Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mvulana auawa baada ya kuingia katika shule ya wasichana usiku Kenya

Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 17 kutoka Kenya amefariki kutokana na majeraha aliyopata wakati aliposhambuliwa baada ya kuingia kisiri katika shule ya wasichana, polisi wamesema.

Moja kwa moja

  1. Ndege ya UN yalazimika kubadili mkondo kufuatia mashambulio ya angani ya Ethiopia

    Ndege ya misaada ya Umoja wa Mataifa ililazimika kughairi kutua Ijumaa huko Mekele, mji mkuu wa Jimbo la Tigray kwa sababu ya shambulio la angani la serikali, msemaji wa UN ameiambia BBC.

    Awali serikali ilithibitisha kufanya shambulio la angani la hivi punde , ikisema inalenga waasi wa Tigray ambao wanadhibiti mji huo. Wanasema raia walilengwa.

    Shirika la chakula la umoja wa mataifa,WFP linasema ndege yake ililazimika kurejea Addis Ababa kutokana na shambulio la hivi punde.

    Ni siku ya nne mashambulio ya angani yanafanywa dhidi ya mji wa Mekelle huku mapigano yakipamba moto kati ya vikosi vya serikali kuu na vikosi vya jimbo hilo la kaskazini mwa nchi.

    Serikali inasema ilishambulia eneo la mafunzo linalotumiwa na wapiganaji wa Tigraya lakini msemaji wa waasi anasema mahali paliposhambuliwa ni chuo kikuu mjini humo.

  2. Wanariadha maarufu Kenya wabeba mwili wa Agnes Tirop

    Faith Kipyegon, Joyciline Jepkosgei, Eunice Sum na Mary Keitany ni miongoni mwa watu 300 walioandamana nyuma ya bango lililosema:‘Malizeni ghasia za kijinsia’ .

    Wanariadha maarufu akiwemo Eliud kipchoge , Julius Yego na Conseslus Kipruto pi walihudhuria.

    Bi Tirop alidungwa kisu nyumbani kwake mapema mwezi huu na maafisa wa polisi wanamzuilia mume wake Ibrahim Rotich jela kama mshukiwa mkuu.

    Anazuiliwa kwa siku 20 , ambapo atachunguzwa kubaini iwapo hali yake ya kiakili iko timamu ili kukabiliwa na mashtaka.

    Mauaji ya bi Tirop yamezua hisia kali miongoni mwa wanariadha wa Kenya kuhusu kile wanachopita inapokuja suala la ghasia za kinyumbani

  3. Mvulana auawa baada ya kuingia katika shule ya wasichana usiku

    Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 17 kutoka Kenya amefariki kutokana na majeraha aliyopata wakati aliposhambuliwa baada ya kuingia kisiri katika shule ya wasichana, polisi wamesema.

    Mwanafunzi huyo wa kidato cha nne alikuwa miongoni mwa wanafunzi sita ambao waliripotiwa kuingia kinyemela katika shule ya wasichana kaunti ya Kiambu ambayo ni jirani na mji mkuu wa Nairobi.

    Maafisa wa polisi wanasema kwamba mwanafunzi huyo aliingia katika bweni la shule hiyo mwendo wa saa kumi alfajiri kabla ya kuonekana na baadhi ya wasichana ambao walipiga kamsa.

    Hatua hiyo iliwavutia walinzi wa shule hiyo , wafanyakazi na mwalimu mkuu. Wavulana watano kati yao walitorokana kwa mujibu wa maafisa wa polisi , mvulana aliyesalia alivamiwa na wanafunzi na wafanyakazi wa shule hiyo.

    ‘’Walimpiga na kumfanya kupata majeraha ambayo yalitishia Maisha yake . Mvulana huyo baadaye alifariki’’ , idara ya jinai ilisema katika mtandao wake wa twitter.

