Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tanzania yathibitisha wimbi la tatu la Corona
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amethibitisha kwamba kuna viashiria vya wimbi la tatu la virusi vya Corona nchini humo.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
‘Fasheni ya Muislam inavyostawi’
Mtindo wa mwanadada kijana Muislam undelea kupata umaarufu, hususan Asia. Nembo kubwa zinachukua mitindo ya kadri na matokeo yake nguo za mtindo wake linaendelea kuwa soko linalokuwa haraka.
Hukumu ya viongozi 9 wa Upinzani Tanzania yabatilishwa
Mahakama Kuu ya Tanzania leo imetengua hukumu ya Mahakama ya Kisutu Ijijini Dar es Salaam, iliyowatia hatiani viongozi tisa wa chama kikuu cha upinzani nchini humo (CHADEMA).
Mwezi Machi mwaka huu Mahakama ya Kisutu iliwatia hatiani viongozi hao, wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwa makosa 12 kati ya 13 ambayo walishtakiwa nayo mwezi February 2018.
Makosa hayo ni pamoja na kuitisha maandamano bila kibali na kusababisha vurugu. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wenzake wakatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 350 za Tanzania ambazo ni sawa na dola elfu kumi na tatu.
Mbowe na wenzake walikata rufaa na sasa Mahakama kuu imeamuru kurejeshwa kwa fedha hizo.
Wakili wa Chadema, Peter Kibatala amenukuliwa akisema wameanza kudai fedha hizo, ‘tumeanza mchakato wa kudai faini, lakini wateja wangu rekodi zao zimefutwa leo’, alisema Kibatala.
Mbali na Mbowe, viongozi wengine walionufaika na hukumu hiyo ni katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika, Naibu katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar ambaye alikuwa mgombea Mwenza urais katika uchaguzi mkuu uliopita, Salum Mwalimu.
Wengine ni Halima Mdee, Esther Bulaya, Esther Matiko ambao ni wabunge na waliokuwa wabunge katika bunge lililopita, John Heche na Peter Msigwa.
Mwingine aliyenufaika ambaye hakuwa amekata rufaa ni aliyekuwa Katibu mkuu wa CHADEMA, Vicent Mashinji aliyehamia CCM.
Tanzania yathibitisha wimbi la tatu la Corona
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amethibitisha kwamba kuna viashiria vya wimbi la tatu la virusi vya Corona nchini humo.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika mkutano wake na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania(TEC), Rais Samia amesema zipo ishara ndani ya nchi hiyo kwamba janga hilo lipo.
‘Kama tunavyojua duniani sasa hivi kuna wimbi la 3 la Corona, tumetoka kwenye wimbi la kwanza Tanzania tumeingia tumeingia, limekwenda limekwenda limepungua kidogo tumeingia wimbi la pili, tumekwenda na sasa wimbi la tatu’.
Rais Samia alisema ‘Ishara ndani ya nchi tayari zinaonekana, tayari tuna wagonjwa ambao wemeshaonekana kwenye wimbi hili la tatu’, alisema Rais Samia akirejea pia kukumbusha ziara yake katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam ‘kama mnakumbuka siku niltembelea Hospitali ya Mwanyamala, kuna wodi Daktari mfawidhi alikuwa anaingiza akanambia humu kuna wagonjwa wenye matatizo ya kupumua, nikamwambia hebu kuwa muwazi, nikamwambia Covid? akanambia eeh Covid, wakati wapiga picha walikuwa wameshatangulia, nikawaambie nyie tuokeni haraka’.
Pamoja na kueleza uwepo wa wimbi hilo la tatu, Rais Samia alitaka kuchukuliwa kwa tahadhari dhidi ya wimbo hilo la tatu la maambukizi ya virusi hivyo vya corona.
- Unaweza pia kusikiliza:
‘Kwa hiyo ni kusema kwamba hili jambo bado lipo, tusijiache bado lipo, tuchukue tahadhari zote, na tunawaomba sana vio wa dini,mlisema hili kwa sauti kubwa kwa waumini wetu ili tujiepushe na vile vifo vya makundi’, alisema Rais Samia.
