Mkuu wa Majeshi Ukraine adai Urusi inaondoa vikosi vyake katika mji wa Kyiv

Chanzo cha picha, Getty Images
Urusi imelazimika kuondoa vikosi vyake kutoka eneo la Kyiv baada ya kushindwa vibaya, mkuu wa jeshi la Ukraine amesema.
Katika taarifa juu ya mapigano hayo, Jenerali Staff alisema kuwa makundi mawili ya kijeshi ya jeshi la Urusi yaliondolewa kupelekwa Belarus, hatua ambayo alisema ni mfano wa vitengo vingi vya kijeshi "vilivyoshindwa kufanikiwa".
Zaidi ya hayo, alibainisha kuwa kuna "kupungua kwa kiasi kikubwa" kwa vikosi vinavyoingia Ukraine kutoka Urusi kwenda Ukraine.
Katika tathmini nyingine ya hivi karibuni, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Urusi imefanikiwa kuizua Ukraine biashara ya kimataifa ya baharini kwa kuweka kizuizi cha majini katika pwani ya Bahari Nyeusi.
Wiki iliyopita Urusi ilisema inapanga kuelekea nguvu zake mashariki mwa nchi hiyo, ingawa tangu wakati huo ripoti za mashambulizi katika miji mikubwa zimeendelea.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
