Afrika Kusini kutegua kitendawili cha mama anayedai kuzaa watoto 10

Mamlaka nchini Afrika Kusini "zinakusanya taarifa" juu ya sakata inayoendelea kuhusu mwanamke wa Pretoria anayedaiwa kuzaa watoto 10, mtandao mmoja wa habari umeripoti.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Olimpiki: Schoenmaker wa Afrika Kusini aweka rekodi mpya ya dunia

    SA

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kwenye Olimpiki za Tokyo, Afrika Kusini imekuwa na mshindi wake wa kwanza wa medali ya dhahabu katika kuogelea kwa kipindi cha miaka 25.

    Tatjana Schoenmaker aliweka rekodi mpya ya dunia katika fainali ya wanawake ya mita mia 200.

    Yeye ndiye mwanamke wa kwanza kuogelea chini ya muda was dakika 2 na sekunde 19.Jumanne, alishinda fedha katika mbio za mita 100.

    Ushindi wake wa mita 100 ulikuwa wa kwanza na muogeleaji wa kike kutoka Afrika Kusini katika kipindi cha miaka 21.

    Schoenmaker alisema ana matumaini ushindi wake utaleta furaha nyumbani baada ya siku za vurugu.Afrika Kusini ilishuhudia maandamano ya vurugu kwa wiki kadhaa na uporaji wa mali uliosababisha zaidi ya watu 300 kufariki dunia na kupotea kwa mali yenye thamani ya mabilioni ya pesa.

  2. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazao ya moja kwa moja. Hadi wiki ijayo kwaheri.

  3. Afungwa miaka mitatu kwa kuwapiga picha wanawake Misri

    Mahakama moja nchini Misri imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela mfanyakazi wa uwanja wa ndege wa Cairo kwa kuwapiga picha kisiri wasafiri wanawake.

    Mmoja wa wanawake hao aliwasilisha malalamishi baada ya kugundua mwanamume huyo amempiga picha sehemu nyeti.

    Uchunguzi wa simu yake ulibaini kuwa aliwafanyia karibu wanawake 20 kitendo sawa na hicho.

  4. Mtoto aokolewa mtoni akielea ndani ya boksi India

    Mtoto huyo mwenye umri wa siku 21 amepelekwa hospitalini

    Chanzo cha picha, ANIL KUMAR

    Maelezo ya picha, Mtoto huyo mwenye umri wa siku 21 amepelekwa hospitalini

    Nahodha wa boti moja katika jimbo la India lililopo eneo la kaskazini la jimbo la Uttar Pradesh amepokea pongezi chungu nzima baada ya kumuokoa mtoto wa kike aliyepatikana akielea ndani ya boksi dogo katika mto Ganges.Soma zaidi.

  5. Kamanda wa zamani wa waasi Liberia ahukumiwa kifungo cha miaka 20

    WAASI

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mahakama nchini Uswisi imemhukumu kamanda wa zamani wa waasi wa Liberia kifungo cha miaka ishirini jela mashitaka kadhaa ya uhalifu wa kivita ikiwemo ubakaji na mauaji aliyohusika katika miaka ya tisini.

    Majaji walidumisha mashitaka ishirini na moja kati ya ishirini na tano dhidi ya Alieu Kosiah ambaye ana kibali cha kuishi Uswisi.

    Ni Mliberia wa kwanza kushitakiwa na kuhukumiwa kwa uhalifu luliofanyika wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza Liberia mwaka 1989 na kumalizika mwaka 2006.

    Takriban watu laki mbili na elfu hamsini waliuawa katika vita hivyo ambavyo watoto walilazimishwa na waasi na majeshi kuwa wapiganaji.

  6. Afrika Kusini kutegua kitendawili cha mama anyedai kuzaa watoto 10

    Miguu ya mtoto mchanga

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mamlaka nchini Afrika Kusini "zinakusanya taarifa" juu ya sakata inayoendelea kuhusu mwanamke wa Pretoria anayedaiwa kujifungua watoto 10, mtandao mmoja wa habari umeripoti.

