi hiyo.
Unaweza pia kusoma:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- ·SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Hjambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja leo Jumapili 10.04.2022.