Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
BBI ilikiuka katiba-Mahakama ya Rufaa ya Kenya yaamuru
Jopo la majaji saba limeamuru kwamba BBI na utaratibu uliotumiwa kuiunda ulikiuka katiba na sheria za nchi hiyo.
Moja kwa moja
Asha Juma
BBI: Raila Odinga atoa tamko baada ya mahakama ya rufaa kutupilia mbali 'Reggae'
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema kuwa uamuzi wa leo kuhusu ‘BBI’ sio mwisho wa mazungumzo haya na wahusika kila mmoja atafanya maamuzi yake kuhusu namna ya kusonga mbele kutokana na uamuzi uliotolewa leo.
Kiongozi wa ODM Raila Odinga alikuwa tayari amedokeza jinsi atakavyopokea uamuzi wa korti .Siku ya Alhamisi alikuwa amesema mapema kwamba hana nia ya kwenda katika mahakama ya juu zaidi nchini kukata rufaa dhidi yauamuzi uliotolewa leo.
Ujumbe wake huo ulitafsiriwa na wadadisi kama njia ya kuwatayarisha wafuasi wake kustahimilimakali ambayo yameambatanana kuzimwa kwa ‘rege’ ambayo Raila amekuwa akikariri kwamba hakuna anayeweza kuizima.
Katika ujumbe wake kupitia twitter Odinga amesema pandehusika zitatathmini uamuzi wa majaji na hatua ya kutupiliwa mbali kwa BBI sio mwisho wa majadiliano kuhusu hatima ya nchi ambayo Wakenya wanaitaka.
Uamuzi huo pia utakuwa na athari katika mkondo na semi za kisiasa nchini humo kwani mageuzi ya katiba yangefanikishamabadiliko ya muundo wa serikali hatuaambayo ingeweza kutumiwa kama chambo kujenga miungano taifa hilo linapojitayarisha kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao .
Ruto atoa ujumbe wake baada ya kutolewa kwa uamuzi wa BBI
Ujmbe wa naibu Rais wa Kenya akielezea jinsi ‘Mungu alivyosaidia Kenya kusitisha muungano kutokana na kuharibu katiba’. Aidha amemuomba ‘Mungu asaidie wasiojiweza kimaisha kuchochea mpango wake wa kufufua uchumi’.
Kama ilivyotarajiwa,kuzimwa kwa ‘rege’ ya BBIimekuwa kamawimbo mtamu kwa maskio yake.Ruto alitumia ukurasa wake wa Twitter kueleza alivyohisi.Alisema Mungu ameshuka kuwasaidia watu wanyonge na maskini ili kuilinda katiba .
Katika ujumbe wake Ruto pia aliongeza kwamba wakati sasa umewadia kwa wanyonge aliowaita ‘hustlers’ kuangazia njia za kuboresha hali zao kiuchumi kupitia mbinu yake ya ‘Bottoms up’ ambayo amekuwa akiipigia debe katika mikutano yake ya kisiasa .
Kwa Naibu wa rais ,uamuzi wa korti ya rufaa utakuwa kama ithibati kwa wafuasi wake na msimamo wake tangia mwanzo wa mchakato wa BBI kwamba lengo lake halikuwa nzuri na hasa kwake kisiasa .Mwafaka wa ‘Handshake’ uliozaa BBI umelaumiwa kwa kuleta mgawanyiko mkubwa kati ya Ruto na rais Uhuru Kenyatta .
Mchakato mzima wa Bbi ulionekana na kambi ya Ruto kama njia ya upande wa kiongozi wa ODM Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta kuelekezasiasa za uchaguzi wa mwaka ujao .
Habari za hivi punde, BBI ilikiuka katiba-Mahakama ya Rufaa ya Kenya yaamuru
Korti ya Rufaa nchini Kenya imeunga mkono uamuzi uliofanywa na Mahakama Kuu mnamo Mei ya kutupilia mbali mchakato wa kurekebisha katiba maarufu BBI
Jopo la majaji saba limeamuru kwamba BBI na utaratibu uliotumiwa kuiunda ulikiuka katiba na sheria za nchi hiyo.
