Mchezaji wa Ufaransa afariki baada ya kupoteza fahamu kwa miaka 39

Mchezaji wa zamani wa ufaransa Jean Pierre Adams , ambaye alikuwa katika koma kwa miaka 39 amefariki akiwa na umri 73.

Moja kwa moja

  1. Taiwan yasema ndege 19 za China zimeingia katika eneo lake la ulinzi wa angani

    tl

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Taiwan imesema uvamizi mkubwa wa ndege za jeshi la China ziliruka katika eneo lake la ulinzi wa angani Jumapili.

    Wizara ya ulinzi ilisema ndege 19 pamoja na ndege za kufanya mashambulio zenye uwezo wa nyuklia ziliingia katika eneo la ‘utambulisho wa ulinzi wa anga (ADIZ).

    Taipei imekuwa ikilalamika kwa zaidi ya mwaka mmoja juu ya misheni zinazofanywa kila mara na jeshi la anga la China karibu na kisiwa hicho.

    China inaiona Taiwan yenye demokrasia kama jimbo lake lililojitenga, lakini Taiwan inajiona kama nchi huru.

    Wizara ya ulinzi ya Taiwan ilisema ndege hizo za China zilisheheninne za kurusha mabomu za H-6 ambazo zinaweza kubeba silaha za nyuklia pamoja na ndege za kushambulia manowari.

  2. Mapacha waliounganika kichwani watenganishwa katika upasuaji wa kipekee huko Israeli

    twin

    Chanzo cha picha, SOROKA MEDICAL CENTRE VIA REUTERS

    Watoto pacha wenye umri wa mwaka mmoja ambao walizaliwa wakiwa wameunganika nyuma ya vichwa vyao wameweza kuonana kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa upasuaji nadra wa kuwatenganisha huko Israeli.

    Operesheni hiyo ya masaa 12 katika Kituo cha Matibabu cha Soroka katika mji wa Beersheba wiki iliyopita ilichukua miezi kadhaa ya maandalizi, na kujumuisha vipandikizi vya kichwa kwa wote wawili.

    Wataalam kadhaa kutoka Israeli na nje ya nchi walihusika.

    Wasichana hao ambao hawajatajwa majina, wanasemekana kupata nafuu "Wanapumua na wanakula peke yao," Eldad Silberstein, mkuu wa idara ya upasuaji katika kituo cha matibau cha Soroka, aliiambia Idhaa ya Israeli ya Channel 12.

    is

    Chanzo cha picha, Reuters

    Ni mara ya kwanza operesheni kama hiyo, ambayo imefanywa mara 20 tu ulimwenguni, kufanywa nchini Israeli.

    Miezi kabla ya upasuaji, mifuko ya silicone yenye iliingizwa vichwani mwao na kupanuliwa mara kwa mara ili kunyoosha ngozi. Ngozi mpya ilitumika kuziba vichwa vyao baada ya mafuvu kujengwa upya.

    Maandalizi pia ni pamoja na uundaji wa mfano halisi wa mapacha kupitia teknolojia ya 3D, alisema Mickey Gideon, daktari mkuu wa upasuaji wa Soroka. "Kwa furaha yetu, kila kitu kilikwenda kama tulivyotarajia," akaongeza.Wasichana hao, ambao walizaliwa mnamo Agosti 2020, wanatarajiwa kuishi maisha ya kawaida kabisa.

    Soma zaidi:

  3. Mayai ya uzazi na manii sasa kuhifadhiwa kwa barafu hadi kwa miaka 55

    Kikomo cha kuhifadhi mayai, manii na kijusi kitaongezwa kutoka miaka 10 hadi miaka 55 chini ya mipango ya serikali

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kikomo cha kuhifadhi mayai, manii na kijusi kitaongezwa kutoka miaka 10 hadi miaka 55 chini ya mipango ya serikali

    Ukomo wa kuhifadhi maya na manii utaongezwa hadi miaka 55 chini ya mpango wa serikali ambao mawaziri wanasema utawapa watu nafasi zaidi ya kuamua wakati wa kuanza familia nchini Uingereza .

    Waziri wa Afya Sajid Javid alisema ukomo wa sasa wa miaka 10 ulikuwa na "masharti makali."

