Urusi yashambulia miji muhimu ya Ukraine huku uvamizi ukizidi

Wanajeshi wa Urusi wameuvamia mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.

Moja kwa moja

  1. Meli iliyobeba magari ya kifahari 4,000 yazama huko Ureno

    Porsche

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Meli ya mizigo iliyokuwa imebeba maelfu ya magari ya kifahari imezama katika visiwa vya Ureno vya Azores, karibu wiki mbili baada ya kushika moto.

    Meli hiyo inayoitwa Felicity Ace, ilikuwa ikisafirisha magari ya kifahari 4,000 yakiwemo aina ya Porsches na Bentleys. Meli hiyo ilikuwa njiani kuelekea Rhode Island nchini Marekani kutoka bandari ya Ujerumani ya Emden wakati moto ulipozuka.

    Wahudumu wote wa meli hiyo waliokolewa wakati moto huo ulipoanza Februari 16. Joao Mendes Cabecas, nahodhawa moja ya bandari iliyo karibu katika kisiwa cha Faial, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba hakuna uvujaji wa mafuta ulioripotiwa hadi sasa lakini alisema kuna hofu kwamba matenki ya mafuta yanaweza kuharibika wakati chombo hicho kikiwa chini ya bahari ya Atlantic katika kina cha mita 3,500 (maili 2.17).

    Ship

    Chanzo cha picha, Reuters

    Jeshi la wanamaji la Ureno limesema hakuna aliyejeruhiwa na moto huo na kwamba wafanyakazi wote 22 wa meli hiyo walipelekwa katika hoteli moja baada ya jeshi la wanamaji, meli nne za wafanyabiashara waliokuwa wakisafiri katika eneo hilo na Jeshi la Anga la Ureno kukamilisha zoezi hilo la kuwokoa.

    Volkswagen imesema uharibifu wa magari hayo yenye bima unaweza kugharimu karibu $155m kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

    Bentley alithibitisha kuwa magari yake 189 yalikuwa ndani ya meli hiyo na kampuni ya Porsche ilisema ilikuwa na magari 1,100 katika meli hiyo.

    Mteja mmoja alituma ujumbe wa twitter akisema kuwa Porsche yake ilikuwa kwenye meli iliyotelekezwa. Mwingine alituma ujumbe wa twitter kwamba alikuwa amerudishwa nyuma.

  2. Biden: ‘Madikteta wasipogharamikia walichopanda husababisha ghasia zaidi’

    Biden

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Marekani Joe Biden amesema kwamba Marekani na Nato zimeonesha kwamba mataifa ya magharibi yanaunga mkono Ukraine.

    Amesema kwamba historia imeonesha kwamba , madikteta ‘wasipogharamikia uchokozi wao husababisha ghasia zaidi’.

    Akiushtumu uvamizi wa Urusi, Biden amepongeza mataifa’ yanayopenda uhuru wa’o kwa kusimama na Marekani. ‘’Putin alifanya makosa , tulikuwa tumejiandaa’’, alisema.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
    • Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
  3. Natumai hujambo. zifuatazo ni habari za moja kwa moja kuhusu matukio tofauti duniani