    Hakuna shirika lolote la habari limefanikiwa kuthibitisha taarifa hiyo iliporipotiwa mara ya kwanza na mtandao wa habari wa Pretoria News wiki iliyopita.

    "Kuna masuala kadhaa muhimu yanastahili kushughulikiwa” kabla ya kuhutubia umma, Waziri wa Ustawi wa Jamii Lindiwe Zulu aliuambia mtandao wa habari wa TimesLive.

    ''Madai hayo ni ya kushangaza, lakini malipo na moshi hapakosi moto. Tunataka kuwajibikia suala hili iwezekanavyo. Tunawajimu wa kufahamisha watu kinachoendelea," alinukuliwa kusema.

    Pretoria News imesema haitabadili msimamo kurusu taarifa ya kwamba Gosiame Sithole alizaa watoto 10 tarehe 7 mwezi Juni.

    Pia imechapisha ripoti kwamba anayedaiwa kuwa baba hajawaona watoto hao wachanga.

    Independent Media, kampuni mama ya wavuti huo wa habari, imeshutumu mamlaka kwa habari ya kujificha ikidai kwamba walitaka "kuficha uzembe unaokumba sekta ya afya ambao uliwahusisha wanasiasa wakuu na wafanyikazi wa umma".

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Bi Zulu alikataa kuthibitisha au kukana kuwepo kwa watoto hao lakini akaongeza kuwa Rais Cyril Rampahosa ataarifiwa kwanza kabla ya matokeo ya uchunguzi kutolewa hadharani.

  7. Niko tayari kwa amani ama vita na Marekani asema Kim Jong -un

    Kim Jong-un's slimmer frame has prompted more speculation about his health

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema nchi yake inahitaji kujiandaa kwa "mazungumzo na makabiliano" na Marekani na "haswa kujiandaa kikamilifu kwa mapambano".Soma zaidi.

  8. Kifo cha Kaunda: Kwanini Tanzania imetangaza siku saba ya maombolezo

    Kaunda

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza siku saba ya maombolezo kufuatia kifo cha mwasisi wa taifa la Zambia Kenneth Kaunda.

    Katika taarifa Rais Samia amemtaja Dkt Kaunda kuwa miongoni mwa viongozi mahiri na jasiri kuwahi kutokea barani Afrika.

    ''Wakati wa uhai wake Hayati Kaunda alitoa mchango mkubwa katika harakati za ukombozi akishirikiana na viongozi wengine akiwemo Baba wa taifa Malimu Julius Nyerere'',ilisema taarifa hiyo.

    kwanini Rais Samia amechukua hatua hiyo?

    Uhusiano kati ya Tanzania na Zambia ulitokana na uhusiano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili wakati wa harakati ya kupigania ukombozi wa Afrika.

    Suala muhimu barani Afrika katika karne ya 20 lilikuwa ni iwapo kuna uwezekano wa kubuni aina mpya ya jamii.

    Kenneth Kaunda nchini Zambia na Julius Nyerere nchini Tanzania waliamua mwelekeo wa nchi zao, na kufanyia majaribio wazo la kuwa na jamii moja isiyoegemea misingi ya ukabila miongoni mwa mambo mengine isipokuwa maendeleo katika mataifa yao.

    Wazo la kuwa na aina mpya ya jamii - ambalo lilikuwa msimamo wa vijana hao wa Kiafrika - lilikuwa muhimu sana kwa maendeleo katika mabara mengine.

    Mzee Kaunda alichapisha vitabu kadhaa vilivyoelezea fikra za ujamaa wa Afrika, ambayo ilifuatwa na viongozi wengine wa Afrika ikiwa ni pamoja na Kwame Nkrumah nchini Ghana na Julius Nyerere nchini Tanzania.

