Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mahakama Kenya yampatia siku 14 rais Kenyatta kuwateua majaji

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameamrishwa kuwateua majaji sita waliosalia kati ya wale 40 , katika kipindi cha siku 14 zijazo,

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Mahakama Kenya yampatia siku 14 rais Kenyatta kuwateua majaji

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameamrishwa kuwateua majaji sita waliosalia kati ya wale 40 , katika kipindi cha siku 14 zijazo,

    Majaji hao sita wanashirikisha Aggrey Muchelule, George Odunga, Weldon Korir na Joel Ngugi, ambao walifaa kuhudumu katika mahakama ya rufaa.

    Hakimu mkuu Evans Makori na msajili wa mahakama kuu Judith Omenge pia waliwachwa nje katika orodha ya majaji waliochapishwa katika gazeti la Kenya.

    Siku ya Alhamisi , Jaji wa mahakama kuu William Musyoka , James Wakiaga na George Dulu walisema kwamba Jaji mkuu Martha Koome, pamoja na tume ya mahakama watakuwa huru kuwaapisha majaji hao sita iwapo Rais Uhuru Kenyatta atashindwa kutekeleza jukumu lake la kikatiba.

    ‘’Siku 14 zitakapokamilika, bila Uhuru kutangaza uteuzi huo, itabainika kwamba uwezo wake wa kuwateuwa utakuwa umekwisha na hivyobasi sita hao watakuwa wameteuliwa kama majaji wa mahakama ya rufaa kama ilivyopendekezwa’’, walisema majaji hao.

  2. Baa na klabu za burudani Kenya kufungwa saa tano usiku

    Baa na klabu zote za burudani zitafungwa mwendo wa saa tano nchini Kenya. Haya ni kwa mujibu wa Waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe.

    Kagwe hatahivo amesema kwamba baa na klabu za burudani zilizo na leseni ya kuhudumu hadi alfajiri zitaruhusiwa kuwa wazi.

    Hapo jana Rais Uhuru Kenyatta aliondoa kafyu ya kutotoka nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri lakini hakugusia suala la kufunguliwa kwa baa na klabu za burudani.

    Hatua hiyo ilishinikiza idara ya polisi kuingilia kati na kuelezea umma kwamba baa zote zitafungwa mwendo wa saa moja kama ilivyokuwa.

    Hatahivyo akihutubia taifa kuhusu hali ya maambukizi ya ugonjwa wa corona, Waziri kagwe alisema kwamba muda wa kufungwa kwa baa zote sasa utakuwa mwendo wa saa tano usiku.

    Katika hotuba yake ya kila siku, Kagwe hatahivyo amewataka Wakenya zaidi kujitokeza ili kupata chanjo ya Corona.

    Katika ujumbe wa Twitter polisi walikua wamesisitiza kuwa baa zifungwe kufikia saa moja usiku licha ya Rais Uhuru Kenyatta kuondoa amri ya kutotoka nje usiku iliyodumu kwa miezi 18.

  3. Madaktari wa Marekani wajaribu kupandikiza figo ya nguruwe kwa binadamu

    Madaktari nchini Marekani wanasema kuwa wamefanikiwa kumpa figo ya nguruwe mtu kwa njia ya upandikizaji katika hatua ambayo inaweza kusaidia kupunguza uhaba mkubwa wa viungo vya kupandikiza.

    Utaratibu uliofanywa katika Kituo cha afya ch NYU Langone mjini New York, Marekani ulihusisha utumiaji wa nguruwe ambaye jeni zake zilibadilishwa ili kuendana naya mwanadamu na cha kufurahisha ni kwamba haikukataliwa na kinga ya mwili wa binadamu.

    Mpokeaji alikuwa mgonjwa ambaye ubongo ulikua umekufa na dalili ya kupona ambaye familia yake ilikubali afanyiwe jaribio hilo kabla ya kutolewa kwenye mashine ya kumsadia kuishi, watafiti waliiambia Reuters.

    Kwa siku tatu figo hiyo mpya ilipandikizwa kwenye mishipa yake ya damu na kuwekwa nje ya mwili wake ili kuwawezesha watafiti kuifikia.

