Moto wa Bunge la Afrika Kusini: Mshukiwa 'alikuwa na vilipuzi'

Polisi walisema Bw Mafe alikamatwa ndani ya majengo ya bunge baada ya kuanza kwa moto, lakini wakili wake alisema mtu asiye na hatia alikuwa amezuiliwa.

Moja kwa moja

  1. Na hadi hapo tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa leo.Hadi hapo kesho panapo majaaliwa

  2. Jiji la pili China lawekwa chini ya ‘Lockdown’

    TH

    Chanzo cha picha, EPA

    Uchina imeweka jiji la pili kwenye kizuizi kamili cha kutotoka nje baada ya kesi tatu tu za Covid zisizo na dalili kugunduliwa.

    Yuzhou - ambayo ina wakazi milioni 1.1 – ilishuhudia mfumo wake wa usafiri ukifungwa na maduka yote muhimu ya chakula yalifungwa usiku mmoja.

    Inafuata hatua kama hiyo huko Xi'an, ambapo watu milioni 13 wamefungiwa majumbani mwao tangu 23 Desemba.

    Hatua kali zinakuja kabla ya Mwaka Mpya wa Mwezi na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi inayotarajiwa kufanyika Beijing.

    Ikiwa imesalia mwezi mmoja kabla ya Michezo kuanza, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Wang Wenbin aliwahakikishia waandishi wa habari China "imeunda mfumo wa ulinzi wa ufanisi na wa hali ya juu".

    Kama sehemu ya mfumo huu, maelfu ya wafanyakazi na watu waliojitolea walianza kuingia kwenye ‘kiputo’ (Eneo maalum la kujitenga) siku ya Jumanne, ambayo itawafanya kuwa hawana mawasiliano ya kimwili na ulimwengu wa nje ili kuzuia kuenea.

    Washiriki na vyombo vya habari vya kimataifa vikiwasili kwenye Michezo hiyo pia watawekwa katika eneo maalum na watabaki kwa muda wote wa kukaa kwao.

  3. Romelu Lukaku aomba msamaha na kurejea kwenye kikosi cha Chelsea, Thomas Tuchel athibitisha

    th

    Chanzo cha picha, BBC Sport

    Romelu Lukaku ameomba msamaha na atarejea katika kikosi cha Chelsea kwa ajili ya mechi ya Jumatano ya nusu fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Tottenham, meneja Thomas Tuchel anasema.

    Lukaku alitolewa kwa sare ya Jumapili ya Ligi ya Premia dhidi ya Liverpool baada ya maoni yake aliyoyatoa katika mahojiano yaliyorekodiwa wiki tatu zilizopita.Wawili hao walikuwa na mkutano "tulivu" siku ya Jumatatu kuhusu mshambuliaji huyo kurejea."

    Aliomba msamaha na amerejea kikosini kwa mazoezi ya leo," Tuchel alisema."Tumempa muda wa kuangalia nyuma. Kwangu mimi, jambo muhimu zaidi lilikuwa kuelewa - na kuelewa wazi - haikuwa kwa makusudi. Hakufanya hivi kwa makusudi ili kuunda aina hii ya kelele kabla ya mchezo mkubwa. "

    Katika mahojiano yaliyorekodiwa mwezi Disemba, mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa rekodi ya klabu ya Chelsea kwa pauni milioni 97.5 alisema "hajafurahishwa" na jukumu lake la kuwa chini ya Tuchel na kwamba angependa kurejea Inter Milan siku za usoni.

    Kabla ya mechi ya Jumapili dhidi ya Liverpool, Tuchel alisema amemuacha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 nje ya kikosi ili "kulinda maandalizi".

  4. Watoto wa Donald Trump wakataa kutoa ushahidi katika uchunguzi wa ulaghai

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Watoto wawili wa Donald Trump wamekataa kutoa ushahidi wa uchunguzi wa ulaghai katika biashara ya familia hiyo.

    Donald Jr, 44, na Ivanka, 40, waliamriwa kutoa ushahidi na Mwanasheria Mkuu wa New York Letitia James.Alifungua uchunguzi wa kiraia mnamo 2019 kwa madai kwamba - kabla ya kuchukua ofisi - Bw Trump alikuwa ameongeza thamani ya mali yake kwa benki wakati akitafuta mikopo.