Katika uamuzi wao majaji hao walisema Rais hana uwezo wa kuongoza mchakato wa mageuzi ya katiba.
Uamuzi huo umepokelewa kwa hisia mseto miongoni mwa viongozi wa kisiasa nchini.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema hakuna haja ya kwenda katika mahakma ya juu zaidi baada ya uamuzi huo kwenda kinyume na matarajio yao.
Mahakama Kuu ilisitisha mchakato wa BBI ikishikilia kuwa Rais na kinara wa chama cha upinzani cha Orenga Democratic Movement(ODM) hawakuwa na ruhusa ya kuanzisha mchakato wa kubadilisha katiba.
Naibu wa rais William Ruto ambaye amekuwa akiupinga mchakato huo alituma ujumbe katika akaunti yake ya twitter ulioonekana kusherehekea uamuzi wa majaji hao . Ruto katika ujumbe wake alisema Mungu amewapigania Wakenya wanyonge na kuzuia kubadilishwa kwa katiba na watu mashuhuri .
Kiongozi wa ODM Raila Odinga katika ujumbe wake naye amesema uamuzi wa mahakama sio mwisho wa mjadala kuhusu hatima ya nchi .
Amesema pande husika zitatathmini uamuzi wa mahakama ambao sasa utakuwa msingi wa majadiliano kuhusu Kenya ambayo wananchi wanaitaka .
Odinga na rais Kenyatta wamekuwa mstari wa mbele kupigia debe mchakato wa BBI na uamuzi wa korti utakuwa na athari kubwa kwa mwelekeo wa siasa za Kenya na hasa kwa Bw.Odinga aliyedaiwa na wapinzani wake kuwa na nia ya kutumia BBI kama daraja la kuingia madarakani
Uamuzi huo umetolewa mubashara kupitia vyombo vya Habari na kuhudhuriwa na mawikili 16 kutoka pande zote mbili ili kufuata masharti ya Wizara ya Afya ya kudhibiti maambukizi ya corona. Mawakili wengine walifuatilia maamuzi hayo kwenye mtandao.
Kano yajiandaa kwa 'harusi ya mwaka'
Mamia ya watu wamekusanyika nje ya kasri la Emir wa mji wa Bichi katika jimbo la Kano nchini Nigeria wakiwa na matumaini ya kujionea sherehe ya harusi ya mwana wa kiume wa Rais Muhammadu Buhari, Yusuf.
Hatua yake ya kumuoa Zahra Bayero, binti wa Emir wa Bichi imewavutia wengi tangu tangazo lilipotolewa mwezi Juni kwamba kamati ya wanachama 145- itafanya maandalizi ya sherehe hizo.
Sherehe ya Ijumaa inajulikana kama fatiha, ambayo hafla ya wanaume peke ambapo ibada za kitamaduni zinafanywa kulingana na dini ya Kiislamu, na inahuduriwa na viongozi wakuu wa serikali ya Nigeria akiwemo, Makamu wa Rais Yemi Osinbajo.
Sherehe ya harusi na dhifa ya chakula cha jioni imepangwa kufanyika siku ya Jumamosi.
Usalama katika mji huo umeimarishwa kabla ya Rais Buhari kuwasili.
Miongoni wa wageni wanaotarajiwa kuhudhuria harusi hiyo ni viongozi wa kisiasa wa Nigeria pamoja na wanasiasa kadhaa wa upinzani akiwemo makamu wa rais wa zamani Atiku Abubakar.
Wakazi wa mji huo pia wamevalia mavazi ya kupendeza kwa ajili ya hafla hiyo kuu.
