Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Vifaru 24 wameuawa nchini Afrika Kusini katika muda wa wiki mbili

Wizara hiyo imelaani kuendelea kwa ujangili na mauaji ya vifaru kwa ajili ya pembe zao, ikisema washukiwa tisa wa uhalifu huo wamekamatwa katika siku 14 za kwanza za mwezi wa Disemba.

Moja kwa moja

  1. Manchester United yaingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka Rudiger

    Kuna tetesi nyingi zinazoendelea kuenea kuhusu hofu ya mipango ya Manchester United ya mwezi Januari.

    Magazeti ya Ujermani ya Bild yanaripoti kuwa uhusiano baina ya meneja wa Manchester United Ralf Rangnick na wawakilishi wa Antonio Rudiger yanaweza kuwaweka mashetani wekundu katika mabishano kwa ajili ya kusaini mkataba na mlinzi huyo mwenye umri wa miaka.

    Paris St Germain, Real Madrid ba Bayern Munich pia wako katika mbio za kumsaka Rudiger, ambaye mkataba wake katika Chelsea unamalizika msimu huu , huku akidai malipo ya pauni £200,000-kwa wiki kusaini mkataba, kulingana taarifa.

  2. Hofu kubwa yatanda Tripoli kabla ya uchaguzi mkuu wa Libya

    Hali ya wasi wasi inaendelea kuongezeka katika mji mkuu wa Libya Tripoli, baada ya watu wenye silaha kuandamana katika mitaa kadhaa ya wilaya za mji huyo kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

    Watu wenye silaha wameyazingira makazi ya waziri mkuu kwa saa kadhaa baada ya kuondolewa na kwa kamanda wa jeshi.

    Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu walichokuwa wakikifanya watu hao, lakini video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii iliibua hofu zaidi katika mji mkuu huo wa Libya.

    Hakuna uhakikza kwamba uchaguzi utafanyika trehe 24 Disemba.

    Uchaguzi huu ni moja ya malengo ya Umoja wa mataifa ya kuhakikisha Libya inakuwa taifa lenye demokrasia na utulivu.

  3. Mlipuko wa homa ya mafua waikumba Kenya

    Maafisa wa Kenya wamethibitisha mlipuko wa homa ya virusi vya mafua aina ya Influenza nchini humo.

    Taasisi ya utafiti wa tiba nchini Kenya (Kemri) ilisema kuwa sampuli kati ya 36 zilipatikana na homa ya influenza A.

    Hospitali ya kitifa ya Kenya -Kenyatta National Hospital (KNH) inatoa chanjo ya mafua ya mlipuko wa mafua (aina ya Influenza A)

    KNH imesema kwa sasa inatoa chanjo hiyo kwa wahudumu afya tu, katika juhudi zinazoungwa mkono na chuo kikuu cha kitaifa cha Washington, ambacho kinafanya utafiti wa magonjwa nchini Kenya.

    “Anayefika wa kwanza ndiye anayepokea chanjo hiyona watu 400 wanaweza kuchanjwa kila siku,” KNH ilisema katika matangazo Alhamisi.

    Hii inakuja wakati Taasisi ya tiba ya Kenya iliyopo mjini Kisumu ilisema ufuatiliaji baina ya Septemba na Novemba mwaka huu kuonyesha kuwa kulikuwa na mlipuko wa Infuenza A.

    Kuliwa na aina nne za virusi za infuluenza : A, B, C na D.

  4. Mohamed Salah: Mshambuliaji wa Liverpool anakaribia kuweka rekodi nyingine ya Primia Ligi

    "Ni wa ajabu.Kusema kweli, hivi sasa, ni mchezaji bora duniani ."

    Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anaweza kuwa mwenye upendeleo, lakini amekuwa na katika fursa bora ya kushuhudia kuimarika na ukomavu wa soka wa mshambuliaji Mohamed Salah – na mchezaji wa kimataifa wa Misri ambaye anaweza kushikilia rekodi nyingine hivi karibuni.

    Salah mwenye umri wa miaka 29 alifunga au kusaidia kufungwa kwa magoli katika mechi ya Jumatatu iliyochezwa nyumbani dhidi ya New Castle iliyowekwa katika nafasi ya 19.

    Mbali na hayo Mo hakuwahi kushindwa kushinda dhidi ya Anfield – halafu Salaha alisawazisha rekodi ya Jamie Vardy ya kufunga mabao au kusababisha bao katika mechi 15 mfulirizo za Primia Ligi.

    Lakini suala la kuweka rekodi sio kitu kipya kwa Salah.