    Mawakili wa Bw Trump wanajaribu kumzuia Bi James kumhoji rais huyo wa zamani wa Marekani na watoto wake.Wamemwomba jaji kufuta ombi "isiyokuwa ya kawaida na isiyo ya kikatiba" ya kutoa ushahidi wao.

    Bw Trump alimshtaki Bi James mwezi uliopita, akimshutumu mwanasheria mkuu - mteule wa Democrat - kwa kutekeleza uwindaji uliochochewa kisiasa dhidi yake, ambaye ni Mrepublican.Alikuwa amemtaka atoe ushahidi wake binafsi katika ofisi yake kabla ya Ijumaa.

    Ombi la Mahakama lililowasilishwa Jumatatu ni mara ya kwanza kwa wachunguzi kusema wanataka kuwahoji Donald Jnr na Ivanka chini ya kiapo.

    Msemaji wa Bi James alisema: "Tuna imani kuwa maswali yetu yatajibiwa na ukweli utafichuka kwa sababu hakuna aliye juu ya sheria."

    Mwana mwingine, Eric, 37, ambaye ni makamu wa rais mtendaji katika Shirika la Trump, alihojiwa mnamo Oktoba 2020.Kesi ya madai ya Bi James ni tofauti na uchunguzi wa jinai unaoendelea huko Manhattan kuhusu shughuli za kibiashara za shirika hilo.

    Donald Jr na Eric walichukua udhibiti wa kampuni hiyo pamoja na Allen Weisselberg, afisa mkuu wa fedha, baba yao alipoingia madarakani Januari 2017.

    Ivanka pia alifanya kazi katika Shirika la Trump, kabla ya kuwa mshauri mkuu wa White House.Bw Weisselberg alikana hatia mnamo Julai kwa mashtaka ya ulaghai wa ushuru.

  5. Moto wa Bunge la Afrika Kusini: Mshukiwa 'alikuwa na vilipuzi'

    th

    Chanzo cha picha, REUTERS

    Mwanamume aliyezuiliwa kwa kuchoma moto bunge la Afrika Kusini mjini Cape Town alipatikana kwenye eneo hilo akiwa na vilipuzi, waendesha mashtaka wamedai.

    Zandile Christmas Mafe, 49, alifikishwa katika mahakama ya jiji kwa mashtaka chini ya Sheria ya Vilipuzi, pamoja na uchomaji moto, wizi na uvunjaji wa nyumba.

    Wakili wake alisema hana hatia katika mashtaka yote.Moto huo ulizuka kwa mara ya kwanza Jumapili, na kuharibu kabisa Bunge la Kitaifa, au chumba cha chini cha bunge.

    Hakuna aliyejeruhiwa na moto huo, lakini umeacha taifa na mshangao.

    Bw Mafe ndiye mtu pekee aliyekamatwa kuhusiana na moto huo.Alionekana mnyonge na ameduwaa mahakamani, anaripoti mwandishi wa BBC Nomsa Maseko kutoka Cape Town.

    Alipofika kizimbani akiwa amevalia kaptula na shati , alitoa maski yake na kuzunguka huku kamera zikimuangazia .

    Polisi walisema Bw Mafe alikamatwa ndani ya majengo ya bunge baada ya kuanza kwa moto, lakini wakili wake alisema mtu asiye na hatia alikuwa amezuiliwa.

    Kesi hiyo iliahirishwa kwa siku saba ili polisi kuendelea na uchunguzi wao.

    Wazima moto wanasema wamefanikiwa kuudhibiti moto huo uliozuka siku ya Jumatatu.Upepo mkali ulisababisha mbao zinazofuka moshi kwenye paa kuwaka moto tena.

    Video ya moto huo wa Jumatatu imechapishwa kwenye akaunti ya Twitter ya bunge:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  6. Hasira za Wakenya kuhusu uhaba wa 'chips' za KFC

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Tawi la Kenya la mkahawa wa vyakula la Marekani, KFC, limeishiwa na vibanzi /chips limesema kupitia Twitter.