Padri wa Ghana aliyeonekana akiwabusu wasichana wa shule aomba msamaha
Padri Baltharzzar Obeng Larbi wa Kanisa la Kianglikana nchini Ghana ametoa taarifa ya kuomba msamaha kwa kuwabusu wasichana watatu wa taasisi ya mafunzo ya St. Monica.
Padri huyo pia ameomba msamaha kanisa na umma kwa jumla akisema tukio hilo lilikuwa ‘’kitendo cha ubinadamu na nilidhani natoa pongezi ya kipekee' kwa wasichana hao waliyokuwa wakijiandaa kwenda kwa mafunzo ya nyanjani.
Kulingana na taarifa hiyo, padri anasema wasichana hao watatu waliokuwa katika mwaka wa tatu wa masomo na walikuwa tayari kuondoka katika chuo hicho.
Pia ameomba "watu wamuombee kwani anakabiliwa na kipindi kigumu."
Baltharzzar Larbi anasema katika hatua ya kuwapongeza "alijaribu kuongezea hisia ya kibinadamu".
Kanisa limebuni kamati ya kuchunguza suala hilo na kuhakikishia umma kwamba itachukua hatua "kulingana na maadili na kanuni za Ushirika wa Anglikana".
Facebook yabuni mbinu mpya ya usalama kwa watumiaji wa Afghanistan
Facebook imefanya iwe vigumu kutafuta akaunti ya Wafhanistan miongoni mwa vipengee vingine vya usalama, huku kukiwa na hofu kwamba Taliban wanatumia mitandao ya kijamii kufuatilia wapinzani wao.
Nathaniel Gleicher, mkuu wa sera ya usalama wa kampuni hiyo kubwa ya teknolojia, aliandika ujumbe kwenye Twitter kusema kuwa Facebook pia "ilizindua kifaa kimoja cha kubofya kwa watu nchini Afghanistan kufunga akaunti zao haraka".
"Wakati wasifu wao umefungwa, watu ambao sio marafiki zao hawawezi kupakua au kushirikisha picha ya wasifu wao, au kuona machapisho yao mtandaoni."
Katika mtandao wa Instagram, ambao unamilikiwa na Facebook, kampuni hiyo "kutoa arifu za pop-up nchini Afghanistan na hatua maalum ya jinsi ya kulinda akaunti yako".
Polisi Uganda wanawasaka watu wanaonunua chapati tano au zaidi
Polisi katika wilaya ya Moroto kaskazini mwa Uganda wameanza kuwakamata watu wanaonunua chapati tano au zaidi, wakishuku huenda wanawalisha wezi wa mifugo katika eneo hilo, Uganda Radio Network (URN) inaripoti.
"Tumepokea taarifa kwamba wale wanaonunua chapati nyingi wanawapelekea wapiganaji misituni," Micheal Longole, msemaji wa polisi wa Karamoja, alinukuliwa URN.
Alisema kukomesha usafirishaji wa chakula kwa wezi hao huenda kukawalazimu kutoka mafichoni na kuwasilisha silaha zao.
Mwanaharakati wa amani wa eneo hilo Mark Koryang alisema mpango huo hautafaulu "Hawa wapiganaji wanaweza kuishi bila hata kula chapati," alisema. Mkazi mwingine aliiambia URN kwamba maafisa wa usalama walihitaji kufanya kazi na watu wa eneo hilo ili kukabiliana na ukosefu wa usalama katika jimbo hilo.
Bunduki 58 zimepatikana katika eneo zima tangu zoezi la upokonyaji silaha lilipoanza mnamo Julai 17, Edrine Mawanda, msemaji wa kitengo cha jeshi anayefanya zoezi hilo, aliiambia URN.
Marekani inatoa zawadi ya dola milioni tano kumsaka mkuu wa zamani wa jeshi la Guinea-Bissau
Marekani imetangaza zawadi ya dola milioni tano (sawa napauni milioni 3.7) rkwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa au kutiwa hatiani kwa mkuu wa zamani wa jeshi la Guinea-Bissau Antonio Indjai.