  9. Watimua mbio mahakamani baada ya kufutiwa kesi Tanzania

    Mahakamani

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wanaume sita raia wa China waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi nchini Tanzania wamezua gumzo kutokana na kitendo walichofanya baada ya kufutiwa mashtaka na kuachiwa huru na Mahakama moja jijini Dar es Salaam.

    Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, washtakiwa hao wafanyakazi wa kampuni ya meli ya Sinota Shipping Company walitoka mahakamani huku wakikimbia na kupanda gari kisha kuondoka mara baada ya kuachiwa huru.

    Hii ni baada ya Hakimu Mkazi, Rashid Chaungu kuwafutia mashtaka baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania( DPP) kuieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao.

    Washtakiwa walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matatu yaliyowafanya wakose dhamana.

    Wanaume hao ni Jin Erhao (35), Chengfa Yang (49), Ren Yuangqing (55), Shu Nan (50), Chen Shinguang (45) na Gu Jugen (57) wote wakazi wa Dar es Salaam.

    Haijabainika kwanini walitoka mbio mahakamani.

  10. Uchaguzi wa urais Iran unaokumbwa na mzozo wa wengine kufungiwa nje

    The economic crisis is one of the main issues for Iranian voters

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Raia wa Iran wanapiga kura kumchagua rais mpya huku mmoja kati ya wagombea wanne akitarajiwa kumrithi Hassan Rouhani ambaye anachukuliwa kama mwenye msimamo mkali.

    Kura za maoni zinaonesha kuwa Ebrahim Raisi, kiongozi wa kidini wa Shia ambaye ni mhafidhina anayeongoza mahakama, ndiye anayependelewa kuchukua wadhifa huo.

    Aliyekuwa gavana wa benki kuu ambaye anachukuliwa kuwa na msimamo wa wastani Abdolnasser Hemmati ndiyo mpinzani mkuu.

    Wapinzani na baadhi ya wanaopendelea mabadiliko wametoa wito wa kususiwa kwa uchaguzi, wakisema kuzuiwa kwa wagombea kadhaa kushiriki uchaguzi huo kumefanya Bwana Raisi kutokuwa na upinzani wa kisawa sawa.

    Kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khamenei amepiga kura yake mapema Ijumaa katika mji wa Tehran na kuhamasisha raia kujitokeza kupiga kura.

    "Kila kura inahesabiwa ... jitokezeni mumpigie kura na kumchagua rais wenu," alisema. "Hili ni muhimu kwa hatma ya baadaye ya nchi yako,"

    Ayatollah Ali Khamenei is the Islamic Republic's second supreme leader

    Chanzo cha picha, AFP

    Kuna minung’uniko mingi miongoni mwa raia wa Iran kuhusiana na changamoto za kiuchumi ambazo wamekumbana nazo tangu Marekani ilipojiondoa katika mpango wa nyuklia wa Iran miaka mitatu iliyopita na kuwekewa tena vikwazo vilivyolemaza nchi hiyo.

    Ushindi kwa mmoja wa wenye msimamo mkali hakutarajiwi kutatiza mazungumzo kati ya Iran na nchi zenye nguvu duniani ambayo lengo ni kuyafufua tena, kulikofanya Iran kukubali kupunguza kasi ya mpango wake wa nyuklia katika sehemu ya mabadilishano ya kuondolewa kwa vikwazo.

    Bwana Rouhani, mwenye msimamo wa wastani ambaye alitafuta kufanya majadiliano na nchi za Magharibi, hawezi kuchaguliwa tena kwasababu ameshahudumu kwa mihula miwili ya miaka minne minne.

    Ni kina nani walioidhinisha wagombea?

    Takriban wagombea 600 wakiwemo wanawake 40, walishiriki zoezi la kutaka kuingia debeni.

    Lakini mwisho wa siku ni wanaume saba pekee ndio walioidhinishwa mwezi jana na mahakimu 12 na wanatheolojia wa Baraza la Guardian, bodi yenye kufanya maamuzi kuhusiana na wagombea waliotimiza vigezo vya kugombea.

