Zaidi ya wanawake 30
wameishtaki kampuni ambayo inamiliki tovuti ya kuonesha video za ngono kwa
madai kuwa wametumiwa vibaya kwa kutumia picha zao za ngono.
Wanawake hao wanasema kuwa
video zao ziliwekwa katika tovuti moja ya video za ngono bila idhini yao na
wamewasilisha kesi mahakamani huko California.
Kesi hiyo inashutumu kampuni
ya Mindgeek kwa kuendesha "biashara haramu".
Katika taarifa yake, tovuti
hiyo na ngono ilitaja madai hayo kama ya "kusikitisha, ya kizembe na
uwongo mtupu".
Tovuti za kuonesha picha za
ngono zinatumiwa bila malipo lakini watumiaji wanaweza kulipa kwa mwezi ili
kupata picha za ubora wa juu na maudhui mengine zaidi.
Na mara nyingi maudhui yake huwa
ni ya watu wanaofuatilia mitandao hiyo na picha hizo huonekana na kila
mmoja.
Hata hivyo, kampuni
iliyoshitakiwa imesema kila video inayowekwa huwa inapitiwa tena na wasimamizi.
Tovuti hiyo ya ngono
imeelezea BBC kuwa: "Haiwezi kabisa kuweka maudhui ambayo ni haramu na
inachunguza malalamishi yoyote au madai yaliyotolewa juu ya maudhui yake kwenye
jukwaa lao."
Ilisema kwamba "ina
hakikisha usalama wa kutosha kwa watumiaji katika historia yake ikiwemo kupiga
marufuku uwekaji wa maudhui ambayo hayajathibitishwa".
Hata hivyo, kituo mshirika wa BBC
nchini Marekani CBS, kimesema kuwa tovuti za kuweka video za ngono
hazihitaji watumiaji wake kuthibitisha utambulisho wao au umri kwa wale
wanaoshiriki video hizo, kulingana na CBS, wala hazitafuti kuthibitisha idhini
za watu wanaoshiriki video zinazowekwa kwenye tovuti zao.
Brown Rudnick LLP, kampuni ya
sheria inayowakilisha walalamishi, imesema madai katika kesi hiyo yako chini ya
‘Sheria ya Ulinzi kwa Waathirika wa Usafirishaji haramu na Unyanyasaji ya mwaka
2000.’
Mmoja wa wanawake waliofungua
kesi ameliambia shirika la CBS kwamba alikuwa na miaka 17 pekee pale mchumba
wake alipomlazimisha kutengeneza video hiyo ya ngono.
Mwanamke huyo ambaye alitumia
jina lisilo la kweli la Isabella, alisema video hiyo baadaye iliwekwa kwenye
mtandao huo wa ngono bila idhini yake na yeye alijua hilo kutoka kwa rafiki
yake.
Tovuti
hiyo ya picha za ngono imesema "inachukulia kila malalamiko kuhusu
utumiaji mbaya wa jukwaa lake kwa uzito mkubwa ikiwemo malalamiko katika kesi
hii iliyowasilishwa mahakami".
Iliongeza
kwamba haikuwa na nia ya kuacha "maneno yaliyotiwa chumvi katika kesi hiyo
kutoonesha ukweli wa kuwa tovuti hiyo imeweka hatua na sera za kiusalama ambazo
zinashinda za tovuti nyingine yoyote ile kubwa mtandaoni ".
Desemba
mwaka jana, uchunguzi uliofanywa na gazeti la New York Times ulishutumu tovuti
hiyo kwa "kutengeneza" video za unyanyasaji dhidi ya watoto na
ubakaji – madai ambayo tovuti hiyo ilikanusha.
Mtandao
huo ulisema kuwa ulitembelewa na watu bilioni 42 mwaka 2019, huku video milioni
6.83 zikiwekwa kwa muda jumla wa kutazamwa wa miaka 169 lakini haikusema ni
wasimamizi wangapi iliajiri.