    Utafiti huo haujakaguliwa au kuchapishwa lakini kuna mipango ya kufanya hivyo inaendelea.

    Kutumia nguruwe kwa upandikizaji sio wazo jipya ikwani sehemu ya moyo wa nguruwe tayari hutumiwa sana kwa wanadamu.

    Na viungo vyao ni mechi nzuri kwa watu linapokuja suala la ukubwa.

  4. Mbuga ya wanyamapori ya Serengeti ndio bora zaidi Afrika

    Mamlaka ya Tuzo ya dunia ya safari(WTA)imeitangaza Mbuga ya wanyama ya Serengeti nchini Tanzania kama mbuga ya wanyama inayoongoza barani Afrika mwaka 2021.

    Serengeti imekuwa ni mbuga ya wanyama inayoongoza Afrika kwa mara ya tatu katika mwaka 2019, 2020 na 2021, imesema taarifa iliyotolewa na mamlaka ya Mbuga za Wanyama nchini Tanzania.

    Mbunga nnyingine zilizoteuliwa katika Mbuga za wanyama zinazoongoza ni pamoja na hifadhi ya wanyama ya kalahari-Central Game Reserve Botwana, Mbuga ya wanyama ya Elosha nchini Namibia, Kidepo Valley National Park Uganda; Kruger National Park ya Afrika Kusini na Hifadhi ya wanyama ya Maasai Mara nchini Kenya.

    Serengeti yenye ukubwa wa kilomita za mraba 14,763, ni maarufu kwa kuwa na aina mbali mbali za wanyama, ndege na mimea wa spishi mbali mbali.

    Aina 70 za spishi za wanyama wakubwa na 500 za ndege hupatikana katika mbuga hii iliyopo Tanzania.

  5. Vilipuzi vililipuliwa katika mali ya mwanaharakati wa Kenya - ripoti

    Polisi nchini Kenya wanachunguza ripoti kwamba washambuliaji walitumia vilipunzi kubomoa nyumba ya mwanaharakati Boniface Mwangi usiku wa jana.

    Katika akaunti yake rasmi ya Twitter, polisi ilithibitisha kupokea malalamishi rasmi kwamba wanaume wanaodaiwa kujihami kwa bastola walivamia eneo la mjengo, kuwaibia wafanya kazi na kujaribu kujaribu kubomoa nyumba iliyokua ikijengwa kwa kutumia vilipuzi.

    Polisi wanasema wamefika eneo la tukio na uchunguzi umeanza.

    Mjengo huo uko katika ploti ya Bwana Mwangi eneo la Lukenya, Kaunti ya Machakos County, Kusini mashariki mwa jiji la Nairobi.

    Hakujaripotiwa majeruhi yoyote. Boniface Mwangi sasa anasema kuwa anahofia usalama wake na wa familia yake.

  6. Korea Kusini yazindua roketi yake ya kwanza

    Korea Kusini imezindua roketi yake ya kwanza kutengezwa nyumbani, kupiga hatua katika harakati za nchi kwenye sayansi za anga za mbali.

    Roketi hiyo ya Korea, inalojulikana kama Nuri, liliondoka Goheung, karibu 500km (maili 310) kusini mwa Seoul.

    Rais Moon Jae-in amesema gari hilo limekamilisha mpango mzima wa safari safari lakini ilifeli kuweka kielelezo cha satelliteyake kwenye mzunguko wa dunia.

    Uzinduzi kama huo ni muhimu katika mpago wa anaganilakini huenda ikawa na vifaa vya kijeshi.

    Korea Kusini inakimbizana na Korea Kaskazini katika uundaji silaha, nchi zote mbili zikijaribu silaha zao mpya hivi karibuni. Kaskazi ilifikisha satellite yake katika mzunguko 2012.

    Nuri iligharimu Korea Kusini karibu dola bilioni 1.62 kutengeza. Roketi hiyo yenye uzani wa tani 200 na urefu wa mita 47.2, ina injini sita za mafuta.

    Katika maoni yake, Rais Moon alikiri uzinduzi huo haukufikia malengo yao, lakini akaongeza: "Sio muda mrefu kabla ya kuweza kuizindua kikamilifu katika njia inayolengwa," shirika la habari la Reuters liliripoti.