    Eshaq Jahangiri, Bwana makamu wa kwanza wa rais wa Rouhani na Ali Larijani, aliyekuwa spika wa bunge ambaye ni mhafidhina ni miongoni mwa wagombea mashuhuri ambao walifungiwa kugombea.

  11. Viongozi wa Afrika waendelea kumuomboleza Kaunda

    Kenneth Kaunda died on Thursday aged 97

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Risala za rambi rambi zimeendelea kutumwa kufuatia kifo cha Rais mwanzilishi wa Zambia Kenneth Kaunda, aliyefariki Alhamisi akiwa na miaka 97.

    Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi alimwelezea rais huyo wa zamani kama “mpiganiaji ukombozi wa nchi wa hadhi ya juu” kutokana na “ alivyojitolea mhanga kwa maslahi ya sio nchi yake tu bali pia kwa mataifa jirani na ubinadamu kwa ujumla”.

    Alisema Kaunda alikuwa ''rafiki wa dhati wa Botswana wakati ilipokuwa inapitia kipindi kigumu'' kutokana na mchango wake katika harakati za kupigania uhuru wa nchi hiyo.

    Rais Masisi ametangaza siku saba za maombolezo kwa heshma ya marehemu kiongozi huyo wa Zambia:

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema nchi yake inaomboleza “kifo cha baba wa uhuru na umoja wa Afrika – Rais Kenneth ‘KK’ Kaunda”.

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Chama tawala cha African National Congress (ANC), kilimtaja Kaunda kama kigogo wa wa Afrika Kusini na mpiganiaji harakati za ukombozi wa Afrika.

    “Dkt Kaunda anashikilia nafasi muhimu katika chama chetu, nchi yetu na watu wa Afrika Kusini. Alitukaribisha Zambia na kuifanya kuwa makao makuu ya ANC kwa zaidi ya miaka 30,” taarifa ya chama hicho ilisema.

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alisema Afrika imempoteza “mpigania ukombozi, mzalendo na mwanamajumui wa kweli”.

    Ruka X ujumbe, 3
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 3

    Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo alimkumbuka kama mmoja wa viongozi wa mwisho waliopigania uhuru ambaye alijitolea kwa njia tofauti.

    Soma zaidi:

    • Kenneth Kaunda - Mwana wa Afrika aliyekuwa na ushawishi ndani na nje ya Zambia
    • Kenneth Kaunda: Alikuwa ni mtu aliyeamini Waafrika katika kujitatulia matatizo yao
  12. WHO: Afrika iko katika wimbi la tatu la maambukizi ya Covid-19

    Millions of vaccine doses are needed

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Afrika inakabiliwa na wimbi la tatu la corona na kuna haja ya kupatikana kwa chanjo zaidi, Shirika la Afya Duniani (WHO)limesema.

    Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona imepita milioni tano huku nchi saba zikiishiwa na chanjo.

    "Afrika inahitaji mamilioni zaidi ya chanjo kwa sasa," Mkurugenzi wa WHO wa kanda ya Afrika Matshidiso Moeti, amesema.

    Afrika Kusini, Morocco, Tunisia, Ethiopia na Misri zimerekodi viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya Corona barani humo.

    Uganda na Namibia zinakabiliwa na wimbi la tatu la maaambukizi huku makumi ya watu wakiripotiwa kufa kila siku.

    Jumla ya watu elfu136,030 wamefariki kutokana na ugonjwa wa Covid -19 katika nchi tofauti za Afrika, kulingana na WHO.

    Kirusi cha Delta kimegunduliwa katika nchi 14 za Afrika huku kirusi cha Beta, kilichogunduliwa mara ya kwanza Afrka Kusini , kikifika katika nchi 25.

    WHO inasema hakuna muda kamili ulitolewa kubaini ni lini chanjo zaidi zitapatikana lakini limesistiza kwamba kuna haja kushughulikia upatikanaji wake kwa dharura.

