Biden: Ulimwengu unakabiliwa na nyakati zenye maamuzi magumu

Chanzo cha picha, Reuters
Katika hotuba yake ya kwanza katika kikao cha Umoja wa mataifa rais wa Marekani Joe Biden ametoa wito wa ushirikiano katika kile alichokitaja kuwa nyakati za ‘maamuzi magumu kwa ulimwengu’.
Hakikisho lake linajiri huku kukiwa na wasiwasi na washirika kuhusu hatua ya taifa hilo kuondoa majeshi yake Afghanistan na mgogoro mkubwa wa kidiplomasia na Ufaransa kuhusu mkataba wa manowari.
Marekani pia imetangaza kwamba itaongeza maradufu ahadi yake ya ufadhili wa mabadiliko ya tabia nchi kufikia 2024.
Akithibitisha kuunga mkono demokrasia na diplomasia , Bwana Biden alisema: Tunapaswa kufanya kazi kwa pamoja kama vile ambavyo haijawahi kutokea.
Kikao hicho cha 76 cha Umoja wa mataifa kinafanyika huku kukiwa na mgogoro wa tabia nchi na mlipuko wa corona , yote yakiwa ni matatizo ambayo yameugawanya ulimwengu.
Ameahidi kuongeza ufadhili wa mabadiliko ya tabia nchi ili kufikia $11.4bn (£8.3bn) kufikia 2024.