    Korea Kusini inapanga kufanya majaribio mengine manne ya chombo cha Nuri hadi 2027 ili kujiimarisha, kulingana na Taasisi ya Utafiti wa Anga ya Korea (KARI) ambayo inasimamia uzinduzi huo.

  7. Diamond, Wizkid miongoni mwa wasanii wa Afrika walioteuliwa kwa Tuzo za Muziki za MTV Ulaya 2021

    Wasanii watano wa Afrika wametuliwa kuwania Tuzo ya MTV Ulaya 2021 katika kitengo cha msanii bora wa Afrika

    Wasinii hao ni pamoja na Msanii wa Tanzania Diamond Platnumz,Wizkid na Tems wa Nigeria, Focalistic wa Afrika Kusini na Amaarae wa Ghana.

    Diamond Platnumz amenukuliwa tovuti ya Musicinafrica akisema: “Nafurahi sana na kujivunia kuteuliwa katika tuzo za MTV EMA 2021, ina maana kubwa kwangu, kizazi changu, taifa la Waswahili na Afrika nzima.”

    Sherehe za tuzo zitatangazwa mnamo 14 Novemba.

    Ifuatayo ni orodha ya wasanii wa kimataifa walioteiliwa kuwania vitengo tofauti katika tuzo hizo.

    Msanii Bora

    • Doja Cat
    • Ed Sheeran
    • Justin Bieber
    • Lady Gaga
    • Lil Nas X
    • The Weeknd

    Pop Bora

    • BTS
    • Doja Cat
    • Dua Lipa
    • Ed Sheeran
    • Justin Bieber
    • Olivia Rodrigo

    Wimbo Bora

    • ‘Kiss Me More’ – Doja Cat ft. SZA
    • ‘Bad Habits’ – Ed Sheeran
    • ‘Peaches’ – Justin Bieber ft. Daniel Caesar, Giveon
    • ‘MONTERO (Call Me By Your Name)’ – Lil Nas X
    • ‘Driver’s License’ – Olivia Rodrigo
    • ‘STAY’ – The Kid LAROI, Justin Bieber

    Video Bora

    • ‘Kiss Me More’ – Doja Cat ft. SZA
    • ‘Bad Habits’ – Ed Sheeran
    • ‘Peaches’ – Justin Bieber ft. Daniel Caesar, Giveon
    • ‘MONTERO (Call Me By Your Name)’ – Lil Nas X
    • ‘Wild Side’ – Normani ft. Cardi B
    • ‘Willow’ – Taylor Swift

    Ushirikiano Bora

    • Black Eyed Peas, Shakira – ‘GIRL LIKE ME’
    • Bruno Mars, Anderson .Paak, Silk Sonic – ‘Leave the Door Open’
    • Doja Cat ft. SZA – ‘Kiss Me More’
    • Lil Nas X, Jack Harlow – ‘INDUSTRY BABY’
    • The Kid LAROI, Justin Bieber – ‘STAY’
    • The Weeknd & Ariana Grande – ‘Save Your Tears (Remix)’
  8. Tembo anaswa katika video akimkanyaga hadi kumuua mamba

    Mtalii kwenye safari alipiga picha ya video wakati mamba aliyejipata pabaya akikanyagwa hadi kufa na ndovu baada ya kumnyemelea ndama wake kwenye mto nchini Zambia.

    Kwenye video hiyo, tembo alimshambulia mamba huyo kwa nguvu kutumia kichwa chake, kabla ya kumkanyaga katika mto huku kundi la watalii likiangalia.

    Tukio hilo nadra lilinaswa na Hans Henrik Haahr na imewekwa mtandaoni na Latest Sightings, idhaa ya YouTube inayoziweka video za wanyamapori zilizorekodiwa kote Afrika.

    "Tembo kwa kawaida ni wanyama wenye amani na wanaojali sana; hata hivyo, tembo wa kike wanaweza kuwa wakali wakati wa kulinda ndama mchanga," Latest Sightings ilisema.