    Sababu ya uhaba huo ni kucheleweshwa kwa meli kunakosababishwa na janga na corona , kulingana na Business Daily Africa.

    "Meli zimechelewa kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa, lakini tunafanya bidii kurejesha kwani makontena ya kwanza yanawasili bandarini kesho," Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo kwa Afrika Mashariki, Jacques Theunissen, alisema katika mahojiano Business Today siku ya jumtatu Kampuni hiyo huwa haitoi viazi nchini Kenya , Bw Theunissen aliwaambia.

    "Sababu ambayo hatuwezi kununua bidhaa za ndani kwa sasa ni kwamba wasambazaji wote wanahitaji kupitia mchakato wa kimataifa wa kuidhinisha ubora ,QA na hatuwezi kukwepa hilo hata kama tutaishiwa ili kuhakikisha kuwa chakula chetu ni salama kwa matumizi ya wateja wetu," Bw Theunissen alieleza.

    Kwenye Twitter, baadhi ya wateja wa KFC walionyesha hasira kwamba mkahawa huo unaagiza viazi kutoka nje.

    "Hili halikubaliki na ni dhihaka kwa wakulima wetu wanaofanya kazi kwa bidii katika Taifa letu," mtu mmoja aliandika.Ikiwa "hawawezi kununua viazi kutoka kwa Wasambazaji wa Kenya, basi sote tuna haki ya kimaadili ya #KususiaKFC" mwingine aliandika.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  7. Mwanamme akamatwa kwa programu iliyotaka ‘kuwauza’ wanawake waislamu

    th

    Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

    Polisi wa India wamemkamata mwanamume wa miaka 21 kuhusiana na programu ambayo ilisambaza picha za wanawake zaidi ya 100 wa Kiislamu ikisema kuwa "wanauzwa".

    Yeye ni mwanafunzi wa uhandisi kutoka mji wa kusini wa Bangalore ambaye utambulisho wake haujafichuliwa.Mashtaka dhidi yake hayako wazi lakini yeye ni "mfuatiliaji wa karibu" wa programu hiyo, Bulli Bai, polisi waliambia BBC Marathi.

    Programu ilipangishwa kwenye jukwaa la wavuti la GitHub, ambalo tangu wakati huo limeiondoa katikati ya hasira na ghadhabu iliyoenea.

    Picha za wanahabari na wanaharakati kadhaa mashuhuri wa Kiislamu zilitumiwa kwenye programu bila idhini yao na kuwekwa "kuuzwa" katika mnada ghushi.Hili ni jaribio la pili la kuwanyanyasa wanawake wa Kiislamu kwa "kuwapiga mnada" mtandaoni.

    Mnamo Julai mwaka jana, programu na tovuti inayoitwa "Sulli Deals" iliunda wasifu wa zaidi ya wanawake 80 wa Kiislamu - kwa kutumia picha walizopakia mtandaoni - na kuzielezea kama "dili za siku".

    Katika matukio yote mawili, hakukuwa na mauzo ya kweli, lakini dhumuni lilikuwa kuwadhalilisha wanawake wa Kiislamu - ambao wengi wao wamekuwa wakizungumza juu ya kuongezeka kwa wimbi la utaifa wa Kihindu chini ya Waziri Mkuu Narendra Modi.

    Sulli ni neno la kudhalilisha la lugha ya Kihindi la mrengo wa kulia la Hindu dhidi ya wanawake wa Kiislamu, na bulli pia ni dharau.

  8. 'Waziri wa zamani wa Tunisia ashukiwa kwa ugaidi'

    tunisia

    Chanzo cha picha, AFP

    Wizara ya mambo ya ndani ya Tunisia imesema waziri wa zamani wa sheria amewekwa kizuizini kwa kushukiwa kwa "ugaidi

    Noureddine Biri wa chama cha Ennahdha alizuiliwa mwishoni mwa juma.

    Amekataa chakula na dawa na alihamishiwa hospitalini siku ya Jumatatu ambapo anaripotiwa kuendelea na mgomo wa kula.

    Waziri wa Mambo ya Ndani Taoufik Charfeddine alisema Jumatatu kwamba kulikuwa na ripoti za vitendo vya kigaidi na kusababisha mamlaka kuchukua hatua.