Bwana Indjai aliongoza mapinduzi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi mwaka 2012 kabla ya kufutwa kazi miaka miwili baadaye katika mpito wa kidemokrasia.
Mamlaka nchini Marekani ilimshtaki mnamo mwaka 2013 kwa tuhuma za kupanga njama ya ulanguzi wa dawa za kulevya aina ya Coccaine na kuuza silaha kwa waasi wa Colombia.
Siku ya Alhamisi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema kuwa Bwana Indjal alikuwa amewekewa marufuku ya usafiri na Umoja wa Mataifa tangu Mei 2012 kutokana na kuhusika kwake katika mapinduzi.
Ilisema alionekana kama mmoja wa watu wenye “ushawishi” mkubwa wanaotumia fedha walizopata kupitia ufisadi kuvuruga shughuli za serikali na utawala wa sheria katika eneo hilo”.
"Indjai iliongoza shirika la uhalifu […] hata wakati alikuwa mkuu wa Kikosi cha Wanajeshi wa Guinea Bissau," ilisema taarifa
Anakabiliwa na mashtaka ya kula njama za ugaidi, njama ya kuagiza dawa za kulevya miongoni mwa zingine.
Vifo vya shambulizi la kigaidi nchini Burkina Faso vyafika watu 80
Idadi ya watu waliopoteza maisha siku ya Jumatano baada kundi la Kijihadi lililovamia wanajeshi waliokuwa wanawasindikiza wananchi imeongezeka kufikia 80 huko nchini Burkina Faso, Mamlaka za nchi hiyo zimethibitisha.
Inakadiriwa kuwa raia wa kawaida waliokumbwa na shambulizi hilo ni 60, huku idadi iliyosalia ikiwa ni ya wanajeshi.
Wanamgambo wa kiislamu 80 pia wamuliwa karibu na mji wa Arbinda hayo yamesemwa na Waziri wa habari nchini humo.
Ni shambulizi la hivi karibuni zaidi kutokea katika ukanda wa Sahel hasa nchini Burkina Faso, ambapo wanajeshi waliojiunga na makundi ya kigaidi hasa la al-Qaeda pamoja na dola la kiislamu wameonekana kushamiri katika mipaka ya Niger na Mali.
Maelfu ya raia wamepoteza maisha na mamilioni kujikuta bila makazi tangu mwaka 2018.
Huku hayo yakiarifiwa Wanajeshi 11 kutoka Mali wameuwawa baada ya shambulizi lililotokea katikati mwa mji wa Mopti, Kiongozi wa jeshi amethibitisha.
Taarifa zinasema kuwa askari wengine tisa walimuziwa vibaya baada ya gari walilokuwemo kupigwa bomu, vilevile msafara wao uliendelea kushambuliwa na risasi.
Kiongozi wa kijeshi nchini Mali ameyataja mashambulizi hayo kuwa ni ya kigaidi huku akiwahusisha kundi hilo kuwa na ukaribu na makundi mengine ya kigaidi ambayo ni al-Qaeda na dola la kiislamu.
Wiki iliyopita mamlaka ya kiusalama nchini Mali ilitoa taarifa ya kuuliwa raia wake 40 na makundi yenye msimamo mkali ya kiislamu huko mashariki mwa nchi hiyo.
Mwanamke na Mwafrika kwa kwanza kuongoza WTO aitwa "Bibi" na gazeti la Uswizi
Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Ngozi Okonjo-Iweala, amekaribisha uamuzi wa mdhibiti wa vyombo vya habari wa Uswizi ambao ulipata kichwa cha habari kinachomfafanua kama "bibi" baada ya uteuzi wake kuongoza bodi hiyo yenye kuegemea ubaguzi wa kijinsia.
Gazeti la Aargauer Zeitung lilikuwa na kichwa cha habari kinachosoma: "Bibi huyu atakuwa mkuu wa WTO", baada ya Bi Okongo-Iweala kuteuliwa mnamo mwezi Machi.