    "Hans alisema alikuwa hana maneno ya kuelezea tukio hilo, na kwamba lilikuwa" la kushangaza "."

    Kukanyagwa huko kulisababisha kifo cha mamba, ilisema.

  9. Mabaa kufungwa usiku Kenya licha ya kafyu kuondolewa-Polisi

    Polisi nchini Kenya inasisitiza kuwa mabaa na klabu za burudani zinatarajiwa kufungwa kufikia saa moja usiku licha ya Rais Uhuru Kenyatta kuondoa amri ya kutotoka nje usiku iliyodumu kwa miezi 18, Tovuti ya The Star imeripoti,

    "Kufuatia kuondolewa kwa kafyu inayohusiana na Corona iliyoondolewa na rais wakati wa sherehe za sikukuu ya Mashujaa [amri iliyopo ya kufunga mabaa saa moja usiku itaendelea kudumishwa kwa sasa. Utekelezaji wa ukiukaji wa hatua hii kuendelea, "Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) ilisema.

    Agizo la NPS linakinzana na taarifa ya awali iliyotolewa na Waziri wa Utalii Najib Balala kwamba shughuli katika sekta ya utalii zitarejelea hali ya kawaida.

    Rais Kenyatta alitaja hatua kubwa katika kampeni ya chanjo ya Covid-19 ya Kenya wakati wa kuondoa amri ya kutotoka nje ambayo ilianza kutekelezwa tangu Machi 2020. Pia alisema makanisa yataruhusiwa kuongeza idadi ya waumini hadi thuluthi mbili.

    Kundi la kutetea maslahi ya wahudumu wa sekta ya burudani nchini Kenya limesema kuwa zaidi ya mabaa 15,000 na migahawa imefungwa tangu Machi na wafanyakazi 90,000 kupoteza ajira.

  10. Trump kuzindua mtandao wa kijamii wa TRUTH Social

    Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametangaza mipango ya kuzindua mtandao mpya wa kijamii, uitwao TRUTH Social.

    Amesema jukwaa hilo "litakabiliana na jeuri ya kampuni kubwa za teknolojia ", akizishutumu kwa kunyamazisha sauti za wapinzani huko Marekani.

    Kampuni ya Trump Media & Technology Group (TMTG), ambayo yeye ni mwenyekiti wake, pia inakusudia kuzindua huduma ya usajili wa mahitaji ya video.

    Bw. Trump alipigwa maarufuku katika mitandao ya kijamii au kufungiwa na mitandao kama ya Twitter na Facebook baada ya kundi la wafuasi wake kuvamia Bunge la Marekani Januari mwaka huu.

    Yeye na washauri wake tangu wakati huo walidokeza kuwa wanapanga kuunda mtandao hasimu wa kijamii.

    Toleo la mapema la biashara yake ya hivi karibuni, TRUTH Social, itakuwa wazi kwa wageni waalikwa mwezi ujao, na kutakuwa na "uzinduzi wa kitaifa" ndani ya miezi mitatu ya kwanza ya 2022, kulingana na taarifa ya TMTG.

    "Tunaishi katika ulimwengu ambao Taliban ina uwepo mkubwa kwenye Twitter, lakini Rais wako mpendwa wa Marekani amenyamazishwa," aliandika Bw Trump.

    Mapema mwaka huu, alizindua Kutoka kwa Dawati la Donald J Trump, ambayo mara nyingi ilikuwa ikiitwa blogu.

    "Kila mtu ananiuliza kwa nini mtu asisimame kupinga makampuni makubwa ya teknolojia? Sawa, tutafanya hivyo hivi karibuni!" aliongeza.

  11. Mkutano wa wadau wa siasa na waziri mkuu Tanzania waahirishwa

    Mkutano wa kati ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jeshi la Polisi na wadau wa siasa nchini uliopangwa kufanyika Dodoma wiki hii. Sababu za kuahirishwa kwake inaelezwa ni ili kutoa nafasi zaidi kwa wadau wengi zaidi kushiriki kikamilifu.

    Mkutano huo uliolenga kujadili maudhui ya utekelezaji wa sheria zinazoratibu shughuli zote za siasa Tanzania' ulikuwa uhudhuriwe pia na waziri mkuu wa nchi hiyo, Kassim Majaliwa.