  4. Rais Somali na Waziri Mkuu wakubaliana kumaliza mzozo kati yao

    Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo na Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble wameripotiwa kukubali kumaliaza uhasama mkali kati yao ambao ulitishia kuvuruga uchaguzi ambao umecheweshwa kwa muda mrefu.

    Mzozo kati ya viongozi hao pia ilitishia kugawanya vikosi vya usalama.

    Ulisababishwa na jinsi serikali ilivyoshughulikia kupotea kwa jasusi wa kike, Ikran Farah, mwezi Juni katika hatua ambayo ilisababisha viongozi hao kuwateua wakuu ujasusi na waziri wa usalama kila mmoja wao.

    Siku ya Alhamisi, Rais Farmajo na Bw. Roble walikutana kwa mara ya kwanza baada ya wiki kadhaa mjini Mogadishu.

    Kulingana na taarifa iliyotolewa na msemaji wa serikali Ibrahim Moalimu, walikubaliana kuwa Abdullahi Mohamed Nur, ambaye aliteuliwa na Waziri Mkuu kama waziri wa usalama, aaendelee kuhudumu katia wadhifa huo.

    Chini ya makubaliano, Yasin Farey, ambaye aliteuliwa na rais kam kaimu mkuu wa ujasusi, ataendeleana kukumu hilo hadi atakayechukua nafasi hiyo atakapotajwa.

    Viongozi hao wawili wamekubaliana kwamba kesi ya jasusi mwanamke aliyetoweka iachiwe mahakama kuamua.

  5. Mwanahabari wa Zambia arejesha dola milioni 4 zilizofichwa nyumbani kwake

    Mwandishi wa habari wa Zambia ametoa $ 4m (£ 3m) zilizopatikana nyumbani kwake mwezi uliopita kama sehemu ya makubaliano ya msamaha wa rushwa, maafisa wametangaza.

    Margaret Chisela Musonda, anayejulikana pia kwa jina la Faith Musonda, pia amesalimisha nyumba yake iliyoko katika eneo la kifahari katika mji mkuu, Lusaka, ambapo kiasi hicho cha pesa za sarafu ya nchini humo na dola za Kimarekani zilipatikana.

    Maafisa hawajafichua jinsi alivyopata pesa na ymakosa yake, lakini walisema alikuwa amekiri kosa.

    Bi Musonda ni mwandishi wa habari mashuhuri ambaye aliwahi kuhudumu katika shirika la habari la serikali. Hajatoa maoni juu ya jambo hilo.

    Katika taarifa, timu ya pamoja ya upelelezi ilisema kwamba makubaliano hayo yatamfanya Bi Musonda aepuke kesi za jinai.

    Ilisema sheria inaruhusu serikali "kutoa msamaha kwa watuhumiwa katika hali fulani kwa masharti kwamba wanakubali makosa na kurudisha kile walichopata kimakosa kupitia vitendo vya rushwa".

    Timu hiyo ilijumuisha maafisa kutoka Tume ya Kupambana na Rushwa, Huduma ya Polisi ya Zambia, Tume ya kupambana na Dawa za Kulevya na Kituo cha Ujasusi wa Kifedha.

    Wazambia kwenye mitandao ya kijamii wameelezea mseto wa maoni kuhusu makubaliano hayo:

  6. Ndayishimiye aanza ziara Tanzania

    Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu, ambapo pamoja na mambo mengine atazungumza na mweyejii wake, Rais Samia Suluhu.

    Hii si ziara ya kwanza ya Ndayishimiye nchini Tanzania, mwaka jana mwezi Septemba alifaya ziara ya siku moja kwa mwaliko wa Rais wa wakati huo, hayati John Magufuli, ikiwa ni ziara yake ya pili nchini humo tangu aingie madarakani mwezi Juni, 2020.

    Tanzania ni nchi ya kwanza kutembelewa na Rais Ndayishimiye mara baada ya kuingia madarakani akichukua nafasi ya hayati Pierre Nkurunziza.