Gazeti hilo liliomba msamaha baada ya kukososlewa vikali kutokana na kichwa chake cha habari na kusemekana kwamba kilikuwa "kisichofaa".
Bi. Okonjo-Iweala, Mnigeria-Mmarekani, ni mchumi msomi wa chuo kikuu cha Harvard na anayeheshimika.
Bi. Okonjo-Iweala, 67, ndiye Mwafrika na mwanamke wa kwanza kuongoza WTO.
Alituma ujumbe Alhamisi kwamba Baraza la Wanahabari la Uswisi lilikuwa sawa kupaza sauti juu ya ubaguzi wa kijinsia.
Katika uamuzi wake Jumanne, mdhibiti wa vyombo vya habari alisema kuwa wameshindwa kubaini ikiwa kuna upendeleo wa ubaguzi wa rangi.
"Hata hivyo, ... ni dhahiri kwamba ikiwa hii ingemhusu waziri wa zamani wa fedha na waziri wa mambo ya nje mwanamume katika nchi ya watu milioni 200, kichwa cha habari 'Babu awa mkurugenzi mkuu wa WTO'hakingeweza kutumika", tovuti ya habari ya Barron iliripoti.
Unayofaa kujua kuhusu kinachofanyika Afghanistan
Imekuwa siku tano sasa tangu Taliban iuteke mji wa Kabul na kuchukua udhibiti wa Afghanistan.
Haya ndio ya hivi punde:
- Taliban wanawatafuta watu waliofanya kazina vikosi vya Nato au serikali ya zamani ya Afghanistan, ripoti ya UN imeonya
- Taliban pia hivi karibuni iliwatesa na kuua watu wa jamii ya walio wachache ya Hazara ambaowaliteswa kwa muda mrefu, kulingana na ripoti tofauti kutoka Amnesty International
- Mashahidi walitoa taarifa za kutisha za mauaji hayo, ambayo yalitokea mwanzoni mwa Julai katika mkoa wa Ghazni
- Nchini Uingereza, waziri wa Mambo ya nje Dominic Raab anakabiliwa na wito wa kujiuzulu baada ya kushindwa kumpigia simu Waziri wa Mambo ya nje wa Afghanistan Hanif Atmar kuomba msaada wa haraka katika kuwaondoa wakalimani wa Afghanistan ambao walikuwa wakifanya kazi kwa jeshi la Uingereza
- Bw Raab, ambaye alikuwa likizo nchini Ugiriki, alikabidhi jukumu hilo kwa waziri mdogo. Ofisi ya Mambo ya nje sasa imeithibitishia BBC kwamba simu hiyo haikufanyika kamwe
- Na huku pakiwa na hofu ya usalama, Facebook imeondoa uwezo wa kutazama na kutafuta orodha ya "Marafiki" kwa akaunti za watu nchini Afghanistan
- Kuna hofu kwamba Taliban wanatumia mitandao ya kijamii kuwasaka wapinzani
China: Sera ya watoto watatu yapitishwa rasmi kuwa sheria
China imefanya marekebisho rasmi kwa sheria zake ili kuwaruhusu wanandoa kuwa na watoto hadi watatu, ili kuongeza kiwango cha kuzaliana.
Kanuni hiyo ilikuwa moja kati ya kadhaa zilizopitishwa Ijumaa kwenye mkutano wa wabunge wa bunge la kitaifa National People Congress (NPC).
Maelezo juu ya sheria yenye utata ya kupambana na vikwazo dhidi ya Hong Kong, ambayo wafanyabiashara wengi walihofia ingewaweka katika wakati mgumu, pia ilitarajiwa.
Lakini vyombo vya habari vya Hong Kong viliripoti Ijumaa kuwa uamuzi huo umecheleweshwa.
China ilitangaza mnamo mwezi Mei kuwa itawaruhusu wanandoa kuwa na watoto hadi watatu, katika mabadiliko makubwa ya sera.