Kwa upande wao mbali na kumpongeza Rais Samia katika jitihada zake za kupambana ugonjwa huo na kuleta maendeleo, Rais wa Baraza hilo la Maaskofula Kanisa Katoliki, Gervas Nyaisonga alitaka kuboreshw akwa sera mbalimbali ili kusaidia utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za afya na elimu.
Kwa zaidi ya mwaka sasa, Tanzania haijatoa takwimu zozote za wagonjwa wala vifo vitokanavyo na maambukizi ya virusi vya Corona, huku Rais aliyepita, John Magufuli alieleza kukamilizika kwa virusi hivyo nchini humo kutokana na njia mbalimbali zilizotumika ikiwemo kufanya Maombi.
Tangu aingie madarakani mwezi Machi mwaka huu kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Magufuli, Rais Samia, amekuwa mstari wa mbele kushughulikia suala hilo, ikiwemo kuunda kamati maalumu ya kuthamini ugonjwa huo.
Mpaka April mwaka 2020, taarifa rasmi ilionyesha Tanzania ilikuwa na wagonjwa 509 wa corona, vifo 21 na waliopona 183.
Unaweza kusoma:
- Virusi vya Corona: Rais wa Tanzania kuunda kamati ya wataalamu kumshauri
- Rais Samia Suluhu Hassan aruhusu balozi na taasisi kuingiza chanjo nchini humo
- Virusi vya Corona: WHO yasema chanjo ya corona inaweza kufika Tanzania ndani ya wiki mbili
BBC yapeleka malalamiko yake dhidi ya Iran kwa Umoja wa Mataifa
BBC imepeleka malalamiko yake kwa Umoja wa Mataifa juu ya unyanyasaji wa wafanyakazi wake wa idhaa ya Persia.
Imesema maafisa wa ujasusi wa Iran wametishia kuwateka nyara wafanyakazi wake waliopo mjini London na kuwarudisha Iran.
Hii si mara ya kwanza kwa BBC kuripoti matatizo ya aina hii kwa Umoja wa Mataifa.
Iran ilikanusha madai hayo mwaka jana, ikiishutumu Idhaa ya BBC ya Persia kwa kusambaza taarifa za uongo kuchochea mapinduzi dhidi ya serikali.
Wakili wa BBC amelitolea wito Baraza la usalama la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za kutatua tatizo hilo.
Jumla ya Wairan milioni 18, sawa na takriban robo ya watu wa nchi hiyo hupokea taarifa za Idhaa ya BBC Persia.
Watu 99 hawajulikani walipo baada ya jengo kuporomoka nchini Marekani
Watu tisini na tisa bado hawajulikani walipo baada ya jengo la gorofa kupromoka nchini Marekani
Tukio hilo limesababuiisha kifo cha mtu mmoja.
Mwandishi wa BBC anasema wahdumu wa uokozi wamekuwa wakiendelea na sughuli ya kuwasaka watu kwenye vifusi vya jengo hilo usiku kucha.
Tazama jinsi lilivyoporomoka katika video hii:
Padri akamatwa kwa shutuma za wizi wa mamilioni ya pesa
Ofisi ya upelelezi ya Rwanda (RIB) imethibitisha kuwa inamshikilia Mkuu wa makasisi wa Kanisa katoliki Parokia ya Rwamagana nchini humo, Jean-Marie Telesphore Ingabire, ambaye anashukiwa kusaidia katika madai ya wizi na kufich ushahidi.
Msemaji wa RIB, Thierry Murangira, ameiambia BBC, kuwa Padre Ingabiri amekamatwa na mamilioni ya fedha yanayodaiwa kuwa ni ya wizi.
"Mkuu wa mapadri wa Parokia ya Rwamagana ya Kanisa Katoliki yuko mahabusu, anashutumiwa wa kusaidia katika madai mashitaka ya wizi, huku uchunguzi ukiendelea,” amesema Murangira.