    Chama cha Ennahdha kimekuwa katika njia panda na Rais Kais Saied baada ya kumfukuza waziri mkuu na kusitisha vikao vya bunge mwaka jana.

    Mwanachama wa chama na wanaharakati amesema afya ya Bw Bhiri iko hatarini kwa kuwa ana ugonjwa wa kudumu na amenyimwa huduma za kitaalamu.

    Mke wake amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa alipatwa na mshtuko wa moyo na kwamba hakupata fursa ya kumuona.

  9. Rais wa Msumbiji na mke wake wamekutwa na corona

    President Filipe Nyusi and his wife are in isolation

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Rais Filipe Nyusi na mkewe wamejitengwa

    Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na mke wake Isaura Nyusi wamekutwa na virusi vya corona na wamejitenga kwa sasa.

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya rais Bw. Nyusi na mke wake wameamua kujitenga kwa kuzingatia muongozo wa afya baada ya kupatikana na virusi , ijapokuwa hawakuonesha dalili zozote.

    Taarifa hiyo ilisema waliamua kufanya vipimo baada ya "shughuli walizokuwa nazo siku chache zilizopita ".

    Kumekuwa na ongezeko la virusi vya corona katika siku za hivi karibuni nchini Msumbiji.

    Nchi hiyo imethibitisha kuwa na watu 193,000 wanaougua Covid-19, huku vifo 2,031 vikirekodiwa.

  10. China: Wakazi wa Xi'an waliofungiwa wabadilishana bidhaa kupata chakula

    Kabichi na sigara

    Chanzo cha picha, WEIBO

    Baadhi ya wakazi waliowekwa karantini katika mji wa China wa Xi wameamua kubadilishana vifaa katika siku za hivi karibuni, huku wasiwasi wa uhaba wa chakula ukiendelea.

    Machapisho kwenye mitandao ya kijamii yanaonesha wakazi wakibadilishana bidhaa tofauti ikiwemo vifaa vya teknolojia ili kupata chakula.

    Karibu watu milioni 13 wamefungiwa majumbani mwao tangu Disemba 23, na hawaruhusiwi kwenda kununua hata chakula.

    Katika siku za hivi karibuni wengi wao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kutoa malalamiko yao.

    Mamlaka zimekuwa zikitoa vyakula vya bure kwa wakazi hao , lakini baadhi yao wanasema wameishiwa na chakula na bado hawajapokea msaada wowote.

    Kanda za video na picha zilizoshirikishwa katika mtandao wa kijamii wa Weibo zinaonesha watu wakibadilishana sigara ili kupata mboga ya kabichi, sabuni ya kuosha vyombo kupata tufaha na taulo za hedhi kupata walau mboga kidogo za majani.

    watu

    Chanzo cha picha, Weibo

    Xi'an ni kitovu cha mlipuko wa sasa wa Covid-19 wa Uchina, na viongozi wamepitisha hatua kali. Lakini usimamizi wa mamlaka za mitaa wa wa kuhakikisha amri ya kutotoka nje inazingatiwa unakabiliwa na ukosoaji mkubwa mtandaoni.

  11. Mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani afikisha miaka 119

    M

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kane Tanaka, mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani, alifikisha umri wa miaka 119 Jumapili, kwa mujibu wa ujumbe wa Twitter uliochapishwa na mjukuu wake wa kike, Junko Tanaka.

    "Ni mafanikio makubwa. (Kane Tanaka) kufikisha umri wa miaka 119," Junko aliandika kwenye tweeter, akiwa na picha ya bibi yake, ambaye alimwona mwezi Disemba. "Natumani utaendelea kuishi maisha kwa furaha na kwa ukamilifu."

    Junko alishirikisha picha kwenye Twitter ya chupa mbili za ukumbusho za Coca-Cola ambazo Tanaka alipewa katika siku yake ya kuzaliwa, zenye lebo zilizoonesha umri wake.

    "Zawadi ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa 1: Natambulisha zawadi ambazo Kane amepokea.tumefurahia sana zawadi hii. Kampuni ya Coca-Cola ilitengeneza chupa ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa ajili yake. Inaonekana (Kane) bado anakunywa Coca-Cola kama kawaida," Junko aliandika kwenye tweeter.