    Lakini je, ni rekodi gani anayoweza kuipata Salah katika kipindi kilichosalia cha msimu huu ?

    Rekodi kuu inaweza kuwa ni ya mfungaji bora zaidi wa magoli wa Liverpool katika Pirimia ligi.

    Robbie Fowler (aliyefunga mabao 128 ya ligi katika mechi 266 kwa ajili ya Reds) ndiye anayeshikilia rekodi hii kwa sasa, akifuatiwa na Steven Gerrard (mabao 120 , mechi 504 ), Michael Owen (magoli 118 , mechi 216 ) na Salah (magoli 109 )

  5. Mchungaji aliyembaka msichana mwanakwaya:Tulikuwa katika mahaba

    Mchungaji wa kanisa la Christ Apostolic Bible katika jimbo laOgun lililopo kusini magharibi mwa Nigeria anaendelea kushikiliwa mahabusu tangu Ijumaa, baada ya kudaiwa kumbaka msichana wa miaka 16 .

    Polisi katika jimbo la Ogun wanaochunguza tukio hilo wanasema mchungaji huyo alipanga na mke wake kumbaka msichana huyo ambaye ni mwanakwaya katika kanisa lao.

    Lakini Mchungaji Peter Taiwo na mke wake wamekuwa wakikwepa kueleza ukweli halisi wa kilichotokea.

    Mchungaji huyo anasema yeye na msichana huyo 'wamekuwa katika mapenzi na wote walipendana kimapenzi.'

    "Nilimwambia aachane na mpenzi wake wa kiume na aniombe chochote anachohitaji"

    Mchungaji huyo alisema wakati msichana alipoumia mguu, niliwasaidia wazazi wake kupata usaidizi wa matibabu yake.

    "Kuanzia siku nilipouangalia mguu wake, msichana alianza kunitumia jumbe za mapenzi na nilikuwa nazijibu. Bado nina jumbe katika simu yangu ," alisema Mchungaji.

    ‘’Tuliongea nikamwambia hakuna kushiriki ngono pamoja lakini tumekuwa tukipendana’’, alisema Mchungaji na kuongeza kuwa "Wakati ule tulipoanza hatukuwa na mahusiano ya kingono, lakini tulionyeshana mapenzi," Pasta Taiwo anasema.

    Hatahivyo mchungaji anakiri kuwa waliingia katika mahusiano ya ngono na msichana na kumfahamisha mke wake, ambaye hakuwa na la kusema.

    Akizungumza na BBC mke wa Mchungaji alisema kuwa hakuwa anafahamu kuwa mume wake alikuwa anamtumia vibaya msichana.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mchunguaji na mkewe washutumiwa kumbaka msichana wa miaka 16
  6. Mkenya mwenye uraia wa Uingereza aweka historia katika Chuo kikuu cha Oxford

    Msomi mzaliwa wa Kenya amekuwa profesa wa kwanza mweusi mwenye umri mdogo katika Chuo kikuu cha kifahari cha Uingereza -Oxford University, imesema taasisi hiyo ya elimu.

    Patricia Kingori pia ni mmoja wa wanawake wenye umri mdogo zaidi kuwahi kutunukia Uprofesa kamili katika historia ya miaka 925 ya Chuo kikuu cha Oxford.

    Profesa Kingori, ambaye ni mwanasosholojia aliyebobea katika kuhusu masuala ya wahudumu wa afya, alieleza kufurahishwa na uteuzi wake.

    "Kutambuliwa kwa kazi yangu kwa njia hii ni heshima kubwa, na ninawashukuru sana watu niliojifunza kutoka kwao na walionisaidia hadi sasa," alisema.

    Pia aliwahi kuwa mshauri wa mashirika kadhaa ya kidunia, ikiwa ni pamoja na WHO, Save the Children na Médecins Sans Frontières (MSF).

    Bi Kingori, ambaye alikulia katika kisiwa cha Caribbean cha St Kitts kulingana na chanzo cha habari cha eneo hilo, amekuwa akielezewa kama "mbunifu" na "mwanamke jasiri" na Chuo kikuu cha Somerville.

    Kufikia mwezi Januari 2021 ni maprofesa 155 pekee kati ya zaidi ya 23,000 wa Chuo kikuu nchini Uingereza waliokuwa ni weusi, kulingana na takwimu rasmi.

