Ukomo wa kuhifadhi maya na manii utaongezwa hadi miaka 55 chini ya mpango wa serikali ambao
mawaziri wanasema utawapa watu nafasi zaidi
ya kuamua wakati wa kuanza familia nchini Uingereza .
Waziri wa Afya Sajid Javid alisema ukomo wa sasa wa miaka 10 ulikuwa na "masharti makali."
Mbinu ya kisasa ya kugandisha inamaanisha
kuwa mayai yanaweza kuhifadhiwa bila ukomo ili kuzuia mayai hayo kuharibika, utafiti
wa Taasisi ya uzazi nchini Uingereza umedokeza.
Mpango huo unahitaji kuidhinishwa
na bunge.
Kwa sasa, miaka 10 ikiisha, wazazi wanatarajiwa lazima waamue ikiwa watafanyiwa tiba
ya uzazi la sivyo seli hizo zitupwe.
Chini ya mfumo huo mpya, watapewa chaguo la kuweka au kutupa seli zilizohifadhiwa
au kijusi kwa vipindi vya miaka 10.
Bwana Javid amesema: "Sheria hio mpya itasaidia kuwaondolea watu hofu ya muda kuyoyoma katika
mawazo."
Aliongeza: "Kwa kufanya mabadiliko haya, tutachukua hatua kubwa kuelekea – sio tu kuwapa watu uhuru kuhusu uzazi wao, bali pia
usawa."
Mwenyekiti wa Jumuiya ya uzazi
nchini Uingereza Dkt Raj Mathur amekaribisha mpango huo.
Alisema kurefushwa kwa ukomo
wa muda "kunalinda uwezo wa wagonjwa wote kufanya uamuzi wa
uzazi wao wenyewe kama watu binafsi na wenza."
Kugandisha
yai, manii na kijusi ni nini?
Ni njia ya kuhifadhi uzazi kwa
kukusanya mayai , mbegu za kiume au kijusina kuzihifadhi ili mzazi mtarajiwa aweze kupata mtoto siku nza baadaye.
Mchakato huo unahusisha
kukusanya mayai 15 kupitia mfumo wa IVF, kuzipoesha na kisha kuzihifadhi katika tangi maalum lenye maji ya nitrojeni.
Mayai hayo halafu yatatumiwa
wakati yanahitajika, lakni ni yale tu yatakayokuwa hai ndio yatatungishwa na manii.
Sampuli ya manii kawaidi
hugawanywa kati ya kontena kadhaa zinazofahamika kama mirija kabla ya
kuzigandisha ili ziweze kutumika kataka tiba tofauti.
Vijusi vinagandishwa wakati wa
tiba ya uzazi ikiwa awamu ya kwanza haikufaulu unaweza kujaribu tena.
Zinaweza kugandishwa kama seli
moja,
katika haua ya seli mbili hadi nane au
baadaye katika hatua ya ukuaji.