Tetesi za Soka Ulya Jumapili 10.04.2022: Haaland, Lukaku, Jorginho, Tielemans, Diallo, Tevez

Romelu Lukaku akichezea Chelsea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chelsea ilimsajili tena Romelu Lukaku kutoka Inter Milan kwa £97.5m mwezi Agosti
Iliyochapishwa

Inter Milan wanataka kumsajili tena mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, kutoka Chelsea msimu wa joto - lakini kwa mkataba wa mkopo. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, anapotarajiwa kusalia Paris Saint-Germain, Real Madrid wanajiandaa kuongeza juhudi za kumsaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland - hatua ambayo italemaza nafasi ya Manchester City ya kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Norway, 21. (Sunday Mirror)

Haaland na kiungo wa Monaco wa miaka 22-Mfaransa Aurelien Tchouameni wanataka kujiunga naReal Madrid -lakini wachezaji hao wawili wanasubiri klabu hiyo ya La Liga kuanzisha mchakato wa uhamisho. (AS -kwa Kihispania)

Erling Braut Haaland

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland

Tottenham na Arsenal wanajiandaa kumenyana katika kinyang'anyiro cha usajiliwa wa kiungo wa are Leicester na timu ya taifa ya England James Maddison, 25. (Sun on Sunday)

Meneja wa Aston Villa Steven Gerrard anapanga kufanya usajilimkubwa wa majira ya kiangazi huku wachezaji takriban wanane wakitarajiwa kuuzwa - beki wa Liverpool Muingereza Joe Gomez, 24 na kiungo wa kati wa Brighton wa Mali Yves Bissouma, 25, miongoni mwa walengwa wakuu wa Gerrard. (Sunday Mirror)

Mkufunzi wa Tottenham Antonio Conte anataka kumsajili kiungo nambari 10 katika uhamisho wa msimu wa joto ili kumpatia nafasi mshambuliaji wa England Harry Kane, 28, kucheza katika safu ya mashambulizi. (Mail on Sunday)

Antonio Conte

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Antonio Conte aliiongoza Chelsea kati ya 2016 na 2018 kabla ya kuwa Inter Milan kwa misimu miwili

Juventus nao wanapania kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea mwenye umri wa maika 30- Mtaliano Jorginho. (Tutto Mercato - Kwa Kiitaliano)

Matumaini ya Manchester United ya kumsajili kiungo wa Leicester City na Ubelgiji Youri Tielemans yamepigwa jeki baada ya wapinzai wao Liverpool na West Ham kusitisha mpango wa kumnunua mchezaji huyo wa 24. (CBS Sports)

United wanatazamiwa kupoteza mamilioni iwapo watashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa, kwa sababu ya kipengele kilichojumuishwa katika mkataba wa ufadhili wa jezi za klabu.

Erik ten Hag anampanga mchezaji wa zamani wa Manchester United Robin van Persie kama msaidizi wake wa ukufunzi iwapo atachukua mikoba ya Old Trafford, hata hivyo kocha wa Ajax bado ana wasiwasi kuhusu nafasi hiyo. (Mail ya Jumapili)

Erik ten Hag

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Erik ten Hag anataka mchezaji wa zamani wa United Robin van Persie kuwa msaidizi wake

Rangers hawana mpango wa kuongeza mkataba wa mkopo wa winga wa Ivory Coast Amad Diallo, 19, kutoka Manchester United hadi mwisho wa msimu huu, au kufanya mazungumzo ya mkataba wa kudumu. (Football Insider)

Manchester City boss Pep Guardiola and Liverpool boss Jurgen Klopp

Chanzo cha picha, BBC Sport