  7. Mwalimu aliyewafunza kisiri watoto wa IS katika kambi kwa maandishi

    Kila siku saa tatu asubuhi, Ilona Taimela aliwasalimia wanafunzi wake na kuwaelezea masomo yao ya siku

    Ratiba yake ya siku ilidumu kwa takriban mwaka mmoja kuanzia Mei 2020 na alishirikiana na waalimu wengine wengi aliokuwa akifundisha nao bila kuwepo.

    Mbali na wanafunzi wa Bi Taimela wanafunzi walikuwa wakifundishwa katika jela za kambi kaskazini-mashariki mwa Syria- mbali na dawati lake nchini Finland.

    Kupitia ujumbe alioutuma kupitia WhatsApp, aliwafundisha masomo Hisabati, Jiografia katika lugha ya Kiingereza na kifinland.

    Wanafunzi wake walikuwa ni Wafinland 23 wanaoishi katika kambi ya al-Hol , yenye mahema makubwa iliyowekwa kwa ajili ya watu wenye uhusiano na kundi la Isramic State.

    Takriban watu 60,000 wanaishi ndani ya kambi hiyo, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto kutoka nchi makumi kadhaa, wakiwemo wanaotoka Ulaya.

    Baadhi ya watoto hao walikuwa ni wanafunzi wa Bi Taimela.

    " Japokuwasikuwafahamu watoto hao, walikuwa na haki ya ya kupata elimu," aliiambia BBC.

    Unaweza pia kusoma:

    • Kwa nini nchi za Kiarabu haziwachukui wakimbizi wa Syria
    • Haki za wakimbizi zinalindwa na sheria za kimataifa, lakini nini kinatokea kiuhalisia?
    • Wakimbizi wa Syria wanahangaika sana
  8. Nyimbo za ndege zawaondoa wasanii wakubwa kwenye chati za muziki Australia

    Albamu inayojumuisha milio ya na sauti za ndege wa Australia walio hatarini kutoweka imeonyeshwa kwa mara ya kwanza katika chati tano bora za muziki za Aria nchini humo.

    Songs of Disappearance zinazidi nyimbo kama za Abba na The Weeknd - bila kusahau nyimbo zinazopendwa zaidi za Krismasi za Michael Bublé na Mariah Carey.

    Imeundwa na BirdLife Australia, albamu hii ina nyimbo za ndege kati ya spishi 53 zilizo hatarini zaidi za Australia.

    Sauti zingine zilichukua saa nyingi za kusubiri msituni kurekodi sauti moja fupi.

    David Stewart, mwandishi wa kurekodi sauti za wanyamapori, ametumia zaidi ya miaka 30 kukusanya sauti za wanyamapori wa Australia ambazo hazijasikika. Ni rekodi zake za ndege ambazo zimetumika kwenye albamu hiyo

    Ilipotolewa tarehe 3 Desemba, kampeni ya mitandao ya kijamii ilizinduliwa ili kupata albamu hiyo katika chati za mauzo ya muziki za Aria ya Australia - na ilifaulu. Songs of Disappearance zimeweka historia kwa kuwa albamu ya kwanza ya aina hiyo kuingia katika tano bora.

    Mapato kutokana na mauzo yataenda kwa miradi ya uhifadhi ya BirdLife Australia.

  9. Vifaru 24 wameuawa nchini Afrika Kusini katika muda wa wiki mbili

    Vifaru 24 wameuawa nchini Afrika Kusini katika takriban wiki mbili, wizara ya mazingira imethibitisha.

    Inasema mizoga saba ilipatikana katika Hifadhi ya Kitaifa ya Kruger, mingine saba katika jimbo la Mpumalanga, sita KwaZulu-Natal na minne Cape Magharibi.

    Wizara hiyo imelaani kuendelea kwa ujangili na mauaji ya vifaru kwa ajili ya pembe zao, ikisema washukiwa tisa wa uhalifu huo wamekamatwa katika siku 14 za kwanza za mwezi wa Disemba.

    Imewahimiza wananchi kusaidia kwa taarifa zozote zinazoweza kusababisha kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa majangili.

    Afrika Kusini ni makao ya karibu 80% ya idadi ya vifaru barani Afrika, ambayo iko chini ya 30,000.

    Mamia huuawa kila mwaka kwa ajili ya pembe zao - nyingi kati yao zikielekea Asia ambako pembe za faru ni kiungo katika dawa na tiba asilia.

    Idara ya mazingira inasema itatoa taarifa kuhusu jumla ya idadi ya vifaru waliouawa kwa ajili ya pembe zao mwaka wa 2021 mapema mwaka wa 2022.

    Tangazo hilo lilichapishwa kwenye Twitter:

  10. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Alhamisi tarehe 16 Disemba 2021