    Msajili msaidizi wa vyama vya siasa nchini Tanzania, Sixty Nyahoza aliiambia BBC kwamba, mbali na waziri mkuu na baadhi ya mawaziri, mkutano huo ulipangwa kuhudhuriwa na pia wadau wote muhimu katika siasa vikiwemo vyama vya siasa, Azaki, waandishi wa habari na viongozi wa dini.

    Kama ilivyonukuliwa na mtandao wa gazeti la Mwananchi la nchi hiyo, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, Juma Ali Khatib amesema mkutano huo hautakuwepo kama ulivyopangwa awali, lakini maandalizi yanaendelea kwa kuwa utafanyika mwezi Desemba, mwaka huu.

    Hata hivyo tarehe ya kufanyika mkutano huo itatangazwa baadaye na utahusisha wadau tofauti wakiwamo wa vyama vya siasa vilivyotangaza kuususia kwa sababu tofauti.

    Kabla ya kuahirishwa kwa mkutano huo, vyama vya Chadema na NCCR Mageuzi vilishatangaza kutoshiriki huku vikitoa masharti kwa Ofisi ya Msajili.

    Alisema wadau wote wameshajulishwa kuhusu kuahirishwa kwa mkutano huo uliotarajiwa kuleta suluhu ya sintofahamu ya kisiasa nchini, hasa mvutano kati ya vyama vya siasa na Jeshi la Polisi.

    Mkutano huo unakuja kufuatia kuwepo kwa mvutano wa muda mrefu kuhusu kuzuiwa kwa shughuli za kisiasa nchini humo, ambapo vyama vya upinzani vimekuwa vikilalamika kunyimwa fursa ya kufanya mikutano ya kisiasa kama sheria zinavyotaka.

  12. Kiongozi wa vuguvugu la kujitenga Nigeria kufikishwa mahakamani leo

    Kesi dhidi ya kiongozi wa vuguvugu la kujitenga nchini Nigeria Nnamdi Kanu inarejelewa leo mjini Abuja

    Bwana Kanu ni kiongozi wa kundi la Indigenous People of Biafra (Ipob), kundi linalotaka kujitenga kwa jimbo la kusini -mashariki mwa Nigeria, ambalo serikali imeharamisha. Anakabiliwa na mashataka ya "ugaidi na uhaini.

    Akipatikana na hatia huenda akafungwa maisha. Nnamdi Kanu amekua akizuiliwa na polisi wa kisiri kulingana na mawakili wake.

    Wiki iliyopita serikali ya Nigeria imefanyia marekebisho mashataka dhidi yake na kuongeza kuwa anaendesha kampuni haramu na kuchapisha taarifa za kuchafua sifa.

    Hali ya taharuki ilipanda mwezi Julai wakati amamlaka ilipokosa kumfikisha mahakamani kumfungulia mashataka.

    Mawakili wake wanataka serikali kuhakikisha anafikishwa mahakamani leo.

    Wanachama wa kundil lake linalotaka kujitenga kwa eneo la Biafra, have been agitating for a breakaway state for the southeast region of the country.

    Kanu alikamatwa mara ya kwanza Oktoba 2015, lakini akatoroka Nigeria 2017 baada ya jeshi kuvamia nyumbani kwake.

    Alikamatwa mwezi Juni mwaka huu. Mawakili wake walishutumu serikali kwa kukiuka sheria za kimataifa na kukiuka haki zake.

  13. Gabby Petito: 'Mabaki ya binadamu' yapatikana katika utafutaji wa Brian Laundrie

    Wachunguzi wanaoongoza shughuli ya kumtafuta mchumba aliyepotea wa mwanablogu wa Marekani aliyeuawa wamepata "mabaki ya binadamu" katika bustani ya Florida, FBI imesema.

    Shirika la upelelezi limesema wakati wa uchunguzi wao walimkuta na vitu vya Brian Laundrie, mtu ambaye alikuwa anataka kujua kifo cha Gabby Petito.

    Bwana Laundrie hakuonekana kwa kipindi cha zaidi ya mwezi baada ya kurejea kutoka safari ambayo alienda bila mpenzi wake.

