Habari za hivi punde, Marekani yatoa onyo jipya la usafiri wa Urusi
Marekani imetoa onyo jipya la usafiri kwa Urusi ambayo inasema mamlaka "inaweza kuwatenga na kuwaweka kizuizini" Wamarekani nchini humo.
Ikitaja uwezekano wa kuwanyanyasa raia wa Marekani, onyo hilo linarudia wito kwa Wamarekani kutosafiri kwenda Urusi au kuondoka "mara moja".
Pia ilionya Wamarekani kuhusu "utekelezaji holela wa sheria za mitaa".
Ushauri huo pia ulisema kulikuwa na ripoti zinazoendelea za raia wa Marekani "kutengwa na kuzuiliwa na jeshi la Urusi" wanapokuwa Ukraine, au wanapohama kwa ardhi kupitia eneo linalokaliwa na Urusi.
"Ikiwa unataka kuondoka Urusi, unapaswa kufanya mipango peke yako haraka iwezekanavyo,"onyo hilo lilisema.
Marekani ilisimamisha ubalozi wake na ubalozi mdogo nchini Ukraine siku chache baada ya Rais Putin kutangaza uvamizi wake.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine

