Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanajeshi wa Urusi waua watu 10 katika foleni ya kutafuta mkate-Mwendesha Mashtaka
Aliwataka wanasiasa wa Marekani waliokusanyika kukumbuka kushambuliwa siku za nyuma - katika Bandari ya Pearl mwaka 1941 na tarehe 11 Septemba 2001 - akisema Waukraine walikuwa wakipitia jambo hilo hilo kila siku.
Moja kwa moja
Vyanzo vya NATO vinasema kuwa Urusi huenda haitaafikia malengo yake ya kijeshi nchini Ukraine
Maafisa wakuu wa jeshi la NATO wanasema Rais Putin ni wazi hajafikia malengo yake ya kijeshi nchini Ukraine hadi sasa na "pengine hatafikia mwisho wa siku".
Lakini waliongeza kuwa vikosi vya Urusi bado vina uwezo wa kufanya "uharibifu mwingi".
Maafisa wa ulinzi walisema kwamba wakati vikosi vya Urusi vimepata mafanikio katika mikoa ya Donetsk na Luhansk, bado vimeshindwa kuizingira Kyiv - jambo ambalo walisema Urusi ilitarajia kufanya baada ya siku chache.
Shambulio lililotarajiwa la Warusi katika eneo la kusini karibu na Odessa pia, hadi sasa, limeshindwa kutimia.
Maafisa wa Nato wanaamini kuwa mpango wa awali wa kijeshi wa Urusi ulijumuisha kuchukua pwani yote ya Bahari Nyeusi ya Ukraine - hadi Moldova.
Walikadiria kuwa jeshi la uvamizi la Urusi lilikuwa likikumbwa na ukosefu wa mafuta na chakula pamoja na kupata hasara. Walisema kuwa Rais Putin tayari alikuwa akitafuta wapiganaji wa kuimarisha jeshi lake.
Afisa mmoja alisema kuna uwezekano mkubwa kwamba ingehusisha kuleta wapiganaji wa kigeni kutoka Syria na wanakandarasi binafsi wa kijeshi - kama vile kundi la Wagner - kwenda Ukraine.
Afisa mwingine aliongeza kuwa hifadhi za kijeshi za Urusi "hazikuwa silaha ya siri".
Maafisa wa Nato wanasema kuwa washirika na mataifa wanachama wanaendelea kutuma silaha kwa Ukraine. Walisema kwamba ni pamoja na silaha za zamani za Soviet, ambazo vikosi vya Ukraine vingekuwa vimefunzwa kutumia, na vile vile nchi za Magharibi zilitoa makombora ya kuzuia vifaru na ndege.
Unaweza pia kusoma
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Putin: Hatutahitaji kuchapisha pesa ili kukabiliana na vikwazo
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema nchi za Magharibi hazitafanikiwa katika kile alichokiita jaribio lake la kutaka kutawala dunia na kuisambaratisha Urusi, Reuters inaripoti.
Putin amekuwa akizungumza katika mkutano wa serikali uliyopeperushwa kwa njia ya televisheni leo asubuhi, akisema kwamba ikiwa nchi za Magharibi zinadhani Urusi itarudi nyuma basi haziielewi Urusi.
Pia alizungumza kuhusu vikwazo vilivyopangwa kuathiri uchumi wa Urusi - lakini akasema benki kuu haihitaji kuchapisha pesa na nchi ina rasilimali za kutosha za kifedha.
“Uchumi na biashara zetu zina nyenzo zote muhimu ili kufikia malengo yote yaliyowekwa, changamoto zitatufanya thabiti tu,” alisema.
Unaweza pia kusoma
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
'Hatuwezi kuondoka kwani wanaweza kutuua'
BBC imekuwa ikizungumza na watu katika mji wa bandari wa kusini wa Kherson ambao ulitekwa na Warusi mapema mwezi huu.
"Askari wa Urusi, wavamizi, wako kila mahali," anasema mmoja wa watu waliozungumza nasi, anayeitwa Olga. "Kherson imetekwa’
“Hakuna anayeweza kutoka mjini au kwenda mjini kwa sababu wanaua watu wa kawaida tu, wanaua watu wasio na hatia, raia waliojaribu kuondoka mjini waliuawa.
"Askari wa Urusi wana orodha ya watu wetu mashuhuri mjini na wanapata tu mahali wanapoishi. Wanaenda huko, wanawakuta na pia wanawaua."
Olga - ambaye hakutaka tutumie jina lake la pili - anadai kwamba watu ambao wameandamana wamekusanywa na kuuawa.
Pia anasema kuna uhaba wa chakula na dawa, na pia matatizo ya gesi, umeme, joto na mawasiliano.
Unaweza kusoma pia:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Vita vya Ukraine: Zelensky afananisha vita nchini mwake na 9/11 katika maombi yake kwa Bunge la Marekani
Rais wa Ukraine aliibua hofu ya mashambulizi ya kigaidi ya mwaka 2001 dhidi ya Marekani alipokuwa akiomba msaada zaidi wa kijeshi katika hotuba ya kihistoria kwa Bunge la Marekani.
Volodymyr Zelensky alisema kupitia kiunga cha video kwamba Ukraine ilikuwa ikivumilia hali kama ya 9/11 kila siku inapopambana na vikosi vya Urusi.
Alizitaka tena Marekani na Nato kutekeleza agizo la kutoruka ndege juu ya Ukraine, akisema: "Ninahitaji kulinda anga."
Rais Biden baadaye anatazamiwa kutia saini msaada wa kijeshi wa $800m (£612m) kwa Ukraine.
Aliwataka wanasiasa wa Marekani waliokusanyika kukumbuka kushambuliwa siku za nyuma - katika Bandari ya Pearl mwaka 1941 na tarehe 11 Septemba 2001 - akisema Waukraine walikuwa wakipitia jambo hilo hilo kila siku.
"Katika historia yenu pana , mna kurasa ambazo zingewawezesha kuelewa historia ya Kiukreni. Tuelewe sasa," alisema.
Pia alirejelea hotuba maarufu ya kiongozi wa haki za kiraia Martin Luther King: "Nina ndoto, maneno haya yanajulikana kwa kila mmoja wenu - leo naweza kusema nina hitaji. Ninahitaji kulinda anga," alisema.
Kiongozi huyo wa Ukraine pia alionyesha video ya mashambulizi ya makombora katika miji ya nchi yake na kusababisha vifo na watu waliojeruhiwa.
Ametoa wito mara kwa mara kwa Nato kuweka amri la kutoruka ndege katika anga ya nchi yake, lakini Nato imekataa.
Agizo hilo juu ya Ukraine litamaanisha kuwa majeshi ya Nato yatalazimika kujihusisha moja kwa moja na ndege zozote za Urusi zinazoonekana katika anga hizo na kuzipiga risasi ikiwa ni lazima.
Unaweza kusoma pia:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Habari za hivi punde, Ukraine yathibitisha vifo vya watu 10 huko Chernihiv
Maafisa wa Ukraine wamethibitisha kuwa watu 10 wameuawa na wanajeshi wa Urusi katika mji wa kaskazini wa Chernihiv.
Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine, maafisa walisema kuwa shambulio hilo lilitokea mwendo wa saa 10:00 kwa saa za huko (08:00 GMT) asubuhi ya leo wakati "watumishi wa Jeshi la Urusi walipowafyatulia risasi watu waliokuwa wamesimama kwenye foleni ya kutafuta mkate karibu duka la mboga".
Bado haijafahamika jinsi watu hao 10 waliuawa, lakini wanahabari wa vyombo vya habari nchini humo wameiambia BBC kwamba kuna uwezekano kuwa wahasiriwa hao walifyatuliwa risasi na mizinga ya Urusi iliyokuwa nje ya mji.
Ubalozi wa Marekani nchini Ukraine umeandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba leo vikosi vya Urusi vimewapiga risasi na kuwaua watu 10 katika mji wa kaskazini wa Chernihiv.
Afrika Kusini yaidhinisha mpira wa mviringo kwa wanawake kuzuia maambukizi ya HIV
Afrika Kusini imeidhinisha matumizi ya mpira wa mviringo mithili ya pete liyoundwa ili kupunguza hatari ya maambukizi ya HIV kwa wanawake.
Ni hatua muhimu katika nchi ambayo karibu theluthi mbili ya maambukizi mapya miongoni mwa wanawake.
Pete hiyo ambayo iliidhinishwa nchini Zimbabwe mwaka jana na bado inaendelea kufanyiwa majaribio katika mataifa kadhaa ya Afrika ina kiwango cha ufanisi cha hadi asilimia 50.
Inafanya kazi kwa kutoa polepole dawa ambayo inapunguza mambukizi ya HIV katika uke na inabadilishwa kila mwezi. Ni mbadala wa dawa zingine zilizopo ikiwa ni pamoja na dawa ya kumeza kila siku.
Mamlaka ya udhibiti wa Afya nchini Afrika Kusini imeidhinisha matumizi ya mpira huo wa mviringo kwa wanawake wenye umri wa miaka 18 na zaidi. Hata hivyo, uzinduzi wake utachelewa kwani idara ya afya inachunguza ufanisi na gharama za pete.
Mkuu wa kijasusi wa Urusi aonya hatma ya nchi hiyo kuamuliwa katika siku zijazo
Mkuu wa shirika la kijasusi la kigeni la Urusi amesema hatma ya nchi hiyo itaamuliwa siku zijazo.
Sergei Naryshkin, ambaye anaongoza SVR, aliambia jopo moja huko Moscow kwamba Urusi "sasa inapitia wakati wa kihistoria"
Hatima ya Urusi inaamuliwa, mahali pake pa baadaye ulimwenguni," Naryshkin alisema.
Hotuba ya mkuu huyo wa kijasusi ilizingatia umuhimu wa uhuru na aliwaambia wajumbe "uhuru na hadhi ya nchi ni dhamana ya ustawi na utu wa raia wetu, hii ni mustakabali wa watoto wetu".
"Katika masuala kama haya, Urusi haijawahi kurudi nyuma na haitarudi nyuma, kwa sababu vinginevyo itakoma kuwa Urusi".
Kabla ya uvamizi wa Ukraine, Naryshkin alikuwa amefedheheshwa na Rais Vladimir Putin kwenye TV ya serikali wakati wa mkutano wa usalama wa kitaifa .Putin alipingana na afisa huyo wa wakati mmoja wa KGB, ambaye alionekana kubadilika badilika alipoalikwa kutoa maoni ya kuunga mkono kutambuliwa kwa maeneo yanayotaka kujitenga nchini Ukraine.
Unaweza kusoma pia:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Maslahi ya kigeni yamechangia ongezeko la mapinduzi- Ecowas
Rais wa Ghana, ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi Ecowas, amesema kuna mwelekeo wa kimataifa kuhusu matukio ya hivi karibuni ya mapinduzi ya kijeshi barani Afrika.
Nana Akufo-Addo aliliambia jukwaa la Umoja wa Afrika kwamba "baadhi ya vyombo vya kigeni vinachukulia mapinduzi barani Afrika kama njia ya kuimarisha matarajio yao ya kikanda".
Amesema ushawishi wa kigeni umechangia kampeni za upotoshaji zinazodhoofisha mamlaka ya serikali katika bara hilo na kuanzisha maandamano ya upinzani.
Bw Akufo-Addo hakutoa maelezo yoyote kuhusu wale aliodhani wanahusishwa na mapinduzi hayo.
Mapinduzi ya kijeshi wa hivi majuzi nchini Burkina Faso, Mali na Guinea yamesababisha wito kwa viongozi wa Afrika kuendeleza utawala bora ili kuzima hali ya kutopendana miongoni mwa raia.
Kondomu na vyandarua vyatoweka katika kashfa ya Kenya
Mamlaka ya Ugavi wa Dawa nchini Kenya (Kemsa) inaangaziwa tena, baada ya maelfu ya mipira ya kondomu, vyandarua na dawa za kifua kikuu zenye thamani ya $100,000 (£77,000) kutoweka kwenye ghala lake.
Dawa zilizopotea zinaaminika kuibiwa na kuuzwa tena kimagendo na kwa wanakemia wa kibinafsi, kulingana na Global Fund.
Mfuko huo pia unaituhumu Kemsa kwa kuzidisha thamani ya dawa kwa mamilioni ya dola, huku baadhi ya dawa zikiwa zimeongezwa bei mara 100 zaidi ya bei yake halisi.
Shirika hilo la serikali bado halijazungumzia madai hayo.
Mfuko wa Kimataifa unafadhili mapambano ya Kenya dhidi ya VVU/UKIMWI, kifua kikuu na malaria.
Kemsa iligonga vichwa vya habari mnamo 2020 baada ya ufichuzi wa kashfa ya udanganyifu kukumba ununuzi wa vifaa tiba vya Covid-19.
Zabuni ya thamani ya dola milioni 78 zilisemekana kupewa watu walio na ushawishi wa kisiasa na wafanyabiashara.
Tukio hilo lilimfanya Rais Uhuru Kenyatta kuvunja bodi yake na usimamizi wake mkuu.
Global Fund, ambayo imetoa zaidi ya $1.4m kwa Kenya katika miongo miwili iliyopita, imependekeza uchunguzi zaidi wa Kemsa kuhusu dawa zilizopotea.
Vita vya Ukraine: Viongozi wa Ulaya wapanda treni kwa ujasiri kukutana na Zelensky
Ukraine imepongeza ujasiri wa viongozi wa Ulaya waliosafiri kwa treni kutoka Poland hadi Kyiv kuonesha mshikamano wao baada ya mji huo kushambuliwa na Urusi.
Mawaziri wakuu wa Poland, Slovenia na Jamhuri ya Czech walikutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Jumanne jioni wakati amri ya kutotoka nje ilianza kutekelezwa mjini Kyiv.
Baada ya hapo, kiongozi wa Czech aliwaambia Waukraine kwamba "hawako peke yao".
Kundi hilo la viongozi ni la kwanza kutoka Ulaya kuzuru Ukraine tangu uvamizi wa Urusi.
"Tunafurahia pambano lako la ujasiri," Petr Fiala aliandika kwenye tweet. "Tunajua kwamba wewe pia unapigania maisha yetu. Hauko peke yako, nchi zetu zinasimama na wewe."
Mateusz Morawiecki wa Poland alisema kuwa Ulaya haitakuwa sawa ikiwa itapoteza Ukraine. Badala yake, aliandika, lingekuwa "toleo lililoshindwa, lililofedheheshwa na la kusikitisha la utu wake wa zamani".
Jenerali wa nne wa Urusi auawa katika mapigano, Ukraine inadai
Maafisa wa Ukraine wanasema wamemuua jenerali wa nne wa Urusi katika ishara kwamba makamanda wa Moscow wanazidi kulazimishwa kuongoza vita kutoka mbele.
Anton Gerashchenko, mshauri katika wizara ya mambo ya ndani ya Kyiv, alidai kwenye Telegram kwamba vikosi vya Ukraine vilimuua Meja Jenerali wa Urusi Oleg Mityaev wakati wa mapigano makali viungani mwa mji wa kusini-mashariki wa Mariupol.
BBC haiwezi kuthibitisha dai hili kwa uhuru na Moscow bado haijatoa maoni yoyote kuhusu ripoti za kifo chake.
Gerashchenko aliandika kwamba Mityaev alikuwa kamanda wa kitengo cha 150 cha bunduki na akachapisha picha ya kile alichosema kuwa afisa aliyekufa.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky pia aliripoti kifo cha jenerali mwingine wa Urusi wakati wa hotuba yake ya usiku kutoka Kyiv, lakini hakumtaja jina.
Urusi inaaminika kuwa na Majenerali Meja wapatao 20 nchini Ukraine wanaoongoza vita .
Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskly amewataka moja kwa moja maafisa wakuu wa Urusi na wanahabari kujiuzulu nyadhifa zao na kuchukua msimamo dhidi ya uvamizi wa nchi yake.
Akizungumza wakati wa hotuba ya usiku kutoka mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv, Zelensky alihutubia moja kwa moja "maafisa wote wa Shirikisho la Urusi"."Ikiwa utasalia ofisini, ikiwa haupingi vita, jumuiya ya kimataifa itakunyima kila kitu," Zelensky alisema. "Kila kitu ambacho umepata kwa miaka mingi. Hili tayari linafanyika."
Unaweza kusoma pia:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Warusi kumpa 'lifti' mwanaanga wa Marekani hadi duniani licha ya mvutano
Mwanaanga wa Marekani sasa atarejea Duniani, baada ya kuhofia kwamba lifti yake ya Urusi huenda isifanikiwe.
Awali ilidhaniwa Mark Vande Hei - ambaye amekuwa anga za juu kwa siku 355 - huenda akaachwa nyuma na chombo cha ISS kutokana na mvutano mkali uliotokea kufuatia hatua ya Urusi kuvamia Ukraine.
Lakini imebainika kuwa atasafiri kwa kutumia chombo cha Urusi hadi Kazakhstan.
Mmarekani huyo wa Warusi wawili watasafirishwa hadi duniani.
"Nawahakikishia kuwa Mark anakuja nyumbani.. Tumewasiliana na wenzeti wa Urusi. Hakuna mashaka yoyote kuhusiana na hilo," Joel Montalbano, Meneja wa Mpango wa Nasa wa Kituo cha Kimataifa cha Anga za juu (ISS) amesema.
Alikiri wanaanga "walikuwa na ufahamu wa kile kinachoendelea" duniani, lakini bado wanafanya kazi pamoja.
Chini ya sheria ya kimataifa ya anga za juu, wanaanga kutoka mataifa yote lazima "watoe msaada wowote unaowezekana" kwa wanaanga wengine inapohitajika, "ikiwa ni pamoja na kutua kwa dharura katika nchi ya kigeni au baharini".
Habari za hivi punde, Jeshi la Ukraine: Tumedungua ndege tatu za kivita za Urusi, na kuangusha makombora mawili
Jeshi la Ukraine limetoa taarufa kwa vyombo vya Habari likisema kwamba limefanikiwa kufanyia uharibifu mkubwa makundi ya jeshi ya Urusi.
Linasema kwamba jeshi lao la angani lilifanikiwa kudungua ndege tatu za kivita za Urusi , helikopta moja , ndege tatu zisizo na rubanina kuyaangusha makombora mawili. BBC bado haijaweza kuthibitisha madai hayo.
Jeshi la Ukraine pia limesema kwamba huku Urusi ikiendelea kushambulia maeneo yalio na wakaazi wengi mijini, wanajeshi wake wameshindwa kusonga mbele , ikiwemo katika maeneo ya Donetsk, Luhansk na Mykolaiv.
‘’Adui anaendelea kupata hasara katika maeneo fulani’’, taarifa hiyo ilisema.
Chapisho la mapema , lilisema kwamba jeshi la Urusi limeshindwa kuyadhibiti maeneo iliyoyateka na kwamba lilikuwa linakaribia kuwaita makadeti wake kwenda katika mstari wa mbele katika vita.
Urusi pia inatafuta wapiganaji wa kigeni ili kufidia maeneo ambayo wanajeshi wake wameuawa ama hata kusalimu amri.
Waziri wa Ulinzi nchini Uingereza katika taarifa yake alisema kwamba : Kutokana na hilo hasara waliopata imeifanya Urusi kushindwa kutekeleza mashambulizi wakati ambapo wanajeshi wa Ukraine wamejizatiti kujibu mashambulizi.
Mzozo wa Ukraine: Ni nini kinachoendelea Ukraine?
Ikiwa ndio mwamzo unajumuika nasi kutoka sehemu yoyote duniani haya ndio matukio ya hivi punde kwa mukhtasari.
- Vikosi vya Urusi vinaendela kushambulia miji tofauti nchini Ukraine huku majumba yakiendela kulipuliwa kwa makombora katika mji mkuu wa Kyiv asubuhi hii.
- Watu wawili wamejeruhiwa baada ya jumba la makazi la ghorofa 12 kulipuliwa katika wilaya ya Shevchenko.
- Amri ya kutotoka nje inatekelezwa mjini Kyiv huku Meya wa jiji hilo akionya kuwa "wako katika kipindi hatari"
- Lakini mazungumzo ya amani yanaonekana kupiga hatua kati ya pande mbili zinazohasimiana huku Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akisema wanaanza "kueleweka zaidi"
- Mpatanishi Mykhailo Podolyak anasema kuna "migongano ya kimsingi" wakati wa mazungumzo lakini "kuna nafasi ya maelewano"
- Kwengineko, Naibu wa Meya wa jiji lililozingirwa la Mariupol anasema kuwa wanajeshi wa Urusi wanawazuilia watu 400, wakiwemo madaktari na wagonjwa, "lkama mateka"
- Vikosi vya Urusi vinaendelea kujitahidi kusonga mbele huku vikipambana na ardhi ya Ukraine pamoja na vikosi vyake, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema.
Unaweza kusoma pia:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Korea Kaskazini yarusha kombora lakini likafeli baada ya kuzinduliwa
Korea Kaskazini imerusha kombora lisilojulikana ambalo lilionekana kushindwa mara baada ya kurushwa, jeshi la Korea Kusini lilisema.
Kombora linaloshukiwa lilirushwa kutoka uwanja wa ndege nje ya mji mkuu Pyongyang.
Uwanja huo wa ndege umekuwa mahali pa kurushwa mara kadhaa, ikiwa ni pamoja na majaribio ya hapo awali ya kile ambacho Marekani inadai kuwa makombora ya balestiki ya mabara (ICBMs).
Inakuja wakati ambapo Korea Kaskazini imeongeza majaribio yake ya silaha katika wiki za hivi karibuni.
"Korea Kaskazini ilirusha kombora lisilojulikana kutoka eneo la Sunan mwendo wa 09:30 leo, lakini inakisiwa kuwa lilifeli mara tu baada ya kuzinduliwa," Wakuu wa Pamoja wa Wafanyakazi wa Seoul walisema katika taarifa.
Tovuti maalum ya habari ya NK News iliwataja mashahidi wakisema walisikia, sauti kubwa "zinazovuma" - sawa na ile ya ndege kubwa zilisikika Pyongyang, ikifuatiwa na "ajali" kubwa. Iliongeza kuwa ilikuwa imeona picha inayoonyesha mpira wenye rangi nyekundu ya moshi juu ya anga ya mji mkuu.
Wanajeshi wa Kenya wauawa katika shambulizi linaloshukiwa kuwa la al-shabab
Zaidi ya wanajeshi 10 wa Kenya wameuawa katika shambulio la kilipuzi kilchotegwa kando y abarabara kusini mwa Somalia.
Wengine watano walijeruhiwa vibaya baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi cha kujitengenezea katika eneo la Gedo, karibu na mpaka wa Kenya-Somalia.
Jeshi la Ulinzi wa Kenya (KDF) halijatoa tamko rasmi kuhusu vifo hivyo - kwa hasira ya Prof J Ole Kiyiapi, alisema kwenye Twitter kwamba kakake, Johnson Olemoi Kiyiapi, alikuwa mmoja wa waliouawa.
Prof Kiyiapi, aliyekuwa mgombea urais, aliambia BBC kuwa alisikitishwa na mamlaka "kwa kutotambua na kuheshimu vifo vya mashujaa". Alisema familia iligundua kuhusu kifo cha mdogo wake Jumanne baada ya maafisa wa kijeshi kuwatembelea nyumbani kwao katika eneo la Bonde la Ufa, lakini hakukuwa na taarifa rasmi.
“Hiki ndicho kinachonitia hasira na huzuni. Vijana hawa walikuwa tayari na wamelipa gharama kubwa kulinda nchi yao, lakini ni kana kwamba KDF wanataka kuweka jambo hili kuwa siri,” aliambia BBC.
Shambulio hilo limehusishwa na kundi la al-Qaeda lenye uhusiano na al-Shabab ambalo limefany amashambulizi kama hayo dhidi ya raia na msafara wa vikosi vya usalama.
Wanajeshi waliouawa ni sehemu ya kikosi cha walinda usalama wa Muungano wa Afrika kilichopelekwa Somalia kusaidia serikali ya nchi hiyo kukabiliana na wanamgambo wa al-Shabab.
Miezi ya hivi karibuni imeshuhudia ongezeko la mashambulio yanayolenga maeneo ya umma, mitambo ya serikali na vituo vya ukaguzi vya usalama.
Habari za hivi punde, Mzozo wa Ukraine: Mashambulizi ya Urusi yapiga majumba Kyiv
Milipuko ilisikika katika mji mkuu wa Kyiv mapema leo asubuhi, kulingana na ripoti za mitandao ya kijamii.
Huduma za dharura za jiji hilo sasa zinasema kuwa jengo la makazi la ghorofa 12 katika wilaya ya Shevchenko lilipigwa na makombora ya Urusi mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi. Jengo jirani la ghorofa tisa pia liliharibiwa, mamlaka zilisema.
Wameongeza kuwa watu wawili walijeruhiwa na 35 walihamishwa kutoka kwa jengo hilo. Moto huo ulizimwa saa 7.45 asubuhi na waokoaji sasa wanatafuta manusura.
Video zilizosambazwa mapema kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha moshi ukifuka angani kutoka kwa majengo.
Wakaazi jijini humo wamesalia majumba yao , wengine wakijificha huku kukiwa na amri ya kutotoka nje ya siku mbili.
Maafisa wameonya kuwa ni wakati "mgumu na hatari" kwa mji huo mkuu.
Unaweza kusoma pia:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani: 'Ukraine itamshinda Putin'
Katika mahojiano na CNN siku ya Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alitabiri Ukraine huru itakuwepo kwa muda mrefu zaidi ya rais wa Urusi.
"Kwanza kabisa, kutakuwa na Ukraine, Ukraine huru kwa muda mrefu zaidi kulikovile kutakuwa na Vladimir Putin," alimwambia mtangazaji Wolf Blitzer.
"Kwa njia moja au nyingine, Ukraine itakuwepo na wakati fulani Putin hatakuwepo."
Unaweza kusoma pia:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Habari za hivi punde, Ving’ora vya kurushwa kwa makombora vyalia katika miji kadhaa ya Ukraine
Ving’ora vyalia katika miji kadhaa ya Ukraine
Ving'ora vya alfajiri vimelia tena katika miji kadhaa nchini Ukraine. Vimelia ili kuwaonya watu kujikinga dhidi ya mashambulio ya makombora yaliorushwa.
Baadhi ya waandishi wa habari wameelekea miji ya Kyiv, Lviv, Ivano, Odesa , Dnipro ili kuripoti yanayoendelea.