Vyombo vya habari nchini Rwanda vilituma taarifa ya kukamatwa kwa Padri Jean-Marie Telesphore Ingabire kupitia Twitter:
Uchunguzi bado unaendelea kubaini kiasi cha pesa kilichohusika, alisema Bw Murangira na kuongeza kuwa kasisi huyo alikuwa akitunza pesa haramu zinazodaiwa kuibwa, jambo lililowafanyawaendelee na wizi.
Vyanzo mbalimbali vinaonesha kuwa watu kadhaa walikamatwa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita kwa tuhuma za wizi , akiwemo ndugu zake Padre Ingabire ambao walipatikana wakiwa wamejifichana "kiwango kikubwa cha fedha ."
Kasisi huyo anasemekana kushindwa kuelezea ni kwa vipi alikuwa na mamilioni ya fedha nyumbani kwake, wakati msako ulipofanyika kwenye makazi yake.
Murangira amsema kuwa RIB inatarajia kupata maelezo zaidi wakati uchunguzi ukiendelea.
Aina mpya ya mtu wa kale yavumbuliwa Israeli
Watafiti wanaofanyia kazi nchini Israeli wamebaini aina mpya ya mtualiyeishi zamani ambaye aliishi karibu na viumbe wetu kwa zaidi ya miaka 100,000.
Wanaamini kwamba mabaki yaliyogunduliwa karibu na mji wa Ramla yanawakilisha moja ya kikundi‘’cha mwisho ‘’cha binadamu wa kale zaidi.
Mabaki yaliyopatikana ni pamoja na sehemu ya fuvu na taya vya mtu aliyeishi kati ya miaka 140,000 na 120,000 iliyopita.
Maelezo ya uvumbuzi huo yamechapishwa katika jarida la kisayansi .
Watafiti hao wanadhani kwamba mtu huyo alitokana na spichi wa zamani ambao walisambaa kwenye eneo hilo, maelfu ya miaka iliyopita na kuongezeka kwa binadamu wa kale (Neanderthals) barani Ulaya na wenzao wanaofanana katika bara Asia.
Wanasayansi wameita uvumbuzi wao mpya jina la "Nesher Ramla Homo type".
Dkt Hila May wa Chuo Kikuu cha Tel Aviv amesema uvumbuzi huo unabadilisha hadithi ya mabadiliko ya binadamu hususan wale wa kale.
Picha ya jumla ya mabadiliko ya binadamu wa kale miaka ya nyuma walihusishwa na karibu na Ulaya.
''Yote ilianzia katika Israel. Tunasema kwamba kikundi cha wakazi kilikua chanzo cha idadi ya watu," aliiambia BBC News.
Museveni atangaza tena maombi, kufuatia wimbi la Corona Uganda
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametanga siku ya mapumziko leo Ijumaa kwa ajili ya kuwaombea wahudumu wa afya pamoja na familia zilizoathiriwa na virusi vya corona.
Nchi hiyo ya Afrika Mashariki inakabiliwa na wimbi la pili la virusivya corona, jambo lililomsukuma raiskuweka amri ya kutotemebea na kufungwa kwa shughuli’’lickdown’’ mapema mwezi huu.
Bunge la Uganda limefngwa kwa muda kwa wiki mbilihuku maafisa wakisema watu 100 katika bunge hilo walipatakana na maambukizi ya virusi hivyo.
Idadi ya vifo vilivyothibitishwa imeongezeka mara 10 katika kipindi cha siku 14 katika kulingana na wavuti wa Our Word in Data,
Chini ya 2% ya watu ndio waliopokea walau dozi moja ya chanjo ya virusi vya corona.
Wakati haya yakijiri , Uingereza imeiongeza Uganda katika orodha yake ya nchi ambazo raia wake wamezuiwa kusafiri kwenda nchini Ungereza.
Ofisi ya mambo ya kigeni na Jumuiya ya Madola (FCO) imesema kuwa kuanzia Juni30, "Uganda itahamia kwenye orodha nyekundu ya kuingia England ".
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Ijumaa tarehe 25.06.2021