Uamuzi huo sasa umepitishwa rasmi kuwa sheria, pamoja na maazimio kadhaa ambayo yalilenga kuongeza kiwango cha kuzaliana na "kupunguza mzigo" wa kulea mtoto, limesema shirika la habari la Xinhua.
Hii ni pamoja na kufuta "ada ya uendelezaji jamii" - adhabu ya kifedha kwa wanandoa hulipwa kwa kuwa na watoto zaidi ya idadi iliyoidhinishwa, kuhimiza serikali za mitaa kutoa likizo ya wazazi, kuongeza haki za ajira za wanawake na kuboresha miundombinu ya utunzaji wa watoto.
Takwimu za hivi karibuni za sensa zilionesha kupungua kwa kasi ya kiwango cha kuzaliana.
Soma zaidi:
Uganda yasitisha oparesheni za mashirika 50 yasio ya kiserikali
Mamlaka nchini Uganda zimesitisha shughuli za mashirika karibu 50 yasio ya kiserikali .
Mashirika mengine yamezuiwa kuendelea na shughuli zao kwa muda usiojulikana, kwa kushindwa kujiandikisha na kupata leseni zao, na mengine kwa kushindwa kuwasilisha mahesabu yaliyofanyiwa ukaguzi wa mapato ya kila mwaka kwa Ofisi ya Kitaifa ya NGO.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi hiyo Ijumaa inasema kwamba mengine yamekuwa yakifanya kazi bila hata kusajiliwa.
Ofisi hiyo, ambayo ni idara ya Wizara ya Mambo ya Ndani inasimamia usajili na shughuli za mashirika yasio ya kiserikali kote nchini
Mengi ya mashirika hayo hushughulika na haki za bnadamu namasuala ya sera ilhali mengine yanafadhiliwa na mashirika ya kidini na yale ya kutetea haki za wanawake
Wale ambao kazi yao zimesimamishwa kwa muda usiojulikana ni pamoja na Chapter Four Uganda, iliyoanzishwa na kuongozwa na wakili maarufu wa haki za binadamu Nicholas Opiyo. Kulingana na taarifa hiyo, shirika hilo halijawasilisha vitabu vyake vya mahesabu tangu 2016.
Opiyo alikamatwa na kufungwa jela mnamo Desemba 2020, na kushtakiwa kwa utakatishaji fedha , wakati mamlaka ilipochunguza chanzo cha fedha kwa shirika lake. Baadaye alipewa dhamana lakini bado anakabiliwa na mashtaka.
Opiyo kupitia ujumbe wa twitter amesema watawasilisha ushahidi na risi za kuthibitisha kwamba wametekeleza sheria zote na kulipia ada zao pamoja na kuwasilisha vitabu vyao vya mahesabu kwa bodi hiyo
Mwanajeshi Canada akabiliwa na kifungo jela kwa kulisha wenzake keki zenye bangi
Mwanajeshi wa Canada ambaye alilisha wanajeshi wenzake keki yenye bangi wakati wa zoezi la silaha sasa anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka mitano.
Koplo Chelsea Cogswell alipatikana na hatia ya kuwapawanajeshi wanane, "kitu cheye dawa za kulevya" pamoja na kuonesha kitendo cha aibu.
Wanajeshi hao walikuwa wameelezea kuhisi kulewa na kuchanganyikiwa wakati wameshika silaha baada ya kula keki alizowapa mnamo mwaka 2018. Uhalifu huo ulitokea miezi mitatu kabla ya bangi kuhalalishwa kote nchini Canada.
Jaji wa Jeshi Cmdr Sandra Sukstorf alitangaza uamuzi huo Jumatano.
Alisema waendesha mashtaka kwamba walithibitisha bila shaka yoyote kuwa wanajeshi walioathiriwa walikuwa wamekula bangi iliyochanganywa na keki, ambayo koplo aliwapa kwa kujua.