    Ndayishimiye alipokelewa na waziri wa mambo ya kigeni wa Tanzania, Liberata Mulamula katika uwanja wa ndege wa Dodoma tayari kukutana na mwenyeji wake Rais Samia, ambaye mwezi Julai mwaka huu alifanya ziara nchini Burundi.

    Katika ziara yake ya kwanza mwezi Septemba 2020, Rais Ndayishimiye alisema katika hotuba yake “Tanzania sio nchi rafiki, lakini ni mzazi kwa Burundi”, kwa msaada wake kwenye uhuru wa Burundi.

    Katika ziara ya sasa Rais Ndayishimiye anatarajia kutembelea miradi kadhaa ya maendeleo katika jiji la Dar es Salaam, na atatembelea Zanzibar, kwa mujibu wa taarifa ya wazara ya mambo ya nje ya Tanzania.

  7. Wabunge wahalalisha utoaji mimba Benin

    Wabunge nchini Benin wamepiga kura kuhalalisha utoaji mimba na kuongeza wigo wa jambo hilo ambalo tayari lilikuwa likifanyika.

    Wanawake sasa wanaweza kutoa mimba katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito iwapo kama ujauzito huo utamsababishia shida katika masuala ya elimu, kazi, maadili au mtoto anaweza kuathiri maisha ya mama au kwa ajili ya maslahi ya mtoto.

    Kabla, utoaji mimba ulikuwa unaruhusiwa kisheria endapo mwanamke alibakwa au maisha ya mama yalikuwa hatarini kwasababu ya ujauzito.

    Benin ilikuwa inaruhusu utoaji mimba kama afya ya mtoto ambaye hajazaliwa itaathirika.

    Sheria mpya , ilipitishwa Jumatano usiku baada ya majadiliano makali bungeni , lakini bado katiba inapaswa kupitishwa mahakamani kabla ya utekelezaji kuanza.

    Waziri wa afya Benjamin Hounkpatin ameunga mkono sheria mpya hiyo na kusema itaweza kuleta haueni kwa wanawake wengi ambao wanapata ujauzito wasioutaka na hivyo kutafuta njia hatari zinazohatarisha maisha yao ili kutoa mimba.

    "Nchini Benin, karibu wanawake 200 wanakufa kila mwaka baada ya kupata matatizo wakati wa kutoa ujauzito ," alisema.

  8. Li Yundi: Mpiga piano maarufu wa China azuiliwa kwa ‘kutumia huduma za kahaba’

    Mpiga piano wa maarufu nchini China Li Yundi amezuiliwa kwa kutumia huduma kahaba, vyombo vya habari vya serikali vinasema.

    Nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 na msichana mwenye umri wa miaka 29, wamekiri kwa shughuli hiyo haramu, polisi wa Beijing walisema katika chapisho mtandaoni . Walikamatwa baada ya mamlaka kupokea dokezo kutoka kwa umma.

    Ingawaje polisi hawakuchapisha jina lake kamili katika ilani hiyo, vyombo vya habari vya serikali baadaye vilithibitisha kuwa ni Li.

    Habari hiyo imewashtua mashabiki wake wengi na nchini China anafahamika kama "Piano Prince".

    Akiwa na miaka 18 tu, Li alikua mpiga piano mchanga zaidi - na mtu wa kwanza kutoka china - kushinda tuzo ya kwanza kwenye Mashindano ya kifahari ya Kimataifa ya Chopin Piano mnamo 2000.

    Ameendelea kutumbuiza kote ulimwenguni na ni jina linalotambulika sana katika maeneo yanayozungumza Kichina

  9. Nigeria yasitisha huduma ya reli baada ya shambulio

    Shirika la reli la Nigeria limesitisha kwa muda huduma za reli kutoka Abuja, kuelekea kaskazini magharibi mwa Kaduna baada ya watu wenye silaha kuwavamia abiria wa treni siku ya Jumatano.