    Mwili wake ulikutwa Wyoming, eneo ambalo wapenzi hao walikuwa wametembelea.

    Katika mkutano na waandishi wa habari, Michael McPherson kutoka FBI alithibitisha kuwa wamepata mwili wa marehemu katika eneo la maegesho , na kukiwa na kitabu ambacho ni cha Laundrie.

  14. Waendesha mashtaka wakata rufaa juu ya hukumu dhidi ya shujaa wa Hotel Rwanda

    Waendesha mashtaka wamewasilisha rufaa dhidi ya uamuzi wa korti juu ya Paul Rusesabagina, mtu aliyeonyeshwa kama shujaa katika sinema ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda.

    Rusesabagina, 67, alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela mwezi uliopita baada ya kupatikana na hatia ya kuunga mkono kundi la waasi lililohusika na mashambulio mabaya mwaka 2018 na 2019.

    Waendesha mashtaka wa Rwanda walikuwa wametaka apewe kifungo cha maisha na walikuwa wameonyesha kutofurahishwa na uamuzi wa kutoa adhabu nyepesi kuliko walivyotaka.

    Rusesabagina alikuwa amejiondoa kwenye kesi hiyo, ambayo vikundi vya haki, wafuasi na familia yake waliitaja kama kandamizi.

    Yeye wala mawakili wake hawakuwa kortini kwa uamuzi huo, ambapo washtakiwa wenzake walihukumiwa kwa kati ya miaka mitatu hadi 20.

    Siku ya Jumatano, binti ya Rusesabagina Carine Kanimba alisema hatua ya upande wa mashtaka kukata rufaa kwa hukumu hiyo ilionyesha kuwa kesi hiyo ilikuwa ya kisiasa.

    Korti ya rufaa inapaswa kuamua baadaye tarehe ambayo itaanza kusikiliza rufaa hiyo.

  15. Wamiliki wa Newcastle United wauliza mashabiki wasivae mavazi ya kitamaduni ya Kiarabu wakati wa mechi

    Newcastle United imewaomba mashabiki wasivae "mavazi ya kitamaduni ya Kiarabu au vazi la kufunika kichwa linalotumika Mashariki ya Kati" kwenye mechi kufuatia kununuliwa kwa kilabu hiyo na wamiliki kutoka Saudi Arabia.

    Wafuasi wengine wa Magpies walivaa nguo hizo wakati walipokusanyika nje ya St James Park 'kusherehekea kununuliwa kwa kilabu hiyo

    Mavazi kama hayo pia yalionekana wakati wa mechi dhidi ya Tottenham katika mchezo wa kwanza wa kilabu chini ya wamiliki wapya.

    "Hakuna mtu katika kikundi kipya cha wamiliki aliyekerwa kwa njia yoyote," kilabu ilisema.

    "Ilikuwa ishara ambayo ilikubaliwa kuwa nzuri na ya kukaribisha kwa nia yake.

    "Walakini, kuna uwezekano wa kuwa kuvaa hivi sio sawa na kitamaduni na kuna hatari ya kukasirisha wengine.

  16. WHO yaonya kuwa janga la Covid 19 litaendelea hadi 2022

    Janga la Covid "litaendelea kwa mwaka zaidi ya inavyotakiwa" kwa sababu nchi masikini hazipati chanjo zinazohitajika, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasema.

    Dkt Bruce Aylward, kiongozi mwandamizi wa WHO, alisema inamaanisha janga la Covid linaweza "kujivuta kwa urahisi hadi 2022".

    Chini ya 5% ya idadi ya watu wa Afrika wamepewa chanjo, ikilinganishwa na 40% katika mabara mengine .

    Uingereza imetoa chanjo zaidi ya milioni 10 kwa nchi zinazohitaji.

    Imeahidi kutoa jumla ya milioni 100.

    Dk Aylward alitoa wito kwa nchi tajiri kutoa nafasi zao kwenye foleni ya chanjo ili kampuni za dawa ziweze kutanguliza nchi zenye kipato cha chini badala yake.

  17. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja hii leo Alhamisi tarehe 21 Oktoba.