Kesi hiyo ya kushangaza inatokana na tukio lililotokea katika Kituo cha Mafunzo ya Kupambana huko CFB Gagetown katika mkoa wa New Brunswick.
Waendesha mashtaka katika kesi hiyo ya kijeshi walisema kwamba Cogswell aliongezea hatari zaidi kwa hali ambayo yenyewe ilikuwa tayari ni hatari wakati alipowapa keki za chokoleti alipokuwa akisimamia kantini wakati wa mazoezi ya silaha uwanjani.
Wanajeshi waliokuwa wanatoa ushahidi walikiri kuhisi "kutojua kinachoendelea", "kuchanganyikiwa" na "kuwa katika tishio fulani" na kuwa "walegevu" baada ya kula keki hizo zilizotengenezwa nyumbani.
Maafisa wa matibabu waliitwa kufanya uchunguzi baada ya wanajeshi kuripoti dalili zao.
Licha ya kwamba ilikuwa siku ya joto, uchovu wa joto uliondolewa.
Baadaye, watano walithibitishwa kuwa na chembechembe za bangi, kama ilivyokuwa kwa keki moja iliyokuwa imefungushwa vizuri kwenye eneo la tukio.
Madhara ya Bangi
- Unaweza kusababisha kuchanganyikiwa na wasiwasi usio wa kawaida
- Ikivutwa na tumbaku, inaweza kuongeza hatari ya ugonjwa kama vile saratani ya mapafu
- Matumizi ya mara kwa mara yamehusishwa na hatari ya kupatwa na magonjwa ya kiakili
- Upungufu wa kudumu wa kiwango cha mtu kufikiria na kufahamu mambo, baada ya kutumia kwa muda mrefu
Pia unaweza kusoma:
Kiongozi mkuu wa kidini Gaza aonya dhidi ya kupinga chanjo ya Covid
Kiongozi mkuu wa Gaza amewataka Wapalestina kupata chanjo haraka iwezekanavyo.
Katika ujumbe wa video, Sheikh Hassan al-Lahhan anasema yeyote anayechelewe kupata chanjo ni “mwenye dhambi”na anaelezea mtu yeyote anayesambaza virusi hivyo bila kukusudia kama “wauwaji wa kutokusudia”.
Kama kiongozi mkuu wa Kiislamu wa Gaza, Sheikh Hassan al-Lahhan anasimamia huduma ya maswala ya kidini katika eneo linaloongozwa na Hamas.
Jaribio la kuhamasisha kuchukua chanjo linakuja wakati viwango vya wanaopata maambukizi ya Covid-19 ikianza kuongezeka tena huko Gaza, ambako mfumo wa afya umelemaa kutokana na vita vya miaka.
Uwasilishaji wa chanjo kwa maeneo ya Palestina yaliyokaliwa umekuwa kwa mwendo wa polepole sana, lakini makundi ya kutoa misaada yanasema habari potofu na kusita kupata chanjo pia kumekuwa pingamizi.
Huko Gaza zaidi ya watu 120,000 wamepokea angalau dozi moja - karibu asilimia 5 tu ya idadi ya watu katika Ukanda huo.
- Watanzania wana maoni yapi kuhusu kupokea chanjo ya Corona?
- Ukweli kuhusu hali ya mtu baada ya kupata chanjo ya Covid-19
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ataka mapigano kusitishwa Ethiopia
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka tena kusitishwa mapigano mara moja katika eneo la Ethiopia la Tigray, ambapo vikosi vya serikali na wapiganaji waasi wamekuwa katikamizozo tangu Novemba mwaka jana
António Guterres alielezea hali ya kibinadamu huko Tigray kama "mbaya" na akasema mashirika ya misaada yanahitaji kufika katika eneo hilo bila vikwazo.
"Mazungumzo kama haya yanaweza kuchangia kushughulikia sababu za msingi za mzozo na kuhakikisha sauti za Waethiopia zinaleta njia ya amani," alisema.
Mamilioni ya watu wamehama makazi yao na mamia ya maelfu wanaishi katika hali ya njaa.