    Mbinu ya kisasa ya kugandisha inamaanisha kuwa mayai yanaweza kuhifadhiwa bila ukomo ili kuzuia mayai hayo kuharibika, utafiti wa Taasisi ya uzazi nchini Uingereza umedokeza.

    Mpango huo unahitaji kuidhinishwa na bunge.

    Kwa sasa, miaka 10 ikiisha, wazazi wanatarajiwa lazima waamue ikiwa watafanyiwa tiba ya uzazi la sivyo seli hizo zitupwe.

    Chini ya mfumo huo mpya, watapewa chaguo la kuweka au kutupa seli zilizohifadhiwa au kijusi kwa vipindi vya miaka 10.

    Bwana Javid amesema: "Sheria hio mpya itasaidia kuwaondolea watu hofu ya muda kuyoyoma katika mawazo."

    Aliongeza: "Kwa kufanya mabadiliko haya, tutachukua hatua kubwa kuelekea – sio tu kuwapa watu uhuru kuhusu uzazi wao, bali pia usawa."

    Mwenyekiti wa Jumuiya ya uzazi nchini Uingereza Dkt Raj Mathur amekaribisha mpango huo.

    Alisema kurefushwa kwa ukomo wa muda "kunalinda uwezo wa wagonjwa wote kufanya uamuzi wa uzazi wao wenyewe kama watu binafsi na wenza."

    Kugandisha yai, manii na kijusi ni nini?

    Ni njia ya kuhifadhi uzazi kwa kukusanya mayai , mbegu za kiume au kijusina kuzihifadhi ili mzazi mtarajiwa aweze kupata mtoto siku nza baadaye.

    Mchakato huo unahusisha kukusanya mayai 15 kupitia mfumo wa IVF, kuzipoesha na kisha kuzihifadhi katika tangi maalum lenye maji ya nitrojeni.

    Mayai hayo halafu yatatumiwa wakati yanahitajika, lakni ni yale tu yatakayokuwa hai ndio yatatungishwa na manii.

    Sampuli ya manii kawaidi hugawanywa kati ya kontena kadhaa zinazofahamika kama mirija kabla ya kuzigandisha ili ziweze kutumika kataka tiba tofauti.

    Vijusi vinagandishwa wakati wa tiba ya uzazi ikiwa awamu ya kwanza haikufaulu unaweza kujaribu tena.

    Zinaweza kugandishwa kama seli moja, katika haua ya seli mbili hadi nane au baadaye katika hatua ya ukuaji.

    Chanzo: HFEA

  4. Kiongozi wa wapiganaji wanaopinga Taliban asema yuko tayari kwa mazungumzo

    tl

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kiongozi wa kundi la wapiganaji wanaopinga kundi la Taliban nchini Afghanistan anayeongza vita vikali dhidi ya Taliban katika Bonde la Panjshir amesema yuko tayari kuingia katika mazungumzo ya amani.

    Ahmad Massoud alisema anaunga mkono mpango, uliowasilishwa na maulama wa kidini, kwa suluhu iliyojadiliwa, na akatoa wito kwa Taliban kusistisha mashambulizi yao.

    Hapo awali, ripoti zilidokeza kwamba Taliban ilikuwa imepiga hatua kubwa kulitwaa eneo la Panjshir.Jimbo hilo, kaskazini mwa mji mkuu Kabul, ni mfano maarufu zaidi wa pingamizi dhidi ya utawala wa Taliban.

    Kikundi hicho cha Kiisilamu kilidhibiti Afghanistan yote wiki tatu zilizopita, kikichukua mamlaka huko Kabul mnamo Agosti 15 kufuatia kuanguka kwa serikali inayoungwa mkono na nchi za Magharibi.

    Katika chapisho kwenye Facebook, Bwana Massoud alisema National Resistance Front of Afghanistan (NRF), ambayo inajumuisha wanachama wa zamani wa vikosi vya usalama vya Afghanistan na wanamgambo wa ndani, watakuwa tayari kuacha mapigano ikiwa Taliban itaacha mashambulio yao.Hakukuwa na jibu la haraka kutoka kwa Taliban.