    Watu walioshuhudia walisema washambuliaji hao walimlenga dereva wa treni ingawa hakuna majeruhi alireripotiwa mpaka sasa.

    Abiria mmoja aliiambia BBC kuwa walisikia mlio mkubwa kabla ya treni haijasimama kwa saa kadhaa.

    Mbunge wa zamani nchini humo, Senata Shehu Sani, aliandika kwenda tweeter kuwa treni ya pili na hivyo kulazimika kurudi Abuja siku ya Alhamisi baada ya mlipuko ulipotokea katika reli hiyo.

    Kampuni ya reli ya Nigeria ilisema huduma hizo zitarudi baada baada ya Ijumaa baada ya ukarabati..

  10. Wanafunzi walivamia bunge DRC wakitaka walimu wao waongezewe mshahara

    Mamia ya wanafunzi wamelivamia bunge nchini DRC wakitaka walimu wao waongezewe mshahara.

    Wanafunzi hao walikuwa wanapeperusha matawi na kuimba "tunataka kusoma" na "ikiwa hatutasoma, tutatumia dawa za kulevya".

    Maandamano ya aina hiyohiyo yalitokea katika mji wa Beni kaskazini mwa Kivu ,kwa mujibu wa radio inayomilikiwa na Umoja Mataifa- Radio Okapi.

    Walimu wamekuwa katika mgomo tangu Oktoba 4, mwanzoni mwa masomo mwaka huu wakitaka waongezewe mshahara na kupunguza umri wa kustaafu pamoja na masuala mengine.

    Serikali imewashutumu viongozi wa dini ambao wanasimamia shule nyingi za msingi , kwa kudai kuwa wanahusika na mgomo huo ingawa viongozi hao wamekanusha madai dhidi yao.

    Makamu wa rais wa Jamuhuri ya demokrasia ya Kongo Jean-Marc Kabunda, amewataka wanafunzi kurudi nyumbani maana haya sio mapambano yao.

    "Nyinyi sio watu wa mtaani, mnapaswa kuwa shuleni na kama hampo shule mnapaswa kuwa nyumbani," alisema.

  11. Mmoja wa Vifaru weupe wa mwisho duniani astaafu mpango wa upandikizaji

    Wanasayansi wameacha kumtumia kifaru mmoja ambaye ni kati ya vifaru wawili weupe waliobaki duniani katika programu wa upandikizaji wakijaribu kuokoa spishi hiyo kupotea.

    Maamuzi ya kusitisha kuchukua mayai ya Najin mwenye umri wa miaka 32- kutokana na tathmini ya hatari za kimaadili kwa kuzingatia umri wake na sababu nyingine.

    Hakuna kati ya Najin au binti yake Fatu aliye na uwezo wa kubeba ujauzito hadi kufanikisha kuzaliwa kwa kifaru mwingine

    Mwaka 2018 , kifaru wa kiume alikufa lakini mbegu zake za kiume zilikusanywa na kutumika kurutubisha mayai ya kifaru jike.

    Mchakato huo unajumuisha kikundi cha wachunguzi wanaotumia teknolojia ambayo ilifanyiwa utafiti kwa miaka kadhaa.

    Mayai yanarutubishwa kwa kutumia mbegu za kiume za vifaru wa kiume wawili waliokufa tayari.

    Mimba kumi na mbili zimetungwa hadi sasa, na wanasayansi wanatarajia kuzipandikiza kwa akina mama waliochaguliwa kutoka kwa idadi ya vifaru weupe wa eneo la kusini.

    • Faru Fausta: Faru mzee zaidi duniani afariki Tanzania
    • Faru weusi ni miongoni mwa wanyama wanaoripotiwa kutoweka
  12. Mabaki ya mchumba wa mwanablogu aliyeuliwa yathibitishwa-FBI

    Mabaki ya binadamu yaliyopatikana katika maegesho ya Florida siku ya Jumatano yamethibitishwa kuwa ni ya mchumba wa mwanablogu aliyeuawa, FBI imesema.