Wadukuzi waiba takribani dola milioni 100 za sarafu za kidigitali Japan
Kampuni moja kubwa ya ubadilishanaji wa pesa za kidigitali nchini Japan imekumbwa na wizi mkubwa wa sarafu zake za kidijitali ambapo wadukuzi wameiba $ 100m (£ 73m).
Kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya pochi zake za sarafu hizo "zimeathirika'
Ni wizi mkubwa wa pili wa pesa za sarafu za kidigitali kufanyika katika siku za hivi karibuni.
Wiki iliyopita, jukwaa jingine la sarafu za kidigitali la Poly lilikuwa katikati wizi mwingine wa $ 600m.
"Tunasikitika kutangaza kwamba pochi za sarafu za kidigitali za #LiquidGlobal zimeingiliwa , tunahamishia mali kwenye mikoba salama," kampuni hiyo ilisema kwenye Twitter.
Zimbabwe: Mwanaume akamatwa baada ya msichana kufariki akijifungua kanisani
Polisi nchini Zimbabwe imemkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 26 baada ya msichana kufariki dunia wakati anajifungua kanisani, kesi ambayo imesababisha hasira miongoni mwa raia na wanaharakati wanaotetea haki za binadamu.
Anna Machaya, 15, anaripotiwa kufariki na kuzikwa mwezi uliopita katika kaburi lililo kanisani eneo la mashariki mwa Marange.
Polisi pia wamewakamata wazazi wake.
Kesi hiyo imeweka wazi unyanyasaji wa watoto kwani inaripotiwa alilazimishwa kuacha shule ili aolewe.
Wazazi wa Anna wanashutumiwa kwa kusema uongo juu ya umri wake na pia waliahidi binti yao wa miaka tisa kumuozesha kwa mtu huyo huyo, Hatirarami Momberume.
Mwanaume huyo anakabiliwa na mashtaka ya ubakaji wa watoto.
Washtakiwa hao watatu bado hawajatoa maoni yao kuhusiana na tukio hilo.
Kifo cha Anna kilichotokea Julai 15, siku chache baada ya siku yake ya kuzaliwa, kimeweka angalizo juu ya tabia ya ndoa za utotoni katika Kanisa maarufu la Apostolic Church nchini Zimbabwe, ambalo mara nyingi hukataa utumiaji wa dawa na matibabu hospitalini.
Zaki Anwari: Mcheza soka wa Afghanistan aanguka kutoka kwa ndege ya Marekani na kufariki dunia Kabul
Mamlaka ya Afghanistan imethibitisha kwamba mwanasoka kijana alifariki dunia baada ya kujaribu kuondoka nchini humo kwa kudandia ndege ya jeshi la Merekani na kuanguka uwanja wa ndege wa Kabul.
Zaki Anwari, 19, alikuwa ameichezea timu ya taifa ya vijana ya Afghanistan.
Maelezo zaidi ya ni lini alifariki dunia bado hayajawekwa wazi.
Tangu Taliban kuteka nchi ya Afghanistan, maelfu ya watu wamejitokeza kwenye uwanja wa ndege wa Kabul, wakati ambapo nchi za Magharibi zinakimbilia kuhamisha raia wao na wenzao wa Afghanistan.
Picha ziliibuka Jumatatu zikionyesha mamia ya watu wakikimbia kufuata ndege ya jeshi la anga la Marekani wakati ikishuka kwenye barabara ya kupaa.
Watu wengine walionekana wakishikilia upande mmoja wa ndege.
Ripoti za vyombo vya habari vya eneo zasema kwamba watu wasiopungua wawili waliuawa baada ya ndege hiyo kupaa.
Kikosi cha anga cha Marekani pia kimethibitisha kuwa mabaki ya binadamu yalipatikana katika vifaa vya kutua vya ndege baada ya kuwasili Qatar.
- Video inayoonesha vurugu katika uwanja wa ndege