      Kane alizaliwa mwaka 1903, na kuolewa na muuza duka la mchele akiwa na miaka 19,na alifanya kazi katika duka hilo la familia mpaka alipofikia umri wa miaka 103.

    • Apple imekuwa kampuni ya kwanza kufikia thamani ya soko ya dola trilioni tatu

      Nembo ya Apple

      Chanzo cha picha, Getty Images

      Kampuni kubwa ya kiteknolojia ya Marekani Apple imekuwa kampuni ya kwanza kupata hesabu ya soko la hisa ya $3tn (£2.2tn).

      Bei ya hisa za kampuni hiyi ilipanda kwa karibu asilimia The firm's share price has 5,800 tangu mwanzilishi mwenza na mtendaji mkuu wa zamani Steve Jobs kuzindua iPhone ya kwanza mnamo 2007.

      Hata hivyo, thamani yake ilishuka kidogo kutoka kwa hatua hiyo muhimu, hadi kumaliza kikao cha biashara cha Jumatatu huko New York kwa $2.99tn.

      Apple imekuwa mmoja wa washindi wakubwa wa janga hili, kwani athari za amri ya kutotoka nje iliyosabbaishwa na virusi vya corona ilifanya matumizi ya vifaa vya rununu kuongezeka.

      Ilichukua zaidi ya miezi 16 kwa thamani ya hisa za Apple kupanda kutoka dola trilioni mbi hadi dola trilioni tatu, baada ya uhitaji wa bidhaa za kampuni hiyo kubwa ya teknoojia duniani kuongezeka wakati amri ya kutotoka nje ilipowekwa ili kudhibiti maabukizi ya corona.

    • Waziri Mkuu wa Haiti anusurika jaribio la mauaji

      Ariel Henry during an event on 20 July 2021 in Port-au-Prince

      Chanzo cha picha, Getty Images

      Watu wenye silaha walijaribu kumuua Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry wakati wa sherehe ya kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa nchi hiyo siku ya Jumamosi, maafisa wanasema.

      Tukio hilo lilitokea wakati bwana Henry alipokuwa akishiriki katika hafla hiyo katika kanisa moja katika mji wa kaskazini wa Gonaïves.

      Video iliyowekwa mtandaoni ilionesha waziri mkuu na msafara wake wakitembea kwa kunyata kuelekea kwenye magari yao huku kukiwa na milio ya risasi.

      Hali ya usalama imezorota sana tangu kuuawa kwa Rais Jovenel Moïse Julai mwaka uliyopita.

      Bw Henry ameahidi kukabiliana na magenge yenye nguvu ambayo yanalaumiwa kwa wimbi la utekaji nyara na kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa ya usambazaji wa gesi nchini humo, na kusababisha uhaba mkubwa wa mafuta.

      Ofisi ya waziri mkuu ilisema "majambazi na magaidi" ndio waliohusika na jaribio hilo la mauaji, na kwamba vibali vya kukamatwa vimetolewa kwa washukiwa hao.

      Ofisi hiyo ilishutumu kundi hilo kwa kujificha nyuma ya kuta kushambulia msafara huo na kutishia askofu kwa kuzingira kanisa, kwa mujibu wa Associated Press.

      Mtu mmoja aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika mapigano ya risasi kati ya watu wenye silaha na vikosi vya usalama, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

      Shambulio hilo ni pigo jingine kwa utawala dhaifu unaoongozwa na Bw Henry, ambaye alikua kaimu mkuu wa serikali ya Haiti wiki mbili baada ya Moïse kuuawa. Mazingira ya jaribio la mauaji hayo yanayoaminika kutekelezwa na kundi lawanamgambolakini bado hawajafahamika.

      Tarehe ya kupiga kurakumchagua rais mpya bado haijatangazwa.

      Kuongezeka kwa ghasia na hali mbaya ya kiuchumi, iliyofanywa kuwa mbaya zaidi na majanga kadhaa ya asili katika miaka ya hivi karibuni, imesababisha idadi kubwa ya Wahaiti kutafuta fursa katika nchi nyingine.

    • Hujambo na karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumanne 04.01.2022