  13. Wanawake waishitaki tovuti ya video za ngono

    WANAWAKE

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Zaidi ya wanawake 30 wameishtaki kampuni ambayo inamiliki tovuti ya kuonesha video za ngono kwa madai kuwa wametumiwa vibaya kwa kutumia picha zao za ngono.

    Wanawake hao wanasema kuwa video zao ziliwekwa katika tovuti moja ya video za ngono bila idhini yao na wamewasilisha kesi mahakamani huko California.

    Kesi hiyo inashutumu kampuni ya Mindgeek kwa kuendesha "biashara haramu".

    Katika taarifa yake, tovuti hiyo na ngono ilitaja madai hayo kama ya "kusikitisha, ya kizembe na uwongo mtupu".

    Tovuti za kuonesha picha za ngono zinatumiwa bila malipo lakini watumiaji wanaweza kulipa kwa mwezi ili kupata picha za ubora wa juu na maudhui mengine zaidi.

    Na mara nyingi maudhui yake huwa ni ya watu wanaofuatilia mitandao hiyo na picha hizo huonekana na kila mmoja.

    Hata hivyo, kampuni iliyoshitakiwa imesema kila video inayowekwa huwa inapitiwa tena na wasimamizi.

    Tovuti hiyo ya ngono imeelezea BBC kuwa: "Haiwezi kabisa kuweka maudhui ambayo ni haramu na inachunguza malalamishi yoyote au madai yaliyotolewa juu ya maudhui yake kwenye jukwaa lao."

    Ilisema kwamba "ina hakikisha usalama wa kutosha kwa watumiaji katika historia yake ikiwemo kupiga marufuku uwekaji wa maudhui ambayo hayajathibitishwa".

    Hata hivyo, kituo mshirika wa BBC nchini Marekani CBS, kimesema kuwa tovuti za kuweka video za ngono hazihitaji watumiaji wake kuthibitisha utambulisho wao au umri kwa wale wanaoshiriki video hizo, kulingana na CBS, wala hazitafuti kuthibitisha idhini za watu wanaoshiriki video zinazowekwa kwenye tovuti zao.

    Brown Rudnick LLP, kampuni ya sheria inayowakilisha walalamishi, imesema madai katika kesi hiyo yako chini ya ‘Sheria ya Ulinzi kwa Waathirika wa Usafirishaji haramu na Unyanyasaji ya mwaka 2000.’

    Mmoja wa wanawake waliofungua kesi ameliambia shirika la CBS kwamba alikuwa na miaka 17 pekee pale mchumba wake alipomlazimisha kutengeneza video hiyo ya ngono.

    Mwanamke huyo ambaye alitumia jina lisilo la kweli la Isabella, alisema video hiyo baadaye iliwekwa kwenye mtandao huo wa ngono bila idhini yake na yeye alijua hilo kutoka kwa rafiki yake.

    Tovuti hiyo ya picha za ngono imesema "inachukulia kila malalamiko kuhusu utumiaji mbaya wa jukwaa lake kwa uzito mkubwa ikiwemo malalamiko katika kesi hii iliyowasilishwa mahakami".

    Iliongeza kwamba haikuwa na nia ya kuacha "maneno yaliyotiwa chumvi katika kesi hiyo kutoonesha ukweli wa kuwa tovuti hiyo imeweka hatua na sera za kiusalama ambazo zinashinda za tovuti nyingine yoyote ile kubwa mtandaoni ".

    Desemba mwaka jana, uchunguzi uliofanywa na gazeti la New York Times ulishutumu tovuti hiyo kwa "kutengeneza" video za unyanyasaji dhidi ya watoto na ubakaji – madai ambayo tovuti hiyo ilikanusha.

    Mtandao huo ulisema kuwa ulitembelewa na watu bilioni 42 mwaka 2019, huku video milioni 6.83 zikiwekwa kwa muda jumla wa kutazamwa wa miaka 169 lakini haikusema ni wasimamizi wangapi iliajiri.

  14. Karibu katika matangazo mubashara leo Ijumaa 18.06.2021.