    Brian Laundrie, alikuwa amepotea kwa zaidi ya mwezi mmoja , na mwili wake uliweza kutambuliwa kwa kutumia vipimo vya meno.

    Laundrie, ambaye alikuwa anafuatiliwa sana katika kifo cha Gabby Petito kwa kuwa alirudi peke yake Florida mwezi uliopita katika safari ambayo alikwenda na mwenza wake.

    Mwili wake ulipatikana baadae huko Wyoming, eneo ambalo wapenzi hao walitembelea.

    Wakili anayewawakilisha wazazi wa Laundrie' wametoa taarifa inayosema: "Chris na Roberta Laundrie wamepata taarifa kuwa maiti iliyopatikana jana ni ya Brian.

    "Hatuna la ziada bali tunaomba watu waheshimu faragha ya Laundries katika kipindi hiki kigumu."

    Jumatano , maofisa walipata sehemu ya mabaki ya binadamu chini ya maji. Vitu vingine vilivyopatikana wakati wa kutafuta ni kitabu cha Brian.

    Wazazi wa Petito waliripoti juu ya binti yao kupotea Septemba 11 baada ya kutomuona au kuwasiliana naye Agosti .

    Wakati ambao bwana Laundrie alirudi Florida bila Petito mnamo Septemba 01.

    Familia ya Petito ilitaka familia ya mchumba wa binti yao ishiriki katika kusaidia uchunguzi lakini hata huyo mchumba naye akapotea pia.

  13. Nyota wa sinema Alec Baldwin amuua mwanamke kutumia bunduki wakati wa kutengezwa filamu yake

    Mwanamke amekufa na mwanaume amejeruhiwa baada ya muigizaji Alec Baldwin kufyatua risasi kutumia bunduki ya maigizo kwenye seti ya filamu huko New Mexico.

    Polisi katika jimbo hilo la Marekani walisema Bw. Baldwin alitoa silaha hiyo wakati wa utengezaji wa filamu yake

    Mwanamke huyo alipelekwa hospitalini lakini alifariki kutokana na majeraha yake. Mwanaume aliyejeruhiwa -mkurugenzi wa filamu, alikuwa akipokea huduma ya dharura.

    Msemaji wa Bw Baldwin aliliambia shirika la habari la AP kwamba kisa hicho kilihusisha utumiaji mbaya wa bunduki ya maigizo.

    Mwanamke huyo ametajwa kama Halyna Hutchins, 42, ambaye alikuwa akifanya kazi kama mkurugenzi wa upigaji picha. Mtu anayetibiwa ni Joel Souza, 48, mkurugenzi wa filamu.

    Polisi bado wanachunguza tukio hilo huko Bonanza Creek Ranch, eneo maarufu la utengenezaji wa sinema, na hakuna mashtaka yoyote yaliyofunguliwa.

  14. Virusi vya Covid huenda viliwaua wahudumu wa afya kati ya elfu 80 hadi 180-WHO

    Virusi vya Covid 19 vimeathiri vibaya wafanyikazi wa huduma ya afya na huenda viluwaua kati ya 80,000 na 180,000, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasema.

    Wafanyakazi wa huduma ya afya lazima wapewe kipaumbele kwa chanjo, mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema

    Vifo hivyo vilitokea kati ya Januari 2020 na Mei mwaka huu.

    Hapo awali, afisa mwingine mwandamizi wa WHO alionya ukosefu wa chanjo unaweza kuona janga hilo likiendelea hadi mwaka ujao.

    Kuna takriban wafanyakazi milioni 135 wa huduma za afya ulimwenguni.

    "Takwimu kutoka nchi 119 zinaonyesha kuwa kwa wastani, wafanyikazi wawili kati ya watano wa huduma za afya ulimwenguni wamepewa chanjo kamili," Dk Tedros alisema.

  15. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Ijumaa tarehe 22 Oktoba 2022